KUPAMBANA
NA ROHO YA HOFU NA KUISHINDA
Bwana Yesu asifiwe sana.Nakukaribisha tena katika mfululizo wa
masomo yangu.Leo tena Bwana amenipa nafasi ya kuweza kukushirikisha maneno yake
pamoja na mafundisho katika somo la kupambana na roho ya hofu na
kuishinda.Karibu sana.
NINI
MAANA YA HOFU
Tafsiri rahisi ya neno hofu ni woga,utisho,kutokuridhishwa(uneasiness) au
mashaka.Lakini kibiblia neno hofu ni Zaidi ya hisia ni roho(spirit)
inayotenda kazi.
2
Timotheo 1:7 7 Basi
usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja
nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu;
Mwamini anapotumiwa na kuwa chini ya Roho mtakatifu kwa ajili
ya kazi maalumu tunaita upako;Upako huu wa Roho mtakatifu unamuwezesha mtu kuwa
na moyo na kuwa jasiri katika kila tendo atendalo;Si hivyo tu bali kuwezeshwa
huku kwa Roho mtakatifu kunamsaidia pia mtu kuweza kufanya mambo mengine ambayo
hapo awali kwa nguvu au kwa hali ya kawaida asingeweza kufanya.
Kutokana na andiko hilo hapo juu tunajifunza kuwepo kwa roho
ya hofu kunaweza kuleta au kuathiri mambo ndani yetu;kwa kugeuza kile cha Mungu
ndani na kukifanya kuwa hasi ndani. Badala ya upako wa kuwezeshwa na Roho
Mtakatifu tunapata upako mwingine wa adui (a
negative destructive anointing)
·
Badala ya Roho Mtakatifu kukuwezesha kuwa
jasiri,roho ya hofu inakupooza
·
Badala ya kupokea hekima,roho ya hofu inakupa
kufanya maamuzi dhaifu.
·
Badala ya upako halisi wa roho Mtakatifu uletao
Baraka,roho ya hofu inakupa roho ya laana.
KANUNI
ZA KUTAWALA HOFU
Kulingana na Warumi
12:1,2 Kulingana na andiko ilo hapo juu tunaona hapa duniani zipo roho
zinazotawala kimfumo katika maisha yetu hapa duniani.Mfumo wa kwanza
unatawaliwa na roho ya uzima,na mfumo mwingine unatawaliwa na roho ya mauti.
Pia katika mistari iyo tunaona pia misingi miwili ya kiutawala
ambayo kila mkristo anatakiwa kuyatawala.
1)
Moja ni
sheria ya uzima katika Kristo Yesu
2)
Pili ni
sharia ya dhambi na mauti
Kila
mwanadamu anayeishi katika dunia hii ni lazima yupo chini ya mfumo war oho
mojawapo hapo.N si vinginevyo.Lakini kitu cha ajabu tunaona japokuwa mtu
anaweza kuzaliwa mara ya pili au kuokoka haimaanishi maisha yake yatakuwa
kwenye mfumo ulio sahihi.
SHERIA Ni
kanuni zilizoanzishwa na zinazotarajiwa kufanya kazi iyo iyo katika nyakati
zote.Kwa mfano sheria ya wizi itafanya kazi popote pale haijalishi mwizi ameiba
kwa mwenye kuweka iyo sheria au sehemu nyingine bado sheria hubaki palepale.
Hivyo hivyo kadhalika pia katika sheria ya roho izo hapo
juu.Kama unaishi chini ya sheria ya roho ya dhambi na mauti huwezi kuepuka
matokeo ya dhambi katika sheria yake na mauti pia.
Katika roho hizi zote huwa na matunda yake ambayo mimi huyaita
kama matokeo yake endapo utakuwa unaongozwa na uzima au dhambi na mauti.
·
Unapoongozwa na roho ya uzima unapata matokeo ya
Amani,furaha,utulivu,ujasiri,hekima maarifa,uhakika wa uzima hata baada ya kufa
na mengineyo mengi
·
Unapoongozwa na roho ya dhambi na mauti unapata
matokeo ya hofu,mashaka,wizi,tamaa,uasherati,ibada ya sanamu,uchoyo,wivu,hasira
na mengine mengi yafananayo na hayo
Ngoja nikupe habari ya kisa kilichowapata wanafunzi wa Yesu
ili uzidi kuelewa kitu ninachokiandika hapa
Mathayo 8:25-26
25 Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha,
wakisema, Bwana, tuokoe, tunaangamia.
26 Akawaambia, Mbona mmekuwa waoga,
enyi wa imani haba? Mara akaondoka, akazikemea pepo na bahari; kukawa shwari
kuu.
Angalia neno la kwanza ambalo Yesu amelisema hapo KWA NINI
MNAOGOPA? Ninyi wa Imani haba.Alilinganisha hofu yao kama watu waliopungukiwa
Imani.Luka na Marko wameelezea kwa aina ya tofauti kidogo ambazo zote zinalenga
Imani haba waliokua nayo (Luka
8:25, Marko 4:40)
Katika vitabu
vyote hizi Yesu analenga kitu kimoja kikubwa;anauliza kuwa ikowapi Imani yenu?
Akilenga kabisa hawa watu wapo chini ya roho ya dhambi na mauti,unapoongozwa na
roho hii ni lazima uwe na hofu na kushindwa kufanya maamuzi hasa wakati wa
tatizo.
Wanafunzi wa Yesu walikuwa wakipiga kelele kwa hofu ikiashiria walikua na
woga,tatizo hapa si ile dhoruba bali roho zilizokuwemo ndani yao ziliwajengea
hofu katika tatizo.
KAMA UNA IMANI HUWEZI KUOGOPA,UNAOGOPA KWA SABABU YA IMANI
HABA ULIYONAYO
Ngoja nikwambie uwiano huu wa roho pamoja na matunda yake
hufanya kazi pamoja na huwa haviachani.Woga ni tunda la roho wa dhambi na mauti
na Imani ni tunda la Roho wa uzima,kwa kila tendo huendana na roho yake.
Huu uwiano unaenda ndani sana kuliko unavofikiria kiini cha
neno Bwana pale lililenga kiwango cha Imani yao iliyosababisha hofu ndani
yao.Ngoja nikuoneshe kitu cha ndani Zaidi karika Imani
Warumi 10:17 16 Basi imani, chanzo chake ni
kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo.
17 Lakini nasema, Je! Wao
hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao
hata miisho ya ulimwengu.
Kumbuka kipaumbele cha Yesu hapa kwa wanafunzi wake kilikua ni
kiwango cha Imani ila kwa upande mwingine kipaumbele cha shetani ni kiwango cha
hofu uliyonayo.Ni mambo yanayoenda sambamba lakini hayafanani
Kwa mfano Bwana amekupa karama nzuri ya kumuimbia lakini
Lakini shetani anakuja na kukwambia na wewe hujui kuimba na kukupa sababu
lukuki kwamba huwezi na wewe na baada ya muda unaanza kuipokea ile hali
unafadhaika hata ikitokea unahitajika kumwimbia Bwana mbele za watu unaanza
kuogopa kwa mawazo kua huwezi na baada ya muda huduma inakufa kabisa.Tatizo
hapa si jingine ni shetani kapandikiza roho ya woga.
WOGA
UNAMPA SHETANI NAFASI YA KUFANYA KAZI ZAKE NDANI YAKO KWA UHURU WA KUKUTAWALA
NA KUKUFANYIA ANACHOTAKA.
Hofu ilifanya mawimbi ya bahari kuingia chomboni na kuwafanya
wanafunzi waanze kupiga kelele wasijue wafanye nini;pindi shetani anapoingiza
roho ya hofu kwako unanyima uwezo wako wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi.
Angalia Yesu alipoamka alianza kuwaambia ikowapi Imani yenu
baada ya kuwakuta wanapiga kelele kama watu wasiokuwa na maamuzi ya kufanya,kwa
namna nyingine Yesu anawauliza kwa nini hili limetokea?kwa nini maji yameingia
chomboni? Kwanini mmeruhusu woga woga wenu katika hili tatizo? Kwa nini
msichukue Imani kwa kukemea dhoruba kwa njia ya Imani.
Hakuna
njia yeyote ambayo shetani ataingia na kuharibu vitu katika maisha yako pasipo
wewe mwenyewe kumfungulia mlango
Unaweza
kujiuliza ni kwa namna gani umempa shetani nafasi ya kuongia ndani yako;ni kwa
kumpa nafasi ya kuendelea kusikiliza kile anachokwambia pasipo kuyakataa na
kuyapuuzia.Unapoendelea kumsikiliza pasipo unaendelea kufungua mlango way eye
kuingia ndani na kuleta hofu.
Ngoja
nikwambie kitu mambo ya Mungu ni halisi na shetani huyachukua na kuyapindua na
kuyafanya yake kama neno la Mungu linasema Imani chanzo chake ni kusikia na
kusikia huja kwa neno la Mungu;Vivyo hivyo woga chanzo chake ni kusikia na
kusikia huja kwa neno la ibilisi.
Linda
milango yako katika nafsi yako masikio yako na machi yako maana ndizo shetani
hushughulika nayo sana katika kukupa habari za hofu
VUNJA
VIFUNGO VYA HOFU
Tambua kuwa hofu huleta vifungo.Pindi roho ya hofu inapoweka
mizizi moyoni mwako unakuwa mtumwa na mfungwa wa hofu.Hii ni kanuni halisi
ambayo inaonekana kabisa kwenye kitabu cha Waebrania
Waebrania 2:14-15 14 awaache huru wale ambao kwamba maisha yao
yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa.
15 Maana ni hakika, hatwai asili ya
malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu.
Hofu ya mauti kama tulivoelezwa hapo juu inamfanya mtu kuwa
katika kifungo cha hofu na dhambi,kama ilivyo katika sheria zile za dhambi na
mauti .Ila Biblia inatwambia hapo hapo kuwa Kristo alilipa gharama kwa ajili ya
kuwakomboa wote wenye roho ya hofu.Yesu alisulibiwa kwa ajili yako kuweza
kulipa gharama ya kuwaweka huru wale wote waliofungwa na hofu.
Imani inaleta uhuru,ndio maana shetani anafanya kazi sana ili
kuweza kuwafanya wakristo wawe katika woga ili kuwaondoa kwenye Imani.Kwa sisi
wakristo kibiblia ni makossa makubwa kuwa katika hali ya hofu
(Warumi14:23) Biblia inatwambia
hatukupokea roho ya hofu;kumbuka kuwa hofu ni kupe katika roho yako anayefyonza
kiwango cha Imani yako ili uangamie.
FANYA
MAAMUZI YA KUPAMBANA NA HOFU
Bila kufanya maamuzi ya kupambana na roho ya hofu katika
maisha yako hutaweza kuishinda hii roho ndani yako,na si tu maamuzi bali
maamuzi yaliyoimara.
Mambo yote ambayo shetani hutuletea ni yale yale ya
kutukatisha tamaa na kutufanya tujione hatuwezi na kutisha ili tuingie na
woga,ila mkristo aliyeokoka na kumfahamu Mungu sawasawa hawezi kutishika na
ushawishi huo wa shetani.(Isaya 41:10)
Isaya
43:5 5 Usiogope;
maana mimi ni pamoja nawe; nitaleta wazao wako toka mashariki, nitakukusanya
toka magharibi;
Maandiko yote hayo yanasisitiza juu ya kitu kimoja ya kuwa
tusiwe na hofu kwa maana Bwana yupo pamoja nasi.Unadhani ni kitu gani
kilichompa Daudi ujasiri wa kukabiliana na Goliath? Embu tuangalie kile ambacho
alikisema
1 Samweli
17:26 26 Daudi
akaongea na watu waliosimama karibu, akisema, Je! Atafanyiwaje yeye atakayemwua
Mfilisti huyo, na kuwaondolea Israeli aibu hii? Maana Mfilisti huyu
asiyetahiriwa ni nani hata awatukane majeshi ya Mungu aliye hai?
Kutahiriwa lilikua ni agano lililowekwa na Mungu kwa Ibrahimu
na katika vizazi vyake vyote kitu ambacho Daudi alimjia nacho Goliath na
kumwambia wewe mfilisti usiyetahiriwa yaani wewe usiye na agano na Mungu huwezi
kunitisha wala kuniogopesha kwani Mungu aliyehai yupo pamoja nami.Haleluyah
Na huo ndio
mtazamo ambao Mungu anataka kila mwamini awe nao,haijalishi ni mtu au tatizo la
aina gani limesimama mbele yako fanya kama Daudi alivyofanya kwa kumwendea
Goliath kwa ujasiri pasipo kujali nguvu alizokuwa nazo.(Zaburi 91:1-2)
·
Kumbuka
kufanya maombi hasa ya kupanda mdaraja ya Imani kwa
jinsi tulivyotangulia kuona hapo mbele kuwa hofu hushambulia ujasiri wetu na
Imani yetu na kutufanya tuingiwe na hofu na mashaka.
·
Hakikisha
humpi Shetani nafasi ya kupenyeza maneno ya ushawishi wake katika
maisha yako kwani kwa njia hiyo hofu na mashaka hufanya kazi ndani yake.Mfano
Ayubu baada ya matatizo na majanga yote kumpata alianza kuingiwa na hofu na
mashaka(Ayubu 3:25)
·
Kuwa mtu
wa msimamo Kati ya watu ambao shetani huwaogopa sana ni watu wenye
msimamo na maamuzi yaliyodhabiti katika kutenda wengi wa watu wenye hofu na
mashaka ni watu wasiokuwa na msimamo katika maisha yao
ONDOA ROHO YA HOFU
Hakuna nafasi ya hofu katika maisha ya mtu aliyeokoka.roho ya hofu
itakuibia mambo yote yaliyo mazuri na ya maana kwako,itaiba Amani na furaha
ndani yako na kuitesa nafsi yako.
Lakini si hivyo tu ila hofu pia hukujengea mazingira ya
kuogopa;kama tulivotangulia kuona kuwa kinyume cha Imani ni hofu.Hivyo huna
budi kuanza kuchukua hatua.
·
Anza kubadilisha namna unavyosema
·
Acha kuzungumza na kuwaza habari za hofu na
mashaka
·
Kemea mawazo ya hofu
·
Anza kutamka Baraka za Mungu pamoja na ahadi zake
kwako
·
Anza kuona malaika wa Bwana wamekuzinguka pande
zote pindi uwapo katika hali ya hatari.
Kwa kuyafanya hayo taratibu utaanza kuona roho ya hofu
inaondoka.Na unapojizoesha kuishi kulingana na kanuni izo utakuwa ni mtu wa
Imani na usiyeweza kuyumbishwa na hofu ya aina yeyote.
MUNGU
AKUWEZESHE KUSHINDA!!
Imeandaliwa
na kuandikwa na; JAMES
F.MZAVA
Mawasiliano;
0762759621, 0653194411
Ubarikiwe sana mtumishi wa Mungu kwa somo lako limenijenga na kuamsha imani iliyokua imeanza kufa ndani yangu sababu ya hofu na mashaka ya maisha.Mungu akutunze.
ReplyDeleteMungu akubariki sana mtumishi wa mungu maana mioyo yetu inachimbika na mashaka na hofu.kwa maneno haya na mistari hii ya biblia tumepata kuponywa.
ReplyDeleteSiogopi tena kwasababu nimelielewa somo Vizuri. By.. JONATHA
ReplyDeleteMwenyezi Mungu akubariki sana Mtumishi. labda tu nikuombe utoe mtiririko wa maombi maana watu wengi wanapokua na hofu hata hawajui waombe namna gani. waandikie jinsi ya kuomba wakati wanapopatwa na hofu.
ReplyDeletemateso tuu
DeleteAmina Mtumishi ubarikiwe , kwa maneno hako mazuri
ReplyDeleteAsante sana
ReplyDeleteAsante sana kwa somo MUNGU akubariki, nimeishi maisha ya hofu kwa miaka mingi hadi inafikia napoteza thamani yangu ambayo MUNGU ameweka ndani yangu,,,,,Kuanzia sasa kwa kutumia damu ya YESU hofu haina nafasi tena katika maisha yangu
ReplyDeleteDah shukrani sana mkuu kwa hili somo la hofu naona sitaogopa tena kwasababu sitaruhusu hofu itawale ndani yangu Mungu mkubwa sana
ReplyDeleteGod bless you sana aisee umetufumbua macho na roho kwakweli
ReplyDeleteMungu akubariki naliingiwa na oga na hofu baada ya kuachwa na mke wangu lakini umesaidia
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteBarikiwa sana mtumishi nilikua na hofu hadi moyo kudunda muda wote ambao nasubiria kuingia ktk mahojiano,baada ya kusoma maandiko yako hofu yote imetoka na ninaimani nitawashangaza
ReplyDeleteMaisha yangu Maajabu yanashangaza ushuhuda, Jinsi nimepata kisanduku chenye nguvu sana ambacho sasa ni pesa yangu mara mbili kutoka mia hadi elfu ya pesa ndani ya masaa 24, na pia jinsi nimerudisha mpenzi wangu wa zamani, sababu kuu niliwasiliana na Dk Lomi kwa msaada mimi kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, basi ananisaidia ni nguvu kubwa ya kumrudisha mpenzi wangu wa zamani, na ananipenda na ananithamini sasa, basi mimi na Dr Lomi tukawa marafiki, baada ya mazungumzo kadhaa namuuliza ikiwa kuna njia anaweza kuniganga ili nipate pesa, hapo ndipo aliponiambia juu ya sanduku hili la uchawi, akaniambia kuna aina na saizi tofauti ya sanduku, aliniambia aina zote za sanduku, ningeweza kumudu ndogo tu ya sanduku, baada ya maombi muhimu anayofanya kwenye sanduku, ananipeleka kupitia huduma ya kujifungua, aliniambia niweke pesa ndani, niliweka ndani ya sanduku 100 euro baada ya masaa 24 nikagundua ilikuwa elfu 10 euro ndani, na nimekuwa nikitumia sanduku kwa miezi 7 sasa, mimi na mchumba wangu tunaishi maisha bora, ikiwa unahitaji b ack mpenzi wako au pesa spell wasiliana na Dr Lomi kwa barua pepe: lomiultimatetemple@gmail.com au WhatsApp namba +2349034287285 unaweza pia kumwandikia kupitia Jina la Mtumiaji la Snapchat: drlomi20 atakusaidia nje, asante kwa kusoma,
ReplyDeleteKwaheri Gerd Ulrich
Habari zenu, nipo hapa kushuhudia, jinsi nilivyo kuwa mwanamitindo tajiri na maarufu duniani mwenye mafanikio makubwa, nimekuwa nikipitia magumu miaka nenda rudi, tangu nilipofiwa na wazazi wangu wote wawili, sikuweza kuendelea zaidi na mshikaji wangu kutokana na Suluhu la kifedha basi, hadi miezi mitano iliyopita, nilimaanisha rafiki ambaye aliniingiza kwenye familia ya freemason, mwanzoni niliogopa kujiunga, kwa sababu nimesoma habari nyingi za uongo kwenye mtandao kuhusu familia ya freemasonry, na ambayo sasa ninaijua. hiyo sio kweli, zote zilikuwa habari za uongo, na napenda kutumia fursa hii kusema asante sana kwa familia ya freemason, ndugu wote wa familia hii, nawashukuru sana kwa support mnayonipa, na kwa waliodhani familia ya freemasonry ni mbaya, haijui sheria na kanuni za huyu jamaa, tafadhali acha kuhukumu ulikuwa hujui, na acha kusambaza habari za uongo, kama una nia ya kuwa mwanachama ufurahie. faida za familia ya freemasonry, contact off anuani icial hapa chini kwa taarifa zaidi.
ReplyDeleteWhatsApp; +31 687 329 133
Barua pepe; info.masonic.oregon@email.cz
Barua pepe; info.masonic.oregon@gmail.com
Au soma zaidi kuhusu sisi kwenye kiungo cha ukurasa wa Facebook; https://web.facebook.com/infomasonicoregon
Mume wangu amerudi!!! Baada ya miaka 1 ya ndoa iliyovunjika, mume wangu aliniacha na watoto wawili na maisha yangu yalivunjika. Nilitaka kuyamaliza, nusura nijiue maana alituacha bila chochote. Nimekuwa nimevunjika kihisia wakati huu wote na maisha yanaonekana kutokuwa na maana. Siku moja mwaminifu, nilipokuwa nikivinjari mtandao, nilikutana na baadhi ya shuhuda kuhusu Dk DAWN. Baadhi ya watu walishuhudia kwamba alimrudisha mpenzi wao wa zamani, wengine walishuhudia kwamba anarejesha tumbo na kuponya magonjwa kwa mimea. Nilipendezwa zaidi na upatanisho na mume wangu, ambao Dk. DAWN aliwezesha kumrudisha mume wangu ndani ya siku 3. Sasa mume wangu amerudi na tumekuwa tukiishi kwa furaha tangu wakati huo. Shukrani zote kwa Dk DAWN. Hapa, ninaacha mawasiliano yake kwa kila mtu. Maana kuna changamoto za aina yoyote,
ReplyDeleteBarua pepe ( dawnacuna314@gmail.com )
Whatsapp: +2349046229159
Asante sana mtumishi neno lako limenipa nguvu na hofu kuondoka taratibu na roho ya umauti na mawazo mabaya ndani yangu yameanza kuondoka naomba mungu pia anisimamie kwa kila hali nayopitia kwa sasa..Na namuomba anipe maisha marefu nizidi kumshinda shetani Amen
ReplyDelete2024 Mungu akubariki sanaaa
ReplyDelete