TUMIA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA KURAHISISHA
MAMBO
Na James F.Mnzava
Sehemu ya Pili(2).
Bwana Yesu asifiwe sana.Nikukaribishe kwa mara nyingine tena
katika mwendelezo mwingine juu ya somo tulilolianza la jinsi ya kutumia maombi
ya kufunga na kuomba katika kurahishsa mambo.
Nipende pia kukutia moyo kwani
kila tatizo unalolipitia lilishapitiwa na wengine kama wewe na wakashida na situ walishinda ila waliacha dawa ili kuwasaidia wengine wanayopitia.Mungu
alishafanya njia juu yetu tatizo tunakuwa wazito kushukua hatua.Ni kidokezo
kidogo tu nilichoona kitakusaidia;tuendelee Zaidi katika sehemu ya pili ya somo
letu.
Kama mkristo uliyeokoka unapaswa kujua ya kuwa mojawapo ya
silaha kubwa ya kumshambulia shetani ni maombi ya kufunga na kuomba.
ANDAA
MWILI WAKO KABLA YA MFUNGO
Watu wengi wamekuwa wakiumia sana mara baada ya maombi yao ya
mfungo kwa sababu ya kutokujua taratibu za kufuata kabla ya kuanza kufunga hasa
katika miili yao.Maana unapokua katika maombi ya kufunga bado mwili unaendelea
kufanya matendo yake kama kawaida.Hivyo nashauri kwa wale watu ambao
wanasumbuliwa Zaidi ya matatizo ya tumbo,nyongo na mengineyo kupata ushauri wa
daktari kabla ya kuanza maombi ya mfungo.Ni vyema Zaidi kama ukizingatia haya
yafuatayo;
·
Kwa wale wenye matatizo kama nilivyotaja hapo
awali ni vyema wakafuata ushauri wa kitabibu Zaidi
·
Weka mipaka katika shughuli zako.Si vizuri
unapokua katika maombi ya mfungo nab ado unashughuli nyingi na kazi ni jambo
ambalo linaweza kusababisha madhara na kuharibu maombi yako.
·
Fanya mazoezi mepesi.Hii itasaidia kuupa mwili
wako hari Zaidi ya mfungo;ni vyema ukawa unatembea kama maili tatu itakusaidia
kuondoa na kupunguza kuchoka
·
Tumia maji.Ndio watu wengi mnaweza mkashangaa kwa
nini nimeshauri kutumia maji;ukifuatilia maombi kwa undani Zaidi maji
yanahusika kwa nafasi kubwa sana maana pindi mwili wako unapoanza kuishiwa
nguvu na kuhisi njaa na nyongo inapoanza kutolewa kwa wingi katika utumbo wako
vinaweza kukusababishia madhara hivyo ni vyema uwe unatumia maji kidogo pindi
unapoingia kwenye maombi nah ii itakusaidia kupunguza makali ya nyogo.
·
Tafuta utulivu.Ndio uhalisia wa maombi ya kufunga
yapo katika utulivu epuka kuingiliana na watu na vitu vingine tafuta faragha na
utulivu katika maombi yako.
·
Kimbia vishawishi.Ndio watu wengi wamekua
wakifunga na bado wanaendelea kujiweka katika maeneo yanayoweza kuharibu maombi
yao ya kufunga kwa wao kuendelea kukaa katika sehemu zinazoweza kuwasababishia
wao kufungua;kwa mfano kujiweka kati ya watu wanaokula vyakula jambo ambalo ni
hatarishi katika maombi yao.
WEKA
RATIBA YA KUKUONGOZA
Kwa maendeleo Zaidi ya kiroho pamoja na mafanikio ni vyema uwe
na ratiba itakayoweza kukuongoza katika maombi yako;ni kwa kiasi gani utazidi
kumtafuta yeye,kulingana yeye,kufunga Zaidi pamoja na kulisoma na kulitafakari
neno lake siku hadi siku.
AINA
MBALIMBALI ZA KUFUNGA
·
Mfungo wa
muda mrefu~wa kutumia maji(unaweza kuchukua siku kadhaa),ila pia kwa
walio imara Zaidi wanaweza kufunga kavu bila kutumia maji au matunda.
·
Mfungo wa
Daniel~hakuna kutumia chakula,mkate na kitafunwa chochote;ni kutumia
maji na juisi pamoja na matunda na mboga mboga.
·
Mfungo wa
siku tatu~huu unaweza kuwa mfungo mrefu au mfungo wa Daniel angalau
waweza kufunga kwa kutumia mlo mmoja
·
Mfungo
mwepesi~Mfungo wa kuanzia asubuhi hadi jioni
·
Mfungo wa
Ndoa~Wengi
watashangaa sana kuona kua kuna mfungo wa ndoa;ndio upo angalia katika andiko
apo chini
1 Wakorintho 7:3-4 3 Mke hana amri juu ya mwili
wake, bali mumewe; vivyo hivyo
mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe.
4 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate
faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na
kiasi kwenu.
Andiko
hilo apo lamaanisha mfungo wa ndoa.Biblia inatwambia kua si mke wala mume
mwenye amri na mwili wake isipokua mwenzake lakini mstari wa nne ndio wenye
lengo kubwa ya kua ikiwa wamepatana kwa muda neno muda hapo linamaanisha mfungo
wa muda katika maombi.
Baadhi ya
maandiko yahusuyo kufunga;
( 1
Samweli 7:5-6, Ezra 8:21-23, Nehemia 9:1-3, Joel 2:15-16,Yona 3:5-10, Matendo
27:33-37)
Kumbuka
Mungu huangalia utayari wako wa moyo katika kufunga kwako wala sio wingi wa
siku za mfungo wako katika mfungo.
Kumbuka kumsikiliza Mungu mara kwa mara kwani anaweza
akakwambia ufunge kwa siku moja au muda mrefu yote hayo ni yake ila muhimu ni
kumsikiliza yeye kwanza.Watu wengi wamekua wakijilazimisha kufunga kwa muda
mrefu wakidhani ndio Mungu atawajibu lakini Mungu hilo haliangalii yeye
huangalia usikivu pamoja na utayari wako katika kufanya lile
alilokuagiza,Haijalishi gharama uliyoitumia ila yeye huangalia Zaidi neno lake
kwako.
DONDOO
MUHIMU KATIKA MAOMBI YA KUFUNGA NA KUOMBA
Kumbuka kujijengea angalau maombi ya mfungo kwa siku moja au
mbili kwa wiki itakusaidia sana na kukuimarisha kiroho
Kumbuka mfungo ni njia mojawapo ya kukutana na Mungu kiurahisi
Zaidi na kupata uwepo wake utakaotusaidia kupambana na yule mwovu
Kumbuka kufunga kunatusaidia Zaidi kushinda majaribu ya aina
mbalimbali
Mambo magumu na mazito hulainishwa na kuisha kabisa kwa njia
ya maombi ya kufunga
Maombi ya kufunga yanakupa upenyo Zaidi ya kuweza kufikia Baraka
zako kirahisi
Kumbuka maombi ya kufunga yanakuwekea ulinzi Zaidi na maadui
zako wote
Kupitia maombi ya kufunga Mungu hushugulika na mahitaji yetu
mengine ambayo hata hatujamuomba kutokana na unyenyekevu wetu kwake
Kupitia maombi ya kufunga ngome na mamlaka ya adui huangushwa
chini na kushindwa kabisa
Maombi ya kufunga yanaongeza kibali Zaidi cha kusikilizwa na
Mungu
Kupitia maombi ya kufunga Mungu hugeuza mabaya yote na kuwa
mema.
ZIPO FAIDA NYINGI MNO KATIKA KUFUNGA NA KUOMBA.ANZA SASA NA
UTAUONA MKONO WA MUNGU KWENYE MAISHA YAKO!!
Amen!!
UBARIKIWE
Imeandaliwa
na kuandikwa na; JAMES
F.MZAVA
Mawasiliano;
0762759621, 0653194411
Barikiwa Sanaa mtumish nmebarikiwa na mafundisho mazur
ReplyDelete