ISHINDE
ROHO YA UCHUNGU
Bwana Yesu asifiwe sana.Kuna kipindi mama mmoja alinifuata na
kuniambia kwa muda wa wiki nzima amekuwa akisumbuliwa sana na uchungu hasa pale
alipokuwa akiwaza familia yake na umekuwa ukimzidia pindi anapomuwaza mme
wake.Jambo ambalo lilikua likimsumbua sana hadi kumfanya kulia wakati
mwingine.Si hivyo tu nimkutana na wapendwa mbalimbali pamoja na wengine ambao
sio wapendwa wakisumbuliwa sana na tatizo hili la uchungu.Ila leo Bwana amenipa
kibali niweze kusema na wewe kuhusu tatizo hili.Inawezekana pia wewe umekuwa
mhanga wa tatizo hili la uchungu;fatana name hadi mwisho wa ujumbe huu naimani
hautakuwa kama ulivo tena ujumbe huu utakubadilisha maisha yako
kabisa.
NINI
MAANA YA UCHUNGU
Neno uchungu ni masikitiko ya ndani,Zaidi ya
kupoteza;huzuni.Hasa ya ndani ya moyo masononeko ambayo mara nyingi hayana
mwisho wa haraka na wa mapema.Hii haiwi ndogo,lakini mara nyingine inahusiana
kumpoteza yule uliyempenda.Inahusianisha hisia za kuwapoteza vitu,watu na
thamani.Watu wengi katika uchunguzi nilioufanya wamekuwa na uchungu hasa kwenye
kuvunjika(break) kwa mahusiano,kupoteza kazi,ujana,kupoteza haki na mengineyo
mengi.
Nipende kukwambia kua uchungu ni moja ya janga kubwa sana
linalowasumbua watu wengi katika dunia.lakini ukijua namna ya kuachilia hali
iyo haitakutesa tena maishani
Mtu yeyote yule aliyeishi katika kimo tofauti na miaka tofauti
katika maisha haya utajua kua uchungu ni janga,roho na hali isiyoepukika;ni
sehemu mojawapo katika maisha ya mwanadamu.Hivyo ni Dhahiri kwamba hatuwezi
kujiepusha na uchungu bali tunaweza kujiepusha na matokeo yatokanayo na
uchungu..
Kikawada watu wengi waingiapo katika hali ya uchungu hupitia
katika hatua hizi zifuatazo;
·
Mshtuko na ganzi na mawazo yasiyo halisi
·
Kutoa hisia za huzuni,ikiwemo kulia
·
Mfadhaiko na ukiwa(loneliness)
·
Hofu ya kuchanganyikiwa(panic)
·
Mawazo ya kujiona una hatia
·
Hasira na kuchukia
·
Mpambano katika kuacha uchungu na kurudi katika
hali ya kawaida(normal life)
·
Taratibu furaha inarejea
JE
WAJUA YA KUWA UCHUNGU NI ROHO
Tafsiri ndogo tu ya neno roho ni pumzi,/ni nguvu(force)
inayochochea au inayoshawishi matakwa ya mtu.Sasa tukirudi kwenye uchungu
tunapata maana halisi juu ya roho ya uchungu kua ni roho ambayo inakuchochea au
kukushawishi ili kuweza kufanya matakwa yake kwa kupenda kwako au kwa kutopenda
kwako.
Kati ya vitu vya kwanza kabisa ambavyo nimewahi kuhudumu na
kupata uzoefu nimetambua ya kuwa uchungu huwatokea watu karibia wote lakini
ajabu huwa na tofauti kutokana na mtu na mtu(spiritual)
Hii ni ya muhimu sana.Moja ya njama kubwa ya udanganyifu
ambayo shetani huitumia katika kuwadanganya watu ni kuwafanya wajione hali
wanazipitia hakuna anayejua ila wewe mwenyewe tu,kitu ambacho ni cha ajabu sana
na uongo wa Dhahiri ila ni mbinu mojawapo ya adui.Hata kumekua na nyimbo kabisa
watu huimba kuwa ``Hakuna ajuaye taabu nilizonazo,hakuna ajuaye huzuni zangu``
ilo sio kweli unajidanganywa mwenyewe.(spiritual work).
Maandiko yameweka haya wazi sana kua hakuna jaribu
linalotupata sisi isipokuwa kawaida za wanadamu;(1Wakorintho 10:13).
KUMBUKA
KUA HALI YEYOTE ILE UNAYOIPITIA KATIKA MAISHA YAKO SI KWAMBA NA WENGINE
WALISHAPITIA, BALI TUNAPITIA SISI SOTE PIA.
Hii ni ya muhimu sana kuelewa.Kama shetani atakufanya uelewe
kuwa hali unayoipitia ni ya kipekee hapo moja kwa moja utakuwa umejitenga na
msaada wowote ambao utakuwa upo halali kwa ajili yako
Njia bora naya muhimu ya kuondokana natatizo la uchungu unahitaji
watu.kujihurumia,na kila majeraha ya matokeo ya uchungu yanaweza kufanyiwa kazi
katika hali ya jeuri.Naamanisha unapoweka furaha yako na kuionesha kwa wengine
inapelekea matokeo hasi ya uchungu kupotea na kuisha kabisa.Pia kumbuka kua
shetani hupendelea kumuangusha mtu mbele ya wenzake na katika jamii ya watu ili
kukuaibisha na kuingiza uchungu na kukufanya kua mateka rahis sana kwake.
Mtume Petro aliliweka wazi sana hili (1 Petro 5:8-9) Petro alisema kua pamoja na mateso na mapito
mbalimbali tunayopitia yaletayo uchungu ndani ya mioyo tujue ya kuwa ipo faraja
maana wapo watu pia wanaopitia mates hay ohayo kama sisi.Ila kwa upande wa
shetani anakwambia matatizo hayo ni yakow ala wengine hawajateseka kama
wewe.kimbia uongo huo wa shetani.
Kijana mmoja alinijia akaniambia kua amekua katika mahusiano
ya mapenzi katika vipindi tofauti tofauti lakini katika vipindi vyote ivo hakua
na mahusiano ya kudumu maana kila msichana aliyekuwa naye amekua akimkimbia na
kua na mahusiano na wanaume wengine.Lakini wakati akiendelea kunielezea shida
yake niligundua alikua na uchungu sana na alikua akilalamika kua kwanini yeye
mambo hayo ya kusaitiwa na wapenzi wake limekua likimtokea.
MADHARA YATOKANAYO NA UCHUNGU
·
HASIRA. Mtu mwenye hali
ya kuwa na uchungu kwa muda mrefu hukumbwa na hali ya kuwa na hasira mara kwa
mara.Na hii hutokana na pale mtu anapokata tamaa kabisa katika hali
aliyomsababishia uchungu na kuanza kufanya mambo kwa pupa na hasira pia
·
MSONGO WA MAWAZO (stress) Unapokuwa katika hali hii mara nyingi wengi wa
watu hukumbwa na msongo wa mawazo na tatizo hapa ni wengi wetu hatujui kuwa
uchungu ni jambo la muda tu
·
KUJIKINAI NA KUJIKATAA
·
KUJIDHARAU
·
MAGONJWA
·
HOFU YA MARA KWA MARA
·
CHUKI
·
NA MENGINEYO MENGI
Nataka ujifunze kitu hapa karibia asilimia 90% ya watu wenye matatizo
mbalimbali wameyafanya yao kwa uongo ndani ya mioyo yao ambao shetani amekua
akiwachochea siku hadi siku jambo ambalo silo.
Nilimpa ushuhuda mwingine wa kijana ambae kwa sasa ameshaoa
ambaye alishapitia hali kama yake na Zaidi yake kabisa na jinsi alivoshinda.Na
lengo hasa apa ni kutaka kufahamisha kua kila hatua unayopitia si tu na wengine
wanapitia bali na sisi sote tunapitia ila katika hali tofauti.baada ya kuongea
na kijana yule na kumuaminisha kua si yeye tu bali wapo walioshinda akapatwa na
furaha ya kuendela Zaidi hadi sasa kijana yule anazidi kuendelea katika
Bwana.Haleluyah
Mtu yeyote ambaye hukataa kupokea faraja na kutiwa moyo juu ya
kufaulu na kushinda kwa wengine ni watu ambao wanawakati mgumu sana pia kuona
ushindi juu ya maisha yao wenyewe.
JIFUNZE
KWA MTUME PAULO
Kitu kingine cha kukumbuka hasa unapopatwa na uchungu tambua
uchungu ni hali yam da/kitambo si janga la kudumu hata kifo ni kutengana kwa
muda tu ipo siku tutakuwa pamoja pia na wale waliotutangulia. (1Thesalonike 4:13-18)
Hapo mtume Paulo anawaambia kanisa la Thessalonike kua pamoja
na kua kifo huleta uchungu kwa watu lakini imewapasa kutambua kwa waamini kua
kifo ni kutengana kwa mda tu (long separation).Ila baadae kuna kuonana tena na
anamalizia kusema farijianeni na maneno hayo.Kumbuka hili pia litaleta faraja.
Mtume Paulo ni mmoja wa mitume waliopata mateso ya uchungu
mwingi kuliko mwingine yeyote yule.Japo mateso yake hayakuhusisha mateso ya
mwili tu lakini pia maumivu ya ndani(emotional pain) ambapo wengi wetu hatuwezi
hata kuwaza kuhusu ilo.Lakini bado anasema dhiki yetu nyepesi …(2Wakorintho 4:17)
Si kwamba dhiki ya Paulo ilikuwa nyepesi kama tunavodhania ila
alichukua mateso yale pamoja na uchungu katika mtazamo mwingine kabisa.Watu
wengi wenye matatizo hasa ya uchungu huchukulia kama tatizo kubwa sana kwenye
maisha yao kitu ambacho sio kizuri.Cha muhimu kutambua apa ni kuwa uchungu huwa
wa muda mfupi ndio maana Paulo anaiita ni dhiki ya kitambo kidogo tu
Tukirudi katika ule mpangilio wa uchungu hapo juu tunaona
kwamba watu wengi wamekuwa wakipambana sana katika ile hatua ya kutafuta kuacha
uchungu na kurudi katika hali zao za kawaida.Ngoja nikupe mfano wa kukusaidia
ukisoma kitabu cha Mwanzo 23 1-4.H apa tunaona tukio lililompata baba Ibrahimu
la uchungu ambapo mke wake sara alifariki jambo ambalo huleta uchungu kwa
yeyote yule.Lakini hebu tuangalie katika mstari wa 3 Ibrahim alifanya nini
baada ya mambo hayo kumpata;
Mwanzo 23:1-3 1 Basi umri wake Sara
ulikuwa miaka mia na
ishirini umri
wake Sara.
2 Sara akafa katika Kiriath-arba, ndio Hebroni, katika
nchi ya Kanaani. Ibrahimu akaja kumlilia Sara na kumwombolezea.
3 Akaondoka Ibrahimu kutoka mbele ya maiti wake, akasema
na wazawa wa Hethi, akinena,
Alichokifanya
hapa Biblia inasema aliondoka mbele ya maiti wake.Alishaachilia kuwa tayari
jambo limeshatokea na kuamka ili kutafuta njia ya kutokea.
na saba ndio
Naamini watu
wengi hasa wakristo wamekuwa wakijifunga katika kifungo cha uchungu kwa
kutokujua kwamba uchungu ni hali na hatua inayotupata sisi sote,na tatizo kubwa
ni wengi wa wakristo kutokujua kanuni bora za kushinda uchungu.Japo hatuwezi
kuwa na aina moja ya uchungu maana watu hutofautiana lakini Mungu alitengeneza
kitu kinaitwa uponyaji.Uponyaji ni hatua inayochukua mda kidogo kidogo sio kama
muujiza jambo ambalo ni la haraka kutokea.
JINSI YA KUSHINDA UCHUNGU
Waebrania 12:14 14 mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu;
shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua, na watu
wengi wakatiwa unajisi kwa hilo.
Katika
Biblia kuna dhambi ambazo ni za nafsi hizi kufanyika ndani ya mioyo ya watu
pasipo kutambuliwa na wengine dhambi izo ni kama uchungu,hasira,tamaa chuki izi
zote hazina vitendo pindi zifanyikapo ila zina mdhara makubwa hata kwa wengine
ndio maana mtume Paulo aliwaambiwa Waebrania kua lisije kuchipuka shina la
uchungu na wengine wakatiwa unajisi kwalo.
Kwanza tambua kua uchungu ni dhambi ya nafsi ambao ukiruhusu ukae nao
moja kwa moja huwaathiri wengine hata wewe pasipo kujua.
1.
JIFUNZE
KUSAMEHE.Kusamehe
sio kujifanya kuwa mambo yako sawa kumbe sio.Kwa tafsiri nzuri ya neno MSAMAHA- ni kitendo
cha kudhili(surrendering) matamanio yetu ya kulipiza
kisasi.
Ile hali ya
kulipiza kisasi kwa wale waliokufanya uumie na kuwa na uchungu iondoe kwa
kuruhusu msamaha ndani yako.Kumbuka msamaha ndicho chanzo cha uponyaji wako.
2.
WEKA MALENGO.Kusamehe kunaachilia nguvu
unayoihitaji kuponya jeraha lakola uchungu.Kama utajiwekea maleongo na mipango
kwamba ni kwa kiasi gani tatizo la uchungu umelipa na sababu zake ni tiba tosha
ya kuponya jeraha lako.Na pia kujiepusha na mitego au visababishi vya uchungu
mwingine kwa kubadilisha aina pia ya maisha unayoishi,kubadilisha marafiki na
watu ulionao.
3.
ACHA KUWAZA NA
KURUDIA RUDIA.Pindi
ukishaondokana na tatizo la uchungu panga mikakati mingine na achilia kabisa
kwani kuwaza tena namna ilivyotokea kunasababisha kurudi tena kwenye tatizo
4.
OMBA NEEMA YA
MUNGU.Inaweza
ikawa ni vigumu sana kuponya majeraha yote yatokanayo na uchungu maana mengine
huwa ni magumu Zaidi yanahitaji neema ya Mungu Zaidi.Jifunze kua mtu wa maombi
ya mara kwa mara maana tabia huondolewa pole pole hasa kama ni muombaji mzuri.
5.
TAFUTA
MSAADA/USHAURI KWA WENGINE.Si mambo yote yanawezekana kutatuliwa na sisi wenyewe tunahitaji
msaada kwa wengine hasa kwa wale waliofanikiwa Zaidi yetu kwa kuwaomba ushauri
kwamba wamewezaje kushinda na kufaulu katika matatizo kama hayo
AMEN UBARIKIWE
Kwa mawasiliano zaidi; 0762759621, 0625782324
Imeandaliwa na kuandikwa na; JAMES F. MNZAVA
Ubarikiwekwa somo zuri
ReplyDelete