UMUHIMU
WA KUHUDHURIA VIPINDI VYOTE KANISANI
Na James F.Mnzava
Bwana Yesu asifiwe sana.Nipende kuwakaribisha tena katika somo
jingine ambalo Bwana amenipa kibali cha kuweza kushirikiana na wewe la kutambua
umuhimu wa kuhudhuria vipindi vyote kanisani.Karibu sana na fatana nami mwanzo
hadi mwisho wa somo hili ni Imani yangu somo hili litabadilisha maisha yako.
Kwa muda mrefu sasa kumekua na tatizo hili kubwa karibia kwa
makanisa yote duniani hasa kwa wakristo waliookoka kutohudhuria vipindi
mbalimbali kanisani wakidhani ni jambo dogo na halina tatizo na ndivyo
ilivyozoeleka kwa asilimia kubwa ya waumini wengi duniani.Ila nipende tu
kuwaambia kua swala la kuhudhuria vipindi mbalimbali ni swala la kiroho na
Mungu mwenyewe aliliagiza hilo kupitia watumishi wake katika maana tofauti
ambazo nitazielezea kidogo hapa chini
Kwa kipindi cha miaka ya nyuma Zaidi ya asilimia sabini na
kidogo ya waumini walikua na hamu na shauku na kuhudhuria ibada nikimaanisha
kati ya watu wanne watatu wao walikuwa na mahudhurio mazuri ya ibada;ila kwa sasa
ni chini ya hamsini hadi arobaini ya washirika hupuuzia ibada na kuona ni jambo
la kawaida na lisiloweza kuwaletea madhara.
Nipende tu kukwambia Mungu hutujua sana maisha yetu pamoja
tunayoyapitia kila siku katika maisha yetu pamoja na mioyo yetu pia.Kila mkristo
hasa wale waliookoka inakupasa kuwepo nyumbani mwa Bwana pasipo kujali muda
wala nyakati unapokuwa na shughuli nyingi,katika ugonjwa au katika sababu
yeyote itakayopelekea kutokuwapo ila unapaswa kuwapo nyumbani mwa Bwana.
Ngoja nikwambie kuwa mkristo
haimaanishi tu kwa yale matendo unayoyafanya siku hadi siku, ila inamaana kubwa
Zaidi kushirikiana pamoja na wenzako na kuwa pamoja katika umoja na ndipo Mungu
alipoamuru baraka.
TAMBUA KIWANGO CHA BARAKA ZAKO KINATEGEMEANA SANA NA
UHUDHURIAJI WAKO KANISANI.MAHUDHURIO DHAIFU HUENDANA PIA NA BARAKA KIDOGO
MAISHANI MWAKO
Biblia inatwambia kwamba kwa wale waliookoka ni familia moja
katika bwana,na nguvu kubwa ya familia ni kuwa pamoja na kushirikiana vitu kwa
umoja.Hivyo tambua kama mkristo fanya bidi sasa kuhudhuria vipindi mbalimbali
ili kuweza kukuza kiwango cha baraka zako.
SABABU ZA
MSINGI ZA KWANINI TUHUDHURIA VIPINDI KANISANI
·
NI TABIA YA MUNGU~ Waebrania 10:25 Maana,
kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena
dhabihu kwa ajili ya dhambi;
Kama maandiko yanavyotwambia kwamba kama
tukifanya dhambi kwa kusudi,basi haitabaki tena dhabihu kwa ajili ya
dhambi.Ngoja nikwambie wengi wetu wamekua na sababu nyingi za kutohudhuria
kanisani nyingine zikiwa hazina maana yeyote ile ambazo tunaziita ni sababu za
makusudi kabisa mbele za Mungu,ni hatari sana maana hakutakua nna dhabihu tena
ya dhambi kwa ajili ya watu wanaofanya ivo.Wengi wetu tumezoea kutambua kwa
haraka tabia njema kuliko zile nzuri nah ii imetupelekea kufanya tabia mbaya
kuliko zile nzuri nah ii ni kutokana na mazoea yetu,na kuwafanya hata wakristo
kutohudhuria vipindi kuona ni jambo la kawaida pasipo kujua kua ni tabia mbaya
kwa Bwana.Ila tabia ya Mungu ni kukubariki na pia kutuona tunakutana pamoja na
kua wamoja kama yeye alivyo Mbinguni
·
NI KILE YESU ALICHOZUNGUMZIA~Luka 14:6 Yesu aliporudi
Nazareth mahali alipolelewa Biblia inatwambia alikuwa ni siku ya sabato na
aliingia kama ilivyokua ``desturi`` yake.Mahali pengine inaandika kama
ilivyokuwa kawaida yake,neno hili desturi likimaanisha alikuwa akifanya jambo
hilo mara zote na mara kwa mara siku zake zote.Yesu ndiye kiongozi wetu
tunayetakiwa kujifunza kwake na si hivyo tu yeye alifwata kile kilichoandikwa
na manabii wa kale,sawa sawa na amri zile kumi za Mungu ``ikumbuke siku ya
Bwana na kuitakasa`` yeye pia alifanya vivyo hivyo.Hivyo kama tunavyosema sisi
ni wafuasi wa Kristo hatuna budi kushika na kufuata yale yote aliyoyashika na
kuyatendea kazi maishani mwetu.
·
NI KUONESHA UPENDO WETU KWAKE.Kwenda kanisani si
tu kwa kujengana bali ni tendo la Imani linaloonesha upendo kwa Mungu na kumtii
(Mathayo 10:32-33).Ndipo sehemu tukapoweza kumtolea Mungu dhabihu zetu za
sifa na shukrani kwake pamoja na matoleo yetu kwa kumshukuru Mungu juu ya yale
aliyotutendea katika maisha yetu
Zaburi
22:22 22 Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu, Katikati
ya kusanyiko nitakusifu.
·
NI MFANO HALISI~Kwenda kanisani ni mfano
halisi.Unapojenga tabia ya kuhudhuria kanisani unafanyika kama kielelezo kwa
wengine,na pia kama nilivyotangulia kusema hapo mwanzo Mungu pia hukubariki kwa
kuwa umeshika amri yake na kuifuata.Kwa wanandoa,wanafamilia endapo mmoja wenu
atakua amezingatia kikamilifu kuhudhuria vipindi vyote kanisani tabia hiyo
hugeuka na kuwa sumaku ya kuwavuta hata na wale wengine wasiokuwa na tabia iyo.
·
NI MUHIMU KWA USHIRIKA~Wakolosai
3:1616 Na kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la
Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye
Moja
ya sehemu ambapo tunaweza kugangwa mioyo yetu ni kanisani,tunaweza kutiana moyo
katika yale magumu tunayopitia kwa kushirikiana pamoja lile ambalo Mungu
ameliweka kwetu.Katika maisha tunapitia mambo magumu,masumbufu
mengi,matukano,shida,adha na mengine mengi ila tunapokutana pamoja Mungu hutupa
neno lake kupitia Roho wake Mtakatifu na kuponya pamoja na kupoza roho
zetu.Kuwepo kwa madarasa mbalimbali ya Biblia kanisani pamoja na vipindi
mbalimbali kunatengeneza upendo pamoja na kukua kiroho Zaidi.
·
NI MUHIMU KWA KUKUZA IMANI ZETU~Moja kati ya neno
zuri sana ambalo huwa napenda kulitumia sana ``Imani haikui yenyewe,bali Imani hukua pamoja na umoja,ufahamu wa Neno
la Mungu pamoja na maombi``Ni moja kati ya misemo ninayopenda kuisema mara
kwa mara nikimaanisha mahali ambapo mnakutana kwa ajili ya Bwana ni lazima
Bwana atazungumza nanyi na moja ya faida ya kusikia sauti ya Mungu ni
kuongezeka Imani.Si hivyo tu bali tunaposhirikishana maneno ya Mungu katika
vipindi mbalimbali kanisani husaidia pia kukuza Imani zetu siku kwa siku
·
NI MUHIMU KWA KUKUA KIROHO~Huu ni ukweli
usiopingika moja kati ya tafiti nilizofanya katika makanisa kadhaa niliyowahi
kutembelea waumini wengi ambao hawana tabia ya kuhudhuria vipindi huanguka
katika majaribu hasa yale mepesi kabisa.Tatizo hapa ni kutokuwa na elimu ya
kutosha katika Mungu,kutohudhuria kanisani kunakufanya ukonde na udhoofu kiroho
na shetani anatumia mwanya huohuo kukushambulia kirahisi.
Kupitia ibada tunaweza kumsifu Bwana na
kumwabudu na pia kunakusaidia kuweza kupata nguvu pamoja na uwepo wake Zaidi kuliko
unapokuwa mwenyewe au katika shughuli zako.
ZINGATIA
HAYA YAFUATAYO
Tambua ya kuwa Baraka zako pamoja na mafanikio yako yapo
katika vipindi unavyovikosa na kuviruka kanisani.Ndio kama nilivyotangulia
kusema mwanzo hatuna budi kama wakristo kuzingatia sana ibada zote kanisani ni sharia
ya Bwana wala sio hiari yetu sawasawa na Bwana alivyonena na Musa katika zile
amri kumi mlimani.
Tambua Mungu wetu anataka tumwambudu na kumsifu kwa pamoja
hekaluni mwake
Yohana
4:23-24 23 Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi
watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao
wamwabudu.
24 Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu
katika roho na kweli.
Tamani kiu na
matamanio yako yawe ni kuwa pamoja na Mungu,kumwabudu na kumsifu;si tu kwa
sababu Mungu hupenda sisi tumsifu bali sisi pia tunahitajika kumsifu yeye kwa
hiari na kwa mioyo yetu yote.(Mathayo
22:37-38)
Tambua kila
mkristo hana budi kujifunza ili afunze na wengine.(Mathayo 5:6,Waebrania 3:12,1Thessalonike 5:11)
Kwenda kwako
kanisani kunakufanya wewe kutembelewa maalumu na Roho mtakatifu.Maana Biblia
inatwambia walipo wawili au watatu kwa ajili ya jina langu nitakuwepo katikati
yao
Kwenda kanisani
kujenga Zaidi mahusiano mazuri na wakristo wengine.Mnapokusanyika sawasawa na
mapenzi ya Mungu Amani ya Bwana hukaa juu yetu sote na kutufanya tuwe pamoja na
umoja
Kwenda kanisani
ni kitendo cha utiifu kwa Mungu.Ndio Biblia inatuagiza kukusanyika na pindi
tunapofanya ivyo tunakuwa tumehesabiwa haki mbele zake kwa kuwa watiifu
sawasawa na maagizo yake.
Kwenda kanisani
kunajumuhisha maombi yetu kwa pamoja.Katika kusanyiko ndio silaha yetu kubwa ya
maombi hufanya mambo ya ajabu Zaidi kwa kuunganisha maombi yetu na kuleta
matokeo makubwa katika mazingira yetu halisi
Zipo faida na Baraka
tele za sisi kuhudhuria ibada nakusihi anza sasa kama ulirudi nyuma hapo awali
omba toba kamilifu kwa Bwana na kusudia kuanza upya na Mungu atafanya
KUMBUKA KIPINDI KIMOJA UNACHOKIKOSA NDICHO
KIPINDI CHA MAANA ZAIDI CHA KUKUTOA SEHEMU MOJA KWENDA NYINGINE.
AMEN UBARIKIWE!! BWANA
AKUWEZESHE
Imeandaliwa
na kuandikwa na; JAMES
F.MZAVA
Mawasiliano;
0762759621, 0653194411
barkiwa mtumishi
ReplyDelete