TUMIA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA KURAHISISHA
MAMBO
Na James F.Mnzava
Sehemu ya kwanza(1)
Bwana Yesu asifiwe sana.Niwakaribishe tena katika somo jingine
tena ambalo Bwana amenipa kibali tushirikishane maneno yake katika somo jingine
la maombi ya kufunga na kuomba kwa jinsi yanavyofanya magumu kuwa mepesi.Fatana
pamoja nami sasa.
NINI MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA??
Watu wengi makanisani wamekuwa wakifanya maombi ya kufunga na
kuomba katika namna tofauti tofauti ambazo nyingine zimekuwa zikileta faida na
pia nyingine zimekuwa zikiwaletea madhara katika maisha yao pasipo kupata
majibu katika maombi yao.
Nakumbuka kuna dada mmoja alikua anasumbuliwa sana na tatizo
la kupata kupata mtoto kwa muda mrefu bila ya kupata bila kupata
mafanikio.Hivyo akaamua kwenda katika huduma mojawapo ya maombezi na baada ya
kuombewa kwa muda mrefu bado tatizo lilibaki pale pale ila mwendesha maombi
alimwagiza yule dada achukue maombi ya kufunga na kujifungia ndani kwa muda wa
siku saba bila kula wala kunywa;na kweli yule dada kwa kuwa aliteseka na tatizo
hilo aliamua kufanya ivo lakini siku moja kabla ya kumaliza maombi yake
alishindwa na kufariki.Je wewe unajifunza nini hapo? Je ni Bwana ndio
aliwaagiza wale wanamaombi kumwambia yule dada kufunga hadi kufa au ni wao
wenyewe?.Hapo nadhani jibu sahihi unalo.
Tafsiri halisi ya neno kufunga ni kuweka kando yale
mambo yote yaliyo na maana,au unayoyapendelea kwa ajili ya kumtafuta Bwana.
Unapofunga
kunakuruhusu kuuadibisha mwili wako kwa ajili ya matamanio yako ya kiroho kwa
Mungu wako.
Hapo nadokeza kwamba yeyeote yule anapokuwa katika mfungo
anautumikisha mwili wake na kuuadibisha kwa ajili ya kukua,kuongezeka kiroho
Zaidi;ndio maana hapa haijalishi umeokoka au la kila mtu anaweza kufanya ivi
kwa ajili ya Imani yake mwenyewe.Mapepo yanafunga,waabudu sanamu wanafunga
pia,wachawi na washirikina na wasioamini wanafunga pia,hii ni kutokana na
kuongeza matamanio yao katika roho zao juu yay ale wanaoyoyaamini.Vivyo hivyo
ata sisi tulioamini Kristo tunafunga kwa ajili ya kuongeza matamanio ya roho
zetu kwa Bwana na kufiisha matendo yale ya mwili na kuongeza tunu Zaidi katika
roho zetu.
Unapofunga
unajiongezea udhabiti na uimara katika maisha yako ya kila siku
Kumbuka neno kufunga linalomaanisha kuuadibisha mwili wako kwa
ajili ya matamanio yako ya kiroho kwa Bwana kunafaa Zaidi na kua na maana Zaidi
endapo ule muda uliouzoesha mwili wako kwa ajili ya mambo yako mengine uutumie
muda huo kwa ajili ya kumtafuta Bwana kwani kufunga pasipo kuomba na kuutafuta
uso wa bwana ni kazi bure.
Jinsi maandalizi ya kujiandaa kwa maombi yako ndio
kutakakuamua mafanikio katika maombi yako.Namaanisha maandalizi mabovu
kutapelekea kuwa na matokeo mabovu hivyohivyo.Kumbuka kufanya maandalizi katika
roho,nafsi na mwili wako pia ili uweze kupata matokeo mazuri ya kufunga kwako.Hebu
tuangalie kidogo hatua muhimu za mwanzo katika kufunga.
HATUA
MUHIMU ZA MWANZO KATIKA KUFUNGA.
·
WEKA NIA NA MALENGO Kwa nini
unafunga? Ni kwaajili ya kupokea tunu na kupandishwa madaraja kiroho,kwa ajili
ya usikivu Zaidi kiroho,mwongozo Zaidi,uponyaji Zaidi,kwa ajili ya matatizo
magumu yaliyoshindikana,kwa ajili ya neema maalumu ya kutuwezesha kuhimili
majaribu tunayokutana nayo.Unapofahamu haya yatakusaidia sana ili uweze kujua
umuhimu Zaidi katika maombi yako;na pia kukufanya uombe kwa Imani Zaidi pamoja
na malengo.
Kupitia maombi ya kufunga tunajinyenyekesha
kwa Mungu ili kumruhusu Roho Mtakatifu aweze kuchochea roho zetu Zaidi,kuamsha
makanisa pamoja na kuponya nchi yetu(2Nyakati
7:14)
·
KUMBUKA KUWEKA AHADI NA KUDHAMIRIA Omba kwa
ajili ya aina ya maombi utakayoenda kuomba wakati unapofunga.Yesu aliwaagiza
wanafunzi wake kwamba wanapaswa kuomba na kufunga ili mambo mengine kwenye
maisha yao yaweze kwenda (Mathayo 6:16 , 9:14-15).Kabla ya kufunga ni
lazima mtu awe ameweka ahadi au mipango ifuatayo ili aweze kutoba Zaidi katika
ulimwengu wa roho mambo hayo ni kama;
1)
Ni
muda gani utafunga? Hili ni swali la muhimu sana kujiuliza kama
umeamua kuingiza kwenye maombi ya kufunga na kuomba utafunga kwa siku
moja,tatu,saba,wiki au mwezi mzima(ila kwa wale ambao bado hawajawahi kuomba
maombi ya kufunga na kuomba ni vizuri kwao kuanza kidogo kidogo)
2)
Ni
aina ipi ambayo Mungu amekuagiza kufunga.Ni jambo jema kumsikiliza Mungu
sana juu ya kile anachokwambia je utakua unatumia maji au kinywaji chochote
hapo ni kutokana na maagizo maalumu kutoka kwa Mungu
3)
Ni aina
gani ya shughuli itaicha kwa muda.Katika kufunga ni jambo la
kiroho na la faragha Zaidi ambalo unahitaji Zaidi kuwa karibu sana na Mungu
hivyo kwa wale watu wenye shughuli nyingi ni vyema kuzipunguza au kuzisitisha
kwa muda kwa ajili ya Bwana
4)
Ni
muda kiasi gani utakao utumia kwa ajili ya kuomba na
kusoma neno.Kufunga kunaendana sana na kuomba pamoja na
kusoma neno la Mungu kwaiyo ni vyema sana kupangilia muda wa kutosha juu ya
ilo.
Kupitia
mambo hayo manne ni mambo ya msingi sana ya kuzingatia pindi unapoaamua kuingia
kwenye maombi ya kufunga na kuomba.
·
ANDAA ROHO YAKO. Kumbuka
msingi mkuu wa maombi yetu ni toba kwanza ni vyema kuanza kwa kuandaa roho zetu
kwaajili ya kumruhusu Mungu kusikia maombi yetu.Hakikisha unatubu dhambi kwanza
na kuwasamehe waliokukosea kwanza.Pia zingatia haya unapoandaa roho yako
1)
Omba ili Mungu akukumbushe pale ulipoanguka na
makossa uliyomkosea
2)
Kiri na ungama kila dhambi ambayo Roho Mtakatifu
anayokukumbusha kuitubia;na pokea msahama wa Mungu kwako(1 Yohana 1:9)
3)
Wasamehe wale wote waliokukosea omba msamaha kwa
wale wote uliowakosea (Mathayo 11:25
,Luka 11:4)
4)
Kuwa msikivu na mwelekevu sawasawa na Roho
Mtakatifu anavyokuelekeza.
5)
Muombe Mungu akujaze na Roho Mtakatifu kama
alivotuahidi (Waefeso 5:18,1 Yohana
5:14-15)
6)
Tafakari juu ya ukuu wa Mungu katika maisha yako
ya kila siku;tafakari neema yake,huruma zake pamoja na mambo yote aliyokutendea
7)
Anza maombi yako ya kufunga kwa kwenda kwa moyo wa
kutarajia kupokea
Itaendelea….
Imeandaliwa
na kuandikwa na; JAMES
F.MZAVA
Mawasiliano;
0762759621, 0653194411
Amina mtumishi.Mungu akubariki kwa somo hilo nzuri
ReplyDeleteBarikiwa mtumishi kwa somo zuri
ReplyDeleteAsante sana...Nimebarikiwa
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeletenimebarikiwa sana nilikuwa natafuta namna ya kupata somo hili naamini ni roho wa mungu kanielekeza mahali hapa ubarikiwe sana
ReplyDeleteamina ubarikiwe kaka
ReplyDeletemungu akuzidishie
ReplyDeleteMungu akubariki kaka nimejifunza kitu kizuri hapa
ReplyDelete