Tuesday, November 10, 2015

UJUMBE KUTOKA KWA BWANA KWA WACHUNGAJI,MAKASISI NA WAKRISTO

 UJUMBE KUTOKA KWA BWANA KWA WACHUNGAJI,MAKASISI NA WAKRISTO: 


 Bwana alinitembelea asubuhi mara tu nilipofika ofisini. Niliuhisi uwepo Wake kisha mkono ukanijia juu ya mabega yangu.Nami nilihisi moto juu yangu na nikaisikia sauti ya Bwana ikiniongelesha akisema: “ yaandike chini na uwaambie.” Hivi ndivyo asemavyo Bwana Mwenyezi Mungu kwa wachungaji, wainjilisti, makasisi na watumishi wengine: “ ghadhabu yangu itawamaliza” Nanyi hamtanyakuliwa, kwani mmeziacha njia zangu na kuwafanya kondoo wangu mali yenu binafsi na chanzo cha utajiri wenu ,Kwa hiyo Bwana hatawanyakua wachungaji hawa,wanjilisti na watumishi wangu waliopenda ufanisi badala ya ujumbe wa kutubu,kubadilika, kuja kwangu ambako kuko karibu na mada ya kunyakuliwa. Kanisa wanalolisema kuwa langu, limekuwa ukumbi wa kujitumbuiza likiongozwa na wachungaji,makasisi na mashemasi wa kanisa. Wala na kunywa na kusherehekea nyumbani mwangu na mbele yangu pasina kuogopa,kutetemeka au kuniheshimu. Oh, Utukufu Wangu umeondoka mahekaluni mwao na uwepo Wangu uliondoka kitambo kutoka makanisani mwao. Wao hawatanyakuliwa wasiponililia mimi Mungu wao kwa uchungu katika toba. Watumishi wangu wamepotoshwa na ulimwengu nao sasa wanafanya mipango ya kuingiza njia za kiulimwengu makanisani. Wao husherehekea siku ya wapendanao kanisani na pia husherehekea siku ya kimataifa ya waongo kanisani ,nao husema katika siku ya kuomboleza ,leo ni siku ya majonzi nasi basi tuvalie mavazi meusi. Wote wamepotoshwa. Wachungaji,wainjilisti na makasisi wametabiri nyakati za utele,nyakati za kukombolewa na kufanikiwa ilhali panakuja humu ulimwenguni misiba na mateso makubwa, na kuharibiwa kwa ulimwengu. Watumishi wangu hawanisikii kamwe. Wamejipotosha na ulimwengu na hata wameziacha njia zangu. Wao hawanitafuti katika maombi ,kufunga na kulitafkari neno langu. Wao hufunga na kuomba ili kuniomba vipawa vya kuponya,miujiza na kutabiri kwa manufaa yao wenyewe. Na hata wao husema: Nitatayarisha ujumbe wa kuhubiri. Nitatayarisha mkutano. Mimi nina shughuli nyingi ya kuwapa ushauri nasaha waumini.lazima niwatunze waumini, nao hawana wakati kwa ajili yangu Mimi, ambaye ndiye mmiliki wa kondoo hawa. Hawa wachungaji hawatanyakuliwa asema Bwana wa majeshi. Ikiwa hamniogopi mimi, basi zirarueni nguo zenu,nyoyo zenu na hata akili zenu kwa machozi na kutubu. Nataka toba la kitaifa la kanisa ,maombolezo na kilio. Mjivishe mavazi ya vumbi na mlie kwa toba la sivyo nyinyi hamtakuja kwangu mbinguni. 2 Kondoo wangu wanakula chakula kilicho oza,kilichorogwa kutokana na jumbe za watumishi Wangu na hawa wachungaji. Wanaekeza kwa ajili ya siku za usoni kwa miradi ya ujenzi kanisani nao hawafahamu kwamba hii miradi yote itakatizwa na maangamizo na majangwa ya ghafla. Baada ya kuliokoa kanisa langu kutoka humu ulimwenguni,hii miradi yote ya ujenzi itageuzwa kuwa bure. Ni viwekezo ambavyo havita zaa chochote. Badala yake yafaa muwekeze katika kuhubiri neno la uhai lisilo bandia. Hubirini badala yake Kufanikiwa kwa nafsi na roho kupitia kwa toba na uzima wa milele. Bwana asema hivi, nalipenda sana kanisa langu,ambalo hunitafuta kila siku na huliogopa jina langu takatifu!! Wakati umekwisha.


Wakati umefika tamati. Saa yaja sasa hivi, nitakapolinyakua kanisa langu. Mara tu baada ya tukio hili, Majanga, misiba, na mateso ya kutisha ambayo haijawahi kuwa humu duniani itaangamiza maisha mengi. Wakati adui yangu atachukua hatamu, hapatkuwa na toba tena,wala wakati wa kunitafuta ,kwani Mimi sitayajibu maombi yoyote, neema itakuwa imeondolewa na Roho wangu Mtakatifu hatakuwa ulimwenguni. Adui atachukua hatamu nanyi mtasaga meno yenu na kupiga mayowe mioyoni mwenu kwa mateso na kuvunjika. Zivunjeni nyoyo zenu sasa na mzifanye zimwage damu ya toba,zipasuenii nyoyo zenu kwa toba katika sekunde za mwisho za wakati uliosalia, la sivyo ghadhabu ya kutisha iwapate. Lakini watu hawa wana roho ya kuasi, nao wameasi na kwenda zao. Hakuna asemaye moyoni mwake, wacheni sasa tumuogope Bwana Mungu wetu apeanaye mvua ya sasa na hata ya awali katika wakati wake.Ametuhifadhi kwa ajili ya wakati teule wa mavuno. Uovu wenu umeyageuza mambo haya, na dhambi zenu zimezuia mambo mazuri kuja kwenu. Kwani miongoni mwa watu wangu panapatikana watu waovu, wananyemelea kama afanyavyo yule amtegae nyoka,wameweka mitego na wamewanasa watu. Kama vile kizimba kilivyojaa ndege basi ndivyo nyumba zao zimejaa udanganyifu, kwa hivyo wao wamekuwa wakubwa na tajiri sana. Wao wamekuwa wanono, wanang’ara, naam, wamezidi matendo ya waovu, wao hawahukumu vyema mambo ya wakiwa lakini bado wanafanikiwa; na haki za wanyonge hawazihukumu au kuzitilia maanani. (Jeremiah 5:24-28) Nyinyi hamtanyakuliwa asema Bwana, isopkuwa mbadilishe mienendo yenu na kutubu. Mimi sitawanyakua wale waliooana na televisheni, sinema na burudani ambazo zimechukua muda wenu mwingi nanyi hamna wakati kwangu miye Mungu na neno langu. Mimi sitawanyakua wakristu waendao kanisani jumapili pekee ili kutuliza ghadhabu yangu juu ya maisha yao ,nao wanadhani kwamba Mimi Mungu sioni wala kuyafahamu yale wafanyao. Jumapili, wao huenda tu kanisani kujionyesha nguo zao nzuri na kupiga gumzo na marafiki wao. Nyumba yangu imekua mtandao wa kijamii . Mimi Yesu Kristo, Bwana wenu sitawanyakua wale wanaoutumia muda wao mwingi kuitazama televisheni au katika kuvisoma vitabu vya riwaya na mambo mengine.Kwa sababu wamezigeuza riwaya hizi pamoja na mafunzo ya kisayansi kuwa washauri wao, badala ya kuwa na Roho Mtakatifu kama rafiki wao wa kweli tena bora. Muumini yeyote aliyesahau kumtafuta Roho Wangu Mtakatifu na amezifanya televisheni na itikadi zingine za kipepo kuwa marafiki wake wa dhati badala ya neno Langu ata achwa nyuma kukumbana na mpinga Kristu na alama ya mnyama muovu. 3 Mapepo yamefaulu kujiipenyeza ndani na katikati ya kanisa na kanisa leo limegeuzwa kuwa na tabia na itikadi za kipepo, badala ya kuwa na neno Langu na tabia zangu Mimi Bwana Yesu. Kanisa kama hili lita achwa nyuma. Wale waishio maisha yao wakiitangaza miili yao kwa kuvaa miundo ya nguo iliyo chafu na isiyokuwa ya heshima, wakiiweka wazi na kuionyesha matiti yao na kuifunua miili yao;huu bila shaka ni mfumo wa kidunia. Wakrsitu hawa wananiambia Mimi Mungu wao, Mungu , tayari nimekupa moyo wangu na hiyo imetosha. Kuhusu sehemu yangu ya nje, niache niitunze kwa kuvaa nipendavyo. Wacha ijulikane kweli kwamba tayari ni mekwisha waacha muishi na kuufurahia ulimwengu. Kwani hamfahamu kuwa Mimi ni Mungu aliye na wivu? Mimi nina wivi kwa ajili yenu lakini nyinyi mnanishiriki na ulimwengu, kamwe sitokubali hivyo. Muumini yeyote ambaye amenigeuza kitu cha kuchezea asemaye moyoni mwake; Mungu sio mbaya hadi hawezi elewa kwamba tunaishi katika karne ya ishirini na moja na kwamba sisi huishi jinsi tuishivyo. Wakati wa Nuhu uovu ulikuwa mchache kuliko sasa, wakati wa luti hapakuwa na uovu kama leo, kwa hiyo tubuni la sivyo hamtakuwa na udhuru. Mimi sitawachukua wale wanunuao,kuuza na kucheza michezo siku yangu takatifu ya kuabudu ya jumapili au jumamosi. Siku yoyote ile viongozi wenu wameweka kwa ajili ya kuniabudu Mimi ni sharti iwe Yangu pekee, Mimi ndiye Bwana. Siku hii lazima itakaswe kwangu pekee. Watu hawaniheshimu Mimi Bwana na Mungu wao. Wao huniambia na kubishana na watumishi wangu wa kweli wakisema hii ni sheria nasi tu katika wakati wa neema.Kwani Bwana wenu hawezi kuheshimiwa na kuogopwa? Kwani neema yamaanisha kumkosea heshima Mungu wenu? Nyinyi hubishana nami hata maombini namna vile mtabishana muunapo ujumbe huu. Mimi sitawachukua waongo,wenye kiburi, waumini wabatili ambao marafiki wao wakuu ni watu wa kawaida nao hujipotosha wenyewe na ulimwengu. Mimi Bwana na Mungu wenu nimewaamuru katika neno langu jitengeni kutoka miongoni mwao nanyi msijihusishe na kongwa zisizo sawa. Mimi sitawachukua wale waongezao maneno yao ndani ya ukweli , wale wawasengenyao watumishi wangu na wachungaji ambao hunitumikia kwa kweli na kulibeba neno langu. Ole wake Yule aongezae na kuondoa kutoka kwa neno langu la unabii ! Huu ndio msimamo wangu, kubalini au kataeni asema Bwana. Mimi Yesu mesia, Mungu wenu na hapana mwingine. Jitayarishe ,jitayarishe Mimi naja upesi!

No comments:

Post a Comment

AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1)

http://bit.ly/3JGDJ4d MWL. JAMES F. MZAVER Minister Truth 0762759621 jamesmzava@gmail.com              AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1) Ukuaji ha...