UMUHIMU WA MAOMBI KATIKA
MAISHA YAKO YA KILA SIKU
Na James F.Mnzava
Bwana Yesu asifiwe sana.Nipende kukukaribisha tena katika
mfululizo mwingine wa masomo na mafundisho yangu.Maombi ni eneo ambalo sote
linatuhusu na kuathiri wengi wetu pia,hatutaweza kuishi pasipo
maombi,hatutaweza kumshinda shetani pasipo maombi,hatutaweza kushinda majaribu
pasipo maombi,hatutaweza kufanikiwa kiroho na kimaisha pia kama
hatuombi.Kiujumla maombi yana asilimia kubwa sana katika maisha yetu sote hapa
duniani.Fuatana nami katika somo hili mwanzo hadi Mwisho bila shaka hautakuwa
kama ulivo.
MAOMBI
NI NINI?
Watu wengi wamekua
wakitafsiri maombi katika aina mbalimbali n ahata wengine wamekuwa
wakipotosha maana halisi kwa kutamka tafsiri zao ambazo sio sahihi.
Maombi ni Kumpa Mungu ruhusa na haki ya kuingia na
kutenda,katika mazingira yetu yanayoonekana na yasiyoonekana.
Najua wengi wamezoea tafsiri mbalimbali lakini katika somo
hili embu tujaribu kwenda na tafsiri hii niliyokupa hapo juu na uone ni kwa
jinsi gani inaweza kufanya kazi katika maisha yako.
TAMBUA
NI KUSUDI TULILOITIWA KUOMBA
Kama wewe umeokoka tambua kabisa Moja ya kusudi kubwa la sisi
kuwepo hapa duniani ni maombi usisahau ilo.
·
2 Nyakati
7:14
14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina
langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao
mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya
nchi yao.
·
Luka 18:11 Akawaambia mfano, ya kwamba imewapasa kumwomba
Mungu sikuzote, wala wasikate tamaa.
·
Waefeso 6:17-18 17 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika
Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
18 pia na kwa ajili
yangu mimi, nipewe usemi kwa kufumbua kinywa changu, ili niihubiri kwa ujasiri
ile siri ya Injili;
·
1
Thessalonike 5:16 16 ombeni bila kukoma;
·
Mathayo
16:19-20 19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa
mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na
lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
Mathayo 18:18-20 18 Amin, nawaambieni,
yo yote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yo yote
mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
19 Tena nawaambia, ya
kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lo lote watakaloliomba,
watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
20 Kwa kuwa walipo
wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
MAKUSUDI YA MSINGI YA MUNGU KATIKA MAOMBI
Maombi ni Zaidi ya kuwasilisha haja zetu na mahitaji yetu kwa
Mungu.Kusudi halisi la Mungu juu ya maombi ni kumjua yeye,kumwabudu yeye na
kuhisi uwepo wa Roho wake katika haja zetu.
Maombi ni njia ambayo tunajifunza kuwasiliana,kuzungumza na
Bwana na kuisikia sauti yake.
Maombi yanaturuhusu kutakaswa na Kristo na kujenga ufalme wake
duniani kama huko Mbinguni
Maombi yanatuwezesha sisi kukaa ndani yake na yeye kukaa ndani
yetu.
Moja ya kati ya siri kuu ya maombi ni nafsi zetu
kufungamanishwa na makusudi ya Mungu kwetu
Maombi situ kile tunachoweza kukipata kwa Mungu;bali Mungu
hutimiza mapenzi na makusudi yake kupitia sisi kama yeye mwenyewe apendavyo
Makusudi ya Mungu lazima yatimie katika kila ombi unaloomba
kwake haijalishi ni kwa namna ulivyotaka au usivyotaka (Zaburi 33:11)
MATARAJIO
YA ROHO ZETU TUNAPOKUWA KWENYE MAOMBI
·
Tunapoongea na
Mungu tunashikamanishwa naye
·
Tunafikia makusudi ya umoja wa pamoja katika
Kristo
·
Katika maombi tunaunganisha yasiyoonekana pamoja
na nafsi zetu na roho zetu katika Bwana wetu
·
Katika maombi tunaweza kuyaita na kuyafanya yanayoonekana
na yasiyoonekana yawe sawasawa na haja zetu kwa njia ya Imani ( Warumi 4:17)
UNAPOOMBA
KUMBUKA HAYA
·
Unamruhusu Mungu kuliheshimu jina neno lake katika
neno lake
·
Unampa fursa ya Mungu kuja na kutimiza yale
aliyoyaahidi kwako na kwa wale unaowaombea
·
Kupitia maombi unafanya ufalme wa Mungu uje
duniani kama huko Mbinguni
·
Unajiwekea hazina ya maombi yatakayokusaidia wewe
na wengine pindi unapokuwa kwenye wakati mgumu
·
Unajipamba kwa mapambo yasiyo na thamani.(Taji ya Baraka na thawabu)
MTUKUZE
MUNGU KWENYE MAOMBI YAKO
·
Maombi yanajenga mahusiano ya kirafiki na halisia
na Mungu (Mathayo 23:37, Yohana 17:3)
·
Jifunze kumtukuza Mungu kwa yale aliyokupa
maishani
·
Jifunze kuomba Mungu afunue kusudi la maisha na
mwito wake kwako
·
Maombi yanajenga Imani katika upendo wa Mungu
·
Jifunze kuomba maombi yanayoendana na ahadi za
Mungu kwako
OMBA
MAOMBI YAPASAYO YATAKAYOKUPA FAIDA
·
Utagundua maisha yanayopasa kuishi pamoja na
ulinzi wa Bwana juu yako
·
Uwezo wako wa kutambua na kusikia sauti ya Mungu
utaongezeka siku hadi siku (Yakobo 1:5,
Yeremia 29:13)
·
Nguvu yako ya kiroho na ya kihuduma itazidi
kuongezeka siku baada ya siku (Yohana
14:12-14 , Matendo 1:8)
·
Utapokea uwezo na kipaumbele wa kusikilizwa na
Mungu hakuna hitaji ambalo Bwana atalinyamazia kwako (Yohana 15:7)
·
Utapokea nguvu mpya ya kuweza kusimama na kushinda
katika majaribu ya aina mbalimbali pamoja na mapambano ya kiroho (2 Wakorintho 10:3-5)
·
Roho Mtakatifu atakufunza Zaidi kuwaombea wengine
walioshindwa na kupitia wewe wengi wataokolewa
·
Utapokea nguvu ya kuweza kuomba juu ya uamsho
katika kanisa lako pamoja na eneo unaloishi (Ezekiel 22:30)
MAOMBI NI YA MUHIMU KWA SABABU NI MAWASILIANO YETU
NA MUNGU
Viongozi wengi wa kidini wamekuwa wakiongelea kuhusu maombi
ila Yesu aliliongelea hilo kwa njia tofauti pia kuomba kwake kulikua tofauti na
kwa aina yake pia(Luka 6:12) Hapa tunaona jinsi alivyokesha usiku kucha
akimuomba Mungu.Alikua akiwasiliana na Baba yake;mawasiliano ndiyo njia kuu ya
kuweza kuelewana na kuishi kwa pamoja na kama yakiharibika hakutakua na Amani wala
utulivu.Hebu chukulia hata kwenye ndoa kama mme na mke hawasiliani unadhani
nini kitatokea?Vivyo hivyo hata sisi na Mungu mawasiliano nay a muhimu sana na
Mungu wetu
.
MAOMBI NI
MUHIMU KWA KUA NI NJIA YA KUSHUKURU
Kabla Yesu hajawalisha wale watu 5,000 alianza maombi yake kwa
kushukuru
Mathayo
15:36 36 akaitwaa
ile mikate saba na vile visamaki, akashukuru akavimega, akawapa wanafunzi wake, nao wanafunzi wakawapa makutano.
Katika
maisha yetu ya kawaida imekuwa ni vigumu kwa watu kutanguliza shukrani kwa
Mungu kabla ya kuanza.Wakristo wengi hasa wanapokuwa katika maombi wengi wao
huanza kuomba kwa kuanza moja kwa moja na matatizo yako jambo ambalo ata Kristo
hakulifanya katika maombi yake yeye alianza kwa kushukuru kwanza.Jifunze
kushukuru
MAOMBI NI MUHIMU KWA KUA NI NJIA YA UPATANISHO
Maana nzuri ya neno upatanisho ni
kuomba badala ya au kutamka badala ya mtu mwingine.Kupitia maombi Mungu ametupa
nafasi ya kuweza kusimama badala yaw engine kwa kuwaombea mahitaji yao na Mungu
akafanya kazi (1Timotheo 2:1).Je ni muda gani unachukua kuomba kwa ajili ya
familia yako,majirani zako,Taifa lako pamoja na wengine wanaokuzunguka?
MAOMBI NI MUHIMU KWA
KUA NI NJIA YA KUSAMEHEWA DHAMBI ZETU
Hatutaweza kupata msamaha wa
Mungu kwa njia yeyote ile isipokuwa ya kumwendea Mungu kwa njia ya maombi (Zaburi 69:5)
AMEN!!
Imeandaliwa
na kuandikwa na; JAMES
F.MZAVA
Mawasiliano;
0762759621, 0653194411
BWANA YESU ASIPHIWE KAKA YANGU JE UKIOTA UKO NA WATU WENGI KWEYE SHEREYE INA MAANISHA NININKAKA
ReplyDelete