JINSI
YA KUTAMBUA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO
NA; JAMES F. MZAVA
Bwana Yesu asifiwe nipende
kukukaribisha tena katika somo langu jipya la jinsi ya kutambua kusudi la Mungu
ndani yako. Moja ya maswali yanayowatatiza watu wengi duniani na wameshindwa
kujua ni wao kutambua makusudi ya wao kuishi katika dunia hii. Wengi wamekua
wakiishi katika maisha ambayo sio yao halisi bali wamekua wakiishi kwa kuiga
iga maisha ya wengine jambo ambalo ni janga kubwa kwa mkristo kua hivyo. Ila
nipende kukutia moyo usikate tamaa kwa maswali uliyonayo hebu fatana nami
katika somo hili mwanzo hadi mwisho na nina Imani kua utapata kitu kikubwa cha
kukusaidia.
NINI
MAANA YA KUSUDI??
Watu wengi wameshindwa kuelewa
maana halisi ya maisha yao jambo liliwapekea kuishi maisha ya wengine. Ngoja
nikupe maana halisi ya kusudi
KUSUDI
~
Ni wazo au lengo lililowekwa ndani ya akili yako ili liwe kama malengo ambayo
kwa hayo yataweza kuongoza maishani ili kutimiza lile ambalo Mungu ameweka
katika maisha yako.
Hebu tuangalie Zaidi katika
Biblia inasema nini juu ya kusudi la Mungu katika maisha ya mwanadamu
aliyemuumba
Yeremia 1:4;10 4 Neno la Bwana lilinijia, kusema,
5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla
hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Na ule mstari wa 10 10 angalia,
nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na
kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.
Mungu anamwambia Yeremia kabla sijakuumba
nalikujua kwa maana nyingine Mungu anajaribu kumwambia Yeremia kwamba
nalitambua kabisa nilichokua nafanya pindi nilipokuumba. Ukiendelea ule mstari
wa kumi hapo juu Mungu anamwambia maana halisi yay eye kumuumba yaani kusudi
lake ni nini hasa kwa kumwambia Yeremia kwamba amemuweka kua nabii wa mataifa
hivyo kusudi kubwa la Yeremia kuwepo duniani yamegawanyika katika sehemu kuu
mbili. Kusudi la kwanza Mungu anamwambia amemuweka kua nabii juu ya mataifa na
kusudi la pili amewekwa kua juu ya mataifa na kazi yake halisi ni kung’oa, na
kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.
Lakini nikwambie siri kubwa iliyofichika hapa
Mungu kabla hajamweka Yeremia kua nabii wake kwa mataifa kulishakua na kusudi
ambalo Mungu alilokwisha kuliweka kabla ambalo aliliona kabisa halitaweza
kufanikiwa pasipo kumuumba mtu ili alitimize.
Hivyo basi tambua kabisa kabla Mungu hajakuleta
hapa duniani alikwisha kuumba kusudi lako ili uweze kuishi kwalo. Yaani wewe
kuishi kwako sio kwa sababu ya kitu kingine ila unaishi duniani kutokana na
kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako. Kwa maana nyingine ni kama hakuna
kusudi hakuna mtu pia, maana Mungu hawezi kumuumba mtu bila kuweka kazi yake
kabla ya kumuumba
KUWEPO KWAKO NI KWAAJILI YA KUSUDI AMBALO MUNGU
ALILIUMBA HATA KABLA YAKO WEWE KUUMBWA; PASIPO KUSUDI HAKUNA MTU.
(No purpose no man)
Nipende pia kukwambia kua Mungu alimpa Yeremia
uwezo hata kabla hajazaliwa ili aziangushe falme na huu uwezo si kwa ajili ya
Yeremia ila ni kwaajili ya kusudi la Mungu. Jifunze hapa kuwa upo uwezo ulionao
juu ya maisha yako si kwa sababu Mungu alikupa ili uwe wako ila ni kwaajili ya
kusudi lake kwa maana Mungu hawezi kumpa mtu kusudi pasipo kumpa uwezo na
mamlaka juu ya falme na mazingira anayoishi
TAMBUA NDANI YA KUSUDI LAKO UPO UWEZO NA MAMLAKA
YA KUAMURU NA KUBADILISHA MAZINGIRA PINZANI JUU YA MAISHA YAKO NA HII SI KWA
SABABU YA WEWE MWENYEWE ILA NI KWAAJILI YA KUSUDI LAKE MUNGU MWENYEWE.
Ngoja nikwambie kitu tambua kwamba mazingira unayoishi
hata kabla hujazaliwa Mungu alishapanga uwepo hapo ili kufanikisha mpango wake
mahali hapo.wengi wamekua wakiogopa mazingira wanayoishi kwa kuyaona ni magumu
nipende tu kukwambia kwamba kukimbia mazingira unayoyaishi sasa sio njia ya
wewe kufanikiwa bali ni kukimbia kusudi
na majukumu ambayo Mungu alikuumbia kwayo.
Mungu alifahamu kabisa mazingira ambayo atakuweka
kwamba utakutana na falme na ngome za adui, anaelewa mapepo, vita ambavyo
utapambana navyo, mapepo ambayo utambana nayo lakini nikwambie kabisa ni lazima
ushinde iwapo utajifunza kuishi na kukaa ndani ya kusudi la Mungu haijalishi
majaribu ni makali kiasi gani ila mwenye kusudi unao upako ndani yake hata
kabla yay eye kuumbwa maana lilianza kwanza kusudi la Mungu ndani yake hata kabla
yake, hivyo ndani yako ipo nguvu na uwezo ambao una uwezo wa kutosha kupambana
na kila aina ya changamoto unazopitia.
Hebu anza kujiangalia sasa kwa upya tena katika
maisha yako, vitu vinavyokuzunguka, vita pamoja na mapambano ya Ibilisi
unayokumbana nayo kila siku hayataweza kukushinda ila utayashinda wewe,
hayataweza kukumaliza bali utayamaliza wewe kwa sababu upo kwenye kusudi lake.
JINSI YA KUTAMBUA KUSUDI LAKO
pamoja na yote hayo niliyokufundisha apo awali
hayataweza kukusaidia vizuri kama hadi sasa hujajua kusudi la Mungu juu ya
maisha yako. Tunapokuja katika swala la kutambua kusudi lako sio kazi rahisi
sana, wengi wetu wamekua wakifanya kila aina ya huduma lakini bado wanaona
wanapwaya, wengine wamejaribu kufanya biashara lakini bado wanapwaya, kila
wanachojaribu kukifanya katika maisha yao wanaona bado kuna kitu kinawadai ambacho bado wanatakiwa kukifanya (kusudi)
lakini pamoja na jitihada zao zote bado wameshindwa kujua ni nini hicho ambacho
kimekosekana kwao
wengine wanaona kupata pesa pamoja na mafanikio
ndio kujua kusudi lako kwenye maisha yako kitu ambacho si sahihi. Ngoja
nikwambie pesa na mafanikio ni matokeo ya ujira baada ya mtu kufanya kazi
Fulani aliyopewa. Hivyo huna haja ya kujisumbua sana juu ya hayo hebu anza sasa
kutimiza kusudi lake kwanza ndani yako alafu utaona kama mungu hatalipia kusudi
lake
KAMA UKITUMIKA KWA UAMINIFU JUU YA KUSUDI LA
MUNGU KWAKO BASI KUA TAYARI KWA MAFANIKIO MAANA KUSUDI LA MUNGU KWAKO LINALIPA
KWA YULE ALIYELITAMBUA NA KULIISHI.
Ili uweze kujua upo ndani ya kusudi la Mungu ni
lazima kiwango cha Amani yako kiendane na kiwango cha kusudi ambalo Mungu
ameliweka ndani yako.
Ngoja nikwambie kwamba lipo jambo umewahi
kulifikiria kulifanya au tayari umekwishalifanya na ukasikia Amani ndani ya
moyo wako hata kama unaliona kama dogo tambua kua hilo ndilo kusudi la Mungu
kwako, na uwe na uhakika si kwamba Mungu atakupa Amani peke yake bali atakupa
pia uwezo, nguvu na mamlaka ya kuweza kupambana na mazingira unayoyapitia na
hajalishi ni magumu kiasi gani lakini ni lazima utayashinda maana Mungu
hakuumba kusudi ndani yako ili lishindwe.
KUSUDI LAKO LINATEGEMEANA SANA NA KIWANGO CHA
AMANI UNAYOISIKIA MOYONI MWAKO NA KWA LOLOTE UNALOLIFANYA KWENYE MAISHA YAKO
Je unasikia Amani kiasi gani unapofanya ilo
unalolifanya sasa? Kama kiwango cha Amani yako ni kidogo kwa unalolifanya sasa
au hapo nyuma basi tambua bado hujatambua kusudi la Mungu ndani yako. Anza
kubadilisha sasa ilo unalolifanya sasa ambalo linakunyima Amani na fanya kile
ambacho unapata Amani moyoni mwako n ahata kama kwa mazingira ya nje watu
wanaweza kuliona ni dogo we jitahidi kulifanya maana katika hilo Mungu ataanza
kukubariki katika hilo.
Nipende tu kukwambia zipo hatua kuu mbili ili
mwanadamu aweze kufikia makusudi ya Mungu kwenye maisha yake ambayo ni kama
ifuatavyo;
1. Ni lazima mwanadamu ampokee Yesu maishani mwake
kama Bwana na mwokozi wa maisha yake. Ilo ndilo jambo kuu muhimu zaid katika
maisha ya kila mwanadamu kwasababu unapompokea Yesu kwenye maisha yako huo ndio
mwanzo wa wewe kutambua kusudi lako kwa maana Yesu ndiye aliyetuumba pamoja na
Mungu baba (Mwanzo 1:26) sasa endapo tutarudi kwake kwa njia ya toba tutafungua
mlango wa yeye kuingia ndani ya maisha yetu na kuanza kutufundisha nini kusudi
lake katika maisha yetu. Kumbuka wewe hukujiumba wewe ila Mungu ndiye
aliyekuumba na hakukuumba tu ila alikupa kazi na makusudi yaw ewe kuwepo ila
kitu ambacho kimekupotezea kusudi lako ni dhambi unazofanya, hivyo basi hatua
ya mwanzo ya wewe kutambua kusudi ni wewe kurudi kwa Mungu kwa njia ya toba ili
Mungu aweze tena kukuonesha kusudi lako katika maisha yako ni lipi hasa.
UBARIKIWE SANA
Itaendelea….
Imeandaliwa na kuandikwa na; James
F. Mzava
Simu namba ; 0756259621
Barua pepe; jamesmzava@gmail.com