FAIDA ZA
KUSOMA NENO LA MUNGU KATIKA MAISHA YA MWAMINI
Sehemu
ya kwanza (1)
Na;
James F. mzaver
NINI MAANA YA NENO LA MUNGU.
Naam twende moja kwa moja katika somo letu hapo juu kabla
kabisa hatujajua umuhimu na faida za neno lazima basi tuweze kuelewa maana ya
neno la Mungu ni nini.
NENO LA MUNGU ~ Ni ujumbe wa kiungu kwa
wanadamu wenye lengo la kuwaokoa, kuwafundisha, kuwaonya, kuwaadibisha katika
makosa yao ili kuwafanya wawe wakamilifu katika Kristo.
NENO
LA MUNGU~ Ni Mungu
mwenyewe na ni Yesu mwenyewe, na ni uzima na uzima ni nuru yetu.
Unaposoma neno unaanza
haya madaraja manne kwanzia kwa Mungu mwenyewe hadi neno linakua na manufaa
kwako yani kuwa nuru yako. Na neno nuru Kiebrania limemaanishwa kama maendeleo
ya watu. Yaani unapozidi kulisoma na kulijua hatima yako ni lazima uendelee
kimaendeleo.
Neno la Mungu kiini
chake ni kutupa uzima tulioupoteza tulipofanya dhambi, na uzima huu ni
kufunuliwa kwa neno lake kwetu. Mtu anapoishi maisha ya mafunuo ya neno la
Kimungu katika maisha yake ni lazima afanikiwe (NASEMA TENA NI LAZIMA
AFANIKIWE)
Yaani maana yake ni hii; MUNGU=NENO=YESU=UZIMA=NURU YA WATU
Yohana
1:1-4
Hapo mwanzo kulikuwako
Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo
alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote
vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
4 Ndani yake
ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
Si hivyo tu katika
Biblia zipo tafsiri mbalimbali zinazoelezea maana ya neno la Mungu na katika
maandiko mengine neno la Mungu likifananisha kama vitu vingine katika lugha ya
picha kama vile upanga (Waebrania 4:12),
neno la Mungu kama taa (Zaburi 119:105), neno la
Mungu kama Kristo Yesu (Yohana 1; 1-4),
neno la Mungu kama vazi (Ufunuo 19:13)
neno la Mungu kama kweli (Yohana 17; 17)
na kadhalika.
Sasa katika sehemu yetu hii ya kwanza tuangalie mfano ambao
Bwana Yesu aliutoa juu ya neno lake
tuangalie (Marko 4:1-20; 21-24,35)
1 Akaanza kufundisha tena
kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkubwa mno, hata yeye akapanda
chomboni, akakaa baharini, mkutano wote ulikuwako juu ya nchi kavu kando ya
bahari.
2 Akawafundisha
mambo mengi kwa mifano, akawaambia katika mafundisho yake,
3 Sikilizeni;
Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda;
4 ikawa
alipokuwa akipanda, mbegu nyingine ilianguka kando ya njia, wakaja ndege
wakaila.
5 Nyingine
ikaanguka penye mwamba, pasipokuwa na udongo mwingi; mara ikaota kwa kuwa na
udongo haba;
6 hata jua
lilipozuka iliungua, na kwa kuwa haina mizizi ikanyauka.
7 Nyingine
ikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea ikaisonga, isizae matunda.
8 Nyingine
zikaanguka penye udongo ulio mzuri, zikazaa matunda, zikimea na kukua, na
kuzaa, moja thelathini, moja sitini, na moja mia.
9 Akasema, Aliye
na masikio ya kusikilia, na asikie.
10 Naye alipokuwa
peke yake, wale watu waliomzunguka, na wale Thenashara, walimwuliza habari za
ile mifano.
11 Akawaambia,
Ninyi mmejaliwa kuijua siri ya ufalme wa Mungu, bali kwa wale walio nje yote
hufanywa kwa mifano,
12 ili wakitazama
watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na
kusamehewa.
13 Akawaambia,
Hamjui mfano huu? Basi mifano yote mtaitambuaje?
14 Mpanzi huyo
hulipanda neno.
15 Hawa ndio walio
kando ya njia lipandwapo neno; nao, wakiisha kusikia, mara huja Shetani,
akaliondoa lile neno lililopandwa mioyoni mwao.
16 Kadhalika na
hawa ndio wapandwao penye miamba, ambao kwamba wakiisha kulisikia lile neno,
mara hulipokea kwa furaha;
17 ila hawana
mizizi ndani yao, bali hudumu muda mchache; kisha ikitokea dhiki au udhia kwa
ajili ya lile neno, mara hujikwaa.
18 Na hawa ndio
wale wapandwao penye miiba; ni watu walisikiao lile neno,
19 na shughuli za
dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga
lile neno, likawa halizai.
20 Na hawa ndio
waliopandwa penye udongo ulio mzuri; ni watu walisikiao lile neno na kulipokea,
na kuzaa matunda, mmoja thelathini, mmoja sitini, na mmoja mia.
21 Akawaambia,
Mwaonaje? Taa huja ili kuwekwa chini ya pishi, au mvunguni? Si kuwekwa juu ya
kiango?
22 Kwa maana
hakuna neno lililositirika, ila makusudi lije likadhihirika; wala hakuna
lililofichwa, ila makusudi lije likatokea wazi.
23 Mtu akiwa na
masikio ya kusikilia, na asikie.
24 Akawaambia,
Angalieni msikialo; kipimo kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa, na tena
mtazidishiwa.
Yesu anawaambia wanafunzi wake juu ya mfano wa neno la Mungu
kwao, japo unakua vigumu sana kwa wanafunzi kuelewa maana ya mfano ule hadi
pale Yesu alipoanza kuwafafanulia maana ya mfano wa Mbegu akiwaambia kua mbegu
ni Neno la Mungu.
Lakini tujiulize swali kwa nini wanafunzi wa Yesu hawakuweza
kuelewa ule mfano?
JIBU – kwa sababu neno la Mungu ni siri si kila mtu
amejaliwa kutambua siri hiyo. (angalia mstari wa 11-13)
NENO LA MUNGU NI SIRI SI KILA MTU AMEJALIWA KULIELEWA,
UNAPOSOMA NENO OMBA KWANZA ROHO MTAKATIFU AKUPE ROHO YA UFUNUO ILI UELEWE USIWE
KAMA WANAFUNZI WA YESU WALIOSHINDWA KUELEWA (WAEFESO 1:17)
Hivyo kama neno la Mungu ni siri tambua kuokoka haitoshi na
kusoma neno hakutoshi kama huna Roho ya ufunuo ili kuweza kuelewa kile ambacho
kimeandikwa ili kikusaidie kuendelea.
Tambua kibiblia kwa sisi tuliokoka ili tuweze kuishi na
kuenenda katika maisha haya ni lazima kila siku tupate neno jipya katika kinywa
cha Bwana, vinginevyo hatuwezi kuishi na kustahimili bila neno. Biblia inasema
kua neno lake ni chakula; kama vile miili yetu haiwezi kuishi bila vyakula
hivyo basi tambua kua hata wewe uliyeokoka huwezi kuishi bila neno la kutosha
(la kushiba) katika maisha yako. Sababu kubwa ya wakristo kurudi nyuma ni
kutosoma neno, sababu kubwa ya wakristo kua na utapia mlo wa kiroho ni kwa
sababu ya kutokua na neno la Mungu la kutosha katika maisha yao ivo ni rahisi
kuchukuliwa katika mafundisho potovu na manyonge.
TAMBUA KILA TAARIFA UNAYOISIKIA NA KUIIFADHI NI CHAKULA.
Ndio mwanadamu ni muunganiko wa vitu vitatu; Roho, Nafsi na
mwili na vyote hivi ili viishi lazima vipate chakula sahihi Roho yako ili iishi
ni lazima ipate neno na muunganiko way eye aliyekuumba yaani Mungu (Yohana 4:23) inapokosa ivyo Roho yako
imekufa hata kama bado unaishi kama huna neno na huna Mungu wewe ni maiti
kiroho unayetembea.
Nafsi yako inahitaji taarifa sahihi zenye maarifa ili nafsi
iishi lazima mtu wa Mungu uwe makini na yale unayoyasikiliza na kujifunza iwe
ni kwa kuona au ata kusikia maana apo ndivyo vyakula vya nafsi yako. Kwa kadri
unapozidi kusoma neno unalisha nafsi yao pia, ndani yako kunakua na uzima si wa
rohoni tu hadi kwenye nafsi yako. Ila kama unajifunza mambo ya kiovu ndivyo
unavyoua nafsi yako katika mambo ya Kiungu.
KADRI UNAPOSOMA NENO NDIVYO KADRI UNAZIDI KUA NA AFYA YA NAFSI
YAKO PIA; UTAWAZA VYEMA, UTATOA MAAMUZI SAHIHI, NA KUA NA MIPANGO SAHIHI.
Turudi kwenye andiko letu la Marko 4 tuendelee kujifunza Zaidi juu ya neno la Mungu kwetu.
Tuangalie mstari wa 33
33 Kwa mifano mingi ya namna hii alikuwa
akisema nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulisikia;
NENO LA MUNGU
LINAENDANA NA KUSIKIA
Tambua kiwango cha neno la Mungu
kutenda kazi katika maisha yako kinategemeana na kiwango unachosikia.
Angalia vizuri mstari wa 33b
anasema kwa kadiri walivyoweza kusikia ndivyo kadiri alivyosema nao neno lake.
Sasa hutaweza kuelewa Zaidi kama sijakupeleka kwenye kitabu cha Warumi tujua
uku kusikia kukoje.
Warumi 10:17
Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la
Kristo.
Ooh kumbe kusikia uku Yesu
alikokua anakusema ni kusikia kwa njia ya Imani, inamaana Imani ni mlango unaoachilia
kiwango cha neno la Mungu katika maisha yako
Inamaana mtu mwenye mafunaa juu
ya neno la Mungu ni yule mwenye kiwango kikubwa cha kiimani, namaanisha kwa
kadiri Imani yako ilivyo ndivyo kadiri ya kiwango utakachoelewa neno lake.
Ngoja nikwambie ni vigumu sana
Mungu kusema nasi kwa sauti yake kupitia neno lake kama hatuna Imani
inayotufanya kusikia.
UNAPOKOSA IMANI UNAKUA MLEMAVU WA
KIROHO.
Labda hujanielewa Biblia
inatwambia kua Imani ni kua na uhakika juu ya mambo yatarajiwayo ni bayana ya
mambo yasiyoonekana (Waebrania 11:1)
Unaposoma au kusikia neno la Mungu jifunze jinsi ya kujenga Imani yako ya sasa
na baadaye ili neno la Mungu liweze kuzaa matunda katika maisha yako.
Turudi kwenye andiko letu la Marko 4 juu ya zile mbegu na maana
zake.
Pale tunaona maeneo manne tofauti katika mbegu ilipopandwa tuangalie maeneo hayo;
Pale tunaona maeneo manne tofauti katika mbegu ilipopandwa tuangalie maeneo hayo;
- 1 kando ya njia
- 2. penye mwamba
- 3. penye miiba
- 4. penye udongo mzuri
Biblia inatwambia katika kila
eneo kulikua na changamoto lakini cha ajabu wote walisikia angalia mistari ya (15, 16, 18 na 20) Biblia unatwambia kila
eneo lilipopandwa mbegu katika ufafanuzi
kila mtu aliweza kusikia ila matokeo hayakua sawa.
Kwaiyo ngoja nikufundishe kitu
hapa kusikia tu haitoshi ni hatua ya mwanzo ya
neno la Mungu na hapa shetani anaweza kukurusu ukasikia lakini asikupe
nafasi ya kukuza kile ambacho umekisikia. Mbegu inaweza kupandwa na shetani
asikusumbue kupandwa kwa ile mbegu ila shida yake ni kuangalia eneo ambapo
mbegu imepandwa kama ni kwenye udongo mzuri shetani huleta vita ili kusudi
akuhamishe katika miba, mwamba na kwenye njia ili usiweze kuzaa matunda ya neno
na hata kama ukizaa basi uzae kwa kiwango pungufu.
TAMBUA ILI MBEGU AU NENO LA MUNGU
LIWEZE KUZAA NI LAZIMA UWE KATIKA ENEO SAHIHI
Tambua eneo sahihi hapa ni mazingira
pale unapolipokea lile neno kunategemeana sana na eneo unapolishwa, unapolipokea
na kulisoma neno. Mazingira ayo yakiwa si sahihi tambu hutaweza kuzaa au kuona
manufaa ya neno katika maisha yako na hata kama ukiyaona utayaona kwa kiwango
kidogo sana.
UBARIKIWE SANA !!
Itaendelea …
IMEANDIKWA NA KUANDALIWA NA; JAMES F. MZAVER
MAWASILIANO; 0762759621
BARUA PEPE; Jamesmzava@gmail.com