Wednesday, February 8, 2017

JINSI YA KUTAMBUA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO

JINSI YA KUTAMBUA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO
                                            NA; JAMES F. MZAVA





Bwana Yesu asifiwe nipende kukukaribisha tena katika somo langu jipya la jinsi ya kutambua kusudi la Mungu ndani yako. Moja ya maswali yanayowatatiza watu wengi duniani na wameshindwa kujua ni wao kutambua makusudi ya wao kuishi katika dunia hii. Wengi wamekua wakiishi katika maisha ambayo sio yao halisi bali wamekua wakiishi kwa kuiga iga maisha ya wengine jambo ambalo ni janga kubwa kwa mkristo kua hivyo. Ila nipende kukutia moyo usikate tamaa kwa maswali uliyonayo hebu fatana nami katika somo hili mwanzo hadi mwisho na nina Imani kua utapata kitu kikubwa cha kukusaidia.




NINI MAANA YA KUSUDI??
Watu wengi wameshindwa kuelewa maana halisi ya maisha yao jambo liliwapekea kuishi maisha ya wengine. Ngoja nikupe maana halisi ya kusudi

KUSUDI ~ Ni wazo au lengo lililowekwa ndani ya akili yako ili liwe kama malengo ambayo kwa hayo yataweza kuongoza maishani ili kutimiza lile ambalo Mungu ameweka katika maisha yako.


Hebu tuangalie Zaidi katika Biblia inasema nini juu ya kusudi la Mungu katika maisha ya mwanadamu aliyemuumba


Yeremia 1:4;10 4  Neno la Bwana lilinijia, kusema,
5  Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.



Na ule mstari wa 10 10  angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.



Mungu anamwambia Yeremia kabla sijakuumba nalikujua kwa maana nyingine Mungu anajaribu kumwambia Yeremia kwamba nalitambua kabisa nilichokua nafanya pindi nilipokuumba. Ukiendelea ule mstari wa kumi hapo juu Mungu anamwambia maana halisi yay eye kumuumba yaani kusudi lake ni nini hasa kwa kumwambia Yeremia kwamba amemuweka kua nabii wa mataifa hivyo kusudi kubwa la Yeremia kuwepo duniani yamegawanyika katika sehemu kuu mbili. Kusudi la kwanza Mungu anamwambia amemuweka kua nabii juu ya mataifa na kusudi la pili amewekwa kua juu ya mataifa na kazi yake halisi ni kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.



Lakini nikwambie siri kubwa iliyofichika hapa Mungu kabla hajamweka Yeremia kua nabii wake kwa mataifa kulishakua na kusudi ambalo Mungu alilokwisha kuliweka kabla ambalo aliliona kabisa halitaweza kufanikiwa pasipo kumuumba mtu ili alitimize.



Hivyo basi tambua kabisa kabla Mungu hajakuleta hapa duniani alikwisha kuumba kusudi lako ili uweze kuishi kwalo. Yaani wewe kuishi kwako sio kwa sababu ya kitu kingine ila unaishi duniani kutokana na kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako. Kwa maana nyingine ni kama hakuna kusudi hakuna mtu pia, maana Mungu hawezi kumuumba mtu bila kuweka kazi yake kabla ya kumuumba

KUWEPO KWAKO NI KWAAJILI YA KUSUDI AMBALO MUNGU ALILIUMBA HATA KABLA YAKO WEWE KUUMBWA; PASIPO KUSUDI HAKUNA MTU.
                                                     (No purpose no man)

Nipende pia kukwambia kua Mungu alimpa Yeremia uwezo hata kabla hajazaliwa ili aziangushe falme na huu uwezo si kwa ajili ya Yeremia ila ni kwaajili ya kusudi la Mungu. Jifunze hapa kuwa upo uwezo ulionao juu ya maisha yako si kwa sababu Mungu alikupa ili uwe wako ila ni kwaajili ya kusudi lake kwa maana Mungu hawezi kumpa mtu kusudi pasipo kumpa uwezo na mamlaka juu ya falme na mazingira anayoishi



TAMBUA NDANI YA KUSUDI LAKO UPO UWEZO NA MAMLAKA YA KUAMURU NA KUBADILISHA MAZINGIRA PINZANI JUU YA MAISHA YAKO NA HII SI KWA SABABU YA WEWE MWENYEWE ILA NI KWAAJILI YA KUSUDI LAKE MUNGU MWENYEWE.


Ngoja nikwambie kitu tambua kwamba mazingira unayoishi hata kabla hujazaliwa Mungu alishapanga uwepo hapo ili kufanikisha mpango wake mahali hapo.wengi wamekua wakiogopa mazingira wanayoishi kwa kuyaona ni magumu nipende tu kukwambia kwamba kukimbia mazingira unayoyaishi sasa sio njia ya wewe kufanikiwa  bali ni kukimbia kusudi na majukumu ambayo Mungu alikuumbia kwayo.


Mungu alifahamu kabisa mazingira ambayo atakuweka kwamba utakutana na falme na ngome za adui, anaelewa mapepo, vita ambavyo utapambana navyo, mapepo ambayo utambana nayo lakini nikwambie kabisa ni lazima ushinde iwapo utajifunza kuishi na kukaa ndani ya kusudi la Mungu haijalishi majaribu ni makali kiasi gani ila mwenye kusudi unao upako ndani yake hata kabla yay eye kuumbwa maana lilianza kwanza kusudi la Mungu ndani yake hata kabla yake, hivyo ndani yako ipo nguvu na uwezo ambao una uwezo wa kutosha kupambana na kila aina ya changamoto unazopitia.



Hebu anza kujiangalia sasa kwa upya tena katika maisha yako, vitu vinavyokuzunguka, vita pamoja na mapambano ya Ibilisi unayokumbana nayo kila siku hayataweza kukushinda ila utayashinda wewe, hayataweza kukumaliza bali utayamaliza wewe kwa sababu upo kwenye kusudi lake.




JINSI YA KUTAMBUA KUSUDI LAKO
pamoja na yote hayo niliyokufundisha apo awali hayataweza kukusaidia vizuri kama hadi sasa hujajua kusudi la Mungu juu ya maisha yako. Tunapokuja katika swala la kutambua kusudi lako sio kazi rahisi sana, wengi wetu wamekua wakifanya kila aina ya huduma lakini bado wanaona wanapwaya, wengine wamejaribu kufanya biashara lakini bado wanapwaya, kila wanachojaribu kukifanya katika maisha yao wanaona bado kuna kitu kinawadai  ambacho bado wanatakiwa kukifanya (kusudi) lakini pamoja na jitihada zao zote bado wameshindwa kujua ni nini hicho ambacho kimekosekana kwao


wengine wanaona kupata pesa pamoja na mafanikio ndio kujua kusudi lako kwenye maisha yako kitu ambacho si sahihi. Ngoja nikwambie pesa na mafanikio ni matokeo ya ujira baada ya mtu kufanya kazi Fulani aliyopewa. Hivyo huna haja ya kujisumbua sana juu ya hayo hebu anza sasa kutimiza kusudi lake kwanza ndani yako alafu utaona kama mungu hatalipia kusudi lake




KAMA UKITUMIKA KWA UAMINIFU JUU YA KUSUDI LA MUNGU KWAKO BASI KUA TAYARI KWA MAFANIKIO MAANA KUSUDI LA MUNGU KWAKO LINALIPA KWA YULE ALIYELITAMBUA NA KULIISHI.




Ili uweze kujua upo ndani ya kusudi la Mungu ni lazima kiwango cha Amani yako kiendane na kiwango cha kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako.
Ngoja nikwambie kwamba lipo jambo umewahi kulifikiria kulifanya au tayari umekwishalifanya na ukasikia Amani ndani ya moyo wako hata kama unaliona kama dogo tambua kua hilo ndilo kusudi la Mungu kwako, na uwe na uhakika si kwamba Mungu atakupa Amani peke yake bali atakupa pia uwezo, nguvu na mamlaka ya kuweza kupambana na mazingira unayoyapitia na hajalishi ni magumu kiasi gani lakini ni lazima utayashinda maana Mungu hakuumba kusudi ndani yako ili lishindwe.




KUSUDI LAKO LINATEGEMEANA SANA NA KIWANGO CHA AMANI UNAYOISIKIA MOYONI MWAKO NA KWA LOLOTE UNALOLIFANYA KWENYE MAISHA YAKO


Je unasikia Amani kiasi gani unapofanya ilo unalolifanya sasa? Kama kiwango cha Amani yako ni kidogo kwa unalolifanya sasa au hapo nyuma basi tambua bado hujatambua kusudi la Mungu ndani yako. Anza kubadilisha sasa ilo unalolifanya sasa ambalo linakunyima Amani na fanya kile ambacho unapata Amani moyoni mwako n ahata kama kwa mazingira ya nje watu wanaweza kuliona ni dogo we jitahidi kulifanya maana katika hilo Mungu ataanza kukubariki katika hilo.



Nipende tu kukwambia zipo hatua kuu mbili ili mwanadamu aweze kufikia makusudi ya Mungu kwenye maisha yake ambayo ni kama ifuatavyo;

1.      Ni lazima mwanadamu ampokee Yesu maishani mwake kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Ilo ndilo jambo kuu muhimu zaid katika maisha ya kila mwanadamu kwasababu unapompokea Yesu kwenye maisha yako huo ndio mwanzo wa wewe kutambua kusudi lako kwa maana Yesu ndiye aliyetuumba pamoja na Mungu baba (Mwanzo 1:26) sasa endapo tutarudi kwake kwa njia ya toba tutafungua mlango wa yeye kuingia ndani ya maisha yetu na kuanza kutufundisha nini kusudi lake katika maisha yetu. Kumbuka wewe hukujiumba wewe ila Mungu ndiye aliyekuumba na hakukuumba tu ila alikupa kazi na makusudi yaw ewe kuwepo ila kitu ambacho kimekupotezea kusudi lako ni dhambi unazofanya, hivyo basi hatua ya mwanzo ya wewe kutambua kusudi ni wewe kurudi kwa Mungu kwa njia ya toba ili Mungu aweze tena kukuonesha kusudi lako katika maisha yako ni lipi hasa.



UBARIKIWE SANA



Itaendelea….

Imeandaliwa na kuandikwa na;    James F. Mzava
Simu namba ;                     0756259621
Barua pepe;                        jamesmzava@gmail.com






14 comments:

AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1)

http://bit.ly/3JGDJ4d MWL. JAMES F. MZAVER Minister Truth 0762759621 jamesmzava@gmail.com              AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1) Ukuaji ha...