KARAMA
ZA ROHONI NA UTENDAJI WAKE (Sehemu ya kwanza)
NA; JAMES F. MZAVER
Bwana
Yesu asifiwe sana niwakaribishe tena katika somo jingine la karama za Roho
Mtakatifu katika maisha ya mwamini. Licha ya kua na uelewa mmbaya katika karama
za rohoni pia kumekua na udanganyifu katika mafundisho ndani ya kanisa la
Kristo katika swala hili, hivyo Bwana amenipa kibali niweze kuleta mfululizo wa
karama za Rohoni kwanzia karama ya kwanza hadi ya mwisho na nina Imani Roho Mtakatifu
atatusaidia ili tuweze kuelewa zaidi. Karibu sana
KARAMA ZA ROHONI NI NINI?
Naam
kabla ya kuangalia karama zenyewe katika maandiko ni vyema kwanza tuweze
kuelewa nini maana ya karama ni nini.
KARAMA ZA ROHONI ~
ni zawadi, za Roho Mtakatifu kwa kila mwamini ndani kanisa kwa lengo la kujenga
kanisa na la kusaidia kazi ya Bwana itendeke.
Hizi
ndizo nyenzo au vitendea kazi katika shamba la Bwana, inakua ni ngumu sana kwa
mwamini au kanisa kuishi bila karama za Roho Mtakatifu ni lazima udumavu
utaonekana tu.
MGAWANYO WA KARAMA ZA ROHONI
Karama
za Rohoni kibiblia zipo katika makundi au mafungu mbalimbali ambayo nitaenda
kukufundisha katika masomo yanayofuata moja baada ya nyingine na jinsi
zinavyotenda kazi ndani ya mwamini na kanisa pia. Biblia inatufundisha juu ya
karama hasa katika vitabu vya (1
Wakorintho 12:4-11 na Warumi 12:6-8) maandiko hayo yanatuonesha aina
mbalimbali za karama tuanze na andiko la
1
Wakorintho 12:4-11
Basi pana
tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.
5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.
6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;
9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;
10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama
5 Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule.
6 Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.
7 Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.
8 Maana mtu mmoja kwa Roho apewa neno la hekima; na mwingine neno la maarifa, apendavyo Roho yeye yule;
9 mwingine imani katika Roho yeye yule; na mwingine karama za kuponya katika Roho yule mmoja;
10 na mwingine matendo ya miujiza; na mwingine unabii; na mwingine kupambanua roho; mwingine aina za lugha; na mwingine tafsiri za lugha;
11 lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama
Mistari hii inatuonesha kwanza mgawanyo kabla
ya karama zenyewe angalia kwa makini kwanza mstari wa 4 hadi wa 6 tunaona
kwanza mgawanyo wa utatu katika utendaji kazi katika kanisa au kwa mwamini
mwenye huduma na vipawa. Anasema pana tofauti za karama bali Roho ni yeye yule
na pana tofauti kati ya huduma lakini Bwana ni yeye yule na pana tofauti za
utendaji kazi na Mungu ni yeye yule.
Maana yake ni hii apo juu kwanza mtoa karama ni
Roho Mtakatifu na mtoa huduma ni Bwana au Yesu Kristo na anayefanya hizo zote
zitende kazi katika aina mbali mbali ni Mungu Baba
Angalia;
ROHO MTAKATIFU
___ ANATOA KARAMA
MWANA (YESU KRISTO) ___ ANATOA
HUDUMA
MUNGU BABA ___ ANAWEZESHA UTENDAJI WOTE
Karama ambazo tumeziona sawa sawa na andiko la
Wakorintho ziko karama 9 ila ziko katika mafungu makuu matatu ambazo
nitazielezea kwa kina katika masomo yajayo. Karama za Roho Mtakatifu na makundi
yake.
KARAMA ZA
UFUNUO
1. NENO LA MAARIFA
2. NENO LA HEKIMA
3. KUPAMBANUA ROHO
KARAMA ZA NGUVU
1. IMANI
2. MATENDO YA
MIUJIZA
3. KARAMA ZA
KUPONYA
KARAMA ZA LUGHA
1. UNABII
2. TAFSIRI ZA
LUGHA
3. AINA ZA LUGHA
Ujumla wake ni karama tisa (9) zile zile na utendaji wake ni chini ya Roho Mtakatifu
mwenyewe, Lakini bado Biblia inatufundisha Zaidi karama Zaidi ya hizi katika
kitabu cha Warumi 12:6-8
Basi
kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa
unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani;
7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;
8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.
7 ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake;
8 mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha.
Sawa sawa na kitabu cha Warumi 12:6-8 tunaona karama Zaidi kama vile karama ya kuonya, kukirimu,
kusimamia na kurehemu. Kumbuka hizi zote ni karama za kuwezeshwa na Roho
Mtakatifu, haina maana kwamba watu wasio na Roho Mtakatifu hawawezi kua na hizi
karama la! Mtu anaweza kua na karama bila ya mwenye karama kua pamoja naye.
Naam huenda hujanielewa vizuri ngoja nikwambie Zaidi juu ya hili ni muhimu sana
kuelewa. Kitabu cha Mathayo 25: 14-30
kinaelezea juu ya talanta. Ipo siri kubwa sana juu ya hii habari hasa mistari
ya mwanzo juu ya kisa hiki cha talanta. Kwanza kabisa maana ya neno talanta
likimaanisha kipawa, uwezo au zawadi. Haina tofauti kabisa na maandiko yetu ya
mwanzo juu ya karama za Roho Mtakatifu katika ugawanyaji wake wa karama katika
maisha ya mwamini. Hebu tangalie basi mstari wa 14 na 15 wa Mathayo 25
Mathayo
25:14-15
14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri,
aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.
15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
Angalia mstari wa 15 mwishoni imeandikwa baada
ya kuwagawia kila mmoja kwa uwezo wake yule Bwana akasafiri. Kiroho andiko hili
liko sawa kabisa na karama za Rohoni katika kanisa. Na juu ya andiko hili
tunaona mambo mawili makuu ya msingi ya kufahamu hasa kwa habari ya karama za
Rohoni.
1. Karama za Rohoni hutegemea Zaidi uwezo wako wa rohoni. Naam angalia
mstari wa 15. Akampa mmoja talanta tano… kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake. Hii
haimaanishi kwamba karama hutolewa kwa kigezo cha uwezo wa mtu kiroho maana
sawa sawa na andilo letu la awali la Wakorintho 12 Roho mwenyewe humgawia kila
ampendaye karama zake. Lakini pia Mtume Paulo anatwambia katika 1 Wakorintho 14:2 …kuhusu kutaka karama
zilizo kuu, ambazo hizi huendana kabisa na uwezo wa kiroho
2. Unaweza ukawa na karama pasipokua na yule aliyekupa karama. Naam hii ni
siri nyingine katika andiko apo juu mstari wa 15 mwishoni kabisa Biblia inasema
“AKASAFIRI” ikiwa na maana hawa
watumwa walipewa talanta yaani karama na Bwana wao na baadaye yule Bwana akasafiri
zake akawaachia karama ambazo walipaswa kuzifanyia kazi ili zizae. Ndugu kua na
karama haimanishi ndio dalili ya mtu kua na Roho Mtakatifu La hasha!! Ni jambo
moja kua na Roho mtakatifu kwenye maisha yako na ni jambo jingine kua na karama
zake kwenye utendaji. Balaa kubwa leo kanisani ni wengi wana karama na wengi
hao hao wenye karama hawana Bwana wa karama katika maisha yao wamebaki wakienda
kwa uzoefu tu pasipo udhihirisho halisi wa Roho Mtakatifu katika maisha yao.
Hivi leo ni jambo la kawaida kuona mkristo aliyeokoka kushindwa ata
kudhihirisha utendaji kazi wa Roho Mtakatifu katika huduma.
Ndugu hayo ni mambo mawili ya msingi sana
kukumbuka katika swala la karama. Karama haina matunda yeyote endapo haisukumwi
na yule aliyekupa, epuka ukawaida kwa kile Mungu alichokujalia kukupa ni hatari
sana
Katika kuongezea juu ya karama 9 za Roho
Mtakatifu Biblia inatwambia yapo matunda 9 pia ya Roho mtakatifu ambayo kwa
wakati mwingine nitayaelezea.
Lakini haya yote katika makundi yake yaani
karama pamoja na matunda ya Rohoni cha umuhimu Zaidi ni kua na tunda la Roho
kwanza na karama badae Karama zote
hutendeka chini ya tunda la Roho katika upendo. Ndugu umuhimu wa karama ni
tunda la Roho japo zipo faida nyingi mbalimbali lakini katika upendo ndilo kuu
Zaidi.
Itaendelea….
UBARIKIWE SANA
Imeandaliwa na kuandikwa na;
James F. Mzava
Simu namba
; 0756259621
Barua pepe; jamesmzava@gmail.com