UMUHIMU
WA KUVAA SILAHA ZOTE ZA MUNGU
Kwa
muda mrefu sasa nimekua nikijiuliza sana kwa nini waombaji wengi hasa waombaji
wa muda mrefu wa makanisani maisha yao hayaendi vizuri au kwa nini hawafanikiwi
katika maisha yao hasa kimwili na kiuchumi?
Fuatana nami katika kuangalia na kujifunza kwa kina kwa nini
ni muhimu hasa sisi wakristo na waombaji kuvaa silaha zote za Mungu
WAEFESO 6:11-19
11 Kwa maana
kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka,
juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa
roho.
12 Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate
kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
13 Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa
dirii ya haki kifuani,
14 na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya
amani;
15 zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo
mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
16 Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho
ambao ni neno la Mungu;
17 kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika
Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;
Kwanza kabisa
katika kuangalia mistari hii kwa makini tunapata aina za silaha ambazo kwa izo
tunaweza kabisa kumshinda shetani.
Zipo silaha
za saba (7) ambazo tunaziona Mtume Paulo amezielezea hapa na silaha hizo zikiwa
zimegawanyika katika makundi mawili
1.
SILAHA ZA KUJILINDA
2.
SILAHA ZA KUSHAMBULIA
1.SILAHA
ZA KUJILINDA
Silaha za kujilinda zimegawanyika katika makundi matano ya
silaha kama yafatavyo
1.
Chepeo ya wokovu
2.
Dirii ya haki
3.
Miguu ya utayari
4.
Ngao ya Imani
Chepeo ya wokovu
2.SILAHA
ZA KUSHAMBULIA
Silaha za kushambulia zimegawanyika katika makundu mawili
kama zifuatavyo:-
1.
Upanga wa roho
2.
Maombi katika roho
Itaendelea…
No comments:
Post a Comment