Masaa 8 Mbinguni
na Ricardo Cid Bwana akasema, “Ninatuma ujumbe huu kwa watu wangu katika dunia,kwa sababu mimi niko hai katika
ulimwengu wa roho.”
Ufunuo 4:1
Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza
niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, Panda hata huku, nami
nitakuonyesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.
Ufunuo 5:11-12
Kisha nikatazama, nikasikia sauti ya malaika wengi sana, idadi isiyohesabika, maelfu na
maelfu. Walikuwa wamekaa kuzunguka kiti cha enzi, wale viumbe hai wanne na wale wazee;
wakasema kwa sauti kuu: “Mwanakondoo aliyechinjwa anastahili kupokea uwezo, utajiri,
hekima, nguvu, utukufu na sifa.”
Tafadhali, kanisa sikilizeni nini kilichotokea katika maisha yangu. Katika ndoto, Bwana alianza
kushughulika nami. Nakumbuka katika ndoto hiyo, Nilitembea nje ya nyumba yangu. Nilitembea katika
mitaa kwa jirani zangu na mara nilihisi kwamba mtu akiniinua mikono yangu juu angani nami nilikuwa
nikitembea mbio juu ya mawingu na nikimtukuza Mungu. Mwangaza mkubwa alikuja juu yangu na sauti
ilisema nje ya mwangaza huo, "Ricardo, Ricardo, acha kazi yako kwa sababu nataka kufanya kitu
kwa maisha yako na kwa kanisa langu juu ya dunia." Baada ya kusikia maneno haya, mimi
nilitetemeka na nikaamka kutoka katika ndoto yangu. Nikainuka na mimi nikaanza kulia kwa Mungu na
kuuliza, "ni kitu gani, hiki Bwana?"
Sauti hiyo ilikuja kwangu kwa nguvu sana. Ilitokea kwangu kwa siku nyingi. Kisha nikaendelea kulala
tena na nikaota ndoto hiyohiyo moja na Bwana alirudia mara kwa mara ujumbe huo kwangu. Baada ya
mara kwa mara kurudia, niliamka na kupiga mayowe kwa sababu sauti ya Mungu iliongezeka kwa kiasi
kila wakati. Niliamka nikiwa natetemeka, nilipiga kelele na wazazi wangu waliniuliza, "Je, kuna tatizo
gani?" Niliwaambia kuhusu ndoto na mama yangu aliniombea na aliniambia, "Kama Bwana
anazungumza na wewe, basi Yeye atakupa ufahamu. "Tuliendelea kuomba usiku kutwa mpaka wakati
wa mimi kwenda kazini asubuhi. Mama yangu aliniambia nijiandae kwenda kazini. Tulimuomba Bwana
2
ishara ili tujue kama yeye ndiye alizungumza na mimi. Nilioga, nikajiandaa, na nikaenda kazini.
Nilikuwa nafanya kazi katika "maabara ya Chile".
Mimi kwa kweli napenda kazi yangu. Nilikuwa nikipitiwa katika kituo cha basi na kwenda kazini.
Mara niliposhuka, mtu mmoja aliniambia kwa haraka, "Unafanya nini hapa? Hautakiwi kuwa mahali
hapa tena. "Katika matukio kadhaa, wengine waliniambia kitu hiko. Jambo la kushangaza ni kwamba
wao hawakuwa wamezaliwa mara ya pili. Hii ni ishara ambayo Mungu alinipa. Baada ya ishara hii,
niliamua kwenda kwa bosi wangu ili niache kazi. Nikamwambia, "Mimi menipasa kuondoka katika
kampuni kwa sababu Mungu ameniagiza kujiondoa." Bwana anapotupa amri, ni LAZIMA kutii. Bosi
wangu alikuwa na wasiwasi kwa ajili yangu na aliuliza, "Je,utakwenda kufanya nini? Wapi utapata kazi
nyingine nzuri kama hii? "Nilimwambia imenipasa kumtii Mungu. Basi, walinifanyia mahafali makubwa
ya kuniaga ya watu elfu mbili kwa ajili yangu. Baada ya hapo, nilikusanya vitu vyangu vyote na kurudi
nyumbani. Nilifika nikiwa nalia, mama yangu alikuwa tayari ananisubiri kwa mbele ya nyumba.
Nilimwambia kuwa niliamua kuacha kazi yangu kwa sababu Bwana alithibitisha ndoto zangu kupitia
watu hao. Yeye akajibu, "Kama Bwana amekuambia, basi namuomba afanye katika maisha yako vile
apendavyo."
Tuliingia ndani na tukaongea mpaka usiku. Basi, niliimuambia ninahitaji kwenda
kitandani kwa sababu Mungu atazungumza na mimi usiku wa leo katika ndoto.
Nilidhani angeongea nami katika ndoto, lakini haikutokea kama nilivyowaza.
Lakini alisema nami kwa njia ya tofauti. Nilipokwenda katika chumba cha kulala na
nilipotoa nguo zangu, chumba kikaanza kutikisika. Na nilianza kupiga kelele, "Ni
tetemeko linaikumba Santiago, Chile." Nilijaribu kuondoka katika chumba changu,
lakini mtu asiyeonekana alinizuia kupita mlangoni. Nilikuwa na uwezo wa
kumuona mama yangu na familia yangu katika chumba hicho na nilipiga kelele
kwa msaada lakini hakuna mtu aliyeweza kunisikia. Sasa najua, kiumbe huyu
asiyeonekana alikuwa ni malaika wa Bwana. Nilirudi nyuma na kujilaza juu ya
kitanda changu na nikalmlilia Mungu, nikaomba aniambie nini kinaendelea.
Sauti ikasema nami. Roho mtakatifu akaanza kusema nami katika sauti nzuri
sana, akisema, “Ricardo, Kwa kuwa umeacha kazi kwa sasa, nitahitaji wewe uende kanisani na uwe
unaomba kwa muda wa saa saba kila siku kwa maisha yako, na kwa kanisa langu duniani.” Baada ya
Bwana kuacha kuongea nami, chumba kikaacha kutikisika. Nikaainua mkono wangu na kuona ya kuwa
ninaweza kuondoka chumbani tena. Kishanikamkimbilia mama yangu na kumueleza “ Nimesikia sauti
ya Roho mtakatifu” na nikatoka nikaanza kuongea kwa sauti nje ya nyumba. Watu hawaamini kuwa
Mungu bado anaongea na watu hata leo lakini nakueleza ni kweli, Anaongea na watu! Kama Bwana
aliweza kuongea na Abrahamu, anaweza kuongea nasi pia na kanisa lake leo. Nikaenda kanisani na
kuongea na Askofu na tukakubaliana kufungua kanisa kila siku asubuhi saa 2 ili niweze kutii agizo la
Mungu alilonipa. Kila asubuhi nilikwenda kanisani na nikaomba saa moja, mawili na kwa mara ya tatu
sikuwa na chochote cha kuombea na nikawa nikimuuliza Mungu, “ Bwana ni kitu gani kingine
niombee?Nimebakiwa na masaa manne yaliyobakia!”
Kisha, nikasikia tetemeko linatokea nyuma ya mlango wa kanisa. Nikahisi kanisa linayumba kushoto
na kuliakama mtu aliyelewa. Lilipokuwa likiyumba, nikasikia sauti ikiongea nami lakini wakati huu
haikuwa sauti kama ile ya kwanzaniliyokuwa kwenye maono. Suti ile ya kwanza ilikuwa ya mamlaka,
lakini wakati huu aliongea nami kwa sauti ya huzuni. Akasema, “Ricardo, Ricardo omba kwa ajili ya
kanisa langu! Kanisa langu si kama lilivyokuwa kabisa, Kanisa langu duniani limebadilika. Kanisa
3
langu limepoteza imani yake. Kanisa langu haliamini kuhusu mimi na wala kuamini kama mimi ni
hai hata leo . Liambie kanisa langu kwamba nipo ni hai!! Omba kwa ajili ya kanisa, kwa sababu
kanisa langu haliombi wala kufunga tena!” Mtikisiko uliacha baada ya yeye kumaliza.Nikaanza tena
kuomba na kutembea juu na chini kwa muda wa masaa manne yaliyobakia nikiwasihi watu wa Mungu
wawe na uhamsho.
Siku ya Alhamisi ya wiki ya pili ya maombi, niliamka na maumivu makubwa katika mifupa yangu na
viungo vyangu na sikutaka kuinuka. Mama yangu alikuwa akiniamsha kwenda kanisani kuomba, lakini
nililalamika kuwa mwili wangu na mifupa yangu ilikuwa ina maumivu. Basi akanishauri kuwa niombee
pale nyumbani. Hata hivyo nilimkumbusha kuwa Mungu ameniambia niombee kanisani. Hivyo
akanisaidia kunivalisha na kunipeleka kanisani. Asubuhi ile kulikuwa na watu wengi waliokuwa
wakiomba pale kanisani, nami nikawaomba waniombee kwa ajili ya mwili wangu kwa sababu ya
maumivu katika mwili wangu. Niliwaeleza kuwa nilikuwa mdhaifu sana kuweza kufanya maombi.
Hivyo walinipaka mafuta na kuniombea mwili wangu na nikapata nguvu za ajabu kutoka kwa
Mungu!!Haleluya! Nikaanza kuomba nikitembea mbele na kurudi nyuma, nikiomba rehema za Mungu
kwa taifa la Chile na kwa familia na watu walioathiriwa na madawa na kwa kanisa.
Nilimaliza maombi na kisha nikarudi tena baadae kwa ajili ya ibada ya usiku. Baada ya Baraka za
askofu,niliinua mikono yangu na nikahisi mtu fulani alipita na kuugusa mgongo wangu. Lilipotokea
jambo hili nilipoteza nguvu zangu zote na nikaanguka sakafuni.Askofu aliniuridha nini kilikuwa ni tatizo
na mimi, na nikajibu hata sifahamu, nikamueleza kuwa sina nguvu na siwezi kuzumgumza vizuri. Kisha
kanisa likanizunguka na kuanza kuniombea kwa lugha huku wengine wakiomba kwa sauti. Baadhi ya
watu walianza kuona malaika akija na kuniuliza niuache mwili wangu. Askofu akakemmea,
“Hautauacha mwili wako!” Aliposema hivyo, Malaika waliacha kuniita ili niuache mwili wangu.
Unaona, Mtu yeyote mwenye mamlaka katika Yesu ataheshimiwa na malaika wa Bwana.
Askofu akaniomba pia, “Kwa muda gani malaika anahitaji akuchukue kutoka katika mwili wako?”
Nikamuuliza malaika, “unanichukua kwa saa moja?mawili?Matatu?”Malaika akajibu, “ hapana,
utaondoka kwa muda wa masaa 8 kwenda kumuona Yesu katika mbingu ya tatu kwa sababu anataka
kuongea nawe.”Kisha malaika akanieleza, “Mimi siye ambaye nitakuongoza wewe kwenda mbinguni,
kwa sababu mimi ni malaika wako ambaye nimekulinda wewe kila siku tokea kuzaliwa katika dunia hii.
Malaika wawili watakuja kutokea mbinguni ili kukuchukua wewe mpaka mbingu ya tatu usiku wa
manane.” Nikamueleza hili askofu na na akaazimia kunichukua mimi kwa gari ya ndugu mmoja katika
kristo kwa nyumba ya mchungaji katika ghorofa ya pili. Nilipofika tu chumbani, tuliweza kusikia mbwa
wakibweka na watu wakilia.
Baada ya maono yangu nilielezwa kuwa wanaume wawili waliovalia mavazi mazuri meupe
yanayong’aa walionekana mtaani na wakaja hadi ghorofa ya kwanza ya nyumba na wakapanda hadi
ghorofa ya pili nilipokuwepo. Malaika hawa ni wazuri. walikuwa na nywele nyeupe zinazong’aa, nyeupe
zaidi ya barafu/theluji, na macho yao yalipendeza kama lulu.Ngozi yao ilikuwa nyororo kama ya mtoto
lakini bado walikuwa wakionekana kuwa na misuli kama wanyayuaji wa vitu vizito(bodybuilders).
Malaika hawa walikuwa na nguvu!! Kisha nikamueleza Askofu, malaika hawa wako mahali hapa
walotumwa kunichukua twende mbinguni.Malaika mmoja akaanza kunisihi niuache mwili wangu.
Lilipokuwa likitokea hili, mifupa yangu ilianza kuniuma tena. kwa hiyo ndugu wangu katika Kristo
pembeni mwangu walianza kunichua na kunieleza kuwa walihisi baridi ikiongezeka katika mwili
wangu.Kwa hiyo walichukua hita ili kuupa joto mwili wangu, nilianza kuogopa na kuanza kwenda huku
4
na huku. Nilianza kuhisi kifo kinanichukua na nikasema kwa sauti wa ndugu zangu hawa katika Kristo, “
Msinizike, nitarudi tena!”
Niliuacha mwili wangu na nikarukia kitandani. Niliwaona ndugu hawa wakiushikamwili wangu na
kusema, “Ameondoka, “Ameuacha mwili wake!” Lakini nilikuwa pembeni yao nikiwaeleza “niko
hapa!” Lakini hawakuweza kuniona kwa sababu ulikuwa ni mwili usioharibika wa kiroho. Ndugu hawa
walianza kuufunika mwili wangu katika blanketi.
Malaika mmoja aliniambia, “Ni wakati wa kuondoka sasa kwa kuwa Bwana anakusubiri!” Kila
mmoja aliushika mkono wangu na kuninyanyua kwenda mbinguni na tulipita katika anga kwa mwendo
wa mwanga. Nitakueleza wewe hivi, hata kama hauamini mojawapo ya mambo haya, Yesu Kristo yupo
na anaishi milele!!
Baadae ,Bwana aliponieleza niurudie mwili wangu , nikimueleza,, “ Ni nani katika dunia ataniamini,
niache tu niishi na wewe!! hakuna atakaye amini huu ufunuo, hakuna atakayeamini kwa sababu hawana
imani! Tatikzo la kukosekana kwa imani ni kubwa sana, ni nani ataamini huu ufunuo?” Bwana akajibu,
“ Kuna mtu fulani ataamini maono haya, ni wale walio wa kanisa langu la kweli wataamini.”
Nilipokuwa nimeuachaa mwili wangu usiku ule nilikuwa nikipaa kwa spidi ya ajabu nikiwa naenda
kwa Bwana. Niliweza kuangalia chini na kuona sayari dunia. Kisha nikapita karibu kabisa na mwezi,
Mwezi huu mzuri uliiangaza anga usiku katika dunia. Kisha, niliweza kuona jua na ukubwa wake kwa
macho yangu; Niliweza kuona miali ya moto ilivyokuwa ikilipuka na kutoa joto mpaka kwenye dunia.
Kisha tuliendelea na kuona nyota nyingi tulizozipita. Mungu aliruhusu mimi nione jua, mwezi na nyota
kwa kusudi: Kusudi hilo ni kuuambia nyinyi nyote kwamba Mungu wetu ni muumbaji mkuu wa
Ulimwengu!!! Si mdogo kwa namna yeyote ile!
Tuliendelea kusafiri kwa mwendo huu mkali hadi tulipofika mahali ambapo hakukuwa na nyota tena.
hakukuwa na uumbaji wowote, ilikuwa ni Giza tu.Niliweza kuangalia chini na kuona nyote zote zikiwa
chini. Nilianza kuogopa na nikawauliza malaika, “Mnanipeleka wapi? Nirudisheni kwenye kitanda
changu duniani” walinishika na kunibana zaidi na kuniwekea miguu yao kwa miguu yangu na kunishika.
Nilianza kulegea kwa sababu ya hofu niliyokuwanayo. Malaika wakaniambia “ Nyamaza Kimya!
Tunakupeleka kwenye mbingu ya tatu ambapo Yesu anakusubiri ili aongee nawe!” Malaika walisimama
na wakati huu niliangalia pande zote na sikuona chochote cha uumbaji, sifahamu nilikuwa wapi, nafikiri
ilikuwa ni mbingu ya pili.
Kisha nikiwa katika hali ya kujiachia malaika wakiwa wamenishika na mara nikajisikia na kusikia kelele
za kutisha juu yangu. Malaika wakanibana na kusema, “ Ricardo, usiogope, Yesu yuko pamoja nasi!”
walipokuwa wakiongea,walisema, “ Inua kichwa chako na uangalie juu yako!” Nilishangazwa sana na
kile nilichokiona kwa sababu kulikuwa na viumbe vilivyokuwa katika mwendo juu yetu. Malaika mmoja
akasema, “ Angalia, tutakuonyesha wewe kile ambacho unakiona juu yetu! Malaika mmoja akanyoosha
mkono wake akapunga huku na huku ili kutoa mwanga uangaze sehemu yote ile ya anga ili kuona kitu
kilichokuwepo mahali pale. Anga lilipokuwa na muangaza hakukuwa na kitu chochote ila mapepo na
mashetani yalikuwa yamezunguka anga lote lile. BWANA AWAKEMEE WOTE KWA JINA LA
YESU!!Biblia ni kweli!! Kila kitu kinachoendelea katika ulimwengu huu ndo kile ambacho unakiona
katika Ufunuo. Yesu anakuja hivi karibuni!! Nawezaje kukushawishi, ni hivi KARIBUNI!!Nikamuuliza
malaika, “Mahali hapa ni wapi?Mmoja akajibu, “ Hapa ni mahali pa ulimwengu wa Giza ambapo
Shetani na malaika zake ( mapepo) wanaishi,” Akaanza kusema, “ Ndio maana kuna uharibifu mwingi
duniani! Mapepo haya yanakuja duniani kutokea mahali hapa na kusababisha uharibifu na uovu wa kila
5
aina na uovu katika makabila ya wanadamu!” Dunia imejaa mapepo!” Kuna mapepo milioni na
milioni , idadi haihesabiki.
Kisha malaika, alianza kunipeleka
niangalie kwa ukaribu na kunionyesha
sura za viumbe hivi na nyingi ya hivi
viumbe vimekwisha onekana kwenye
Runinga. Viumbe hivi ni VIBAYA!!
Niliona viumbe vilivyofanana na viumb
vya kwenye michezo ya runinga ya
Thundercats na Power Rangers na katuni
ya caricatures ambavyo ni halisi kabisa
kwa maisha ya duniani. Wabunifu wote
wa muvi na michezo hii wameweka
mkataba na shetani kutoa vitu hivi
kwenye runinga na sinema!! Michoro yote ile inatokea katika ulimwengu war
oho ambao niliuona. Unafikiri kwa nini watoto wa siku hizi wamekuwa wakaidi?? ni kwa sababu
mapepo haya yanawanigia watoto hawa wanapokuwa wakiangalia maonyesho haya ambayo
yanawaoyesha wao (mapepo). Ndiyo maana imetupasa kuwafundisha watoto kuchagua nini cha
kuangalia kwenye TV. Malaika aliniambia hiki ni halisi na kweli. Mapepo haya yote yapo na watu
wanafanya makubaliano na shetani ili kuleta mapepo haya duniani. Haya mapepo yanaanza kunitukana
mimi, na kanisa, na Baba, na Bwana Yesu na Dunia kwa sababu hawamuheshimu Mungu au uumbaji
wake wowote.
Kisha nikaona kiumbe halisi kabisa kiitwacho Hugo, huyu ni katuni maarufu sana nchini Chile. Ilikuwa
inaogopesha kuangalia. Alikuja karibu yangu na kunieleza, “Tutaenda duniani na kuwaua watoto wote!”
Kwa nini unafikiri watoto wanaua watoto wenzao? Ni kwa sababu baadhi yao husema kuna kitu kilikuja
kutoka katika runinga na kuniambia nifanye hivi au vile. Mapepo haya hupanda chuki duniani, Bwana
akomboe na kusafisha Chile!! Mmoja wa malaika akaniambia “Endelea kuangalia!” Na mapepo
yakasema, “Tumejaribu kuharibu kanisa, lakini hatuwezi kwa sababu tunapomuuua mmoja, basi
wanainuka maelfu kuchukua nafasi ya kifo chake!” Tokea kuanza kwa kanisa, Shetani amejaribu
kuliharibu, kanisa ambalo huubiri injili ya kweli na kufanya kazi ya Mungu, lakini hawezi kwa sababu
Yesu anatulinda! Utukufu kwa Mungu! Kisha mapepo yakasema, “Ngoja tufanya jambo jipya, ngoja
tuingie makanisani, kwa sababu pale kuna wengi ambao ni wetu! Tutaenda kuwatumia watu hawa
kusambaza umbea na kuleta migawanyiko katikati ya ndugu ndani ya kanisa.” Shetani anazunguka kila
mahali akitafuta kuharibu wale wanaopenda haki ya Mungu. Kama andiko linavyosema:
1Petro 5:8 Muwe macho; kesheni! Maana adui yenu, Ibilisi, huzungukazunguka kama simba
angurumaye akitafuta mawindo.
Sikutaka kuendelea kuona tena, lakini malaika akaniambia niendelee kuangalia matukio yanayotokea.
Niliona mapepo yakiruka kila kona pindi nyota moja ing’aayo ilipokuwa inakuja. nyota hii ilipokuwa
inatokeza na kusogea, ilikuwa inaleta sifa nyingi na ibada kwa Bwana. Hii haikuwa nyota kama nyota,
kumbe ilikuwa ni mamilioni ya malaikawakiwa juu ya farasi weupe wakimtukuza Mungu wa Majeshi!!
Walikuwa wakiimba “Mtakatifu,Mtakatifu, Mtakatifu, ni yeye aishie enzi na enzi! Bwana ndiye Alpha na
Omega, Mwanzo na Mwisho na kila chenye pumzi na kimsifu Bwana!” Kisha nikaaona vita kubwa na
6
sikuona mapepo tena. “Usiogope kabisa kwa sababu kuna malaika wengi zaidi upande wetu zaidi ya
upande wa adui!”
Malaika walifa ya njia mpaka mbingu ya tatu. Walijigawa katika makundi mawili, moja kulia na jingine
kushoto.Ilikuwa ni njia iliyowazi mpaka mbingu ya Tatu! Njia hii ilinyooka mpaka mbinguni na uliweza
kuona Mji mtakatifu wa Mungu. (Kuna picha ya satellite duniani ambayo imechukua picha kutokea katika mji huu. Mji huu
Mtakatifu upo! Hii imetokea kwenye radio na TV.) Nilweza kuona njia ya utukufu na malaika wa ajabu. Waliisafisha
njia yote kuwafukuza mapepo na hawakuacha kumsifu Mungu na kubariki Jina lake! Malaika
wakaniweka mbele yao na kuniambia, “ Imekupasa kusubiri hapa!”
Kwa mbali, niliangalia na kutokea katika mji huu niliona mtu fulani akiwa na mazazi mazuri meupe
amepanda farasi mweupe. Mtu huyu alipokuwa akizidi kunisogelea, malaika waliendelea kusifu jina la
Mungu na kumtukuza. Mtu huyu alikuja mpaka umbali wa mita 4 tokea nilipo. Kiumbe huyu alikuwa
mzuri, alikuwa ni mzuri zaidi ya wale malaika wengine. Nilitegemea angeongea nami, lakini
alichokifanya ilikuwa ni kuniangalia na kusema kwa sauti, “Mimi ni malaika mkuu Mikaeli ambaye
ninajukumu la kukulinda wewe pamoja na kanisa la Duniani!” Nilimuona malaika mkuu Mikaeli uso
kwa uso na alikuwa ni kiumbe cha thamani sana! Aligeukia upande wake na kuonyesha njia ya mimi
kuingia mji Mtakatifu. Alisema, “Ingia! Bwana Yesu anakusubiri!” Nilikuwa nikitembea katika njia ile
nikifuata mji ule na nilipokuwa nikitembea, Malaika walikuwa wakiimba na kumsifu Bwana. Nililia na
kulia nilipokuwa nikiuangalia mji ule.
Mji ulikuwa umeumbwa kwa dhahabu halisi angavu na mlango wa kuingilia ulikuwa umeundwa kwa
lulu. Sakafu ilikuwa ni ya muonekano wa kioo angavu(crystal). Sijawahi kuona kitu kama hiki duniani
na hakuna mwanadamu awezaye kukiunda. Msanifu wa majengo ya mbinguni ni Bwana wetu na Mungu
wa Ulimwengu wote.Nilikuwa nje ya mji na milango yote ilikuwa imefunguliwa. Na milango hiyo ikiwa
bado hii wazi, niliweza kuona ndani na katika kuta kulikuwa na madini ya Rubi na safira na lulu
ambayo yaling’aa. Na ndani ya mji ule kulikuwa na sauti milioni na milioni ya sauti zikimsifu Mungu!
Nilitetemeka kutokea nje ya mji niliposikia hivi. nilisikia sauti moja ambayo ilitikisa mbingu na nyuma
ya sauti hii ilikuwa ni mamilioni na mamilioni ya sifa kwa Mungu yakisifu “Mtakatifu,
MtakatifuMtakatifu ndiye mwanakondoo wa Mungu na Baba ambaye utukufu una yeye na heshima
milele na milele AMEN!” Sauti kubwa ikasikika ikisema “IWENI WATAKATIFU KWA SABABU
MIMI NI MTAKATIFU! NI WATAKATIFU TU NDIO WATAKAOINGIA KATIKA MJI HUU!KWA
SABABU PASIPO UTAKATIFU HAKUNA ATAKAYEMWONA BWANA.” Bila utakatifu hakuna
atakayemuona Bwana.
Sauti ikasikika ikisema, “Ingia” na nikaingia ndani ya mji ule. Na nikaona Kiti cha ajabu cha enzi
kimezungukwa na moto. Na moto unatoka katika kiti kile cha enzi, Nikatulia kimya na nikamuona Yesu
, Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana! Nilijihisi mdhaifu mbele zake na nikaanguka chini
nikaishiwa na nguvu.Mkono wake ukatoka kwenye miali ile ya moto na kunishika na akasema,
“Simama kwa miguu yako!” Nilipata nguvu na nikasimama. Nilianza kugusa miguu yake na mikono
yake na mwili. Nilipoona uso wake, muonekano wake ni tofauti sana na wachoraji wa dunia
wanavyochora katika michoro yao! Watu wengi wanaunda miungu ya mbaona wengine taswira
mbalimbali! Lakini nataka nikuambie hivi ndugu yangu, Yesu Yule hafanani na taswira hizo. Ni Mungu
mwenye misuli na nguvu! Si Mungu wa ukawaida, Ni Mungu mwenye nguvu zote!! Anasema, “Mimi si
Mungu niliyeumba na mbao, au chaki,Ni Mungu ninayeishi!” Anaendelea, “Liambie kanisa langu
duniani mimi ni halisi!! Ni kweli ninaishi na nipo! Waambie watu wangu kuwa Mbinguni ni Halisi
na ninawasubiri!” Aliniambia,“Njoo, tembea pamoja nami na nitakuonyesha jambo moja kubwa.
7
Tuliangalia chini na niliweza kuona dunia na vitu vyote vilivyofanywa kwenye dunia. Yesu akasema,
“Ninaweza kuona kila kitu ambacho kanisa langu linafanya!” Anajua kila kitu tunachokifanya na
mimi niliweza kuona wengi wenu kutokea mbinguni. Yesu akaniambia, “Angalia katika kanisa langu!”
Niliweza kuona ndugu kwa ndugu, na makanisa kwa makanisa. Yesu akaniambia, “Kanisa langu
limepoteza imani yake,hawataki kuniamini, uovu umeongezeka duniani na watu hawataki kuamini
kuwa nipo. Waambie watu wangu ninakwenda kufanya kitu kikubwa duniani! Kanisa langu linarudi
nyuma badala ya kukua.” Bwana alianza kulia kwa ajili ya kanisa lake na akasema, “ Hili kanisa si
kanisa langu! Nikamuambia Bwana, “Bwana usiseme hivyo! Wewe unajua kuwa tu kanisa lako.”
Bwana Yesu akajibu, “Hapana kanisa langu linatembea kwa nguvu za miujiza,ishara na maajabu!
Kanisa langu limepungua! Hatahivyo, waambie, nitakuja kuwafufua tena!”
Aliniambia niendelee kutembea pamoja nae na tulikwenda mahali fulani penye mlango na mlango
ulikuwa umetengenezwa kwa dhahabu halisi.Nilianza kukimbia huku na huku kwenye mtaa uliofanywa
kwa dhahabu na nikawa ninachukua vumbi la dhahabu na kujipaka kwenye mwili wangu. Na Yesu
aliniambia nirudi na akaniambia kuna mitaa ya dhahabu mbinguni. “ Hii yote ni urithi kwa watu
wangu,” Bwana akasema. “ Lakini kwenye kanisa langu kuna wezi wengi ambao wananiibia fungu la
kumi na sadaka! Waambie watu wangu hakuna mwizi atakayeingia kwenye ufalme wa Mungu!”
Inabidi turekebishe maisha yetu kwa ajili ya Bwana.Kisha tuliona meza ndefu sana kwa ajili ya watu
mamilioni ikiwa na chakula cha kutosha na vinywaji. Kulikuwa na mataji mengi na glasi kwa ajili ya
watu kunywea. Bwana akasema, “Yote haya yameandaliwa kwa ajili ya watu wangu!” Meza hii
iliandaliwa kwa ajili ya harusi ya Mwana kondoo.
Kuna dada mmoja katika Kristo ambaye pia alipelekwa mbinguni na kasha aliona malaika wakienda na
kurudi wakiwa wanatayarisha chakula cha Harusi hii! Nikamuambia Bwana, “ Kwa nini dada huyu
aliona malaika wakitayarisha vitu hivi, lakini mimi sioni matayarisho yoyote yanayofanyika? Bwana
akajibu, “Ni kwa sababu matayarisho yote yamekamilika!” Kuna mataji kwa wote wanaofanya kazi na
ni watii kwa Bwana. Kisha nikamuuliza, “ Bwana utakuja lini basi,kama maandalizi yote
yamekamilika?Itachukua muda gani mpaka utakaporudi? Nionyeshe muda, Ni muda gani umebaki
katika saa ya mbinguni?” Watu wengine wamekuwa na maono ya muda, wakionyesha kuwa itakuwa ni
usiku muda ambao Bwana Yesu atarudi. Niliuliza, “ Ni lini saa itagota katika mshale wa saa sita
usiku?Je ni dakika moja imebakia? dakika tano?” Bwana Yesu akausoma uso wangu kwa muda
kidogo, kasha akajibu, “Ricardo,mbinguni hakuna muda tena!” Kisha nikaitikia, “Vizuri bwana ,
kama hakuna muda tena, kwa nini bado haujarudi?” Yesu akanyanyua mkono wake na kuchukua
kidole gumba chake na vidole vyake vingine na kunionyesha alama inayoonyesha kitu fulani kidogo
sana na akasema,“Muda wote uliobakia ni Neema ya Mungu kwa wale waliorudi nyuma warejee tena
na kutubu na kuifanya kazi ya kwanza.” Na Bwana wa Majeshi hajarudi kwa sababu ametupa sisi sote
muda kidogo sana wa kutubu na Muda huo unaitwa, “ Muda wa neema/rehema ya Baba” Yesu anarudi
muda wowote, ni lazima tuanze kumtafuta kwa moyo wetu wote na tufunge na kuomba na tuzifanye kazi
za kwanza. Nimemaliza kila kitu. Yesu alirudia, “ Tuko kwenye muda wa Neema ya Mungu!”
Kisha malaika alitokea upande wetu wa kuume akisema kwa sauti, “Muda umewadia!! muda
umekwisha. Maandalizi yote yamekamilika! Yesu anampokea bibi harusi wake( kanisa)!” Bwana Yesu
anarudi na kila ishara iliyoko kwenye maandiko inatimia! Sinema zinaonyesha kitu fulani cha kutisha
kinakuja. Wanasayansi wanatambua kitu fulani kikubwa kitatokea, hawajui ni kitu gani
hicho!Hatahivyo, Sisi kanisa tunatambua kwamba Yesu anarudi hivi karibuni! Malaika walipomaliza
kusema, kasha mamilioni ya malaika walianza kuruka na kushangilia kwamba bibi harusi(kanisa)
linarudi mbinguni. Nikaendelea kumuuliza, “ Kitu gani kinaendelea?” Lakini hakuna aliyeonekana
8
kujali, wote walikuwa wakishangilia kwa habari njema. Nilijumuika na malaika na kuanza kulisifu jina
la Yesu pia! Wakati huo nilipoinua mikono yangu nilihisi mtu fulani ameninyanyua kuondoka mbinguni
na kunirudisha chini kwa spidi ya ajabu.
Hivi sasa, malaika wanashangilia kwamba Bwana Harusi anarudi. Nilirudi duniani na niliachwa pale
madhabahuni kanisani ambapo nitakuwa ninaomba kila siku. Muda ni mfupi sana!! Kama hutaki
kuniamini mimi, basi usiamini. Lakini anakuja na itakuwa ni ujio wa milele. Watu wa Mungu
hawaamini katika unyakuo. Tafadhali amka, Kwa jina la Mungu amka katika ukweli!! (Ricardo analia).
Bwana Yesu alikuwa karibu yangu, na aliniambia, “Ricardo, hivi ndivyo ambavyo unyakuo utakuwa
kama utatokea hivi sasa!” niliweza kuona dunia yote na Roho mtakatifu mzuri ambaye anatupa amani
na furaha ya kuishi katika dunia.Kisha nikaona kama mvuke ukiingia kanisani na ukanizunguka na
nikamuuliza Bwana, “Hii ni nini?” Akasema, “Hiki ndicho nakiita Unyakuo.”Kisha nikaona watu
wakivunja milango ya kanisa, wakitaka kuja ndani, na kupayuka, “Watoto wangu wako wapi? Wote
wametwaliwa!” Watoto wote katika ulimwengu wametwaliwa kwa sababu Mungu hata waacha nyuma.
Mtu wa kwanza kuingia katika kanisa alikuwa ni Mwalimu wa kwaya, akapayuka, “ Kanisa liko wapi!
nimeachwa nyuma! Nimebaki! Nimebakia!” Baada ya mwalimu wa kwaya, niliona wachungaji
wengine, waumini wa wakiume na wa kike,na waangalizi wa kanisa wote wanalia, “Nimeachwa
nyuma!” Wazazi wengi na wanandoa wengi waliwatafuta wale wawapendao na watu wale walioko
kanisani wakawajibu, “Muwapendao hawako mahali hapa! Bwana amewachukua,” Watu hawa
walianza kulia, “Yaani kumbe ni kweli, Yesu amekja na kuchukua bibi harusi!”.
Watu walikuwa wakilia na kuomboleza wakitamani kama tu wangemuamini Yesu Kristo. Kila mtu
asiyemuamini Yesu kama Masihi amepotea! Nikaona watu wengi na wachungaji wakilia na watu
walianza kuwadai wachungaji, "Kwa nini wewe hukuhubiri ukweli, kwa nini hukufundisha utakatifu
na kunionya mimi kuhusu yote haya? Ni kwa sababu yako nimeachwa nyuma! "Wengi wataachwa
nyuma kwa sababu hawaishi maisha matakatifu. Tunahitaji kuhubiri utakatifu wa kweli na kuwafundisha
watu toba ya kweli! Niliona jinsi watu walivyopiga wachungaji na kuwakatakata na kuondoa nywele
zao. Wachungaji walilia na kuomba watu wasiwadhuru. Watu hawakuacha kwa sababu walikuwa sasa
na mapepo.
Kuna makanisa kabisa ambayo yataachwa nyuma. Nilimuona kaka mmoja alikuwa anajaribu
kuyakwarua macho yake mwenyewe kwa sababu ya huzuni kuu. Na watu walipigiza vichwa vyao
sakafuni na kwenye kuta kwa sababu hawakutambua kuwa Yesu alikuwa ndiye jibu pekee. Kwa sababu
watu walitaka kuendelea katika dhambi na uovu na kuishi maisha vile walivyotaka. Watu walijikata
wenyewe na kupigiza vichwa vyao mpaka kiasi cha kuona fuvu zao zikiweka ufa na walianguka chini.
Damu ilitiririka bure ndani ya kanisa kwa watu ambao walikuwa wakijijeruhi wenyewe. Kisha nikaona
kijana akipiga kelele kwa Mungu, "Tafadhali Bwana, nichukue!" Alikuwa amechelewa mno. Yesu
alikuwa tayari amekwishakuja na kulipokea kanisa lake. Hapo nilianguka chini kwa sababu niliona
mambo mengi zaidi ya kutisha.
Yesu akaniambia, "Katika dhiki kuu, kutakuwa na matatizo makubwa haijawahi kutokea kabla."
Kisha nikauliza, "Kwa nini watu wanaruka nyuma baada ya kuumizana vibaya wao wenyewe?" Bwana
Yesu akajibu, "Kwa sababu kwa wakati huu, watu watatamani kifo, lakini hawatakipata. Kifo
kitakuwa kimetoweka katika uso wa dunia. Nilimwuliza Bwana, "Kwa nini wachungaji wote hawa na
watu wameachwa nyuma?" Na Bwana akasema, "Kwa sababu ninajua mioyo yao. "Mungu anatujua sisi
.. Anajua yote ya mioyo yetu. Nilianguka chini, karibu kuzimia. Yesu alisema, "nimetaka kukuonyesha
9
hili ili kwamba uonye kanisa langu na kuwapa matumaini. Waambie kwamba kama watu watatubu
sasa, mimi nitawasamehe wakati bado kuna muda. Nitafanya jambo kubwa katika dunia. "
Tafadhali,fungua macho yako. Kanisa la kiinjili nchini Chile linaongezeka. "Waambie watu wangu
kama wataomba msamaha, nitawasamehe." kisha nikaona maono mengine na nikaona moto umefunika
mbingu nzima. Yesu akasema, "Je, umeweza kuona? Huo moto uliona juu ya nchi/dunia, ni moto juu
ya nchi ya Chile. Kwa sababu Chile itakuwa kwa ajili ya Kristo! Mungu ataibadili Chile! " kisha
nikaona moto unataka kuja juu ya Chile na Yesu akasema," Macho ya Baba yangu yako juu ya Chile.
"Mara moto utakapokaa juu ya Chile, nchi nyingine zitaona na kujua kuwa Mungu yuko mahali hapo.
Kanisa lote duniani litafurahi kwa sababu Uwepo wa Mungu unatembea Chile. Bwana alinichukua
katika maono mpaka mahali paitwapo "Paseo Humada"
Akanionyesha watu waliokuwa vilema na walio na matatizo. Kisha nikaona waamini wa kweli
wakiomba juu ya viwete wasio na miguu na wakitiisha viungo kukua. Viungo vilitii na kukua mbele ya
macho yao. Watu wasio na mikono waliiota mikono kwa upya mara moja. Wakati huu, Bwana
ataonesha miujiza ya uumbaji. Katika makanisa watu ataponywa. Katika siku hii, wafu watafufuliwa na
Mungu akutumia wewe ndani ya Chile kufanya miujiza hiyo kama mitume wa zamani walivyofanya
katika Biblia.
Huo ni ufunuo mzima ambao Mungu alinipa (Ricardo Cid). Yeye anakuja hivi karibuni. Maranatha! Amina!
Ndugu aliyefasiri ufunuo wa Ricardo Cid wa Masaa 8 Mbinguni ni Peter Kahale ni kijana aliyeokoka na
anampenda Yesu na mwenye shauku ya kuhubiri injili ya Yesu Kristo.
Friday, October 30, 2015
UKWELI KUHUSU MBINGUNI NA KUZIMU-USHUHUDA WA KWELI
1
MBINGUNI NA JEHANAM www. Mnamo mwaka wa 1987, mchungaji Park alifariki
kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu. Lakini kwa neema ya Mungu, maisha yake
yaliongezwa kwa miaka mingine ishirini. Lakini kwa miaka minne ya kwanza kati ya hii miaka
ishirini hakuweza kuongea kutokana na hali yake. Alikuwa na miaka takribani hamsini
alipofufuliwa. Katika kifo chake Bwana alimuonyesha Mbinguni na Jehanamu.
Nataka ufahamu kwamba, ukiwa mwenye kiburi na majivuno utajiletea
laana. Nilikuwa na kanisa kubwa mno lenye washirika elfu tano lakini
Mungu alinichapa kichapo kutokana na kiburi changu.Sasa namuogopa
Mungu.
Nilikuwa na mali ya takribani dola million mia moja hamsini. Nilikuwa na magari matano ya
kifahari .Lakini baada ya mkasa wa kufa na kufufuliwa kwangu nilipeana vyote. Tafadhali
kumbuka kwamba wokovu hauwezi kupatikana kupitia kwa mali uliyonayo ila ni kwa imani
pekee. Na sasa nawasihi mashemasi wote, wazee wa kanisa na viongozi wengine wa makanisa
kuwatumikia wachungaji wao kwa mioyo yao yote.
Mnamo Desemba kumi na tisa mwaka wa 1987, baada ya kumaliza kula chakula cha mchana
nilipokuwa napumzika, nilianza kuhisi uchungu mkubwa mno, ulikuwa uchungu nisioweza
kuustahimili nami nilihisi kana kwamba nitakufa. Kisha nikapoteza fahamu. Niliamka miezi
minne baadaye nikiwa katika hali mbaya sana tena mahututi, kisha Daktari akaniambia
kwamba nitakufa.
Sehemu zote za mwili wangu zilikunjana vibaya kutokana na
kupooza kwanga. Hata jamii yangu haikuwaruhusu washirika wa
kanisa langu kunitembela kutokana na jinsi mwili na hali yangu
ilivyokuwa mbaya. Mwishowe nikafariki.
Nilipofariki, niliwaona watu wawili wakiingia chumbani
mwangu. Lakini watu hawa waliingia chumbani mwangu kupitia
ukuta. Nikapiga ukulele nikauliza, “kina nani nyinyi? Nyumba
yangu itaporomoka mkiingia jinsi mlivyofanya.” Mmoja wao akasema, “sisi tu malaika
tulioshuka kutoka mbinguni, tumetoka katika ufalme wa Mungu”. Mwangaza mkali ulimulika
kutoka kwa Malaika wale.
2
Malaika aliyekuwa mkono wangu wa kulia akajitambulisha hivi, “mimi humtekelezea Yesu kazi
za ujumbe katika ufalme wake. Yesu aliniita akaniamauru nishuke duniani nije nikuchukue
Mbinguni. Wewe umefariki lakini kwa vile jamii yako inalia kwa huzuni sana, Yesu anataka
kukuongezea muda kidogo wa ziada wa kuishi duniani. Lakini kwa sasa anataka kukuonyesha
Mbinguni na Jehanamu. Yeye atakuonyesha nawe utawashuhudia watu wa ulimwengu. Na
idadi ya wale wangetokomea Jehanamu itapunguka, nayo idadi ya wale watakao enda
Mbinguni itaongezeka kupitia kwa ushuhuda wako. Huu ndio utakuwa ujumbe wako.
“Mungu ametuagiza tukuambie usichelewe kwani ukichelewa basi hautaweza kuzuru
Mbinguni na Jehanamu”.
Kisha malaika aliyekuwa mkono wangu kulia akasema, “tangu pale ulipozaliwa hadi wakati
ulipoaga dunia, nimekuwa nawe”. Mimi sikuelewa
alichomaanisha malaika huyo lakini sasa nimefahamu alikuwa
malaika wangu mlinzi. Basi nikasema, “siwezi kwenda! Nami
sitaenda! Mimi ni mchungaji! Siwezi kukutana na Bwana katika
hali hii niliyonayo.Nataka tukutane naye nikiwa mtu mwenye
afya. Mimi pengine nitapokea makemeo mengi kuliko pongezi
kutoka kwa Bwana. Mimi ni mtu mwenye kiburi na majivuno
na sasa nimelaaniwa tena ni mgonjwa. Nitawezaje kuingia mbinguni? naogopa sana.Tafadhali
rudini mbinguni mumsihi Bwana aniponye .Kisha mtarudi mnichukue mbinguni kupitia kwa
ndoto.Tafadhali nawasihi mniombee msamaha kwa Bwana kwa niaba yangu”.
Lakini malaika hawakuwa wakiisikia hoja yangu. Wakanivua nguo zangu kisha wakasema
zilikuwa chafu mno na hazifai kuvaliwa mbinguni. Nao wakanivisha vazi jeupe.
Wakanishika mikono yangu nasi tukapaa moja kwa moja
hadi mbinguni. Tulipaa mawinguni na nilipotazama chini
nikaona dunia ilikuwa ndogo. Wakaniacha niende karibu na
njia ya dhahabu isiyokuwa na mwisho. Nikaona mwangaza
mkali mno. Nikauliza, “mwangaza huu watoka wapi?” nao
wakanijibu kwamba watoka mbinguni.
Nikawaza, “Lo ni pakubwa mahali hapa!” Nikaona kikundi
cha watu waliovalia mavazi meupe wakipaa mbele yetu.
“Kina nani wale?” nikauliza. Malaika akajibu. “Hao ni wale waliomtumuikia Yesu kwa kutii na
kufuata kuongozwa na Roho mtakatifu. Miili yao imekufa duniani. Sasa nafsi zao zinaelekea
mbinguni”. Huyo malaika mwingine akaendelea. “Kuna malango kumi na mbili mbinguni.
Wakati nafsi iliyookoka inapowasili mbinguni, ni sharti iingie kupitia moja wapo ya malango
3
haya.” Tulikuwa tumesimama katika lango la kusini lakini lilikuwa limefungwa. Tulipokuwa
tunangoja nikamuuliza malaika. “Mbona lango halifunguki?” naye akanijibu “ni kwasababu
hauuimbi wimbo wa kuabudu wa mbinguni.” Nikamuuliza malaika, “nilikuwa na kiburi tena
mwenye majivuno na ndio sababu ya mimi kulaaniwa na ugonjwa, ikiwa mimi sio mkakamavu
wa kuziimba nyimbo za kuabudu za duniani, nitawezaje kuziimba nyimbo za kuabudu za hapa
mbinguni nami sijawahi kuzisikia?”
Naye malaika akanijibu, “ulivyosema ni kweli lakini sharti ujitayarishe kuabudu. Wewe ni mtu
mwenye majivuno lakini jitayarishe kuimba.” Nao malaika wakaanza kuimba na walipokuwa
wakiimba nami pia nikaanza kuimba nao. Kuimba kule kukawa kawaida kwangu, basi tukaingia
ndani.
Eneo la mbinguni lilikuwa zuri ajabu hata siwezi kueleza kwa maneno ya humu duniani. Nami
nikasema “ Bwana! Asante Sana! Japo nilikuwa mwenye kiburi na majivuno na aliyelaaniwa
kwa ugonjwa, umenileta mbinguni kunionyesha sehemu zake.”
Kisha nikasikia sauti ya Mungu, “mchungaji wangu mpendwa PARK Yong GYU”, nakukaribisha.
Umefanya safari ndefu sana kuja hapa.”
Sauti yake ilijawa na upendo tena ilikuwa nyororo sana.
Nami nakamjibu huku nikilia kwa machozi, “Bwana…” wale malaika mara moja wakasema,
“umekuwa mchungaji kwa miaka ishirini, kwani hauyajui maandiko”, mbinguni hakuna
machozi. Tafadhali usilie hapa” sikuweza hata kulia. (Ufunuo 21:4)
Bwana akaniuliza maswali matano:
1. Uliutimia wakati wako kiasi gani kuisoma bibilia?
2. Ulitoa sadaka kiasi gani?
3. Mara ngapi umeeneza injili kwa watu?
4. Je? Ulitoa zaka ipasavyo?
5. Uliutumia mda wako kiasi gani katika maombi?
Nikashindwa kulijibu swali la tano. Naye Bwana akanikemea kwa ajili ya swali hilo la tano.
“Baada ya kuwa mchungaji wa kanisa kubwa ukawa mvivu wa maombi. Kuwa na shughuli
nyingi sio udhuru kwangu!” ilinibidi nitubu kuhusu hili jambo baadaye. “Malaika hao
watakuonyesha sehemu nyingi hapa mbinguni na pia jehanamu. Tazama jinsi utakavyo. Nawe
utaondoka baada ya kuzishuhudia sehemu tofaui za mbinguni na pia jehanamu.” Lakini Bwana
hakuniruhusu niutazame uso wake.
4
Malaiaka wakanipeleka sehemu tatu tofauti za mbinguni.
Sehemu ya kwanza, niliwaona watoto wadogo wakiishi
pamoja. Sehemu ya pili paliishi watu wazima. Sehemu ya
tatu palikuwa na nafsi ambazo ziliingia mbinguni
chupuchupu. Hata kama waliwahi kuingia mbinguni, wao
waliingia kwa njia ya aibu.
Watu wengi waliniuliza umri wa wale watoto. Walikuwa kana
kwamba waliokuwa shule ya chekechea. Kila mtoto alikuwa na malaika wake mtoto wa
kuandamana naye.
Mbinguni nafsi nyingi zitakuwa na makao yao binafsi. (Yohana 14:2)
Lakini kuna wale amabao hawakuwa na makao. Hii nitafafanua baadaye. Tena wale watoto
hawakuwa na makao yao. Nami nikauliza, “ hawa watoto pia ni nafsi ,mbona hawana makao?”
Malaika akanijibu, “hata jinsi duniani watu huhitaji vifaa vya kujengea nyumba , hali ni hiyo
hiyo hapa mbinguni. Wakati mtu anapoihudumia kanisa na watu wengine kwa utiifu katika
Bwana, haya matendo mema ndio huwa vifaa vya kumjengea mtu nyumba hapa mbinguni”.
Wakati vifaa hivi vinapotolewa basi malaika waliopewa jukumu la kumjengea mtu nyumba
huanza kazi ya ujenzi hapa mbinguni. Kwa vile hawa watoto walikuwa chini ya umri wa
kuwajibika, basi hawangeweza kujilimbikizia au kupata vifaa vya kujijengea nyumba hapa
mbinguni. Kwa ufupi, hawakuwa na muda wala nafasi ya kujikusanyia vifaa vya kujengea
nyumba na ndio maana hawana makao.”
Nami nikanedelea kuuliza maswali, “nitafanyaje nikiwa duniani ili nipate vifaa vingi vya
kuijengea nyumba yangu hapa mbinguni?” nao wakanijibu, “kuna vitu saba impasavyo mtu
kuvifanya ili kupata na kujilimbikzia vifaa vya kujengea nyumba.”
1. Kwanza ni malimbikizi yao ya sifa na kumuabudu Mungu.
2. Pili ni wakati wautumiao kuisoma bibilia.
3. Tatu ni wakati wautumiao kuomba.
4. Nne ni wakati wautumiao kueneza injili.
5. Tano ni sadaka wazitoazo kwa Bwana.
6. Sita ni utiifu katika kutoa zaka.
7. Saba na ya mwisho ni ule wakati mtu autumiao kuitumikia kanisa kwa njia yoyote ile.
Haya ndiyo matendo ya utiifu yamwezeshayo mtu kukusanya vifaa vya kujengea nyumba zao
huko mbinguni.
5
Palikuwa na watu wengi amabao hawakuwa na nyumba huko mbinguni .Wengi wa wale
ambao hawakuwa na makao huko mbinguni ni wachungaji, ,mashemasi na hata wazee wa
kanisa. Nami nikauliza kwa udadisi, “Basi hawa watoto wanaishi wapi?”
Malaika akanijibu, “wao huishi hapa”.
Nilipotazama hapa na pale, niliona
wamekusanyika pote kwenye bustani la maua.
Bustani hilo la maua lilikuwa zuri ajabu na
lilikuwa na harufu nzuri sana isiyopatikana
humu duniani.
Eneo lile lilikuwa nzuri kushinda jinsi
ninavyoweza kueleza kwa maneno yangu
binafsi.
Mahali pa pili palikuwa na watu wazima
waliokuwa waaminifu. Kuna tofauti kati ya wokovu na kutuzwa. Mahali hapo palikuwa na
nyumba nyingi sana. Nazo nyumba hizo zilijengwa kwa vito vizuri sana pamoja na mawe ya
thamani ambayo ni adimu mno. Baadhi ya makao yale yalikuwa marefu sana kama zile
nyumba ndefu za gorofa humu duniani. Wale watu amabo walimtumikia Bwana kwa uaminifu
wakiwa humu duniani walikuwa na nyumba zilizojengwa kwa vito vizuri pamoja na mawe ya
thamani ambayo ni nadra sana.
Katika mahali hapa, watu walionekana kana kwamba wana umri wa
miaka ishirini hadi thelathini. Hapakuwa na wake au waume kulingana na
jinsia. Hapakuwa na watu wagonjwa, wazee au viwete.
Niliwahi kumjua mzee mmoja aitwaye Oh Im Myung. Alifariki akiwa na
miaka sitini na tano. Alikuwa mtu mfupi mno, urefu wake ulikuwa kama
wa watoto wa darasa la pili hivi. Aliteseka sana kutokana na ugonjwa wa
nyongea lakini yeye alibobea sana katika mambo ya bibilia.Alikuwa ameaandika mafafanuzi
mengi sana ya bibilia .Nilikutana naye mbinguni naye alikuwa buheri wa afya . Mbinguni ni
mahali pazuri sana. Nina matarajio mengi sana. Tafadhali aminini yale ninayowaambia
wapendwa wenzangu.
Mahali pa tatu palikuwa na wale ambao waliokolewa kwa njia ya aibu. (Wakorintho 3:15). Kijiji
hiki kilikuwa kikubwa sana, na kilikuwa ni kikubwa zaidi ya mahali pale pa pili ambapo nyumba
zilijengwa kwa vito vya thamani na mawe ya thamani yaliyo nadra.
6
Nilifika mahali hapa kwa kasi sana nikiwa nimeabiri gari la farasi wa dhahabu.Palikuwa mbali
sana na sehemu nzuri za mbinguni ambazo niliziona hapo awali.
Nikawauliza wale malaika, “naona jangwa kubwa mno na viwanja, mbona sioni nyumba?”
malaika akanijibu, “kile unachotazama ni makao”.
Niliona nyumba kubwa sana tena pana ambazo zilinikumbusha
nyumba za kuku au mabohari. Makayo haya hayakuwa mazuri
bali yalikuwa chakavu. Kijiji hiki na nyumba zile zilikuwa za zile
nafsi ambazo ziliokolewa kwa aibu. Palikuwa na nyumba
kubwa tena nyingi sana ambazo ziliikuwa chakavu. Mji huu ni
mkubwa mara kadhaa zaidi ya pahali ambapo nafsi zilizotuzwa
zinapokaa.
Malaika akasema, “ je ? Waona nyumba mbili kubwa zilizoko kushoto na kulia kwako?” nami
nikamjibu “naam nimeziona”.
Malaika akasema kwamba alitaka kunionyesha nyumba hizo mbili haswa.Akasema “nyumba
iliyopo mkono wa kulia ni ya wale waliokuwa wachungaji duniani. Nayo iliyoko mkono wa
kushoto ni za wazee wa kanisa.
Tulipofika mbele ya nyumba zile nikaona zilikuwa kubwa ajabu. Nami nikabaki kinywa wazi!.
Tulipofungua mlango na kuingia matarajio yangu yalikuwa ni kama tunaingia nyumba ya kuku.
Badala ya kuona maelfu ya kuku mahali pale, niliona nafsi . Malaika akanishauri nitazame kwa
makini kwani nitaweza kuwatambua wachungaji maarufu katika historia. Ilikuwa ukweli.
Niliwatambua wachungaji wengi katika historia. Niliwahi kumuona mchungaji mmoja
haswa,nami nikamuuliza malaika, “namjua mchungaji huyo amabaye ni mkorea, najua jinsi
alivyo kuwa maarufu na ile kazi amemfanyia Bwana . Mbona yuko hapa? Sielewi!”
Nikauliza kwa udadisi, “hii ilifanyikaje? Mbona hakuwa na vifaa vya
kumjengea nyumba?” Malaika akanijibu, “wakati alipokuwa akifanya
kazi yake ya uchungaji, alipenda kusifiwa sana na watu. Alipenda
kuheshimiwa sana. Pia alipenda kutumikiwa. Hakuwa na kujitolea wala
utumishi kwa upande wake.” Huyu mchungaji aliheshimika sana Korea
tena alikuwa bingwa mkubwa katika historia ya kanisa la Korea. Lakini
hakutunukiwa chochote!
7
Enyi wachungaji mlio huko nje, tafadhali sikieni. Inawapasa kuwaongoza watu zaidi ya ile ibada
ya jumapili kanisani. Sharti uwatembelee majumbani mwao. Sharti uwatunze masikini, viwete
na wazee.
Wachungaji waliotumikia bila ya kujitolea maisha yao, ambao walipenda kutukuzwa hawana
zawadi yoyote mbinguni.
Baada ya Mimi kuvishuhudia vitu hivi mbinguni na kurudi hapa ulimwenguni, nilipena vyote
nilivyokuwa navyo vikiwemo magari yangu ya kifahari. Maisha yetu ni ya muda mfupi tu.
Kataika bibilia maisha ya mwanadamu ni takribani miaka sabini hadi themanini. Lakini ni
Mungu pekee ajuaye atakapofariki mtu. Yeyote aweza kufa kabla ya miaka sabini au
themanini. Niliamua kupena vyote nilivykuwa navyo hata nguo zangu.
Wale niliowaona wamepokea wokovu kwa aibu walikuwa wachungaji,wazee wa
kanisa,mashemasi na hata waumini wa kawaida.Palikuwa na umati wa wazee wa kanisa na
mashemasi katika nyumba hizi chakavu. Lakini hata hivyo, ni bora kuliko jehanamu. Licha ya
hayo, mtu gani angependa kuingia mbinguni kwa njia hii?. Mimi sitaishia mahali pale pa aibu.
Hata nguo zao zilikuwa chakavu.
Ni masharti yapi yampasayo mkristu kufuata ili apate makao yanayopendeza mbinguni?
Kwanza ni sharti tueneze injili kwa watu wengi kabisa iwezekanavyo. Nasi tutaieneza injili vipi?
Malaika akaniambia, “hebu dhania kwamba pana mtu asiyekuwa muumini au asiyeokoka
ambaye hamjui Bwana. Wakati uamuapo kumuenezea injili mtu huyo, basi vifaa vya
kukujengea nyumba mbinguni vitatolewa. Unapozizdi kuuombea wokovu wao, basi vifaa zaidi
hutolewa kwa ajili yako. Lazima uendelee kuwatazama na kuwaanagali, kuwatembelea na
kuwaeleza kuhusu injili. Hii itakuongezea vifaa zaidi kwa
ujenzi wa nyumba yako.
Ikiwa mtu atasema hawezi fika kanisani kwa sababu hana
nguo nzuri basi lazima umpatie. Ikiwa mtu atasema hana
miwani ya kusomea, basi wewe mpe. Ni sharti umpe mtu
Yule chochote uwezacho ili yeye aweze kuongozwa kwa
Bwana.
Wale waishio kwenye nyumba zilizo nzuri zaidi ni wale ambao wameeneza injili kwa wingi.
Kisha malaika akanisindikiza mahali ambapo watakatifu waliishi katika makao mazuri. Hapa
ndipo walioeneza injili kwa wingi waliishi. Ilikuwa ni kama sehemu ya hali ya juu huko
mbinguni.
8
Katika historia ya ukristo kuna watu wanne ambao wana moja wapo za nyumba kubwa sana
tena za kupendeza sana. Malaika akanionyesha nyumba ya mwinjilisti wa kimarekani D.L
Moody, mchungaji wa uingereza John Wesley, mwinjilisti wa kiitaliano na mwinjilisti wa
kikorea mchungaji Choi Guu Nung. Hawa wane wana mmoja wapo za nyumba kubwa sana
mbinguni. Wanne hawa waliyatumia maisha yao yote kuieneza injili kwa watu hata mpaka
wakati wa kufa kwao.
Katika Waumini wa kikorea, palikuwa na muumini wa kawaida alieykuwa na jumba kubwa.
Huyu muumini alijenga makanisa mengi. Alikuwa amepeana magunia elfu tatu ya mchele kwa
masikini. Kwa kisiri aliwasiadia maelfu ya wachungaji na viongozi wa kanisa katika hali ya
kifedha. Yeye pia aliwasaidia wanafunzi waliokuwa wakisomea thiologia na waliokuwa katika
vyuo vya masomo ya bibilia. Alimchukua mchungaji wa miaka sitini na tano nyumbani mwake
naye akamtunza vyema.
Mchungaji huyu alikuwa amefukuzwa kutoka kanisa lake.
Nikasikia malaika akisema, “kuna vifaa vimewasili!”. Nikamhoji malaika
aliyekuwa kulia kwangu kuhusu vifaa hivi vilivyowasili, naye
akaniambia. vifaa hivi ni vya shemasi wa kike kutoka kanisa dogo. Kwa
kweli yeye hupokea vifaa kila siku. Ingawa yeye ni masikini, yeye huja
mapema kwa ibada ya asubuhi kila siku. Yeye huawaombea washirika
themanini na saba kila siku. Amalizapo kusali yeye huisafisha kanisa.
Nikasikia malaika mwingine akisema kwa sauti, “utoaji maalum
umeasili, bintiye shemasi wa kike ametoa pesa kidogo amabzo ndizo
zote alizokuwa nazo na kumpa mama yake. Lakini shemasi yule hakuzitumia kwa ajili yake
binafsi bali alimnunulia mchungaji mayai matano na jozi mbili za soksi”. Ingawa itaonekana ni
sadaka kidodgo yeye alipeana vytoe alivyokuwa navyo siku hiyo.
Hivi vikawa vifaa maalum vya kuijengea nyumba yake mbinguni.
Pili, wale ambao pia wana nyumba kubwa ni wale waliojenga
makanisa au majumba mengine kwa ajili ya ufalme wa Mungu
wakitumia rasilmali zao.
Mbinguni pia nilikutana na mzee aitwaye Choi, kati ya wazee wa
kikorea na mashemasi walioko mbinguni, yeye alikuwa na
nyumba nzuri zaidi. Nyumba yake ilikuwa ndefu kuliko jumba ndefu zaidi nchini Korea. Choi
alijenga makanisa mengi nchini Korea kwa kutumia mali yake.
9
Nikamuuliza malaika, “na nyumba yangu je?, bado iko katika hali ya kujengwa?” Naye malaika
akanijibu, “ndio”. Nikamsishi niione nyumba yangu lakini wakaniambia haikuruhusiwa. Nilizizdi
kumsishi na baada ya kusisitiza kwangu , wale malaika wakanijibu kwmaba Bwana sasa
ataruhusu.
Tukaingia kwenye gari livutwalo na farasi na tukasafiri mbali sana mpaka mahali pengine.
Nilijawa na matarajio. Nikauliza, “ nyumba yangu I wapi?” malaika akanijibu, “iko pale”. Lakini
ikaonekana ni kana kwamba mahali pale palikuwa ni msingi tu tayari kwa kujengwa.
Nami nikauliza kwa sauti, “mbona mkanifanyia hivi? Hii itawezekanaje? Itakuaje nyumba yangu
I katika eneo linalokuwa?” Nikiwa mnusurika wa vita vya kikorea , niliuza nyumba yangu ya
kipekee ili nijenge kanisa. Hili kanisa mwishowe lilikuwa hadi likawa na washirika elfu tano.
Niliandiaka vitabu vingi kwa muelekezoa wa Roho mtakatifu. Kitabu kimoja kikauza sana.
Kupitia kwa mapato ya kitabu hicho nikajenga shule ya kikristo. Shule hiyo ikawawazaa
wachungaji mia mbili arubaini. Katika hatamu yangu kama kiongozi, nilipeana udhamani kwa
zaidi ya watoto mia nne waliokuwa masikini. Nimewajengea nyumba wajane ili waishi mle. Hii
yote iligharimu pesa nyingi sana. Saa mbona mambo yakawa hivi ? kwa nini nyumba yangu imo
eneo ambalo bado linakua? nimeghadhibika sana”.
Malaika akajibu kwa ukali, “wewe haufai kamwe kuishi kwenye nyumba nzuri mbinguni kwani
umeheshimiwa na watu idadi isiyoweza hesabika”. “Kila wakatai ulipojenga au kufanya jambo
nzuri, ulisifiwa na watu. Hata vyombo vya habari huko duniani vilikusifu. Kwa ajili ya hii
matendo yako yote yalikuwa ni bure”. (Mathayo 6:1)
Nikaitazama nyumba yangu katika eneo lile ambalo ndilo mwanzo linajengwa. Lilikuwa liko kati
ya nyumba zingine tatu. Lilikuwa na gorofa tatu pekee. Nyumba yangu Ilikuwa na vyumba vingi
vidogo katika orofa mbili za kwanza. Nikamuuliza malaika. “mbona
nina vyumba vidogo hivyo?” naye malaika akanijibu” vyumba hivyo
ni vya wana na mabinti wako.” “Nina watoto wane pekee” nami
nikamjibu. Malaika akanifafanulia “la sio za watoto wa kidunia bali
ni za wale amabao uliwainjilisha na wakaokoka”. Nikapendezwa
sana nikauliza “li wapi chumba changu kikuu cha kulala?.” Malaika
akasema ki juu ya paa. Hii ikanitatiza sana. Chumba changu
hakikuwa kimemaliza kujengwa. Kwa sauti ya kukasirika nikasema,
“ni ndogo sana! Mbona ni vigumu kuimaliza?”. Malaika akajibu, “wewe bado hujafa, hatuwezi
kuimaliza nyumba yako au vyumba vyake kwasasbabu hatujui kama vifaa zaidi vitatolewa.
Umeelewa?”
10
Tulipoingia chumbani mwangu, nikaona vyeti vikining’inia ukutani , basi nikaenda kuvisoma.
Cheti cha kwanza kilieleza nilipokuwa na miaka kumi na minane nikiishi kwenye nyumba ya
watoto mayatima. Siku ya krismasi, nilikuwa narudi kutoka ibada
ya asubuhi kanisani nikamuona mzee Fulani akitetemeka pale
barabarani. Nikalitoa koti langu nikampa. Tendo hilo likanipa tuzo
mbinguni. Cheti cha pili kilieleza tukio lilo hilo lakini ilikuwa kwa
ajili ya mkate niliomnunulia mzee huyo kutumia pesa zangu kidogo
nilizokuwa nazo. Zile pesa sio muhimu. Kitendo lazima kaindamane
na imani au kujitolea kwa kweli. Kiasi cha pesa au zile dola
hazikuwa muhimu.
Tuliondoka mahali pale tukarudi. Tulipokuwa njiani mmoja wa
wale malaika akaniuliza , “ je umesononeka? Nitakuambia
jinsi ya kujengewa nyumba ya kupendeza”. “Bwana alisema
urudipo duniani, lazima uwaambie watu kuhusu mbinguni na
jehanamu jinsi ulivyzishuhudia. Pili Bwana anataka ujenge
mahali pa kuwakusanya wachungaji wazee wa kike na
mashemasi ambao hawana makao au pa kwenda.Ikiwa
utafanya hivi kwa uaminifu basi utakuwa na nyumba nzuri.
JEHANAMU
Wale Malaika wawili wakanipeleka jehanamu. Wakasema, “sasa utazuru jehanamu. Wewe
haufahamu ukubwa wa jehanamu.” Nilizizdi kusema kwa sauti “nipakubwa sana! Niapakubwa
sana!” . Hapa ndipo mahali nafsi zizlizolaaaniwa milele huwekwa. Ilihisika kana kwamba
jehanamu ni kubwa sana mara elfu kuliko dunia. Nusu ya jehanamu ilikuwa nyekundu na nusu
ingine ilikuwa nyeusi tititi. Nikawauliza malaika “mbona sehemu hii ni nyekundu?” nao
wakanijibu. “Kwani hufahamu, ni madini ya kiberiti yanayoungua. Nusu ya pili ni giza. Watu
wafanyao dhambi na kuishia hapa watateswa toka pande
zote”. Kuna makanisa mengi sana duniani na nyingi yazo
zimejawa na watu wengi amabao wengi wao sio
wakristu wa kweli. Wao ni wale wajao kanisani tu. Kanisa
za kweli zitaamini kwa ukweli kwamba kuna mbingu na
pia jehanamu.
Maisha ya wakristu wengi yana machafuko mengi kwani hawaamini kwa dhati kuwa kuna
mbinguni na jehanamu.
11
Nafsi moja iingiapo mbinguni, nafsi elfu moja zilizolaaniwa huingia jehanamu. Uwiano wa wale
waingiao mbingunia na wale waingia jehanamu ni moj kwa elfu. (Mathayo 7:14)
Mimi ni mchungaji wa kiprisbiteriani aliye fahamika sana. Nimehitimu kutoka chuo kikubwa
cha masomo ya kibilia nchini Korea. Sikuamini hivi visa kuhusu jehanamu na mbinguni. Lakini
sasa mimi ni Yule aandikaye mashuhudio yangu ili kuwashuhudia wengine.
Ingawa waweza amini wewe ni mkrsito, ikiwa unayaishi maisha kulingana na matakwa ya
mapepo basi utaishia jehanamu.
Mahali pa kwanza nilipopaona ni mahali pa madini ya kiberiti yanayoungua.wewe huwezi hata
kudariria jinsi mioto ya jehanamu ilivyo. Hakuna awezaye kuusthimili moto huo.
Watu waliojehanamu hutamka mambo matatu. Kwanza pana joto jingi na wanahisi kufa (luka
16:24)
Pili, wana kiu kingi na wanahisi kufa. Tatu utasikia wengi wakiitisha maji (zecheria 9:11)
Na mateso haya ni ya milelel!. Watu wengi husema tuko uhuru
katika Kristo nao huishi maisha yao watakavyo. Nikamuuliza malaika,
“wale waliomo humu wamefanya nini?” wakanijibu . “kikundi cha
kwanza ni wasio waumini, wale ambao hawajaziinjilisha jamii zao
lazima watubu”. Malaika akaendelea, “kundi la tatu ni la wale
waliomwamini Yesu lakini hawakutubu dhambi zao”. Ni lazima
tutubu dhambi zetu na kumkiri Yesu ni Bwana. Tusitende dhambi.
Kunyamaza tu sio kutubu. Kwa mioyo iliyopondeka yatupasa kutubu.
12
WAKRISTU JEHANAMU
Kisha nikawaona wachungaji wengi, wazee wa kanisa na mashemasi wakiwa jehanamu.
Nikawauliza malaika. “Nawafahamu watu hawa, walimtumikia Bwana kwa uaminifu wakiwa
duniani. Walifariki wakati mwingine iliopita na sote tulidhani wako mbinguni na Mungu, lakini
sasa nawaona wote jehanamu tena wanalia kwamba moto ni mkali sana, mbona wako hapa?”
palikuwa na wachungaji wengi, wazee wa kanisa,mashemasi na waumini wa kawaida wengi .
Malaika akajibu, “mchungaji Park Yong GYUU mtu anaweza onekana kuwa mfuasi wa kweli wa
Yesu kutoka nje lakini Mungu ndiye aijuaye roho ya mtu na yale yaliyomo ndani mwake”.
Hawakuichukua jumapili kuwa siku takatifu. Walipenda shughuli za kutafuta pesa jumapili. (Jer
17:27)
Mashemasi wengi na wazee wa kanisa waliyashutumu mahubiri ya
wachungaji wao .(zaburi105:15) (hesabu 12:8-9)
Hawakutoa zaka ipasavyo. (Malachi 3:9) hawakuomba.
Hawakueneza injili kwa watu kamwe . (Ezekiel 33:6). Wengi wa
wazee hawa na mashemasi waliwasumbua wachungaji wao na
kuyapinga mamlaka yao.
Waliyatatiza majukumu na shughuli za wachungaji . Wakiwa vitandani mwao karibu kufa.
Walidhani kuwa walikuwa wamefanya kazi nzuri hapa duniani, kwa hiyo hawakutubu dhambi
zao. Hii ndio sababu walitupwa kwenye mioto ya jehanamu.
Kisha nikaona mfalme na mwana wa mfalme
waliowatesa wakristo nchini Korea. Mfalme
huyu na huyo mwana wa mfalme waliwakata
vichwa wengi wa waumini wa kwanza nchini
korea. Waliwekwa katikati mwa jehanamu
ambapo moto ulikuwa mkali zaidi kuliko
sehemu zingine zote.
Niliwaona Hitler,Stalin, Mae Zedong na mhubiri mashuhuri kutoka Korea kaskazini aitwaye
mchungaji Kang, shujaa Fulani wa kijapanisi na wengine wengi.
Kisha tukawasili mahali penye giza totoro hadi hungeweza kuona mahali ukanyagapo. Nikapiga
kelele, “malaika! kuna giza jingi sana, mimi nitaonaje chochote?” malaika akanipapasa begani
mwnagu akasema “ngojea kidogo tu”.
13
Baada ya muda kidogo, niliweza kuiona idadi ya watu wasiohesabika waliokuwa uchi. Wote
walijawa na wadudu waliowatambaa miili yao . Hakuna sehemu ya miili yao iliyosazwa kwani
yote ilifunikwa kabisa na wadudu wale.
Wale watu wakiwa uchi walijaribu kuwafukuza wadudu wale huku wakisaga meno. Nikauliza ,
“ni nini walichokifanya watu hawa walipoishi duniani?”.
Hawa ni wale walioshutumiana na kusengenyana, hawakujali yale
waliyoambiana. (Mathayo 5:22) niliwaona mapepo wakizidunga na
kuzitoboa tumbo za watu wale wakitumia mundu. Singeweza
kuzistahimili kelele zao. Nikawauliza malaika, “ni nini walichofanya
watu hawa walipokuwa duiniani?”
“watu hawa walikuwa na kazi, majumba na hata jamii, lakini
hawakumtolea Bwana Mungu. Hawakuwasaidia masikini, makanisa
yao au kazi za Mungu, walikuwa wabanifu tena walafi. Hata
walipokutana na masikini waliwapuuza na hawakuwajali. Walijali tu masilahi yao na ya jamii
zao. Walivaa vizuri na kula vizuri na walikua na maisha ya starehe. Hii ndio sababu tumbo zao
zinatobolewa kwani tumbo zao zilijaa tama”. ( methali 28:27)
Lilikuwa ni jambo la kuogofya sana. Baada ya kushuhudia jambo hilo, niliporudi duniani,
nilipeana pesa na mali yangu yote kwa watu wengine. Wokovu hauwezi patikana kwa pesa au
mali. Ni kwa imani pekee. Jehanamu hakustahimiliki na ni pahali duni. Ni mahali pa mateso.
Niliona pia watu amabao vichwa vyao vilikatwa kwa msumeno mkali sana. Nikamuuliza
malaika, “ni nini walichokifanya watu hawa? Ili wastahili mateso namna hii?”
Naye akanijibu, “ Mungu aliwapa akili ili wawaze mambo yaliyo
mema tena yenya manufaa. Lakini hawa watu walikuwa na
mafikira potovu tena machafu. Walifikiri kuhusu mambo ya tama
na anasa”. (Mathayo 5:28)
Kish nikawaona watu wanadungwa na kukatwa vipande vipande.
Ilitisha sana. Nikauliza “vipi kuhusu watu hawa? walifanya nini?, Hata wateswe nama namna
hii?.” Malaika akaibu “hawa walikuwa mashemasi na wazee wa kanisa ambao
hawakuzitumikia kanisa zao. Hawakutaka wala kupenda kuzitumikia kanisa zao wala
kuzifanyia kazi. Wao walipenda tu kupokea na kupokea vitu kutoka kwa washirika wa kanisa”.
(Zecheria 11:17, hosea 6:5)
14
Nliwaona wazee wa kanisa ,mashemasi na waumini wa kawaida wakiteswa
na mapepo. Mapepo yalitengeneza shimo katika ndimi zao na kuingiza
kamba kupitia matundu yale kwenye ndimi zao. Kisha mapepo
yakawaburura kwa kamba ile. Nikauliza tena. “walifanya nini duniani?”
malaika akajibu, “wao walifanya dhambi nne tofauti. Kwanza
waliwashutumu wachungaji wao. Waliongea mabaya kuwahusu.
Waliwasengenya na kuwakejeli wachungaji wao.” ()akobo3:6)( mathayo
12:37)
Nawasihi nyote mliofanya matendo kama haya tubuni! Tubuni!
Malaika akaendelea , “pili waliwasumbua wakristo wengine hadi hata wale waliokuwa
waaminifu wakaathirika na kuacha kuja kanisani na hata wengine waliacha kuamini. Walifanya
kila wawezavyo kuwafanya wakrsisto waaminifu wasitende kazi ya Bwana. Waovu hawa
walisababisha waumni wengi wajikwae . mwisho kuna wake na waume waliokunywa pombe
na kuwatusi watu wa jamii zao. Niliona mapepo wakitoboa tumbo za waume na wake wale
kutumia msumari mkubwa. Niakuliza , “ walifanya nini hawa?
Malaika akanijibu . “ hawa ni waume na wake walioishi pamoja
pasina kuoana pia wana hatia ya uavyaji mimba kwani waliwahi
kushika mimba pia na hawajatubu.”.
Nikaoana kundi la watu. Mapepo waliikata midomo yao kama
vile mtu akatavyo nyama au mboga kwa vipande vidogo.
Niakuliza, “mbona watu hawa wanateswa hivi? Malaika
akajibu, “ hawa ni wana na mabinti , na mabinti na wana katika sheria waliojibizana na
wazazia wao. Kile iliwapasa kufanya ni kuomba msamaha badala ya kufanya mambo kuwa
mabaya zaidi. Wengi wao walitumia lugha ya matusi, waliwashambulia wazazi wao mananeo
makali.waliasi. hii ndio sababu midomo yao inakatwa viapande vidogo.”
Wandugu, sote tutakufa siku moja, lakini hatujui itakuwa lini. Tafadhali sameheaneni kila
wakati na ipasavyo ikibidi. Tubu na utubu tena na fanya hivi hata siku nzima ikikubidi.
Wandugu wapendwa nilizipuuza shuhuda kama hizi . nilikuwa mchungaji wa kiprisbiteriani wa
kihifadhina aliyepuuza mambo kama haya. Lakini sasa lazima niwashuhudie yale niliyo yaona.
15
Tafadhali usisite kuishi maisha matakatifu. Tafadhali epuka hukumu hii iliyojaa mateso mengi.
Usiishi kwa ajili ya mwili wako bali jiwasilishe kwa ufalme wa Mungu.
Tafadhali waombee wasiomjua Yesu. Waenezee watu injili na uzae
matunda ya kiroho .Tafadhali omba asubihi sana na ifanye jumapili
kuwa takatifu. Toa zaka ipasavyo. Jilimbikizie tuzo mbinguni na sio
humu ulimwenguni. Naomba na kukubariki kwa jina takatifu la Yesu.
Sunday, October 4, 2015
USHUHUDA WA KWELI WA MBINGUNI NA KUZIMU
Ushuhuda wa Rodolfo Acevedo Juu ya Mbinguni, Kuzimu na Hali ya Kanisa la Leo
Ufuatao
ni ushuhuda wa Mwinjilisti Rodolfo kutoka Jamuhuri ya Domonika, ambao
Bwana alimwonyesha kuhusiana na kuzimu, mbinguni pamoja na mambo
yanayoendelea katika Kanisa la siku za leo.
Utangulizi
Mimi
ni Mwinjilisti Rodolfo Acevedo Hernandez kutoka Jamuhuri ya Dominika. Koo langu
limeathirika kutokana na usimuliaji wa ushuhuda huu lakini bado nitafanya hivyo
tena leo hata kama kuna upinzani. Utukufu ni kwa Mungu! Tupo hapa kuhubiri Neno
la Bwana Yesu Kristo na ninaenda kutoa ushuhuda ambao ulibadili maisha yangu na
maisha ya maelfu kwa maelfu ya watu wengine!!
Hebu
tuende kwenye Ufunuo 1:14-15: “Kichwa
chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho
yake kama mwali wa moto; na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana
kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.”
Kwa
kuwa sikuridhika kuwa kwenye hali ileile ya kiroho niliyokuwa nayo,
nilijifungia kanisani kwangu kwa siku nane; siku nane za kufunga na kuomba,
nikiwa nimejifungia na Bwana Yesu. Kabla ya kuanza zile siku nane, Bwana,
aliniambia hivi kupitia maono, “Rodolfo,
ni wakati sasa ujiweke wakfu kwa ajili yangu,” na nilipewa vazi
jeupe ambalo liliandikwa maneno: “Utakatifu kwa Yehova.” Baaya ya
maono yale, mama mmoja mmisionari kutoka kwenye kanisa langu aliniambia,
“Rodolfo, niliota kuwa Bwana ananiambia nikueleze kwamba: “jitenge na madhabahu (maana nilikuwa
mhubiri); ninaenda kukuonyesha jambo kubwa ambalo litabadili maisha ya mataifa
duniani.” Kwa hiyo, ndipo nikaanza mfungo wangu wa siku nane kwa
Bwana.
Nilipata changamoto
Kwenye
siku ya nne ya mfungo na maombi, nilikuwa nikiomba madhabahuni na ghafla, mbele
yangu yalitokea mapepo mawili, ambayo niliyaona kama unavyoweza kumwona mtu uso
kwa uso. Mapepo haya yaliniambia, “Rodolfo, hatutakubali wewe uvuke kizuizi
chetu”, kisha mara moja yalitoweka. Nilianza kuwa na hofu kubwa maana unapoona
viumbe wa rohoni kimwili, inaogopesha sana! Viumbe hawa walikuwa warefu na
walikuwa na harufu ya salfa kama vile ndio wametoka moja kwa moja kwenye shimo
la jehanamu. Walitumwa kuja kuniambia kuwa hawako tayari kuruhusu mimi nivuke
kizingiti walichoweka. Lakini shetani ndiye pekee mwenye ukomo; Bwana Yesu
Kristo alimshinda kwenye msalaba wa Kalvari. Utukufu kwa Mungu, haleluya!
Zilipopita
siku saba, nilimwambia Bwana, “Bwana, siwezi kuendelea zaidi. Mwili wangu ni
dhaifu. Sina nguvu za kutosha. Bwana, tafadhali nisaidie. Siwezi kutimiza jambo
hili. Tafadhali, nisamehe; nipe nguvu.”
Ghafla,
nilihisi mtu anatembea nyuma kuelekea kwangu, na akasema sikioni mwangu, “Rodolfo, usiache kuendelea na jambo hili
hadi tukuonyeshe mambo ambayo uko karibu kuyaona.” Nilitiwa moyo na kujisikia ni mwenye nguvu
zaidi. Siku iliyofuata, ilikuwa ni Jumapili. Nilijisikia dhaifu kidogo asubuhi.
Jioni wakati wa ibada, kulikuwa na ujumbe wenye nguvu kutoka kwa
Mwinjilisti Ruben Bells. Alipomaliza,
nilikuwa nawasalimu ndugu zangu wote katika Kristo. Nilianza kuhisi kama pumzi
zinaniishia. Nikawa nashindwa hata kupumua.
Ndugu
wa kanisani wakanizunguka na kuanza kuomba. Ghafla, nilihisi kana kwamba
kupitia kucha na vidole vyangu, kulikuwa na sindano zinapenya mwilini mwangu.
Ubaridi wa zile sindano ulipenya mwilini kama hewa ya baridi na nikahisi pumzi
yangu ya mwisho imeondoka na kwamba moyo wangu umesimama. Nilidondoka sakafuni
na ndugu zangu wakaanza kujaribu kuniamsha. Walikuwa kama ndugu 12 hivi.
Ghafla, nilihisi roho yangu ikitoka kwenye mwili na nikawa nautazama mwili
wangu nikiwa nje, ukiwa umelala sakafuni. Hao wapendwa hawakujua kilichokuwa
kikiendelea kuhusiana na mimi. Dada mmoja ambaye alikuwa ni nesi aliwaambia,
“Amepata mshtuko wa moyo.” Nilikuwa natamani kwenda kwao na kurudi kwenye mwili
wangu lakini nikawa nashindwa.
Kuzimu
Ghafla,
nilihisi mwanga umepotea na nikaanza kupaa juu. Kule juu kuna mtu
alinisimamisha na nikaanza kushuka chini hadi nikafika mahali ambako nilihisi joto
kali mno! Kisha, nikaona milango miwili myeusi inayonuka sana. Hapo ilikuwa ni
kuzimu na kulikuwa kunatisha sana!
Nilipokuwa
ndio niingie ndani ya ile milango, joka kubwa, ambalo kichwa chake kilijaa
miiba na mwili wake ulifunikwa kwa nyembe badala ya magamba ya kawaida,
lilitangulia kuingia kwenye gereza hilo. Nilipokuwa naingia kwenye milango ile,
niliona macho ya kila aina ukutani, yakiwa yananiangalia. Lakini macho yale
yalikuwa yamechorwa ukutani. Mara niliona macho mawili yananijia na kumbe lilikuwa
ni pepo ambalo kifuani lilikuwa na bamba lililoandikwa: ‘Mimi ni Kisasi.’
Hukumu ya watumishi wasio waaminifu
Wakati
huohuo, mapepo zaidi yalianza kutoka ukutani. Lile pepo linaloitwa Kisasi
lilisema kwa sauti, “Mfalme Belzebub, tumempata mmojawapo aliye mkubwa ambaye
aliendesha vita dhidi ya sisi, ufalme wa giza …” Biblia inasema: “Maana ingalikuwa heri kwao kama
wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu
waliyopewa.” (2 Petro 2:21). Kanisa linalomjua Bwana ni lazima
liendelee kuwa thabiti na kutambua kuwa Yesu ndiye tumaini PEKEE kwa ajili ya
wokovu wa roho zao.
Nikiwa
ningali pale, lile pepo Kisasi lilikuja karibu yangu na kuniambia, “Rodolfo,
nataka unitoe kama ambavyo ulifanya kule duniani.” Lilipokuwa likisema haya
tena na tena, lilikuwa linaendelea kunitesa. Na nikaona mapepo mengi
yamejipanga tayari kwa ajili ya kunitesa!
Mateso
ya kuzimu kwa ajili ya wachungaji, wahubiri, na wainjilisti wanaoacha nguvu na
upako wa Mungu ni makali zaidi kuliko yale ya roho zingine kule kuzimu! Uwe
thabiti katika mwendo wako na Mungu! Hii ni saa ya Kanisa kuwa imara. Wakati ni
sasa. Muda wa kuchezacheza kanisani umeshapita. Ni lazima tuwe na ujasiri na
kuzishinda nguvu za kuzimu kwa jina la Yesu – Yeye peke yake ndiye nuru.
Mara
kulitokea pepo lililoruka na kutupa mkuki kwangu ambao ulipita kwenye moyo
wangu. Nilihisi maumivu yasiyoweza kuelezeka. Pia nilihisi kama vile kulikuwa
kunanyesha salfa kule kuzimu. Nilihisi nyama ya mwili wangu inatoka kwenye
mifupa na minyoo ikaanza kupekecha mifupa yangu.
Biblia
inasema,“ambamo humo funza wao
hafi, wala moto hauzimiki.” (Marko 9:48); na pia kwenye inasema, “Funza wametandazwa chini yako, na vidudu
vinakufunika” (Isaya 14:11). Kuzimu ni mahali halisi. Yesu na Agano
la Kale wanazungumzia kuhusu kuzimu.
Mara
niliona kundi la mapepo wanaleta jeneza, lakini lilikuwa ni jeneza tofauti na
haya tunayoyafahamu hapa duniani. Lile pepo Kisasi lilinishika sehemu ya chini
ya mdomo wangu na kuniambia kwa dhihaka,
“Rodolfo, nataka unitoe! Nguvu zako ziko wapi? Upako wako uko
wapi? Uko wapi utukufu wako uliokuwa nao?”
Ujumbe
ninaotaka uupate hapa ni kuwa, wakati mwingine kwa sababu tunahubiri, tunadhani
kuwa upako ule ni wetu, na kwamba zile nguvu ni zetu, na kwamba uponyaji ni
wetu. Biblia inasema kuwa utukufu unatoka kwa Mungu na utukufu ni wake pekee.
Kwa sababu hiihii, ibilisi alitupwa nje ya Mbingu maana alitaka kutwaa utukufu
wa Mungu. Kwa hiyo, wengi wanadhani kuwa wagonjwa wanaponywa kutokana na nguvu
zao; na wenye mapepo wanafunguliwa kutokana na nguvu zao! Acha nikuambie kuwa,
kile ambacho Bwana amekupa ni zawadi kutoka mbinguni. Ni rehema za Mungu kwa
lengo la kuwafungua wanaoteswa, na pia ili roho ziweze kuokolewa.
Mimi ni ‘Niko’
Mapepo
yalipokuwa yananiingiza kwenye lile jeneza, nilihisi upepo na kama kuna kitu
kimedondoka sakafuni. Pepo Kisasi na mapepo mengine yalikimbia haraka na
kujificha mbali na uwepo wake. Nilikuwa niko sakafuni kutokana na kuteswa na
yale mapepo; na jambo la kwanza nililoona ambalo sitakaa nilisahau … Oh,
Utukufu kwa Mungu! Niliona ‘mtu’ akiyejaa nuru … Haleluya!
Niliona
makovu kwenye miguu yake. Nilipoinua kichwa changu, nilimwona huyu mtu wa
ajabu, akiwa na mkanda kifuani mwake ulioandikwa: “Mimi ni MFALME WA WAFALME,
na BWANA WA MABWANA.” Alikuwa amevaa taji kubwa sana la dhahabu kichwani
mwake. Alinyoosha mkono wake kwangu na
kusema, “Rodolfo, MIMI NI YESU na
ninaenda kukuonyesha mambo mengi humu kuzimu, mbinguni pamoja na hali ya Kanisa
langu duniani.” Alinishika mkono na kusema, “Twende sasa, Rodolfo.”
Ukahaba
Niliona
amefungua chumba kikubwa ambamo kulikuwamo mwanamke. Akasema, “Naenda kukuonyesha adhabu ambayo shetani
huwapa wale ambao walikuwa wakifanya ukahaba duniani. Kahaba anapokufa, anakuja
kwenye sehemu hii. Angalia kwa makini, Rodolfo.” Niliangalia na
kuona ndani ya chumba kile, mwanamke ambaye alikuwa amekaa mkao wa hatari sana,
na nikaliona joka lilelile ambalo nililiona hapo mwanzo. Joka hili liliingia
kwenye chumba kile kisha likajiingiza kwenye sehemu zake za siri. Kumbuka
nilikuambia kwamba ngozi ya joka hili haina magamba ya kawaida bali ni
nyembe.
Joka
hilo lilipoingia, lilimharibu kabisa viungo vyake vya ndani, kisha likatokea
mdomoni. Pepo linalosimamia ukahaba duniani linaitwa, “Metresa” au “Martha”, au
“The Domineur”. Wakatoliki wengi wana “mtakatifu”
huyu akiwa kama mwanamke ambaye mwili wake umeviringwa na nyoka; na pepo
hili ndilo ambalo linawatesa makahaba kuzimu.
Bwana
aliniambia kwamba ulikuwa ni wakati wa kuondoka hapo na tukamwacha mwanamke
yule akilia kutokana na mateso na maumivu. Alikuwa akisema, “Nahitaji mtu wa
kunisaidia!” Bwana akaniambia, “Rodolfo,
hukumu imeshawekwa kwa ajili yao! Sasa
Rodolfo, nitaenda kukuonyesha sehemu ambako shetani anawatesa wanawake ambao
walitoa mimba za watoto wao duniani!”
Utoaji mimba
Ghafla,
nilimwona mwanamke akiwa katika mkao wa kujifungua na nikaona pepo baya sana
ambalo mikono na miguu yake ilikuwa kama ya farasi na mwonekano wake kama wa
mnyama na alikuwa na keekee (drill) mikononi mwake. Keekee hii ilikuwa imejaa
minyoo. Minyoo hii ilikuwa ni mikubwa sana na meno yao yalikuwa makali na miili
yao ilijaa miiba iliyochongoka. Pepo lile liliingiza ile keekee kwenye sehemu
zake za siri hadi akaonekana kama mwenye mimba.
Pepo
lile likaanza kumpigia kelele, likimwambia kuwa azae huko kuzimu kwa kuwa
alikataa kuzaa duniani. Kisha likasema, “Utukuzwe, utukuzwe shetani! Huu ni
ufalme wako!”
Nilipomwuliza
Bwana kwa nini adhabu ilikuwa kali kiasi kile kwa mwanamke yule, Bwana akasema,
“Rodolfo, adhabu imeshawekwa kwa
ajili ya mwanamke huyu!” Biblia inasema kwamba wauaji hawataingia
kwenye Ufalme wa mbinguni. Watu
wanatoa mimba au kuwaua watoto huku wakiamini kuwa huko ni kama kuua tu mnyama
lakini kile hasa wanachofanya ni kuua mwanadamu mwenye roho na mwili.
Pepo
lile liliendelea kumpazia sauti, likimwambia amtukuze shetani maana ule ulikuwa
ni ufalme wake. Wale minyoo walianza kutoka kupitia tumboni mwa yule mwanamke
huku wakiharibu kabisa sehemu za ndani ya mwili na kutoka wakiwa na vipande vya
nyama midomoni mwao. Ungeweza kuona maumivu makali aliyokuwa akiyahisi. Bwana
akaniambia, “Tuondoke kwenye sehemu hii.”
Shetani anashambulia watoto na familia
Tulienda
kwenye sehemu iliyoonekana kama kuna fito nyeusi. Nikaanza kuona watoto wengi
kule kuzimu. Nikamwuliza Bwana, “Kwa nini kuna watoto huku kuzimu?” Lakini
Bwana akaniambia kuwa wale hawakuwa watoto; na kwamba ufalme wa mbinguni ni wa
watoto na inabidi uzaliwe upya ili kuingia kwenye ufalme wa mbinguni.
“Sasa,
Bwana vipi kuhusu watoto hawa?” niliuliza.
Bwana
akaniambia tena, “Rodolfo, hawa si
watoto”, kisha akaniambia nisikilize maagizo ambayo shetani alikuwa
anawapatia.
Nilipogeuka,
nikaona kuwa kumbe hawakuwa watoto bali ni mapepo na walikuwa wanacheza mchezo
unaoitwa Nintendo. Nikaanza kuona kila aina
ya ‘programming’ na michezo ya kishetani, huku wakitoa alama na mijongeo kwa
kutumia mikono yao, vyote vikiwa na makusudi ya kishetani.
Bwana
alipowaamuru wageuke, ndipo nikaona jinsi sura zao zilivyo mbaya, za kutisha na
zinazotia kinyaa. Shetani aliwapa maagizo akisema, “Wanangu, nendeni mkaue,
mkaibe, na kuharibu.” Alikuwa yuko sahihi kwa sababu Biblia inasema kuwa
shetani haji ila kuiba, kuchinja na kuharibu lakini Yesu alikuja ili kuleta
uzima na uzima tele. (Yohana 10:10).
Wakati
huo, hivi vipepo vidogo viliingia duniani na Bwana akaniambia kuwa hii ndiyo
sababu watoto wa duniani wanajiua. Hivi sasa, wanasayansi na wanasaikolojia ya
watoto hawaelewi ni kwa nini watoto wanajiua. Miezi michache iliyopita, mtoto
wa kiume wa miaka 12 alimuua mama yake kwa kisu; mwingine alijinyonga hapa
Marekani; na mtoto wa miaka 7 alimwua mama yake, wadogo zake na yeye mwenyewe
kwa bastola ambayo aliipata. Mtoto mwingine alijitupa kutoka ghorofa ya pili na
kufa. Barua wanazoacha hawa watoto zinasema kuwa maisha hayana maana pamoja na
mambo mengine mengi.
Haya
yanatokea kwa sababu mapepo yanaingia kwenye miili yao na kutawala fahamu zao
na kuwafanya wachukue uamuzi wa kujiua. Iweni makini enyi wazazi na kile ambacho
watoto wenu wanaangalia kwenye televisheni. Kile ambacho watoto wenu
wanaangalia kwenye intaneti au wanachosikiliza kwenye redio kina athari kubwa.
Mapepo yanaingia kupitia televisheni, redio, muziki na michezo ya vichekesho ya
kishetani. Utukufu ni kwa Mungu, haleluya, kwa kutuamsha!!
Kisha
Bwana akaniambia, ni kwa sababu hii ndoa nyingi zinaharibiwa, maana baadhi ya
wazazi wanalaumu watoto wakidhani kuwa kwa sababu ya mtoto fulani, basi ni
lazima wapeane talaka. Lakini mtoto si tatizo. Tatizo ni mashambulizi ya kipepo
dhidi ya umoja wa ndoa na familia. Mwiteni Yesu Kristo! Liite Kanisa! Omba
ufanyiwe maombi ili kuwa na nyumba isiyo na mashambulizi ya kipepo! “Sasa,
Rodolfo,” Bwana akasema, “ni
wakati wa kutoka wenye sehemu hii.”
Ibada ya sanamu
Tulipotoka
kwenye sehemu ile, nilimwona mwanamke ambaye alikuwa amemezwa kabisa ndani ya
moto. Mwanamke huyu alikuwa akilia sana akisema, “Kufa, kufa, kufa! Nitoe
humu!”
Kile
nilichoona ni kwamba, mwanamke huyu alishika mikononi mwake picha ya ‘Moyo mtakatifu
wa Yesu’ kulingana na taratibu na mapokeo ya Kikatoliki.
Nikauliza,
“Bwana, huyo ni mwanamke gani?”
Bwana
akasema, “Rodolfo, mwanamke huyo ni
bibi yako.” Biblia inasema kuwa waabudu sanamu hawataingia kwenye
ufalme wa mbinguni (Gal. 5:20, Efe. 5:5). Bwana alinionyesha maisha ya
bibi yangu yalivyokuwa duniani na nikaona kwamba kweli alikuwa ni mwabudu
sanamu. Nikasema, “Bwana, tafadhali msaidie.”
Bwana
akaniambia, “Rodolfo, sina cha
kufanya! Hukumu imeshawekwa kwa ajili yake!” Kisha akaniambia, “Naenda kukuonyesha kile ambacho kitakuletea mateso duniani. Wengi hawataamini
kile ambacho unaenda kukiona. Lakini usiwe na wasiwasi, nitakuwa pamoja na
wewe.”
Celia Cruz (Malkia wa Salsa) yuko kuzimu
Mara
nilimwona mwanamke ambaye miguu yake ilikuwa inapondwapondwa kwa visu ambavyo
vilifika hata kwenye magoti yake kwa wakati uleule. Mwanamke huyu alikuwa
akiteswa na mapepo mengi.
Bwana
alinionyesha video ya Celia Cruz akifanya mikataba ya kishetani kule Hollywood
kwa kutumia damu; na nikamwona akifanya mambo mengi ya kishetani. Bwana
akasema, “Alikuwa ni mwabudu
shetani. Alikuwa ni mfanya ibada ya sanamu. Alikuwa ni mchawi akiwa na maagano
mengi ya damu. Kwa hiyo, muziki wake ulikuwa ukishika sana chati za juu.
Ilikuwa ni vivyo hivyo kwa kundi lake la wanamuziki.” Na Bwana
akanisikizisha muziki wake mmoja unaoitwa ‘Yemaya’, ambao ni maarufu sana kwenye
ulimwengu wa Kihispania. Lakini unapoimba wimbo ule na kurudiarudia, maana yake
hasa ni: ‘Mfalme shetani, njoo utawale ndani yangu!’ Na Bwana akaniambia, “Hukumu imeshapangwa kwa ajili ya Celia Cruz.”
Mwasisi wa Mashahidi wa Yehova yuko kuzimu
Tuliendelea
kutembea na Bwana akanionyesha mwanamume mmoja mweupe ambaye mikono yake
ilikuwa imetanuliwa. Na kitu cha ajabu kuhusiana na mtu huyu ni kuwa alikuwa na
upanga mzuri sana ndani ya ulimi wake na upanga huu ulipenya hadi kichwani na
kutokeza nje. Miguu yake ilikuwa imefungwa kwa minyororo na mgongo wake ulikuwa
umejaa nyembe sehemu mbalimbali kwa namna kwamba, vyovyote ambavyo
angejisogeza, ni lazima zinamkata. Nilipomwona mtu huyu katika hali hii,
nikamwambia Yesu, “Bwana, tafadhali
msaidie. Fanya kitu, Bwana Yesu. Hebu ona jinsi anavyoteseka kwa maumivu.”
Bwana akaniambia, “Je, unajua huyu
ni nani?”
“Hapana,
Bwana,” nilisema. Niliona jinsi visu vilivyopenya kwenye ngozi yake na kisha
kwenye mifupa na jinsi vilivyotokeza upande mwingine. Mtu huyo alipiga tu
kelele kwa maumivu.
Bwana
akaniambia, “Hukumu juu ya mtu huyu
imeshatolewa. Sasa nitakuambia huyu ni nani.”
Kutokana
na unabii huu, Bwana akasema, “Itakubidi
kukimbia kutoka mji mmoja hadi mwingine maana jambo hili litakuletea mateso makubwa,
lakini nitakuwa pamoja na wewe.”
Akaendelea kusema, “Rodolfo, huyu
mtu ni Charles T. Russell.” Nikasema, “Bwana, yeye ni nani?” Bwana
akaniambia kwamba mwanamume yule alikuwa ni mwanzilishi wa kanisa la Mashahidi
wa Yehova. Nikaomba, “Bwana, tafadhali msaidie,” na Bwana akasema, “Hapana, Rodolfo.” Kisha Bwana
alifanya ishara kwa mkono, na mara moja nikaona roho nyingi zikiangukia kwenye
shimo la kuzimu kwa kila namna. Walikuwa wakiangukia humo kichwa kwanza, miguu
kwanza, tumbo kwanza, n.k.
“Rodolfo, kutokana na huyo mtu aliyelaaniwa,
roho hizi zote zinaangukia kuzimu. Mtu huyu alifundisha kwamba Mungu ni Mungu
wa upendo tu. Biblia inasema kwamba Mungu ni moto ulao. Mtu huyu, Charles
Russell, aliondoa maneno ‘hell’ kutoka
kwenye Biblia na akaondoa maneno yote ‘sheol’ na ‘Abaddon’. Pia, alikana uungu
wa Yesu Kristo na pia alikana uungu wa Roho Mtakatifu, halafu akaweka tu neno
Yehova kwenye Biblia. Aliondoa maneno Yesu na Roho Mtakatifu. Kutokana na mtu
huyu aliyelaaniwa, roho hizi zote zinaangukia kuzimu.” (Ufu.
22:18-19). Kisha Bwana akasema: “Namlaani
mtu huyu.”
Tafadhali
enyi Mashahidi wa Yehova mnaonisikiliza wakati huu, si lengo langu kuwakwaza.
Tokeni ndani ya kundi hilo na mje kwa Yesu haraka. Mimi siwachukii na wala
sichukii dini yenu lakini mko ndani ya mahali pabaya. Njooni kwa Yesu.
Anawangoja kwa mikono iliyo wazi kabisa. Charles Russell yuko kuzimu kwa sababu
alifundisha uongo!! Msifuate uongo wake.
Tulipoondoka
sehemu hii, milango hii ya gereza ilijifunga na moto ukawaka na mwanamume huyu,
Charles Taze Russell, alipiga kelele na kumlaani Yesu tena na tena kwa sababu
Yesu alisema, “Hukumu imeshaamuliwa
kwa ajili ya mtu huyu.”
Kisha
Bwana akasema, “Rodolfo, sasa
nitakuonyesha magereza meusi ya kuzimu. Hii ni adhabu ya kupita kiasi ya shetani
kwa roho zilizoko kuzimu.”
“Hapana,
Bwana, tafadhali! Tayari nimeshaona mambo ya kutisha. Niondoe hapa, tafadhali
…”
Bwana
akasema, “Haya, Rodolfo, sitafanya
kingine chochote kama hauniruhusu. Nitakupeleka mbinguni sasa.”
Mbinguni
Tuliondoka
kwa kasi sana na tukafika mahali hapa. Malaika wawili walinisimamisha mbele ya
milango hii iliyokuwa mizuri sana. Walikuwa wazuri
sana. Hawa malaika wawili
waliniambia, “Rodolfo, ukiwa na mavazi hayo ya dhambi, huwezi kuingia kwenye
ufalme wa Mungu.” Kwa hiyo, walinipatia mavazi mapya ambayo yameandikwa: Utakatifu.
Ujumbe sahihi
Wachungaji,
wainjilisti, wahubiri na wamisionari, tafadhali samahanini na mnisikilize.
Mungu hajawaita kuhubiri kuhusu utajiri au unabii juu ya hilo. Mungu amewaita
kuhubiri kuhusu utakatifu na utakaso, maana bila utakatifu, hakuna atakayemwona
Bwana. Pelekeni neno la utakatifu na
kulihubiri!!!
Malaika
waliniruhusu kuingia na Yesu alikuwa ananingoja na akaniambia, “Rodolfo mwanangu, karibu kwenye Ufalme wa
Mungu wako.” Tulianza kutembea. Niliona kuwa barabara zilikuwa za
dhahabu tupu, na nikaona mto uliokuwa kama kioo; ni maji halisi! Niliona pia
almasi na mapambo kwenye mitaa, kitu ambacho watu wa duniani wanaweza kuuana
kwa ajili yake! Kisha Bwana alinishika mkono na kuniambia, “Sasa
nitaenda kukuonyesha hekalu.” Hekalu lilikuwa zuri sana! Niliona
bilauri za dhahabu, vyombo vya dhahabu na nikasikia wimbo mzuri ambao ulikuwa
unaimbwa na watoto. Bwana akaniambia kuwa waliokuwa wanaimba ni watoto ambao
duniani watu waliwakataa lakini wana uzima kwenye ufalme wa mbinguni. Utukufu
kwa Mungu, haleluya!
Mavazi ya harusi, chakula cha harusi, mataji
Tuliendelea
kutembea mbinguni na nikaona mavazi meupe mazuri, yaliyopambwa kwa dhahabu
pamoja na mataji juu yake. Bwana akaniambia lilikuwa ni Kanisa lake. Kwamba
linatakiwa kuwa takatifu na lililotakaswa. Taji ni taji ya uzima na kwamba
Bwana atakwenda kulipatia Kanisa.
Tulipotoka
pale, niliona msururu mrefu wa watu waliovaa mavazi meupe. Niliona malaika
wawili wakubwa, wenye sura nzuri ukiwatazama machoni. Niliona amani na upendo.
Malaika mmoja akasema, “Karibu kwenye ufalme wa Mungu wako.” Malaika mwingine
alipiga makofi. Niliona jinsi watu walivyo na furaha kuwa pale na sasa naelewa
kile ambacho mtume Paulo alichosema kwamba, mateso ya dunia hii yanayopita si
lolote ukilinganisha na utukufu unaotungojea kule mbinguni.
Bwana
alinipeleka mahali ambako niliona meza ndefu sana isiyo na mwisho. Meza ilikuwa
ya dhahabu. Kitambaa kilichoifunika kilikuwa cha dhahabu, bilauri za dhahabu,
visu na nyuma za dhahabu, viti vya dhahabu, n.k. Kisha nikaona mataji makubwa
kwa madogo na Bwana akaniambia kuwa yale mataji makubwa ni ya watumishi wake,
pale watakapokuja kwenye harusi ya Mwanakondoo.
Akasema, “Kwa vile harusi ya
Mwanakondoo iko karibu kuanza, niko karibu kuja kuchukua Kanisa langu. Waambie
kuwa ninakuja kulichukua Kanisa langu.”
Nikamwuliza
Bwana, “Je, na haya mataji madogo ni ya nani?”
Akasema, “Hayo mataji madogo ni ya watu walio ndani ya Kanisa ambao wanaishi katika utakatifu lakini hawafanyi chochote kwa ajili ya Ufalme. Lakini nakwambia, usiridhike kupokea taji dogo bali fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya taji kubwa. Fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Mungu ili aje kukupa thawabu ya uzima.”
Akasema, “Hayo mataji madogo ni ya watu walio ndani ya Kanisa ambao wanaishi katika utakatifu lakini hawafanyi chochote kwa ajili ya Ufalme. Lakini nakwambia, usiridhike kupokea taji dogo bali fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya taji kubwa. Fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Mungu ili aje kukupa thawabu ya uzima.”
Jambo
la ajabu lilikuwa kwamba, kila kiti kina jina nyuma yake na hakuna mtu mwingine
yeyote ambaye atakikalia zaidi ya mwenye jina hilo!
Hali ya Kanisa la leo
Bwana aliniambia, “Sasa Rodolfo, naenda kukuonyesha hali halisi ya Kanisa ilivyo hivi
sasa.”
Nilimwona samaki mdogo akimsifu na kumwabudu Yesu kwa sababu Biblia inasema: Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana! (Zab 150:6).
Kwa
hiyo, Bwana alinionyesha dunia ambako ningerudi kwenda kuhubiri kile
nilichokiona. Lakini nikawa na picha kwamba sikuwa na kumbukumbu kuhusiana na
dunia na Bwana akanipa ufahamu kwamba, mtu anayeingia mbinguni, anasahau kila
kitu kilichotokea duniani! Lakini sivyo ilivyo kuzimu. Kila anayeingia kuzimu,
anakuwa na kumbukumbu za kila kitu alichotenda alipokuwa duniani, familia zao,
na kwamba wasingependa waende kuzimu! Hayo nayo ni mateso mengine yanayoongezwa
juu yao. Lakini yule anayeingia mbinguni, akili yake inabadilishwa ili ifanane
na ufahamu wa kimbingu.
Bwana
asifiwe! Kwa sababu hiyo, si Petro, wala Mariamu, wala Stephano, wala Elisha au
Yohana mwenye kumbukumbu ya kile alichofanya alipokuwa duniani. Baada ya maisha
yao ya duniani, wala hawana tena habari kamwe na kile kinachoendelea hapa.
Petro wala hawezi hata kuwaza kuwa Kanisa Katoliki wanamwomba yeye au mtakatifu
mwingine yeyote. Na Yesu akasema, “Hakuna jina jingine chini ya mbingu
litupasalo kuokolewa kwalo.” Huyo ni Yesu Kristo, Mwana wa Mungu
Aliye Hai. Na Mariamu alisema kule kwenye harusi ya Kana, “Lolote
atakalowaambia, fanyeni.” Na … waabudu shetani wako Vatican. Wanaficha njia
zote za dhambi za makasisi kutembea na watawa; makasisi kutuhumiwa kunajisi
watoto na hata hapa kwenye Jamuhuri ya Dominika. Na Wakatoliki wanaendelea
kuamini uongo huo. (Tafadhali ona pia ushuhuda mwingine wa ajabu: “Prepareto meet your God – Angelica Zambrano” Sehemu ya 1&2
ambao unaongelea zaidi kuhusiana na masuala ya Ukatoliki).
Watumishi wanaolenga fedha na wasio waaminifu
Sasa
Bwana alianza kulia pale alipoanza kunionyesha mimi hali ya Kanisa. Ghafla,
nilimwona mchungaji duniani amebeba begi kubwa lililojaa fedha. Bwana
akaniambia, “Hawa ni wahubiri na
wainjilisti wanaojitajirisha kutokana na matoleo kwa sababu wanafundisha uongo
kwa watu wangu na kuwafanya watu wangu wapotee.”
Nawaambia
enyi wahubiri na wainjilisti, mhubirini Yesu hata kama hakuna zaka au sadaka
mnazopokea. Litakaseni Kanisa!
Mara
niliona fedha za kwenye lile sanduku zimetoweka. Nilimwuliza Bwana naye
akaniambia, “Kama ambavyo fedha zake zimetoweka, ndivyo na yeye atakayotoweka pamoja
na mpinga Kristo. Lakini bado ninayo masalia ya watu wangu ambao
hawajanajisika.”
Naona
siku hizi jinsi wahubiri wengi, wachungaji, wainjilisti, n.k. walivyo matajiri
na mamilionea. Hata hivyo, waumini wa makanisa yao wanaogelea kwenye umaskini,
uhitaji wa chakula, huku mchungaji akiwa katika utajiri na wala hawasaidii!
Wainjilisti wengi ni mamilionea wakubwa na hata mabilionea wakiwa na magari ya
kifahari kupita kiasi. Je, Msamaria mwema yuko wapi?
Pia
niliona wachungaji wengi wakihudumu kwenye madhabahu lakini nikamwona huyu
mmoja akimalizia kuhudumu siku ile, akaondoka nyumbani alikokuwa mke wake, na
kwenda kukutana na hawara yake ambaye anaishi naye pia; huku akiwa naye ni
mshirika wa kanisa lake!
Nilimwona
pia mwinjilisti akiondoka kanisani kwake na baada nyumba chache tu kutoka
kwenye kanisa, akaenda kukutana na kahaba. Ni mwinjilisti yuleyule aliyekuwa
akihudumu kwenye madhabahu! Bwana, tafadhali uturehemu!
Matendo yasiyo matakatifu – kujichua
Baada
ya hapo, Bwana alinionyesha kundi la vijana wa Kanisa, kwamba wanapoondoka
kanisani wanaenda kwenye sehemu ya giza maana wanadhani kuwa Bwana hawaoni.
Wanapoenda huko wanaanza kujichua (kupiga punyeto) na kuzini dhidi ya miili yao
wenyewe. Baada ya hapo, wanarudi na kuhudumu madhabahuni! Viongozi wa vijana,
viongozi wa Kanisa! (Kama unahitaji msaada wa kushinda dhambi hii,
angalia video hii).
Muziki usio na utakatifu kanisani
Sasa
Bwana alinionyesha disko na Kanisa na akaniambia, “Angalia kwa makini.” Na mimi nikaangalia na kuona kwamba
Kanisa lilikuwa ni sawasawa tu
na lile disko! Hakukuwa na tofauti yoyote!
Walikuwa na mfumo uleule wa sauti, muziki uleule! Vifaa vilevile kutoka duniani
vinaingia kanisani!
Dunia
inatakiwa kubadilika iingie kwenye Ukristo lakini si Ukristo kuingia duniani!
Tunaileta dunia kanisani! Pia niwaambie hili: Hatuwezi kumsifu na kumwabudu
Mungu kwa kutumia Reggaeton, kwa Bachaton au Rock. Hata leo zipo nyimbo za
Kikristo anazoimbiwa Mungu na pia zinaimbwa duniani kwa kutumia maneno
yaleyale! Hazimtaji Mungu bali zinataja tu neno ‘upendo.’
Niliona
pia muziki wa Rap na Perreo kanisani na hilo halikubaliki. Biblia inasema kuwa
tunatakiwa kumwabudu Bwana katika uzuri na utakatifu (kwa ajili ya kuabudu kwa
kweli, tazama Kol. 3:16 na Yoh. 4:23-24). Muziki wa Rock ni wa kishetani na
ulibuniwa kuzimu. Wachungaji na
wainjilisti, tafadhali, ondoeni makanisani muziki huo uliolaaniwa!!!
Bwana alinionyesha wanamuziki ambao wameshapotoka.
Kwa upande mmoja wanaimba kanisani, na kwa upande wa pili wanaingia mikataba ya
kuimba hata kwenye mahoteli kama waimbaji wa kujitegemea. Wanaenda kanisani
kumsifu Bwana!
Ngoja niwaambie: muziki kama huo Bwana wala
haukubali na tafadhali, samahani, ni lazima niwaambie ukweli - kile kinachotoka
kwa Mungu ni kitakatifu na kimetengwa kwa ajili ya Mungu peke yake. Na kile
ambacho wanamuziki wa leo wanakifanya, wanaenda kuimba kanisani, kisha
wanapotea kutoka kwenye huduma, maana wanaonekana kama vile wanamwimbia Mungu
kwa mkataba. Kwa hiyo, wanadhani hawana ulazima wa kuwapo pale muda wote wa huduma;
wanaondoka mapema. Bwana aliniambia, “Kwa
bahati mbaya, kanisa la aina hiyo halitaingia kwenye ufalme wa mbinguni.”
Masalia walio watakatifu
Baada
ya hapo, Bwana alinionyesha kundi la watu – maelfu kwa melfu ya watu
wanaojilinda katika utakatifu. Kwa mfano, nilimwona dada akimwambia mwingine, “Umekula
leo? Nina kipande cha mkate nyumbani.” Nilimwona mwingine akiwa amebeba jozi ya
viatu akimpelekea mwingine ambaye hana. Nikamwona mwingine akiwatia moyo wale
wasio na nguvu. Wengine, kutokana na kujua matatizo ya wenzao, walikuwa
wakiwasaidia na kuwaombea katika mahitaji yao bila mtu mwingine kujua.
Lakini
leo, katika makanisa mengi, kuna masengenyo mengi kwa sababu watu hawajui kukaa
kimya kuhusiana na watu wengine. Tubu leo! Yesu Kristo anataka kukupatia
ukombozi na wokovu. Anaweza kukupatia zawadi ya toba.
Utukufu
kwa Mungu!
Msifuni na kumwabudu Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana!
Msifuni na kumwabudu Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana!
Rehema
zake zadumu milele.
Mwinjilisti
Rodolfo Acevedo
Subscribe to:
Posts (Atom)
AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1)
http://bit.ly/3JGDJ4d MWL. JAMES F. MZAVER Minister Truth 0762759621 jamesmzava@gmail.com AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1) Ukuaji ha...
-
JINSI YA KUTAMBUA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO NA; JAMES F. MZAVA Bwana Yesu asifi...
-
KUPAMBANA NA ROHO YA HOFU NA KUISHINDA na:James F.Mnzava Bwana Yesu asifiwe sana.Nakukaribisha tena katika mfululizo wa masomo y...
-
KARAMA ZA ROHONI NA UTENDAJI WAKE (Sehemu ya kwanza) NA; JAMES F. MZAVER Bwana Yesu asi...