JIFUNZE
JINSI YA KUSAMEHE NA KUSAHAU
Na James F. Mzava
Na James F. Mzava
sehemu ya kwanza(1)
Bwana Yesu asifiwe sana. Nipende kukukaribisha tena katika
somo jipya la jinsi ya kusamehe na kusahau na nina Imani kua somo hili litakua
somo mojawapo la kubadilisha maisha yako kabisa. Ni wazi kua sisi kama binadamu
tunapotia katika mambo mbalimbali yapo yanayotufurahisha na yapo
yanayotuhuzunisha, na hata mara nyingine tunakua na uchungu mioyoni mwetu
kutokana na historia za nyuma ya maisha yetu ambayo tumeyapitia kwa kufanyiwa
mambo yasiopendeza katika maisha yetu na kutufanya tushindwe kusamehe na hata
tukisamehe bado kumbukumbu zinaendelea kutusumbua sana katika maisha yetu bila
kufutika lakini leo nipende kukutia moyo ufatane nami katika somo hili na Mungu
atakubariki
NINI
MAANA YA MSAMAHA
Ni wazi kabisa katika maisha haya yapo makwazo mengi sana ambayo
twapata, mara nyingine hata kwa watu wa karibu nasi wametumika kama mwiba
kutuchoma na kutujeruhi mioyo yetu kiasi cha kushindwa kuwasamehe kabisa. Na
huenda kwako pia kuna mtu ulishasema “huyu sitamsamehe kamwe” au umewahi kusema
“nimemsamehe lakini sitasahau” na mengineyo mengi
Hebu nikwambie kitu hapa je wajua kutosamehe kwako au
kutosahau makosa uliyotendewa kunaweza kukakufanya kua chini ya mtu huyo katika
moyo wako(kifungo). Basi
fuatana nami vizuri utanielewa na kwanza kabisa nianze kuelezea nini maana ya
msamaha.
Au kwa tafsiri nzuri ya neno msamaha kibiblia ni~ kuachilia kosa liende (to let go an offence)
Neno MSAMAHA, kwa maana
nyepesi na nzuri limebeba mambo makuu mawili ndani yake;
®
Kutolipiza kisasi japokuwa
unayo haki ya kulipiza kisasi.
® Ni tendo la imani na tena la
hiari kwa kuwa unayo sababu, uwezo, na haki ya kulipiza kisasi kutokana na yale
uliyo umizwa.
Nimeona nikupe tafsiri hizo kwanza japo kuna tafsiri nyingine
nyingi ila katika somo ningependa kwenda na tafsiri hizo huku tukisimamia neno
kuu la msingi wa somo katika Mathayo
Mathayo 6:14-15
14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa
mbinguni atawasamehe ninyi.
15 Bali
msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
MSAMAHA NI TENDO LA HIARI
Jambo ambalo
nataka ujifunze katika mistari hiyo apo juu tambua ya kwamba msamaha nit endo
la hiari. Yesu ameweka hiari kwa yeyote
yule kuhusiana na msamaha kama twahitaji kusamehewa na Baba ni budi kusamehe
ila kama hatuhitaji basi hatutasamehewa vilevile.
Na kama ni tendo la kihiari
lipo ndani ya uwezo wetu kuweza kulibeba au kuliacha. Na ni kwanini watu wengi wanashindwa kusamehe
ni kutokana na kushindwa kujua tendo la kihiari bali wamebaki wakishikilia
makosa waliotendewa.na ninaposemea neno hiari simaanishi jambo lingine lolote
Zaidi ya maamuzi, namaanisha msamaha ni jambo la kimaamuzi la kuacha kufatilia
makosa uliyotendewa na kuanza ukurasa mpya wa furaha
KUSAMEHE
KUNAHITAJI GHARAMA YA KUSAHAU MAANA KUTOSAHAU KOSA NI KIDUNGO KWAKO NA SIKU
ZOTE MFUNGWA HANA MAAMUZI YAKE MWENYEWE, HIVYO ILE DHAMBI ITAKUTUMIKISHA TU.
Lakini katika
hiari hii ni lazima uimbatanishe na Imani. Kwa nini nasema Imani ni kwasababu
pindi tunapokosewa mioyo yetu huumia na kujeruhika jambo linalotufanya
tushindwe kusamehe na kusahau ata kama ni kwa hiari lakini Biblia inatwambia ya
kwamba kazi mojawapo ya Imani ni saburi yaani taraja ambalo latusadia kuganga
mioyo yetu iliyoumizwa kutokana na makosa mbalimbali tuliyokosewa
Yakobo 1:2
2 mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.
Ndio
unapoingia katika jaribu lolote moja kati ya vitu shetani kutumia kutujaribu ni
kwa kutufanya sisi kushindwa kusamehe makosa. Ndio unapoweka Imani juu ya
jaribu unalopitia katika kuumizwa kwako na kutendewa uovu chukua hatua ya Imani
ambayo ni ya hiari kwa kuachilia makossa hayo ndani ya moyo wako na kukumbuka
msahama ambao Yesu alikusamehe makossa yako mengi pale msalabani na wewe
achilia kama vile yesu sema imekwisha juu ya maumivu haya na umwachie yeye
mwenye Imani yenye saburi kwa ajili ya kukupa tumaini jipya. Na ukifanya ivo
utaanza kuona badala ya kuhisi maumivu ya moyo juu ya mabaya uliyotendewa Mungu
ataachilia saburi iliyoko ndani ya Imani uliyonayo na kukupa furaha tupu juu ya
jambo unalopitia (Yakobo
1:1)
MSAMAHA NI HATUA INAYOANZWA NA MAOMBI
Ndio
unaweza ukashangaa lakini ndivyo ilivyo msahama
ni lazima uanzwe katika maombi kwa kuanza kuachilia nafsi yako katika kifungo
cha dhambi.
Kama
mwanzo nilivotangulia kusema kwamba unaposhindwa kumsamehe mkosaji wako
unajiweka katika kifungo cha uovu ambacho kama usipoweza kujua kitakugharimu
sana katika maisha yako, hivyo ni vyema wewe kama mkristo kuanza kujifungua
katika kifungo cha kutosamehe kwa njia ya maombi.
Pale
tu utakapoanza kuwaombea waliokukosea mema na kuanza kuwaombea Baraka za Mungu
ziwe kwako ndipo unapojiitoa katika kifungo cha dhambi ya kutosamehe na hapo
ndipo utakapoanza kuona hatua kubwa juu ya maisha yako.
(Mathayo 6:12-13, luka 17:3-4, Marko 11:25)
Endelea
kuwaombea mema na mafanikio maana pasipo kujua hilo katika ulimwengu war oho
maombi yako hubadilisha ule uchungu wako na kua furaha na kuwapa wakosaji wako
uchungu na kukosa Amani. Oooh haleluya!!
MSAHAMA
NI JAMBO LA WAZI
Ndio
katika msahama kibiblia ni tendo la wazi wala sio la siri kama wengi
wanavofanya. Ndio maana Yesu hajatukomboa sisi kwa siri bali aliwambwa
msalabani kwa ajili ya kuchukua makossa yetu na akatusamehe kabisa makossa
yetu. Na bible inatutaka sisi tufanye ivo ivo
Luka 17:1-4
Akawaambia wanafunzi wake, Makwazo hayana budi kuja,
lakini ole wake mtu yule ambaye yaja kwa sababu yake!
2 Ingemfaa zaidi
mtu huyo jiwe la kusagia lifungwe shingoni mwake, akatupwe baharini, kuliko kumkosesha
mmojawapo wa wadogo hawa.
3 Jilindeni;
kama ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu msamehe.
4 Na kama
akikukosa mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema,
Nimetubu, msamehe.
Ukiangalia
mstari wa tatu kuna neno linasema “mwonye” katika tafsiri nyingine ya biblia
linasema “mwambie” usikubali kukaa kimya katika makwazo yanayokuja juu yako
maana shetani nia yake ameyaandaa kwaajili ya kukuangusha. Hatua yako ya wewe
kumwambia mkosaji wako kinakupa kibali cha kuondokana na anguko la makwazo
yanayokujia. Na hii ni siri ambayo watu wengi wameshindwa kuijua badala yake
wamekua kimya na kubaki kusema “nimeshamsamehe, siwezi kumsahau yule mtu” na
mengineyo mengi, jambo ambalo ni kosa. Tunapaswa sisi kama wana wa Mungu kukiri
na kusema kwa wakosaji wetu yale waliotukosea ili msamaha uwepo wa Amani.
Unapoweza
kufanya ivo Mungu huleta Amani yake ndani yenu kwa kua Mungu wetu pekee ndiye
anayeweza kuufanya mwanzo mmbaya uwe mwema kwa mara nyingine
Wakolosai 3:12
mkichukuliana,
na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana
alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.
Tambua pia
unaposamehe ndio mwisho wa kosa acha kuendelea kufikia yaliyopita jifunze
kufanya Amani na ata kama yule aliyekukwaza ana jambo jema au amefanikiwa katika
jambo Fulani furahi pamoja naye ndio maana ya msamaha ni uwezo wa kuachialia
kosa liende na kukaribisha Amani katika moyo wako.
HATUA ZA MSAHAMA
1. Kubali maumivu na tafuta mlango wa kutokea
Mara nyingine
ni inakua vigumu kukubali kuwa umeumizwa na hii ni kutokana na sisi wenyewe
kujiaminisha kwamba hatujaumizwa na makosa tuliyotendewa jambo ambalo si sahihi
hata kidogo. (1 Wakorintho 10:13)
Tambua ya
kwamba hutaweza kutibu maumivu yako pasipo kukubali kwanza kwamba umeumizwa na
unahitaji msamaha ili uondokane na maumivu hayo.
Ndio hii itakusaidia pindi pale unapotaka
kusamehe jambo la kwanza ni kukubaliana na kile ulichotendewa.
Andiko hapo juu linasema kwamba Mungu yeye ni mwaminifu na
atafanya mlango wa kutokea tambua mtu wa Mungu hakuna lolote litakalokuja kwako
ata kama litakua kubwa kiasi gani tambua kabisa Mungu ameshatengeneza mlango
ili utoke kwa ushindi. Hebu sasa acha kuwalaumu watu na kuwachukia mtukuze
Mungu ata katika watesi wako uuone mkono wa Bwana.
2.
Jifunze
nafasi ya Yesu kwako na fanya kama yeye
Ndio pindi unapokua katika hatua ya mfadhaiko hebu anza
kutafakari msamaha wa Yesu jinsi alivokusamehe dhambi zako pasipo kujali maovu
yako. Nikwambie kitu utakapojikita na ukizama rohoni badaye utaona nguvu za
Mungu juu yako za kukutia nguvu na utashangaa kuona u mwepesi na mwenye moyo wa
msahama. Ipo nguvu kubwa katika kutafakari kifo na msamaha wa Yesu pale
msalabani.
Unapotafakari Zaidi utaona ivi kama Yesu angekataa kutusamehe
je tungekua na uzima tena? Hasha!! Tungeangamia wote hakika. Ila yeye
katusamehe bila kujali sisi tulivo na huo ndio msamaha wa kweli na wewe
tafakari kwanza kama ingelikua ni wewe ndio umekosea na ukagomewa msamaha je
ingelikuaje kwako?
Jifunze kwa Bwana na yeye atakuwezesha kusamehe wengine na
jifunze kutenda yale unayopenda kufanyiwa kama ulipenda msamaha wa Yesu
msalabani basi na wewe samehe ( Mathayo 7:12)
3.
Kumbuka kwamba Mungu alituagiza tusamehane
Mara nyingi katika biblia Yesu alipokua akifundisha juu ya
maombi jambo la kwanza kutuambia ni kusamehe kwanza wakosaji waliotukosea ili
maombi yetu yajibiwe
Marko 11;
25-26
25 Nanyi, kila
msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye
mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
26 Lakini kama
ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
4. Achilia maumivu na usahau
Pindi
utakapokua umeshatekeleza izo hatua apo juu huna budi tena kuendelea kukaa na
maumivu ya makosa yale yale bali achili yote kwa Mungu kwa Imani huku ukisubiri
taraja lako ambalo ndio saburi.
Epuka tabia ya
kuendelea kufanya mambo yatakayorudisha maumivu yako jitenge na vitu hivo maana
kuendelea kua mnyonge na mwenye hasira ndio kutafanya uumie Zaidi achilia mbali
maana Amani haiwezi kukaa mahali palipo na uchungu
5. Endelea kusamehe ata kama kumbukumbu zinarudi
Ndio nipende
kukwambia msamaha sio jambo jepesi ndio maana ni gumu sana kutendeka kama
ipasavyo wengi wa watumishi wa Mungu hawasamehi na hii ni mojawapo ya dhambi
mbaya ambayo itawapeleka watu kuzimu.( 1
Yohana 1:9)
Ndugu jifunze
kusamehe najua upo utofauti mkubwa kati ya akili yako na hisia zako, mara
nyingi hisia zitaamsha kumbukumbu zako juu ya maumivu uliyoyapata cha kufanya
hapo ni kuendelea kuomba rehema na masamaha na Mungu ni mwaminifu atafanya
mlango
6. Jifunze kuombea waliokukosea
Ndio hii
itakusaidia sana na hapa unaweza kujiuliza je kama niliokosana nao sina
mawasiliano nao tena au hata nikiwasiliana nao kutazuka ugomvi umeshindwa kujua
namna ya kuongea na mkosaji wako, usijali hiyo sio kazi yako kazi yako kubwa ni
kwenda mbele za Mungu na kuwaombea Amani ya Bwana huko walipo na Mungu
atawapatanisha kwa njia yake mwenyewe na kwa uaminifu wake kwenu. (Waefeso 4:31)
Itaendelea…
Imeandaliwa na kuandikwa na; JAMES F.MZAVA
Mawasiliano; 0762759621, 0653194411, 0625782324
Pia kwa kujifunza zaidi juu ya kusamehe fuata link hii https://wingulamashahidi.org/2018/11/20/samehe-kutoka-ndani-ya-moyo-wako/
ReplyDelete