TAMBUA
NAMNA YA KUSHINDA TAMAA ZA UJANA
Sehemu ya kwanza(1)
Bwana Yesu asifiwe sana.Nakukaribisha tena katika masomo yangu
ya kujengana katika Bwana.Na leo nimepewa kibali kingine tushirikiane katika
somo jingine la namna gani kijana ataweza kushinda tamaa na kuziweza.KARIBU
SANA
Nakumbuka kipindi Fulani tukiwa katika mkesha wa vijana
kanisani kwetu baada ya maombi na neno tulianza kipindi cha maswali na nakumbuka kati ya maswali
yaliokuwa yakisumbua sana vijana ni pamoja na hili ni kwa kiasi gani kijana
ataweza kushinda tamaa.Nakumbuka vijana walitoa maoni yao katika swali lakini
bado kulionekana wengine kutokua na uelewa wa kile kilichokuwa kinajibiwa
pale.Si hivyo tu nimepitia pia katika makanisa mbalimbali na nikakumbana na
aina ya maswali kama hayaKiufupi kila sehemu na kila eneo linalomuhusu kijana
pamekua na tatizo hili la namna gani wanaweza kushinda katika mtihani huo;usiwe
na hofu fuatana nami katika somo hili utapata kitu cha kukusaidia.
NINI
MAANA YA TAMAA
Kila siku katika luninga,filamu,magazeti na vijarida mbalimbali
kwa namna moja au nyingine vimekua vikiwavita vijana wengi katika tamaa
kutokana na picha chafu na filamu za ngono.Na hili huwajengea vijana wengi kuwa
na mawazo ya tamaa na kuwa kama mfumo wa maisha yao ya kila siku,jambo ambalo
linawafanya kua mfungwa katika tamaa.
Tamaa ni hisia,mihemko zinazotamaniwa na mwili.Na hii inaweza
ikawa tamaa ya ujuzi,ngono au ya nguvu/utawala.
Tambua ya kua tamaa ni roho;ninaposema roho naamanisha kuwa ni
nguvu(force) inayoweza kukuchochea kufanya au kutenda jambo kinyume na matakwa
yako binafsi.Mtume Paulo analielezea hili vizuri kwenye kitabu cha (Warumi 7:17-19)
17 Kwa maana
najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa
kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
18 Kwa maana lile
jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo.
19 Basi kama lile
nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile
dhambi ikaayo ndani yangu.
Kama nilivosema kua roho yeyote humfanya mtu kutenda yale
inayoyataka kupitia nafsi ya mtu ambayo ndio inayoweza kufanya maamuzi ya
kutenda.Sasa tunaposema tamaa ni roho ni roho inayochochea kwa kupenda au kwa
kutokupenda kwa kutenda au kufanya
tamaa.
Mstari wa 17 Paulo anasema maana ndani ya mwili wangu halikai
neno jema (body principle) Tafsiri nyingine inasema ni ile roho ikaayo ndani
yangu.ndiyo inayomfanya aweze kutenda asiyopenda.
Kwa undani andiko hili Paulo alikuwa akiongelea mwili wake
mwenyewe kua hawezi kuumiliki kwa kile kilichopo ndani yake hakimpelekei
kushinda mwili wake mwenyewe japo alikuwa Mtume mkubwa lakini bado lilikua
tatizo kwake.
Ngoja nikwambie kitu njia bora ya wewe kuweza kushinda tamaa
ni jinsi gani wewe mwenyewe umewekeza nini ndani yako mwenyewe;unaweza ukawa
umeokoka lakini bado tatizo liko palepale tatizo si wokovu ulionao tatizo ni
ndani unaongozwa na aina gani ya roho??
Ngoja nikwambie japokua umeokoka na inawezekana Mungu
anakutumia vizuri lakini tatizo linakuja kwenye tamaa zinakushinda kabisa namna
ya kuziweza.Jua ya kuwa miili yetu inaongozwa na kile kilichomo ndani kama ni
kibaya hata kama umeokoka bado utakua na tatizo lile lile.Hapa nazungumzia roho
ya asilia.Ambayo hii huwa kwa kila mwanadamu huwa na tamaa lakini je unaroho ya
aina gani ili iweze kuishinda
Roho ndio inayochochea mtu kufanya yale mtu anayotaka na
asiyotaka kwa kufanyia kazi kwenye nafsi yako na baadaye mwili unafanya
kuitikia.
Mathayo
5:27-28 27 Mmesikia
kwamba imenenwa, Usizini;
28 lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye
mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
Andiko apo juu linatwambia amtazamaye mwanamke kwa kumtamani
amekwisha kuzini naye moyoni mwake.Hebu jiulize kutokana nahuo mstari ni mara
ngapi tumekua tukizidi hata pasipo sisi kujua?
Ila maana kubwa sana hapo ni neno ``amekwisha
kuzini naye moyoni mwake`` kama ulinielewa hapo juu nilisema kua tamaa
ni roho itendayo kazi ndani ya moyo wa mwanadamu kwa kusisimua baadhi ya viungo
kwenye mwili wa mwanadamu.
Ngoja nikuoneshe jinsi nilivojifunza andiko hili na kunisaidia
katika hali ya tamaa;Pindi nionapo picha chafu,majarida machafu au mwanamke
mwenye kuvaa kimatamanio,kwa haraka nimeshafahamu image imeshaingia ndani ya
moyo wangu ninachokifanya ni kuacha kuangalia na kuanzisha jambo jipya ndani;
linaloweza kunitoa kimawazo katika mtego huo kwa kuangalia ndani yangu;hapo pia
hutegemea sana aina ya mazingira uliyojijengea hasa kwa Mungu
Asilimia kubwa ya vijana wanaoanguka katika tamaa ni wale
wanaoathiriwa na mazingira wanayoishi;hivyo huwajengea mioyo yao kuwa katika
hali iyo iyo ambayo ni ngumu pia kukomboka.
KUTOELEWA
ASILI YA TAMAA
Jinsi tamaa inavyofanya kazi imekua haieleweki kwa watu.Kwa
maana tamaa ya mtu mmoja ni tofauti sana na ya mwingine.Nipende tu kusema kua
tamaa ni Zaidi ya mihemuko ya mwili kwa sababu neno tamaa ni hali inayojumuisha
mihemuko ya mwili pamoja na moyo ikitendewa kazi na roho.
Tamaa
ni kupata(feeling) raha ya tendo la ndoa (sex gratification) kwa yeyote
isipokuwa mke au mme wako wa ndoa;Ndio maana Yesu alisema ``kwa kumtamani
amekwisha kuzini …``.
Mfano halisi wa hichi ninachokisema hapa ni pale yule mwanamke
aliyekua akitaka kuuwawa kwa kupigwa mawe kwa sababu ya uzinzi ila Yesu
akachora chini kwamba yeyote ambaye anajiona hana dhambi awe wa kwanza kumtupia
mawe uyu.Ivi unajua maana halisi ya habari ile? Watu wengi hasa makanisani
tumekua wakwanza kuwahukumu wengine hasa wale waangukao kwenye tamaa huku wengi
wetu bado tatizo ilo litusumbua. itaendelea...
mawasiliano; 0762759621, 0653194411
Imeandaliwa na JAMES F. MNZAVA
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDelete