KWANINI IMANI?
Nawasalimu katika jina la Bwana Yesu kristo.Unaweza ukawa na
maswali mengi sana kuhusiana na Imani.Ila leo nimeona ni vyema tukashirikishana
maana halisi ya Imani na jinsi inavyotenda kazi.
Kwanza kabisa nipende kukujulisha haya yafatayo ambayo
yataweza kukusaidia kwenye hili somo.Je unafahamu maana ya Imani?,je unafahamu
umuhimu wa Imani?,je wajua inachukua Imani ili tuweze kuamini Kristo,je wajua
kua unachukua Imani kuamini kile ambacho Mungu amekisema ni sahihi na kweli? Je
wajua unachukua Imani kuamini na kutembea kwa kila tendo kwa kila siku? Bila shaka
majibu ya maswali yote hayo ni kweli na hakika.
Lakini nipende kukwambia kwamba japokua kama Imani yako
haiendelei kukua katika mahusiano yako na kristo hutaweza kua na Imani kuona
ufalme wa Mungu kwako pamoja na matendo yake kwako katika maisha yako na si
hivyo tu pia hata katika maisha na vitu vinavyokuzunguka.
Imani uliyonayo ndani yako itabainisha matokeo ya kiwango cha Imani
ambacho Mungu atafanyia kazi katikati yako.kama huna Imani ya Mungu kutenda
katikati yako/kupita basi kutakua hakuna
nafasi ya kuona fursa au matokeo halisi katika mazingira yako,bali kutakua na
nafasi nzuri yaw ewe kutokuona mambo yakichukua nafasi ya kutendeka.
Ngoja nikwambie kitu ambacho kitakusaidia kwenye maisha
yako,utakubaliana na mimi kua yale mambo ambayo umeyatumia kwenye maisha
yako;muda,pesa,nguvu ndivyo ambavyo vitapiga kelele kuonyesha ni Imani gani
uliyonayo hasa unapovikosa.je unapokosa mambo muhimu katika maisha yako ni nini
tumaini lako la baadae katika kupata tena na kutazamia tena?
Unaposoma kwenye injili zote za Yesu kwenye Agano jipya utaona
jinsi Yesu alivyokuwa na upendo na mar azote alimjibu kila aliyekua na tatizo
awe na IMANI.Bwana aliipenda Imani.Ndiyo aliipenda Imani hasa pale watu walipoweka Imani ta tegemeo
kwake.
Mathayo 8:5-13 5 Hata alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia,
6 akamsihi, akisema,
Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana.
7 Yesu akamwambia,
Nitakuja, nimponye.
8 Yule akida akamjibu,
akasema, Bwana, mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu; lakini sema
neno tu, na mtumishi wangu atapona.
9 Kwa maana mimi nami
ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, mwenye askari chini yangu; nikimwambia
huyu, Nenda, huenda; na huyu, Njoo, huja; na mtumwa wangu, Fanya hivi, hufanya.
10 Yesu aliposikia
hayo, alistaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona
imani kubwa namna hii, kwa ye yote katika Israeli.
11 Nami nawaambieni,
ya kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi pamoja na
Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo katika ufalme wa mbinguni;
12 bali wana wa ufalme
watatupwa katika giza la nje, ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
13 Naye Yesu
akamwambia yule akida, Nenda zako; na iwe kwako kama ulivyoamini. Mtumishi wake
akapona saa ile ile.
Mstari kwa 10
unamaana Zaidi katika maandiko haya hapo tatizo kutatuliwa kwa uyu Akida si
kwamba Yesu alimwambia atakwenda amponye binti yake bali ni Imani tu
iliyokuwemo kwa akida huyu.Ngoja nikwambie Mungu ndiye muweza wa yote lakini
linapotokea tatizo kwetu sisi wanadamu uwezo wake hutegemea sana kiwango cha
kuamini kwetu(Imani) katika yeye.Wakati Mungu alipomuumba mwanadamu alimpa kitu
kimoja cha muhimu sana kitu icho ni nguvu ya kuamua na kuamini.Yaani Mungu
alitufanya kuwa waamuzi katika mambo yetu yote hapa duniani na pia alitupatia
nguvu katika Imani.
NINI TAFSIRI YA IMANI
Imani ni kichochezi kinachosababisha mambo kutokea katika
ulimwengu halisi kabla hata hayajaonekana Dhahiri au kutokea kwa uhalisia wake.
Imani ni uthibitisho,mhuri wa mambo ya ndani yasiyokuwepo
na kuyajengea fursa na nafasi kutokea katika mazingira ya kawaida ya baadaye.
Imani ni hatua ya nafsi na moyo ya kutengeneza mazingira
ya ndani yasiyokuwepo katika mazingira halisia na kuyafanya yawepo sawasawa na
mazingira yaliyoandaliwa kabla.
Naamini kabisa katika tafsiri izo
ambazo Bwana amenipa zitakusaidia kuweza kuelewa nini maana ya Imani.Natambua
wengi wetu tumezoea tafsiri ile ya Waebrania ila pia ni vizuri ukichukua na
hizi zitakusaidia Zaidi kuweza kukuza kiwango chako cha uelewa.(Ebr 11:1,Rum 10:17-21)
Maandiko mengine (Mathayo 15:21-28,Marko 5:21-24,Luka
19:1-10)
Pia kitu cha
kushangaza ni kwamba Bwana Yesu mar azote aliposemea kuhusu Imani alitwambia
kwamba hata ukiwa na Imani kama punji ya haradali(ndogo sana) tunaweza kuhamisha
milima.Kwa maana mengine kiwango tu kidogo cha Imani ulichonacho kama utaweza
kukitumia ipasavyo kitaweza kufanya mambo makubwa na ya ajabu na kuwashangaza
wengi.(Mathayo 17:20,1Wakorintho 13:2).
JE WAJUA KUA IMANI NI MBEGU?
Hapa Yesu alilinganisha
Imani yetu kama punji ya haradali,nimefatilia hii punji ya haradali nimepata
kuona kua ni mbegu ndogo mno sana yaani ni mbegu ndogo mno duniani kote.Hebu
jaribu kufikiria kwanini Yesu aliamua kufananisha Imani ya wanafunzi kama
haradali? Ila ilo bado lisikupe shida tambua ukubwa wa mmea haungalii punji au
mbegu ya mmea wenyewe cha muhimu ni mbegu na inapopandwa tunategemea
iote.nipende kukwambia kua Imani uliyonayo inatafuta mahali ambapo utaweza
kuipanda ili iweze kuota na kuzaa.Kila mtu unayemuona amefanikiwa kiimani ni
mtu ambaye alishaipanda Imani yake kabla ya matokeo yenyewe ya Imani yake
kutokea.Hebu tuangalie mfano wa Ibrahim ni kwa nini anaitwa baba wa Imani? Si tu
kwasababu alikua na Imani bali ni matokeo ya kupanda kwa Imani yake kwa Bwana
kwa isaka na hadi leo tunaona mti wa Imani na matunda yake ya Ibrahimu.
Mbegu yako ya Imani
inakua na maana sana kama umeipanda mahali sahihi na kuisimamia ili iendelee kukua.Imwagilie
na kuilisha mbegu yako ya Imani kwa kuipa chakula na lishe bora kwa kusoma neno
la Mungu.Nasema haya kwa sababu Biblia inatwambia kua chanzo,kiini cha Imani huja
kwa kusikia maneno ya Mungu.
Imani yako ni
ngumu kukua na kuendelea kama wewe binasfi hutakuwa na mazingira ya kusikia
sauti ya Mungu na kusoma neno lake.Jenga mazingira ya kumwomba Mungu na
kuliabudu jina lake.Mambo hayo yote ndiyo yanayolisha Imani yako na kuifanya
izidi kukua siku hadi siku.haleluyah (Mathayo 17:20)
Ngoja nikwambie
kitu cha kukusaidia ukisoma (Waebrania 4:16) inasema nasi tunao ujasiri;ambapo
neno hili likiashiria hasa IMANI ya kumkaribia Mungu na kiti chake cha neema.Hapa
kuamini au kua na ujasiri ni kitu kimoja … na pia kutembea katika Imani iyo au
ujasiri huo siku kwa siku ni hatua nyingine.
KWANINI IMANI NI YA MUHIMU?
Pasipo Imani haiwezekani kumpendeza Mungu….kila amwendeaye
Mungu imempasa aamini yeye yupo…(Waebrania 11:6)
Yesu ni chanzo cha Imani yetu,tumaini na msaada wetu (Yohana
14:6)
Tambua chanzo cha Imani yako huja kwa kusikia (Warumi 10:17)
Tambua kua Imani ni kipawa na hivyo hugawanywa kama roho
apendavyo (Efeso 2:8)
Hivyo tambua ya kuwa kama Imani ni kipawa huwezi ukapata
popote au kwa uwezo wako binafsi inakupasa umuombe Mungu kwanza,na baada ya
kuomba amini ya kuwa umeshapokea na itakuwa kwako.Sasa kazi kwako kutembea nayo
maana tayari ni yako.
Unaweza kuomba Zaidi kupewa Imani Zaidi maana usipojenga
mazingira ya kukuza Imani yako kama nilivokwambia apo juu Imani itaweza
kupunguka.ila kwa upendo wa Bwana tunaweza tukamuomba Imani Zaidi pindi
tunaonapo tumepungukiwa (Luka 17:5)
·
ILA AMINI KUWA KILE AMBACHO BWANA AMESEMA KWAKO NI
KWELI,NA HATA USIPOKIONA KIMETOKEA KWA NAMNA UNAYOTAKA UTAFANYA KWA NJIA
NYINGINE USIYOIJUA.
Tukiangalia sura nzima ya Waebrania 11 tunaona sura karibia yote inaelezea kuhusu
wazee wetu wa Imani waliotutangulia wenye tabia asili kama za kwetu lakini
walimwamini Mungu kwa kile alichokisema kwao hata kama hayakutokea kama wao
walivotaka.Na tunaona hata mengine hayakutokea kabisa kwenye maisha yao lakini
bado waliamini na kuishi kwayo.Naamini waliweza kuhuzunika hasa kwa yale ambayo
hayakutokea kwenye maisha yao lakini bado walikua na subira na Imani kwa Mungu
kua bado atafanya ata kama sio kwao atafanya kwa vizazi vyao vinavyofata.Haikua
Imani ndogo ya namna hii.
Hebu jiulize
swali unafanya nini endapo ahadi za Mungu kwako bado hazijatimia kwenye maisha
yako?
IMANI
NI KITENDO
Tambua kua katika Imani iliyotimilika ni jambo moja.Japokua si
kusema tu unaamini bali ni kutenda kile ambacho unakiamini,ili kuonesha ni
kiasi gani unaamini.Haleluyah
Watu wengi leo wamekua wazito kuwashirikisha wengine matendo
ya Mungu kwao wakiogopa labda watawakera au kuwaudhi au kukataliwa nao.Ngoja
nikwambie kitu kama unahitaji kumuona Mungu akitembea kwenye maisha yako na
maisha ya watu wanaokuzunguka huna budi kuchukua hatua. (taking risks is a
part of stepping out)
·
Bwana John Wimber alisema katika kitabu chake cha Imani
alisema kua Imani ni kitendo cha kujihatarisha
·
FAITH IS SPELLED R.I.S.K
Usifikirie sana kujihatarisha kwako kuliko fursa uliyonayo kuwapatanisha
watu na Bwana ili waweze kuuona ukuu wake;usifikirie sana ni kiasi gani unaweza
kwenda vibaya au ukakosea;Zaidi ya kumwambie Mungu akujaze Imani yake ili uweze
kuwaambia wengine ukuu wake(Matendo 1:8) Mstari huu unalenga hasa namna ya
kuwaeleza watu kile tulichokiamini tukiwa na kisto(IMANI)
WASHIRIKISHE
WENGINE IMANI ULIYONAYO
Ni jambo jema sana kuwaambia kile unachoamini kwa kile ambacho
umekiwekea kwa Bwana maana kumbuka kua Imani sio tendo la siri ni vyema
uwashirikishe wengine kile unachokiamini katika Bwana.
·
Elezea Kusudi la Mungu na Amani yake (warumi
5:1,yohana 3:16,10:10)
UMUHIMU WA IMANI
1.
KUMPENDEZA
MUNGU. Mungu anapendeza sana na mtu mwenye Imani kubwa na Zaidi ya
apo hakuna njia nyingine unayoweza kumpendeza Mungu(ebra 11:6)
2.
KUHESABIWA
HAKI.
Abraham alishesabiwa haki kwa ajili ya Imani (Mwanzo15:6)
3.
TUNAFANYIKA
KUWA WANA WA MUNGU. Kupitia Imani tunakuwa watoto wa Mungu yaani
warithi ahadi zile za Mungu alizotuahidia kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu
ni jambo la Baraka sana kupata heshima kubwa namna hii.ni kwa njia ya Imani tu
4.
KUISHI
MILELE. Wale wenye Imani katika Bwana tunaamini kuishi milele (Galatia
3:11)
5.
MAOMBI
YANAJIBIWA KWA IMANI.Mungu huwajibu sana wale wenye Imani kwamba
ataweza kufanya hata kama kwa kibinadamu tunaona haiwezekani ila kwake kuna
tumaini bado.Hapa wale watu wenye hofu,wasiwasi na mashaka Mungu hashughuliki
nao ni vyema kujenga Imani ndani ya Bwana atatenda tu maana hajawahi kushindwa
(Marko 11:22-24)
6.
KUPOKEA
AHADI
7.
IMANI NI
NGAO.Katika
dunia hii ya uovu hatutaweza kuishi bila ya kuwa na ngao ambayo ndiyo Imani yetu
(efeso 6:16)
8.
TUNASAMEHEWA
DHAMBI KWA IMANI (marko 2:5)
9.
UHAKIKA
WA WOKOVU
Kumbuka kwa kadiri unavozidi kuweka tumaini
lako kwa Mungu ndivyo kiwango cha Imani yako kinazidi kuongezeka siku hadi
siku.
Kumbuka pia kuwa Imani inatuba shuhuda juu ya
kunena na kutangaza matendo makuu ya Mungu aliyotutendea siku hadi siku.
Kumbuka pia Mungu yupo wazi sana na halisia Zaidi
endapo kama atapata mtu mwenye Imani dhabiti duniani katika kufanya mapenzi
yake (2 Nyakati 16:9a).Huu umekua
moja kati ya mistari yangu ya muhimu sana kwenye maisha yangu ya kuwa macho
yapo duniani kote nanazunguka na kutafuta kama kuna mwenye Imani ya kweli mtu
mwaminifu ili kutenda jambo pamoja naye.Hapa ni wewe mwenyewe kuwa mnyenyekevu
ili Mungu akufanye vazi lake akuvae ili uweze kutumika sawasawa na mapenzi
yake.
Kumbuka Imani si kitu kirahisi kukupata hivyo
pia hata watu wa Imani huwa nadra sana kuwapata.(zaburi 20:6).Ni kweli watu
wengi husema kuwa wanamtumainia Bwana lakini matendo yao ni tofauti sana na
kile wanachokisema maana Imani ni matendo na pasipo matendo haifai imeshakufa. itaendelea...
IMEANDIKWA NA KUANDALIWA NA; JAMES MZAVER
MAWASILIANO: 0762759621, 0625782324
UBARIKIWE SANA
No comments:
Post a Comment