Ushuhuda wa Rodolfo Acevedo Juu ya Mbinguni, Kuzimu na Hali ya Kanisa la Leo
Ufuatao
ni ushuhuda wa Mwinjilisti Rodolfo kutoka Jamuhuri ya Domonika, ambao
Bwana alimwonyesha kuhusiana na kuzimu, mbinguni pamoja na mambo
yanayoendelea katika Kanisa la siku za leo.
Utangulizi
Mimi
ni Mwinjilisti Rodolfo Acevedo Hernandez kutoka Jamuhuri ya Dominika. Koo langu
limeathirika kutokana na usimuliaji wa ushuhuda huu lakini bado nitafanya hivyo
tena leo hata kama kuna upinzani. Utukufu ni kwa Mungu! Tupo hapa kuhubiri Neno
la Bwana Yesu Kristo na ninaenda kutoa ushuhuda ambao ulibadili maisha yangu na
maisha ya maelfu kwa maelfu ya watu wengine!!
Hebu
tuende kwenye Ufunuo 1:14-15: “Kichwa
chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu nyeupe, kama theluji; na macho
yake kama mwali wa moto; na miguu yake kama shaba iliyosuguliwa sana, kana
kwamba imesafishwa katika tanuru; na sauti yake kama sauti ya maji mengi.”
Kwa
kuwa sikuridhika kuwa kwenye hali ileile ya kiroho niliyokuwa nayo,
nilijifungia kanisani kwangu kwa siku nane; siku nane za kufunga na kuomba,
nikiwa nimejifungia na Bwana Yesu. Kabla ya kuanza zile siku nane, Bwana,
aliniambia hivi kupitia maono, “Rodolfo,
ni wakati sasa ujiweke wakfu kwa ajili yangu,” na nilipewa vazi
jeupe ambalo liliandikwa maneno: “Utakatifu kwa Yehova.” Baaya ya
maono yale, mama mmoja mmisionari kutoka kwenye kanisa langu aliniambia,
“Rodolfo, niliota kuwa Bwana ananiambia nikueleze kwamba: “jitenge na madhabahu (maana nilikuwa
mhubiri); ninaenda kukuonyesha jambo kubwa ambalo litabadili maisha ya mataifa
duniani.” Kwa hiyo, ndipo nikaanza mfungo wangu wa siku nane kwa
Bwana.
Nilipata changamoto
Kwenye
siku ya nne ya mfungo na maombi, nilikuwa nikiomba madhabahuni na ghafla, mbele
yangu yalitokea mapepo mawili, ambayo niliyaona kama unavyoweza kumwona mtu uso
kwa uso. Mapepo haya yaliniambia, “Rodolfo, hatutakubali wewe uvuke kizuizi
chetu”, kisha mara moja yalitoweka. Nilianza kuwa na hofu kubwa maana unapoona
viumbe wa rohoni kimwili, inaogopesha sana! Viumbe hawa walikuwa warefu na
walikuwa na harufu ya salfa kama vile ndio wametoka moja kwa moja kwenye shimo
la jehanamu. Walitumwa kuja kuniambia kuwa hawako tayari kuruhusu mimi nivuke
kizingiti walichoweka. Lakini shetani ndiye pekee mwenye ukomo; Bwana Yesu
Kristo alimshinda kwenye msalaba wa Kalvari. Utukufu kwa Mungu, haleluya!
Zilipopita
siku saba, nilimwambia Bwana, “Bwana, siwezi kuendelea zaidi. Mwili wangu ni
dhaifu. Sina nguvu za kutosha. Bwana, tafadhali nisaidie. Siwezi kutimiza jambo
hili. Tafadhali, nisamehe; nipe nguvu.”
Ghafla,
nilihisi mtu anatembea nyuma kuelekea kwangu, na akasema sikioni mwangu, “Rodolfo, usiache kuendelea na jambo hili
hadi tukuonyeshe mambo ambayo uko karibu kuyaona.” Nilitiwa moyo na kujisikia ni mwenye nguvu
zaidi. Siku iliyofuata, ilikuwa ni Jumapili. Nilijisikia dhaifu kidogo asubuhi.
Jioni wakati wa ibada, kulikuwa na ujumbe wenye nguvu kutoka kwa
Mwinjilisti Ruben Bells. Alipomaliza,
nilikuwa nawasalimu ndugu zangu wote katika Kristo. Nilianza kuhisi kama pumzi
zinaniishia. Nikawa nashindwa hata kupumua.
Ndugu
wa kanisani wakanizunguka na kuanza kuomba. Ghafla, nilihisi kana kwamba
kupitia kucha na vidole vyangu, kulikuwa na sindano zinapenya mwilini mwangu.
Ubaridi wa zile sindano ulipenya mwilini kama hewa ya baridi na nikahisi pumzi
yangu ya mwisho imeondoka na kwamba moyo wangu umesimama. Nilidondoka sakafuni
na ndugu zangu wakaanza kujaribu kuniamsha. Walikuwa kama ndugu 12 hivi.
Ghafla, nilihisi roho yangu ikitoka kwenye mwili na nikawa nautazama mwili
wangu nikiwa nje, ukiwa umelala sakafuni. Hao wapendwa hawakujua kilichokuwa
kikiendelea kuhusiana na mimi. Dada mmoja ambaye alikuwa ni nesi aliwaambia,
“Amepata mshtuko wa moyo.” Nilikuwa natamani kwenda kwao na kurudi kwenye mwili
wangu lakini nikawa nashindwa.
Kuzimu
Ghafla,
nilihisi mwanga umepotea na nikaanza kupaa juu. Kule juu kuna mtu
alinisimamisha na nikaanza kushuka chini hadi nikafika mahali ambako nilihisi joto
kali mno! Kisha, nikaona milango miwili myeusi inayonuka sana. Hapo ilikuwa ni
kuzimu na kulikuwa kunatisha sana!
Nilipokuwa
ndio niingie ndani ya ile milango, joka kubwa, ambalo kichwa chake kilijaa
miiba na mwili wake ulifunikwa kwa nyembe badala ya magamba ya kawaida,
lilitangulia kuingia kwenye gereza hilo. Nilipokuwa naingia kwenye milango ile,
niliona macho ya kila aina ukutani, yakiwa yananiangalia. Lakini macho yale
yalikuwa yamechorwa ukutani. Mara niliona macho mawili yananijia na kumbe lilikuwa
ni pepo ambalo kifuani lilikuwa na bamba lililoandikwa: ‘Mimi ni Kisasi.’
Hukumu ya watumishi wasio waaminifu
Wakati
huohuo, mapepo zaidi yalianza kutoka ukutani. Lile pepo linaloitwa Kisasi
lilisema kwa sauti, “Mfalme Belzebub, tumempata mmojawapo aliye mkubwa ambaye
aliendesha vita dhidi ya sisi, ufalme wa giza …” Biblia inasema: “Maana ingalikuwa heri kwao kama
wasingaliijua njia ya haki, kuliko kuijua, kisha kuiacha ile amri takatifu
waliyopewa.” (2 Petro 2:21). Kanisa linalomjua Bwana ni lazima
liendelee kuwa thabiti na kutambua kuwa Yesu ndiye tumaini PEKEE kwa ajili ya
wokovu wa roho zao.
Nikiwa
ningali pale, lile pepo Kisasi lilikuja karibu yangu na kuniambia, “Rodolfo,
nataka unitoe kama ambavyo ulifanya kule duniani.” Lilipokuwa likisema haya
tena na tena, lilikuwa linaendelea kunitesa. Na nikaona mapepo mengi
yamejipanga tayari kwa ajili ya kunitesa!
Mateso
ya kuzimu kwa ajili ya wachungaji, wahubiri, na wainjilisti wanaoacha nguvu na
upako wa Mungu ni makali zaidi kuliko yale ya roho zingine kule kuzimu! Uwe
thabiti katika mwendo wako na Mungu! Hii ni saa ya Kanisa kuwa imara. Wakati ni
sasa. Muda wa kuchezacheza kanisani umeshapita. Ni lazima tuwe na ujasiri na
kuzishinda nguvu za kuzimu kwa jina la Yesu – Yeye peke yake ndiye nuru.
Mara
kulitokea pepo lililoruka na kutupa mkuki kwangu ambao ulipita kwenye moyo
wangu. Nilihisi maumivu yasiyoweza kuelezeka. Pia nilihisi kama vile kulikuwa
kunanyesha salfa kule kuzimu. Nilihisi nyama ya mwili wangu inatoka kwenye
mifupa na minyoo ikaanza kupekecha mifupa yangu.
Biblia
inasema,“ambamo humo funza wao
hafi, wala moto hauzimiki.” (Marko 9:48); na pia kwenye inasema, “Funza wametandazwa chini yako, na vidudu
vinakufunika” (Isaya 14:11). Kuzimu ni mahali halisi. Yesu na Agano
la Kale wanazungumzia kuhusu kuzimu.
Mara
niliona kundi la mapepo wanaleta jeneza, lakini lilikuwa ni jeneza tofauti na
haya tunayoyafahamu hapa duniani. Lile pepo Kisasi lilinishika sehemu ya chini
ya mdomo wangu na kuniambia kwa dhihaka,
“Rodolfo, nataka unitoe! Nguvu zako ziko wapi? Upako wako uko
wapi? Uko wapi utukufu wako uliokuwa nao?”
Ujumbe
ninaotaka uupate hapa ni kuwa, wakati mwingine kwa sababu tunahubiri, tunadhani
kuwa upako ule ni wetu, na kwamba zile nguvu ni zetu, na kwamba uponyaji ni
wetu. Biblia inasema kuwa utukufu unatoka kwa Mungu na utukufu ni wake pekee.
Kwa sababu hiihii, ibilisi alitupwa nje ya Mbingu maana alitaka kutwaa utukufu
wa Mungu. Kwa hiyo, wengi wanadhani kuwa wagonjwa wanaponywa kutokana na nguvu
zao; na wenye mapepo wanafunguliwa kutokana na nguvu zao! Acha nikuambie kuwa,
kile ambacho Bwana amekupa ni zawadi kutoka mbinguni. Ni rehema za Mungu kwa
lengo la kuwafungua wanaoteswa, na pia ili roho ziweze kuokolewa.
Mimi ni ‘Niko’
Mapepo
yalipokuwa yananiingiza kwenye lile jeneza, nilihisi upepo na kama kuna kitu
kimedondoka sakafuni. Pepo Kisasi na mapepo mengine yalikimbia haraka na
kujificha mbali na uwepo wake. Nilikuwa niko sakafuni kutokana na kuteswa na
yale mapepo; na jambo la kwanza nililoona ambalo sitakaa nilisahau … Oh,
Utukufu kwa Mungu! Niliona ‘mtu’ akiyejaa nuru … Haleluya!
Niliona
makovu kwenye miguu yake. Nilipoinua kichwa changu, nilimwona huyu mtu wa
ajabu, akiwa na mkanda kifuani mwake ulioandikwa: “Mimi ni MFALME WA WAFALME,
na BWANA WA MABWANA.” Alikuwa amevaa taji kubwa sana la dhahabu kichwani
mwake. Alinyoosha mkono wake kwangu na
kusema, “Rodolfo, MIMI NI YESU na
ninaenda kukuonyesha mambo mengi humu kuzimu, mbinguni pamoja na hali ya Kanisa
langu duniani.” Alinishika mkono na kusema, “Twende sasa, Rodolfo.”
Ukahaba
Niliona
amefungua chumba kikubwa ambamo kulikuwamo mwanamke. Akasema, “Naenda kukuonyesha adhabu ambayo shetani
huwapa wale ambao walikuwa wakifanya ukahaba duniani. Kahaba anapokufa, anakuja
kwenye sehemu hii. Angalia kwa makini, Rodolfo.” Niliangalia na
kuona ndani ya chumba kile, mwanamke ambaye alikuwa amekaa mkao wa hatari sana,
na nikaliona joka lilelile ambalo nililiona hapo mwanzo. Joka hili liliingia
kwenye chumba kile kisha likajiingiza kwenye sehemu zake za siri. Kumbuka
nilikuambia kwamba ngozi ya joka hili haina magamba ya kawaida bali ni
nyembe.
Joka
hilo lilipoingia, lilimharibu kabisa viungo vyake vya ndani, kisha likatokea
mdomoni. Pepo linalosimamia ukahaba duniani linaitwa, “Metresa” au “Martha”, au
“The Domineur”. Wakatoliki wengi wana “mtakatifu”
huyu akiwa kama mwanamke ambaye mwili wake umeviringwa na nyoka; na pepo
hili ndilo ambalo linawatesa makahaba kuzimu.
Bwana
aliniambia kwamba ulikuwa ni wakati wa kuondoka hapo na tukamwacha mwanamke
yule akilia kutokana na mateso na maumivu. Alikuwa akisema, “Nahitaji mtu wa
kunisaidia!” Bwana akaniambia, “Rodolfo,
hukumu imeshawekwa kwa ajili yao! Sasa
Rodolfo, nitaenda kukuonyesha sehemu ambako shetani anawatesa wanawake ambao
walitoa mimba za watoto wao duniani!”
Utoaji mimba
Ghafla,
nilimwona mwanamke akiwa katika mkao wa kujifungua na nikaona pepo baya sana
ambalo mikono na miguu yake ilikuwa kama ya farasi na mwonekano wake kama wa
mnyama na alikuwa na keekee (drill) mikononi mwake. Keekee hii ilikuwa imejaa
minyoo. Minyoo hii ilikuwa ni mikubwa sana na meno yao yalikuwa makali na miili
yao ilijaa miiba iliyochongoka. Pepo lile liliingiza ile keekee kwenye sehemu
zake za siri hadi akaonekana kama mwenye mimba.
Pepo
lile likaanza kumpigia kelele, likimwambia kuwa azae huko kuzimu kwa kuwa
alikataa kuzaa duniani. Kisha likasema, “Utukuzwe, utukuzwe shetani! Huu ni
ufalme wako!”
Nilipomwuliza
Bwana kwa nini adhabu ilikuwa kali kiasi kile kwa mwanamke yule, Bwana akasema,
“Rodolfo, adhabu imeshawekwa kwa
ajili ya mwanamke huyu!” Biblia inasema kwamba wauaji hawataingia
kwenye Ufalme wa mbinguni. Watu
wanatoa mimba au kuwaua watoto huku wakiamini kuwa huko ni kama kuua tu mnyama
lakini kile hasa wanachofanya ni kuua mwanadamu mwenye roho na mwili.
Pepo
lile liliendelea kumpazia sauti, likimwambia amtukuze shetani maana ule ulikuwa
ni ufalme wake. Wale minyoo walianza kutoka kupitia tumboni mwa yule mwanamke
huku wakiharibu kabisa sehemu za ndani ya mwili na kutoka wakiwa na vipande vya
nyama midomoni mwao. Ungeweza kuona maumivu makali aliyokuwa akiyahisi. Bwana
akaniambia, “Tuondoke kwenye sehemu hii.”
Shetani anashambulia watoto na familia
Tulienda
kwenye sehemu iliyoonekana kama kuna fito nyeusi. Nikaanza kuona watoto wengi
kule kuzimu. Nikamwuliza Bwana, “Kwa nini kuna watoto huku kuzimu?” Lakini
Bwana akaniambia kuwa wale hawakuwa watoto; na kwamba ufalme wa mbinguni ni wa
watoto na inabidi uzaliwe upya ili kuingia kwenye ufalme wa mbinguni.
“Sasa,
Bwana vipi kuhusu watoto hawa?” niliuliza.
Bwana
akaniambia tena, “Rodolfo, hawa si
watoto”, kisha akaniambia nisikilize maagizo ambayo shetani alikuwa
anawapatia.
Nilipogeuka,
nikaona kuwa kumbe hawakuwa watoto bali ni mapepo na walikuwa wanacheza mchezo
unaoitwa Nintendo. Nikaanza kuona kila aina
ya ‘programming’ na michezo ya kishetani, huku wakitoa alama na mijongeo kwa
kutumia mikono yao, vyote vikiwa na makusudi ya kishetani.
Bwana
alipowaamuru wageuke, ndipo nikaona jinsi sura zao zilivyo mbaya, za kutisha na
zinazotia kinyaa. Shetani aliwapa maagizo akisema, “Wanangu, nendeni mkaue,
mkaibe, na kuharibu.” Alikuwa yuko sahihi kwa sababu Biblia inasema kuwa
shetani haji ila kuiba, kuchinja na kuharibu lakini Yesu alikuja ili kuleta
uzima na uzima tele. (Yohana 10:10).
Wakati
huo, hivi vipepo vidogo viliingia duniani na Bwana akaniambia kuwa hii ndiyo
sababu watoto wa duniani wanajiua. Hivi sasa, wanasayansi na wanasaikolojia ya
watoto hawaelewi ni kwa nini watoto wanajiua. Miezi michache iliyopita, mtoto
wa kiume wa miaka 12 alimuua mama yake kwa kisu; mwingine alijinyonga hapa
Marekani; na mtoto wa miaka 7 alimwua mama yake, wadogo zake na yeye mwenyewe
kwa bastola ambayo aliipata. Mtoto mwingine alijitupa kutoka ghorofa ya pili na
kufa. Barua wanazoacha hawa watoto zinasema kuwa maisha hayana maana pamoja na
mambo mengine mengi.
Haya
yanatokea kwa sababu mapepo yanaingia kwenye miili yao na kutawala fahamu zao
na kuwafanya wachukue uamuzi wa kujiua. Iweni makini enyi wazazi na kile ambacho
watoto wenu wanaangalia kwenye televisheni. Kile ambacho watoto wenu
wanaangalia kwenye intaneti au wanachosikiliza kwenye redio kina athari kubwa.
Mapepo yanaingia kupitia televisheni, redio, muziki na michezo ya vichekesho ya
kishetani. Utukufu ni kwa Mungu, haleluya, kwa kutuamsha!!
Kisha
Bwana akaniambia, ni kwa sababu hii ndoa nyingi zinaharibiwa, maana baadhi ya
wazazi wanalaumu watoto wakidhani kuwa kwa sababu ya mtoto fulani, basi ni
lazima wapeane talaka. Lakini mtoto si tatizo. Tatizo ni mashambulizi ya kipepo
dhidi ya umoja wa ndoa na familia. Mwiteni Yesu Kristo! Liite Kanisa! Omba
ufanyiwe maombi ili kuwa na nyumba isiyo na mashambulizi ya kipepo! “Sasa,
Rodolfo,” Bwana akasema, “ni
wakati wa kutoka wenye sehemu hii.”
Ibada ya sanamu
Tulipotoka
kwenye sehemu ile, nilimwona mwanamke ambaye alikuwa amemezwa kabisa ndani ya
moto. Mwanamke huyu alikuwa akilia sana akisema, “Kufa, kufa, kufa! Nitoe
humu!”
Kile
nilichoona ni kwamba, mwanamke huyu alishika mikononi mwake picha ya ‘Moyo mtakatifu
wa Yesu’ kulingana na taratibu na mapokeo ya Kikatoliki.
Nikauliza,
“Bwana, huyo ni mwanamke gani?”
Bwana
akasema, “Rodolfo, mwanamke huyo ni
bibi yako.” Biblia inasema kuwa waabudu sanamu hawataingia kwenye
ufalme wa mbinguni (Gal. 5:20, Efe. 5:5). Bwana alinionyesha maisha ya
bibi yangu yalivyokuwa duniani na nikaona kwamba kweli alikuwa ni mwabudu
sanamu. Nikasema, “Bwana, tafadhali msaidie.”
Bwana
akaniambia, “Rodolfo, sina cha
kufanya! Hukumu imeshawekwa kwa ajili yake!” Kisha akaniambia, “Naenda kukuonyesha kile ambacho kitakuletea mateso duniani. Wengi hawataamini
kile ambacho unaenda kukiona. Lakini usiwe na wasiwasi, nitakuwa pamoja na
wewe.”
Celia Cruz (Malkia wa Salsa) yuko kuzimu
Mara
nilimwona mwanamke ambaye miguu yake ilikuwa inapondwapondwa kwa visu ambavyo
vilifika hata kwenye magoti yake kwa wakati uleule. Mwanamke huyu alikuwa
akiteswa na mapepo mengi.
Bwana
alinionyesha video ya Celia Cruz akifanya mikataba ya kishetani kule Hollywood
kwa kutumia damu; na nikamwona akifanya mambo mengi ya kishetani. Bwana
akasema, “Alikuwa ni mwabudu
shetani. Alikuwa ni mfanya ibada ya sanamu. Alikuwa ni mchawi akiwa na maagano
mengi ya damu. Kwa hiyo, muziki wake ulikuwa ukishika sana chati za juu.
Ilikuwa ni vivyo hivyo kwa kundi lake la wanamuziki.” Na Bwana
akanisikizisha muziki wake mmoja unaoitwa ‘Yemaya’, ambao ni maarufu sana kwenye
ulimwengu wa Kihispania. Lakini unapoimba wimbo ule na kurudiarudia, maana yake
hasa ni: ‘Mfalme shetani, njoo utawale ndani yangu!’ Na Bwana akaniambia, “Hukumu imeshapangwa kwa ajili ya Celia Cruz.”
Mwasisi wa Mashahidi wa Yehova yuko kuzimu
Tuliendelea
kutembea na Bwana akanionyesha mwanamume mmoja mweupe ambaye mikono yake
ilikuwa imetanuliwa. Na kitu cha ajabu kuhusiana na mtu huyu ni kuwa alikuwa na
upanga mzuri sana ndani ya ulimi wake na upanga huu ulipenya hadi kichwani na
kutokeza nje. Miguu yake ilikuwa imefungwa kwa minyororo na mgongo wake ulikuwa
umejaa nyembe sehemu mbalimbali kwa namna kwamba, vyovyote ambavyo
angejisogeza, ni lazima zinamkata. Nilipomwona mtu huyu katika hali hii,
nikamwambia Yesu, “Bwana, tafadhali
msaidie. Fanya kitu, Bwana Yesu. Hebu ona jinsi anavyoteseka kwa maumivu.”
Bwana akaniambia, “Je, unajua huyu
ni nani?”
“Hapana,
Bwana,” nilisema. Niliona jinsi visu vilivyopenya kwenye ngozi yake na kisha
kwenye mifupa na jinsi vilivyotokeza upande mwingine. Mtu huyo alipiga tu
kelele kwa maumivu.
Bwana
akaniambia, “Hukumu juu ya mtu huyu
imeshatolewa. Sasa nitakuambia huyu ni nani.”
Kutokana
na unabii huu, Bwana akasema, “Itakubidi
kukimbia kutoka mji mmoja hadi mwingine maana jambo hili litakuletea mateso makubwa,
lakini nitakuwa pamoja na wewe.”
Akaendelea kusema, “Rodolfo, huyu
mtu ni Charles T. Russell.” Nikasema, “Bwana, yeye ni nani?” Bwana
akaniambia kwamba mwanamume yule alikuwa ni mwanzilishi wa kanisa la Mashahidi
wa Yehova. Nikaomba, “Bwana, tafadhali msaidie,” na Bwana akasema, “Hapana, Rodolfo.” Kisha Bwana
alifanya ishara kwa mkono, na mara moja nikaona roho nyingi zikiangukia kwenye
shimo la kuzimu kwa kila namna. Walikuwa wakiangukia humo kichwa kwanza, miguu
kwanza, tumbo kwanza, n.k.
“Rodolfo, kutokana na huyo mtu aliyelaaniwa,
roho hizi zote zinaangukia kuzimu. Mtu huyu alifundisha kwamba Mungu ni Mungu
wa upendo tu. Biblia inasema kwamba Mungu ni moto ulao. Mtu huyu, Charles
Russell, aliondoa maneno ‘hell’ kutoka
kwenye Biblia na akaondoa maneno yote ‘sheol’ na ‘Abaddon’. Pia, alikana uungu
wa Yesu Kristo na pia alikana uungu wa Roho Mtakatifu, halafu akaweka tu neno
Yehova kwenye Biblia. Aliondoa maneno Yesu na Roho Mtakatifu. Kutokana na mtu
huyu aliyelaaniwa, roho hizi zote zinaangukia kuzimu.” (Ufu.
22:18-19). Kisha Bwana akasema: “Namlaani
mtu huyu.”
Tafadhali
enyi Mashahidi wa Yehova mnaonisikiliza wakati huu, si lengo langu kuwakwaza.
Tokeni ndani ya kundi hilo na mje kwa Yesu haraka. Mimi siwachukii na wala
sichukii dini yenu lakini mko ndani ya mahali pabaya. Njooni kwa Yesu.
Anawangoja kwa mikono iliyo wazi kabisa. Charles Russell yuko kuzimu kwa sababu
alifundisha uongo!! Msifuate uongo wake.
Tulipoondoka
sehemu hii, milango hii ya gereza ilijifunga na moto ukawaka na mwanamume huyu,
Charles Taze Russell, alipiga kelele na kumlaani Yesu tena na tena kwa sababu
Yesu alisema, “Hukumu imeshaamuliwa
kwa ajili ya mtu huyu.”
Kisha
Bwana akasema, “Rodolfo, sasa
nitakuonyesha magereza meusi ya kuzimu. Hii ni adhabu ya kupita kiasi ya shetani
kwa roho zilizoko kuzimu.”
“Hapana,
Bwana, tafadhali! Tayari nimeshaona mambo ya kutisha. Niondoe hapa, tafadhali
…”
Bwana
akasema, “Haya, Rodolfo, sitafanya
kingine chochote kama hauniruhusu. Nitakupeleka mbinguni sasa.”
Mbinguni
Tuliondoka
kwa kasi sana na tukafika mahali hapa. Malaika wawili walinisimamisha mbele ya
milango hii iliyokuwa mizuri sana. Walikuwa wazuri
sana. Hawa malaika wawili
waliniambia, “Rodolfo, ukiwa na mavazi hayo ya dhambi, huwezi kuingia kwenye
ufalme wa Mungu.” Kwa hiyo, walinipatia mavazi mapya ambayo yameandikwa: Utakatifu.
Ujumbe sahihi
Wachungaji,
wainjilisti, wahubiri na wamisionari, tafadhali samahanini na mnisikilize.
Mungu hajawaita kuhubiri kuhusu utajiri au unabii juu ya hilo. Mungu amewaita
kuhubiri kuhusu utakatifu na utakaso, maana bila utakatifu, hakuna atakayemwona
Bwana. Pelekeni neno la utakatifu na
kulihubiri!!!
Malaika
waliniruhusu kuingia na Yesu alikuwa ananingoja na akaniambia, “Rodolfo mwanangu, karibu kwenye Ufalme wa
Mungu wako.” Tulianza kutembea. Niliona kuwa barabara zilikuwa za
dhahabu tupu, na nikaona mto uliokuwa kama kioo; ni maji halisi! Niliona pia
almasi na mapambo kwenye mitaa, kitu ambacho watu wa duniani wanaweza kuuana
kwa ajili yake! Kisha Bwana alinishika mkono na kuniambia, “Sasa
nitaenda kukuonyesha hekalu.” Hekalu lilikuwa zuri sana! Niliona
bilauri za dhahabu, vyombo vya dhahabu na nikasikia wimbo mzuri ambao ulikuwa
unaimbwa na watoto. Bwana akaniambia kuwa waliokuwa wanaimba ni watoto ambao
duniani watu waliwakataa lakini wana uzima kwenye ufalme wa mbinguni. Utukufu
kwa Mungu, haleluya!
Mavazi ya harusi, chakula cha harusi, mataji
Tuliendelea
kutembea mbinguni na nikaona mavazi meupe mazuri, yaliyopambwa kwa dhahabu
pamoja na mataji juu yake. Bwana akaniambia lilikuwa ni Kanisa lake. Kwamba
linatakiwa kuwa takatifu na lililotakaswa. Taji ni taji ya uzima na kwamba
Bwana atakwenda kulipatia Kanisa.
Tulipotoka
pale, niliona msururu mrefu wa watu waliovaa mavazi meupe. Niliona malaika
wawili wakubwa, wenye sura nzuri ukiwatazama machoni. Niliona amani na upendo.
Malaika mmoja akasema, “Karibu kwenye ufalme wa Mungu wako.” Malaika mwingine
alipiga makofi. Niliona jinsi watu walivyo na furaha kuwa pale na sasa naelewa
kile ambacho mtume Paulo alichosema kwamba, mateso ya dunia hii yanayopita si
lolote ukilinganisha na utukufu unaotungojea kule mbinguni.
Bwana
alinipeleka mahali ambako niliona meza ndefu sana isiyo na mwisho. Meza ilikuwa
ya dhahabu. Kitambaa kilichoifunika kilikuwa cha dhahabu, bilauri za dhahabu,
visu na nyuma za dhahabu, viti vya dhahabu, n.k. Kisha nikaona mataji makubwa
kwa madogo na Bwana akaniambia kuwa yale mataji makubwa ni ya watumishi wake,
pale watakapokuja kwenye harusi ya Mwanakondoo.
Akasema, “Kwa vile harusi ya
Mwanakondoo iko karibu kuanza, niko karibu kuja kuchukua Kanisa langu. Waambie
kuwa ninakuja kulichukua Kanisa langu.”
Nikamwuliza
Bwana, “Je, na haya mataji madogo ni ya nani?”
Akasema, “Hayo mataji madogo ni ya watu walio ndani ya Kanisa ambao wanaishi katika utakatifu lakini hawafanyi chochote kwa ajili ya Ufalme. Lakini nakwambia, usiridhike kupokea taji dogo bali fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya taji kubwa. Fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Mungu ili aje kukupa thawabu ya uzima.”
Akasema, “Hayo mataji madogo ni ya watu walio ndani ya Kanisa ambao wanaishi katika utakatifu lakini hawafanyi chochote kwa ajili ya Ufalme. Lakini nakwambia, usiridhike kupokea taji dogo bali fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya taji kubwa. Fanya kazi kwa bidii kwa ajili ya Mungu ili aje kukupa thawabu ya uzima.”
Jambo
la ajabu lilikuwa kwamba, kila kiti kina jina nyuma yake na hakuna mtu mwingine
yeyote ambaye atakikalia zaidi ya mwenye jina hilo!
Hali ya Kanisa la leo
Bwana aliniambia, “Sasa Rodolfo, naenda kukuonyesha hali halisi ya Kanisa ilivyo hivi
sasa.”
Nilimwona samaki mdogo akimsifu na kumwabudu Yesu kwa sababu Biblia inasema: Kila mwenye pumzi na amsifu Bwana! (Zab 150:6).
Kwa
hiyo, Bwana alinionyesha dunia ambako ningerudi kwenda kuhubiri kile
nilichokiona. Lakini nikawa na picha kwamba sikuwa na kumbukumbu kuhusiana na
dunia na Bwana akanipa ufahamu kwamba, mtu anayeingia mbinguni, anasahau kila
kitu kilichotokea duniani! Lakini sivyo ilivyo kuzimu. Kila anayeingia kuzimu,
anakuwa na kumbukumbu za kila kitu alichotenda alipokuwa duniani, familia zao,
na kwamba wasingependa waende kuzimu! Hayo nayo ni mateso mengine yanayoongezwa
juu yao. Lakini yule anayeingia mbinguni, akili yake inabadilishwa ili ifanane
na ufahamu wa kimbingu.
Bwana
asifiwe! Kwa sababu hiyo, si Petro, wala Mariamu, wala Stephano, wala Elisha au
Yohana mwenye kumbukumbu ya kile alichofanya alipokuwa duniani. Baada ya maisha
yao ya duniani, wala hawana tena habari kamwe na kile kinachoendelea hapa.
Petro wala hawezi hata kuwaza kuwa Kanisa Katoliki wanamwomba yeye au mtakatifu
mwingine yeyote. Na Yesu akasema, “Hakuna jina jingine chini ya mbingu
litupasalo kuokolewa kwalo.” Huyo ni Yesu Kristo, Mwana wa Mungu
Aliye Hai. Na Mariamu alisema kule kwenye harusi ya Kana, “Lolote
atakalowaambia, fanyeni.” Na … waabudu shetani wako Vatican. Wanaficha njia
zote za dhambi za makasisi kutembea na watawa; makasisi kutuhumiwa kunajisi
watoto na hata hapa kwenye Jamuhuri ya Dominika. Na Wakatoliki wanaendelea
kuamini uongo huo. (Tafadhali ona pia ushuhuda mwingine wa ajabu: “Prepareto meet your God – Angelica Zambrano” Sehemu ya 1&2
ambao unaongelea zaidi kuhusiana na masuala ya Ukatoliki).
Watumishi wanaolenga fedha na wasio waaminifu
Sasa
Bwana alianza kulia pale alipoanza kunionyesha mimi hali ya Kanisa. Ghafla,
nilimwona mchungaji duniani amebeba begi kubwa lililojaa fedha. Bwana
akaniambia, “Hawa ni wahubiri na
wainjilisti wanaojitajirisha kutokana na matoleo kwa sababu wanafundisha uongo
kwa watu wangu na kuwafanya watu wangu wapotee.”
Nawaambia
enyi wahubiri na wainjilisti, mhubirini Yesu hata kama hakuna zaka au sadaka
mnazopokea. Litakaseni Kanisa!
Mara
niliona fedha za kwenye lile sanduku zimetoweka. Nilimwuliza Bwana naye
akaniambia, “Kama ambavyo fedha zake zimetoweka, ndivyo na yeye atakayotoweka pamoja
na mpinga Kristo. Lakini bado ninayo masalia ya watu wangu ambao
hawajanajisika.”
Naona
siku hizi jinsi wahubiri wengi, wachungaji, wainjilisti, n.k. walivyo matajiri
na mamilionea. Hata hivyo, waumini wa makanisa yao wanaogelea kwenye umaskini,
uhitaji wa chakula, huku mchungaji akiwa katika utajiri na wala hawasaidii!
Wainjilisti wengi ni mamilionea wakubwa na hata mabilionea wakiwa na magari ya
kifahari kupita kiasi. Je, Msamaria mwema yuko wapi?
Pia
niliona wachungaji wengi wakihudumu kwenye madhabahu lakini nikamwona huyu
mmoja akimalizia kuhudumu siku ile, akaondoka nyumbani alikokuwa mke wake, na
kwenda kukutana na hawara yake ambaye anaishi naye pia; huku akiwa naye ni
mshirika wa kanisa lake!
Nilimwona
pia mwinjilisti akiondoka kanisani kwake na baada nyumba chache tu kutoka
kwenye kanisa, akaenda kukutana na kahaba. Ni mwinjilisti yuleyule aliyekuwa
akihudumu kwenye madhabahu! Bwana, tafadhali uturehemu!
Matendo yasiyo matakatifu – kujichua
Baada
ya hapo, Bwana alinionyesha kundi la vijana wa Kanisa, kwamba wanapoondoka
kanisani wanaenda kwenye sehemu ya giza maana wanadhani kuwa Bwana hawaoni.
Wanapoenda huko wanaanza kujichua (kupiga punyeto) na kuzini dhidi ya miili yao
wenyewe. Baada ya hapo, wanarudi na kuhudumu madhabahuni! Viongozi wa vijana,
viongozi wa Kanisa! (Kama unahitaji msaada wa kushinda dhambi hii,
angalia video hii).
Muziki usio na utakatifu kanisani
Sasa
Bwana alinionyesha disko na Kanisa na akaniambia, “Angalia kwa makini.” Na mimi nikaangalia na kuona kwamba
Kanisa lilikuwa ni sawasawa tu
na lile disko! Hakukuwa na tofauti yoyote!
Walikuwa na mfumo uleule wa sauti, muziki uleule! Vifaa vilevile kutoka duniani
vinaingia kanisani!
Dunia
inatakiwa kubadilika iingie kwenye Ukristo lakini si Ukristo kuingia duniani!
Tunaileta dunia kanisani! Pia niwaambie hili: Hatuwezi kumsifu na kumwabudu
Mungu kwa kutumia Reggaeton, kwa Bachaton au Rock. Hata leo zipo nyimbo za
Kikristo anazoimbiwa Mungu na pia zinaimbwa duniani kwa kutumia maneno
yaleyale! Hazimtaji Mungu bali zinataja tu neno ‘upendo.’
Niliona
pia muziki wa Rap na Perreo kanisani na hilo halikubaliki. Biblia inasema kuwa
tunatakiwa kumwabudu Bwana katika uzuri na utakatifu (kwa ajili ya kuabudu kwa
kweli, tazama Kol. 3:16 na Yoh. 4:23-24). Muziki wa Rock ni wa kishetani na
ulibuniwa kuzimu. Wachungaji na
wainjilisti, tafadhali, ondoeni makanisani muziki huo uliolaaniwa!!!
Bwana alinionyesha wanamuziki ambao wameshapotoka.
Kwa upande mmoja wanaimba kanisani, na kwa upande wa pili wanaingia mikataba ya
kuimba hata kwenye mahoteli kama waimbaji wa kujitegemea. Wanaenda kanisani
kumsifu Bwana!
Ngoja niwaambie: muziki kama huo Bwana wala
haukubali na tafadhali, samahani, ni lazima niwaambie ukweli - kile kinachotoka
kwa Mungu ni kitakatifu na kimetengwa kwa ajili ya Mungu peke yake. Na kile
ambacho wanamuziki wa leo wanakifanya, wanaenda kuimba kanisani, kisha
wanapotea kutoka kwenye huduma, maana wanaonekana kama vile wanamwimbia Mungu
kwa mkataba. Kwa hiyo, wanadhani hawana ulazima wa kuwapo pale muda wote wa huduma;
wanaondoka mapema. Bwana aliniambia, “Kwa
bahati mbaya, kanisa la aina hiyo halitaingia kwenye ufalme wa mbinguni.”
Masalia walio watakatifu
Baada
ya hapo, Bwana alinionyesha kundi la watu – maelfu kwa melfu ya watu
wanaojilinda katika utakatifu. Kwa mfano, nilimwona dada akimwambia mwingine, “Umekula
leo? Nina kipande cha mkate nyumbani.” Nilimwona mwingine akiwa amebeba jozi ya
viatu akimpelekea mwingine ambaye hana. Nikamwona mwingine akiwatia moyo wale
wasio na nguvu. Wengine, kutokana na kujua matatizo ya wenzao, walikuwa
wakiwasaidia na kuwaombea katika mahitaji yao bila mtu mwingine kujua.
Lakini
leo, katika makanisa mengi, kuna masengenyo mengi kwa sababu watu hawajui kukaa
kimya kuhusiana na watu wengine. Tubu leo! Yesu Kristo anataka kukupatia
ukombozi na wokovu. Anaweza kukupatia zawadi ya toba.
Utukufu
kwa Mungu!
Msifuni na kumwabudu Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana!
Msifuni na kumwabudu Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana!
Rehema
zake zadumu milele.
Mwinjilisti
Rodolfo Acevedo
I have been blessed after reading this testimony vigilantly and becoming among the one who faithfully will narrate this story to others JESUS help me;by Obadiah Gowelle from Tanzania +255757281311
ReplyDelete