Saturday, November 14, 2015

TAFSIRI NA ALAMA MBALIMBALI KWENYE NDOTO

TAFSIRI NA ALAMA MBALIMBALI KWENYE NDOTO

Na James F. Mnzava




Bwana Yesu asifiwe sana.Nikukaribishe tena kwenye somo jipya la tafsiri na alama mbalimbali katika ndoto.Ndoto nyingi zimekua kama mafumbo makubwa yanayowatatiza sana watu kwenye ulimwengu huu wa sasa hasa linapokuja kujua maana na tafsiri ya vile walivoota.Fatana nami katika mfululizo huu ili uweze kupata kitu cha kukusaidia.


NINI MAANA YA NDOTO
Kwanza kabisa tuanze kujua nini maana ya ndoto;maana watu wengi wamekuwa wakiwapotosha wengine kwa tafsiri ambazo sio sahihi.

NDOTO ~ ni mfuatano/mtiririko wa picha,mawazo, na mihemko ya hisia ambazo kikawaida hutokea katika ufahamu pindi mtu anapokuwa amelala.


Na mara nyingi ukubwa wa ndoto huanzia sekunde hadi dakika 20-30 kwa ndoto;na ni mara chache sana mtu kuota Zaidi ya muda huo japo wapo wengine wanaoota ndefu Zaidi.

Nimekua nishangaa sana na kuvunjika moyo sana hasa ninaposoma baadhi ya vitabu pamoja na majarida mbalimbali na mafundisho yanayopotosha maana na tafsiri ya ndoto kwa watu;jambo ambalo linazidi kuwapoteza watu siku hadi siku.Watu hao wamekua wakiandika tafsiri za uongo na kuwadanganya watu kuhusiana na vitu mbalimbali kama picha,rangi,wanyama na vinginevyo na kuwapa tafsiri ya vitu hivyo vitu ambavyo huwapoteza kabisa watu.


Nipende tu kuwaambia na kuwa kila ndoto inayoiota huwa na maana na pia huwa na tafsiri yake kutokana na mazingira unayoishi pamoja na ufahamu wako kiroho.Namaanisha kuwa unaweza ukaota ndoto inayofanana kabisa na mtu mwingine lakini tafsiri zikatofautiana kutokana na mtu na mtu na pia mazingira mnayoishi.

Ndoto ni njia maalimu sana ya Mungu kuwasiliana nasi.Unapoota unakuwa kimya na vitu vyote vinakuwa katika hali ya utulivu;hivyo huwezi kukwepa mawasiliano hayo na Mungu,pia ni kipindi ambacho panakua hakuna usumbufu wowote mwili unakua umepumzika kazi inabaki kwenye ubongo na ufahamu wako kufanya kazi kifanisi Zaidi kuliko mchana. Wengine huweza kuzidi hapo ila asilimia

Na pia kikawaida mtu wa kawaida huweza kuota ndoto tatu hadi tano kwa usiku mmoja kwa asilimia kubwa hua hivyo

Nimelihakikisha hili;Mungu hutumia kipindi hicho kuzungumza mambo ya ndani sana ya kuashiria mambo yaliyopo na yatakayokuja baadaye.


 Ayubu 33:14-15 14  Kwa kuwa Mungu hunena mara moja, Naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali.
15  Katika ndoto, katika maono ya usiku, Usingizi mzito uwajiliapo watu, Katika usingizi kitandani;

Mara zote Mungu husema nasi lakini tatizo hatujali na kuelewa maana ya kile anachokisema kwetu sawa sawa na mstari wa 14

Sababu kubwa ya mtu kukumbuka ndoto au kile alichokiota kwa kushtuka;kwa sababu unapokuwa kwenye ndoto kuna hatua kama nne (four stages) za kulala ambazo katika hatua mojawapo iitwayo (REM)~rapid eye movement hii ni aina mojawapo katika zile hatua nne za usingizi katika kulala;Ambapo hapa sasa ubongo huwa katika hali ya juu sana katika kufanya kazi huku mwili ukiwa katika ganzi ya kutojitambua,ndipo kitendo cha (REM)  hufanyika yaani macho huzunguka zunguka kwa kasi.Hapa huashiria mtu huota ndoto.

Sasa kama mtu anaweza kuamka baada ya (REM) Ni lazima ndoto hiyo ataikumbuka;au baada ya kila (REM)

Nadhani hadi hapo utakuwa umepata picha kidogo juu ya ndoto jinsi inavyotokea;ambapo tumeona hutokea katika kipindi cha (REM) ~hatua mojawapo ya usingizi.
Pia mtu yeyote asije akakwambia kwamba haoti ndoto kwa sababu kitendo cha mwanadamu kufunga macho na kuanza kulala huanza kuota tatizo kubwa tu hapo ni kusahau kile alichokiota.

Na kama nilivotangulia kusema hapo awali kuwa mwili hauwezi kupokea mambo ya rohoni(ndoto) wakati mtu anapoamka ndio maana watu wengi wanaota lakini wanasahau kwa sababu ya utofauti kati ya mwili na roho.

KWA NINI WATU WENGI HUSAHAU WALICHOKIOTA?
Hili ni swali ambalo wengi wamekuwa wakijiuliza sana ni kwa nini pindi wanaota ndoto usiku wanapoamka asubuhi huwa wameshasahau kile walichokiota;Usijali ngoja nikwambie wakati tunapolala ubongo huwa active sana na hufanya kazi kubwa kuliko kipindi kile ambacho mtu anakuwa hajalala bado.Tatizo la kusahau ndoto linatokana na kutokuamka mara moja (kushtka,kuzinduka) wakati tunapoota yaani watu wanamazoea ya kulala na kuota pasipo kuamka pindi waotapo na kungoja hadi asubuhi waamke.Wakati ambapo roho zetu haziwi active tena kama kile kipindi tulichokuwa tunaota.
Ndio maana unaweza ukawa unaota ndoto nyingi katika usiku mmoja lakini ukajikuta unazisahau zote napengine ukawa unakumbuka kidogo tu ile ndoto uliyoota wakati wa mapambazuko.

Ngoja nikwambie jizoeze mazoea ya kuamka pindi uotapo ndoto yeyote pindi unapolala na kuiandika;weka daftari yako maalumu kwa ajili ya ndoto ambapo kila ndoto ambayo utakuwa unaota uweze kuiyandika.
Maana
KUMBUKA HAKUNA NDOTO YEYOTE UNAYOIOTA AMBAYO HAINA MAANA,KILA NDOTO UNAYOOTA NI UJUMBE WENYE MAAGIZO NA MAELEKEZO TOKA KWA MUNGU ANAYOKUPA KATIKA KUKUONGOZA MAISHANI.

KumbukaPindi tunapoenda kulala roho zetu zinakua active sana kuliko miili yetu

MUHIMU;Pindi unapoenda kulala ni vizuri kulala na kidaftari kidogo(notebook) na kua na tabia ya kuamka Zaidi ya mara tatu kwa usiku mmoja.Itakusaidia kutoweza kusahau ndoto unazoota

Kumbuka pia wakati unapoenda kulala sio tu unalala bali unaenda kufanyia kazi hatima yako kupitia roho yako kwa njia ya ndoto.

Kulala si kitendo cha kupumzika,bali ni kitendo na mlango wa kwenda kwenye malengo yako usisahau hilo siku zote.

NIkukumbushe tena kuwa ndoto zote unazoziota zenye kuanzia usiku wa manane kwenda alfajiri huwa na maana sana na Mara nyingi Mungu hutumia muda huo kusema na watoto wake;ni vyema kutosahau hilo

Shetani haogopi kwa sababu tunaota ndoto,bali huogopa kitendo cha sisi kuamka pindi tunapomaliza kuota ndoto kwa kuunganisha mawasiliano yetu kati ya mwili na roho ili iweze kufanya kazi na tuweze kukumbuka kile tunachokiota.
Mtu ambaye amejizoesha kuamka pindi aotapo ndoto huwa hatari sana kwa shetani kwa sababu huwa na kumbukumbu zote;na kumbuka kama nilivosema hapo juu kwamba ndoto ndizo zilizobeba hatima ya maisha 
yako,mafanikio,kuendelea na namna ya kuishi maishani ni muhimu sana kulielewa hili kwa kuwa mwangalifu sana kwa kile unachoota kila ulalapo.

Pia nipende kuwaambia wale watu ambao mara nyingi hupuuzia ndoto zao na kutokuamka na kuanza kuomba kwa kile walichokiota shetani huwa hana haja na watu hao kwa sababu hatima zao zipo mikononi mwake.

Mara nyingi kwenye Biblia Mungu amekuwa akiitumia njia ya ndoto kama njia yake kubwa ya kuongea na wengi hasa wale ambao hawakuteuliwa katika kazi maalumu kama unabii au ukuhani;na hii ni kwa sababu ndoto ni haki ya kila mkristo

Yoel 2:28 28  Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono;ya wote

Usichanganyikiwe hapa Mungu ndiye chanzo cha ndoto zote tunazoota lakini sio ndoto zote hutoka kwake.

AINA ZA NDOTO

1.      NDOTO ZITOKAZO KWA MUNGU.Kama nilivosema hapo awali Mungu pia hutumia njia ya ndoto kuwasiliana nasi pindi tunapokua tumelala(Ayubu 33:14-16,Yoel 2:28) Hizi ndoto za aina hii mara nyingi huleta msisimko ndani ya roho na nafsi pia kuashiria jambo jema au baya na mara nyingi ni ndoto zinazokua na mapambano Zaidi kwani shetani hutaka sana kukusahaulisha kile ambacho Bwana alikuotesha.


2.    NDOTO ZITOKANAZO NA SHUGHULI NYINGI ZA SIKU.Hii ni hakika kabisa na ndivo ilivyo hasa kwa watu waliozoea sana kufanya shughuli moja mda mrefu mara nyingi huota mambo waliokua wanafanya kwa siku nzima;nimewahi kuona mtu anaota ndoto huku akiwa anacheka na kuongea na nilipofuatilia Zaidi mtu yule mchana alikua anaongea sana na kucheka.Hapo ubongo hufanya kazi ya kukumbusha na kurudia kile ulichofanya,kusikia na kuona katika shughuli zako za kila siku


3.    NDOTO ZITOKAZO KWA SHETANI.Zipo ndoto zitokazo kwa shetani adui wa nafsi zetu ambazo mara zote huwa na mifadhaisho na kuogofya sana na mara nyingi ndoto hizi hazisahauliki kwa sababu shetani huhitaji sana kuharibu hatima yako ndio maana ni vigumu sana kusahau.(1 Samweli 28)
.

JINSI GANI UTAWEZA KUTUNZA NA KULINDA NDOTO ZAKO

1.      JIFUNZE KUOMBA ~Jenga mazingira ya kuomba mara kwa mara pindi unapoota ndoto ya aina yeyote iwe imetoka kwa Bwana au kwa shetani huna budi kuziombea maana zote huwa haziji bure.Na pia ni muhimu kabla ya kulala uombe ili Mungu akuwezeshe kujua maana ya tafsiri juu ya kile ulichokiota;ili kisipotee bure



2.    MSIKILIZE MUNGU~Chukua muda wako wa kutosha na wa utulivu kwa ajili ya kumsikiliza Mungu juu ya kile ulichokiota na pindi unapohisi Amani moyoni mwako ni njia mojawapo ya Mungu kuridhia kile ulichokiona.Ndoto inayokupa Amani na kukupa utulivu inakupa ujue kabisa ndoto iyo imetoka kwake;maana kumbuka ni Mungu mwenyewe ndiye anaweza kutupa Amani juu ya yale tunayoyaota.(Mathayo 2)


3.    JIFUNZE KUANDIKA NDOTO ZAKO~Kama nilivotangulia kusema jenga mazingira ya kulala na daftari ili uweze kuandika kile unachokiota hii itakusaidia kuweza kukumbuka yale uliyoyaota na kuyapa muda ili yawe Dhahiri baadaye


4.    TAFUTA USHAURI TOKA KWA MUNGU~Watu wengi pindi waotapo ndoto huanza kuhangaika kwenda kwa watu mbalimbali ili kupata tafsiri(Mwanzo 41) Jambo ambalo sio zuri kwa Bwana maana ndoto husiana na hatima binafsi ya mtu wala sio kwa wengine penda kumuomba Mungu ili aweze kukupa tafsiri juu ya kile ulichoota.Pia Mungu huweza kukuongoza pia kwa mtumishi wake kwa ajili ya kukupa tafsiri jua inategemea sana kwa Amani utakayoiskia pale unapopewa tafsiri.


5.     SUBIRI NA ACHA ITOKEE~Baada ya kufanya mambo hayo hapo juu unapaswa kusubiri mapenzi ya Mungu yatokee kwa yale uliyoyaota.Kumbuka ndoto nyingi huwa wazi na kweli ila kuwa mwangalifu Zaidi katika ndoto zile ambazo zinakaa Zaidi kwenye ufahamu wako na haziondoki kwa haraka.


ALAMA MUHIMU KATIKA NDOTO

·        FARASI~Anaashiria mtu;hali ya maisha yake na roho yake pia (Mathayo 7:24-27 ,2Timotheo 2:20-21)
·        Samaki~Watu
·        Majani makavu~Kuchakaa na kuwa ukiwa
·        Majani mabichi~Neema na ustawi
·        Ngazi~Kuongezeka,kukua mafanikio
·        Mbuzi~Ulafi
·        Mbwa~uzinzi
·        Kondoo~Unyenyekevu,upole
·        Mkono~Bwana atatenda makuu kwa mkono wake
·        Maji~neema,kurudhika na kuendelea
·        Daftari na kalamu~Elimu na mafunzo mbele yako
·        Kuku~papara na kuhangaikia mambo yasiyokuhusu
·        Mwewe mweusi~Mkuu wa anga wa eneo
·        Paka~uchawi wa eneo
·        Nyoka~Njama,shetani,Ibilisi,Njama
·        Kipara~werevu,uzamani,wingi wa maarifa
·        Nzige~uharibifu,hasa wa kipawa au huduma
·        Asali~uponyaji,ulinzi na uzuri
·        Unapoona ulimi upo nje ya kinywa~roho ya usengenyaji,umbea,kugombanisha
·        Unapoota unaumwa na kichwa~wachawi na wanga wamekushambulia
·        Unapoota unatembea lakini hufiki~Jambo unalolofanya sasa linakupotezea muda fanya jambo jingine achana na hilo.
·        Unapoota umezaliwa tena~Bwana anakufanya upya hasa katika matendo yako(kubadilishwa)
·        Unapoota unaitwa na mtu usiyemjua~Roho ya mauti
·        Unapoota watu waliokufa wanakuita~Maagano,mauti
·        Unapoota unafanya mapenzi na ndugu yako wa kuzaliwa~Uhusiano wako na ndugu yako utaharibika muda sio mrefu,pia utapata aibu
·        Unapoota unalia na hakuna anayekufariji~Huna uhusiano mzuri na watu
·        Unapoota ndugu wako wa karibu amekuja kukutembelea na kukuaga~Roho ya mauti ipo juu yake
·        Unapoota upo mbele za watu wengi wanakusikiliza~Bwana atakutukuza na kukujulisha mbele za wengi
·        Ukiona nyumba/chumba kipya~ Huashiria mawazo chanya;huduma na maisha mapya katika eneo jingine jipya
·        Unapoota upo uchi~Aibu;mambo yako yatakuwa hadharani na kuonekana,kuwa mwangalifu katika siri zako kwa watu
·        Unapoota unaoa au kuolewa~Bwana ameona upweke na ukiwa wako atakupatia mtu wa kuwa na wewe maishani
·        Unapoota unavuka mto lakini umelowana ~Jaribu unalopitia utalishinda ila kwa taabu nyingi,Lakini utavuka
·        Unapoota umelala na mtu wa jinsia ambayo sio yako~Kuwa mwangalifu na aina ya mahusiano uliyonaoyo yatapelekea kumkosea Mungu
·        Unapoota mti mkubwa uliostawi sana~Mungu atakuinua na kukufanya mkuu
·        Unapoota upo ziwani unavua samaki~Mungu atakufanya kuwa mvuvi wa watu;atakutumia kuwaleta watu kwake
·        Unapoota umeumwa na nyoka~Kuwa mwangalifu sana kwani adui atakushambulia
·        Unapoota unakimbizwa na watu usiowajua kwa nia ya kukudhuru na ukawazidi mbio~Uwe mwangalifu kwani shetani atatumia mapepo yake na wachawo kukushambulia lakini hawatakushinda.
·        Unapoota  unakula lakini hushibi~Roho ya kutotosheka na kutapanya mali
·        Unapoota umekatwa kichwa~Mamlaka yako yamehamishwa na kwenda kwa mtu mwingine.
·        Unapoota unavalishwa joho~Bwana atakufanya kuwa mpatanishi kwa wengine.
·        Unapoota shamba zuri limejaa mazao~Ni kipindi ambacho Mungu atakurejeshea kwa wingi mafanikio yako
·        Unapoota matunda yaliyoiva~Ni wakati wa mafanikio yako tayari
·        Unapoota mto mkubwa uliojaa mamba~Vikwazo na balaa vimewekwa mbele
·        Unapoota mlima mkubwa mbele yako~Jaribu mbele yako
·        Unapoota umekufa~Ni taarifa kwako kwa mambo uliyonayo yamekwisha.
MUHIMU
Nipende tu kuwaambia na kuwa kila ndoto inayoiota huwa na maana na pia huwa na tafsiri yake kutokana na mazingira unayoishi pamoja na ufahamu wako kiroho.Namaanisha kuwa unaweza ukaota ndoto inayofanana kabisa na mtu mwingine lakini tafsiri zikatofautiana kutokana na mtu na mtu na pia mazingira mnayoishi.

ZIPO TAFSIRI NYINGINE NYINGI SANA ILA KAMA UTAKUWA NA SWALI LOLOTE KUHUSU NDOTO USISITE KUWASILIANA NAMI KWA BARUA PEPE HAPO CHINI.


Imeandaliwa na kuandikwa na;                 JAMES F.MZAVA



                                           
                            jamesmzava@gmail.com 





29 comments:

  1. Asante.. Mungu akubariki.

    ReplyDelete
  2. Nini maama ya kuota unatapika?

    ReplyDelete
  3. Nimeota nimeumwa na nyoka kidoleni nikamtoa.

    ReplyDelete
  4. Mara nyingi hua naota kua nimekufa lkn naskia kinachoendelea ila cwezi fanya lolote.

    ReplyDelete
  5. Nimeona natoa vitu vichafu mdomini Kama vyakula vyakula flani hivi...ila syo kutapika kiivo.


    Nikaota nakimbizwa na vijana tulikuwa t unasoma nao, ila haeakunidhuru sema nlijificha sehemu ambako niliona kinyesi kikubwa saana. Nini hicho??

    ReplyDelete
  6. Nimeona natoa vitu vichafu mdomini Kama vyakula vyakula flani hivi...ila syo kutapika kiivo.


    Nikaota nakimbizwa na vijana tulikuwa t unasoma nao, ila haeakunidhuru sema nlijificha sehemu ambako niliona kinyesi kikubwa saana. Nini hicho??

    ReplyDelete
  7. Naaaan nimependa somo lakoteule wa Bwana,waweza kunipa namba yako pls kwa msaada zaidi?

    ReplyDelete
  8. Mara nyingi,naota nipo shuleni,
    2=nakimbizwa na watu
    3=nikifanya mapenzi
    4nakuvuka mto


    Jina rangu,Richard remmy
    Tl 0763504933

    ReplyDelete
  9. Naaaan nimependa somo lakoteule wa Bwana,waweza kunipa namba yako pls kwa msaada zaidi?

    ReplyDelete
  10. nimeota tupo watu wengi tunafukuzwa na mamba katika makazi yetu, na mmoja nikamuua lakin akaja mwingine na akatusumbua sana, lkn baadae nikiwa kweny harakat za kutafuta mbinu za kumuangamiza، yule mamba akatokea kunizoea... kutonizuru na alikuwa akipigana hata na mamba wengine wanajaribu kunidhuru

    ReplyDelete
  11. Mimi naota tunagombana na Mme wangu kila cku

    ReplyDelete
  12. Mimi niliota na simama katikati ya kondoo wengi.maana take ni mini?

    ReplyDelete
  13. Mimi niliota na simama katikati ya kondoo wengi.maana take ni mini?

    ReplyDelete
  14. Mimi niliota na simama katikati ya kondoo wengi.maana take ni mini?

    ReplyDelete
  15. Mtaalamu vp ukiwa unaota afu unashtuka shutka Kila unapoanza kuota ni tatiz gn

    ReplyDelete
  16. Mtumishi mi naota mama yangu amejufa nisaidiw

    ReplyDelete
  17. Mtumishi mi naota mama yangu amejufa nisaidiw

    ReplyDelete
  18. Mtumishi mi naota mama yangu amejufa nisaidiw

    ReplyDelete
  19. Naota mtumishi wa Mungu ananimwagiya mafuta kicwani mafuta mengi na akanambiya ni pige makoti aniombeye alafu akanambiya eti nisiludi kwayaleyote

    ReplyDelete
  20. Ubarikiwe ndugu,Mungu azidi kukuinua

    ReplyDelete
  21. Asante kwa somo zuri sana mtumishi.
    Yaani mimi ni muota ndoto. Huwa naota sana na kuna ndoto watu waliniotea,
    zinanichanganya sana. Nitakutafuta mtumishi. Ubarikiwe na Bwana Yesu!

    ReplyDelete
  22. Nimeota napanda mlima nilipotaka kufika nyumba yetu ikaanguka nika shuka.mlimani nika Anza zugumza na mzazi wg kike kwenye ndoto

    ReplyDelete

AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1)

http://bit.ly/3JGDJ4d MWL. JAMES F. MZAVER Minister Truth 0762759621 jamesmzava@gmail.com              AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1) Ukuaji ha...