Huduma ya kimataifa "Mwanga wa
Mataifa" inakuletea:
Ufunuo wa Mbinguni na Kuzimu wa vijana 7
Kwa pamoja kama kundi,vijana hawa 7 wa
Kikolombia walichukuliwa na Yesu Kristo na walionyeshwa Mbinguni na
Kuzimu.Sikiliza maneno yenye utukufu wa Mbinguni na Ubaya wa Kuzimu.
Kutokana na kumbukumbu tumeweza kuandika shuhuda 6 tu, zilizo tafsiriwa kutoka kanda ya kihispania,Picha ziliongezwa baadaye na hazikuwa sehemu ya ushuhuda .Claudia Alejandra Elavezabal ndiye alite tafsiri |
Ufunuo wa Mbinguni
--- (Ushuhuda wa kwanza, Esau) ---
2
Wakorinto 12:2 :
Namjua mtu mmoja katika Kristo,yapata sasa miaka kumi na minne-kwamba alikuwa katika mwili sijui;kwamba alikuwa nje ya mwili sijui;Mungu anajua-mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
Namjua mtu mmoja katika Kristo,yapata sasa miaka kumi na minne-kwamba alikuwa katika mwili sijui;kwamba alikuwa nje ya mwili sijui;Mungu anajua-mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
Tulikuwa ndani ya chumba,wakati tulipo pata uzoefu huu wa kwanza.Chumba
kilianza tena kujaa na utukufu wa Bwana. Ulikuwa na nguvu sana kiasi
kwamba ulikiangazia chumba chote. Chumba kilikuwa kimejaa utukufu
wake,ilikuwa ni jambo zuri kuwepo mbele zake.
Yesu alituambia, "Watoto
wangu wakiume,sasa nitawaonyesaho Ufalme wangu, tutakwenda kwenye utukufu
wangu." Tulishikana mikono na tuliinuliwa juu.
Nili angalia chini na niligundua kuwa tulikuwa tunatoka nje ya miili
yetu. Tulipotoka nje ya miili yetu tulikuwa tumevaa mavazi meupe na
tulianza kwenda juu kwa mwendo wa kasi sana.Tulifika mbele ya malango yaliyo
fuatana ambayo ni njia ya kuingilia kwenye ufalme wa Mbinguni. Tulishangaa kile
kilicho kuwa kina tutokea. Shukrani nyingi,Yesu mwana wa Mungu
alikuwepo pale pamoja nasi, pamoja na malaika wawili ambao kila mmoja alikuwa
na mabawa manne.
Malaika walianza kuongea nasisi, lakini hatukuelewa
kile walicho kuwa wanasema . Lugha yao ilikuwa tofauti sana na ile ya kwetu,
haikufanana na lugha yeyote ile ya duniani. Malaika hawa walikuwa
wakitukaribisha na waliifungua milango ile mikubwa sana. Tuliona eneo la
ajabu sana, lenye vitu vingi tofauti tofauti. Tulipoingia ndani, amani ya kweli
ilijaza miyoyo yetu. Bibilia inatuambia kuwa Mungu atatupa amani ipitayo
fahamu za kibinadamu (Wafilipi 4:7)
Kitu cha kwamza kukiona
ilikuwa ni swala,hivyo nilimuuliza mmoja wapo wa marafiki zangu, "Sandra,
je unaangalia kitu kile kile ninacho kiangalia?" hakuwa
analia wala kupiga makelele tena, kama wakati ule tulipo onyeshwa
kuzimu. Alikuwa akitabasamu na alisema: "Ndiyo Esau,
ninamwaangalia Swala!" Hivyo nilijua kuwa kila kitu kilikuwa halisi,
kweli tulikuwa kwenye Ufalme wa Mbinguni. Hofu zote ambazo tuliziona kule
Kuzimu haraka zilikuwa zimesahaulika. Tulikuwa mahali pale tukiufurahia utukufu
wa Mungu. Tulikwenda mahali pale ambapo Swala yule alikuwepo, nyuma yake
ulisimama mti mkubwa sana! Ilikuwa ni katikati ya bustani.
Bibilia inatuambia katika Ufunuo 2:7 "Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.Yeyey ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu"
Mti huu ni ishara ya Yesu, kwasababu Yesu ni uzima wa milele. Nyuma ya ule mti kulikuwa na mto wenye maji angavu. Ulikuwa mweupe na mzuri sana, hatukwa tumewahi kuona tena kitu kama hiki duniani. Tulitaka tuu kubaki mahali pale. Mara nyingi tulimwambia Bwana, "Bwana tafadhali! Usitutoe mahali hapa! Tunataka kuwepo hapa milele! Hatutaki kurudi tena duniani Bwana alitujibu "Ni muhimu kwamba mrudi mkatoe ushuhuda wa kila kitu ambacho nimekiandaa kwa wote wale wanao nipenda, kwa sababu ninarudi mapema sana na ujira wangu u pamoja nami"
Tulipo ona mto, tulifanya
haraka na tukaingia ndani yake. Tulikumbuka msitari ule unao
sema;Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena,mito ya maji yaliyo hai
itatoka ndani yake.. (Yohana 7:38) Maji ndani ya mto huu
yanaonekana yana uzima yenyewe, hivyo tulijizamisha wenyewe ndani
yake. Ndani na nje ya yale maji tuliweza kupumua kawaida. Mto ule
ulikuwa na kina kirefu sana na kulikuwa na samaki wa rangi tofauti wakiogelea
ndani yake. Mwangaza ndani na nje ya maji ulikuwa wa kawaida; Mbinguni ,
mwanga hautoki kwenye kitu fulani,kila kitu kimetiwa mwangaza wake.
Bibilia inatuambia kuwa Bwana Yesu (Ufunuo 21:23). Kwa mikono yetu,
tulichukua baadhi ya samaki, nje ya maji, hawakufa. Hivyo tulimkimbilia
Bwana na kumuuliza kwanini? Bwana alitabasamu na alijibu kwamba Mbinguni
hakuna tena kifo, hakuna kilio tena, hakuna maumivu tena (Ufunuo 21:4)
Tuli uacha ule mto na tulikimbia kila mahali tulipo weza, tulitaka kugusa na kuwa na uzoefu wa kila kitu. Tulitaka kurudi na kila kitu nyumbani kwa ababu tulishangazwa sana na vitu vya mbinguni. Kwa kifupi huwezi kuvielezea kwa maneno. Wakati Mtume Paulo alipochukuliwa Mbinguni, aliona vitu ambavyo hakuweza kuvielezea kwa maneno, kwa sababu ya ukuu wa vitu vya Ufalme wa Mbinguni. (2 Wakorinto 12) Kuna vitu ambavyo tuliviona ambavyo hatuna jinsi ya kuvielezea.
Baadaye tulifika kwenye
eneo kubwa sana; eneo la ajabu na zuri sana. Eneo hili lilikuwa limejaa
mawe ya dhamani sana: dhahabu, emiradi, rubi na almasi. Sakafu ilikuwa
imetengenezwa na dhahabu halisi. Baadaye tulikwenda hadi eneo lenye vitabu
vikubwa vitatu. Cha kwanza kabisa kilikuwa ni Bibilia ya dhahabu.
Katika Zaburi inatuambia kwamba neno la Bwana linasimama imara mbinguni hata
milele. (Zaburi 119:89) Tulikuwa tukiangalia
Bibilia kubwa ya dhahabu; kurasa, maandiko, kila kitu kilifanywa kwa dhahabu
halisi.
Kitabu cha pili tulicho kiona kilikuwa kikubwa zaidi ya ile Bibilia. Kilikuwa wazi na malaika alikuwa amekaa pale akiandika ndani yake. Pamoja na Yesu , tulisogea karibu kuona nini mbacho malaika yule alikuwa. Malaika alikuwa akiandika kila kitu kilicho kuwa kina tokea duniani. Kila kitu kilicho tokea; pamoja na tarehe, saa, kila kitu kina andikwa pale. Hili linafanyika ili neno la Mungu litimie pale linaposema na vitabu vikafunguliwa; kwamba watu juu ya nchi wakahukumiwa sawa na matendo yao yaliyo andikwa kwenye vitabu hivyo (Ufunuo 20:12). Malaika alikuwa akiandika kila kitu ambacho watu walikuwa wakikifanya hapa duniani,kizuri au kibaya, vyote viliandikwa.
Tuliendelea hadi kwenye kile kiitabu cha tatu. Kilikuwa kibwa zaidi ya kile cha pili.Kitabu kilikuwa kimefungwa, lakini tulikisogelea. Sisi sote 7, tulikichukua kile kitabu toka mahali pake, kutokana na amri ya Bwana, na tulikiweka juu ya nguzo.
Nguzo zile nazile za
miraba kule Mbinguni ni za ajabu sana! Hazikufanywa kama kwa mawe duniani. Nguzo zile za miraba zilikuwa
kama za vito, zilikuwa zimefanywa kwa mawe ya dhamani. Baadhi zilikuwa
zimefanywa kwa almasi, nyingine kwa emiradi, nyingine kwa dhahabu halisi na
nyingine kwa mchanganyiko wa mawe ya aina tofauti. Niligundua kwa hakika kuwa
Mungu ndiye mmiliki wa vitu vyote, kama ilivyo andikwa katika Hagai
2:8, "Dhahabu ni mali yangu, na fedha
ni mali yangu." Nina elewa kuwa MunguI ni tajiri sana na anamiliki
utajiri wote duniani. Nina elewa pia kuwa dunia na vyote viijazavyo ni
mali ya Mungu wetu na anataka kuwapa wale wote wanao omba kwa imani Bwana anasema, "Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa uridhi wako."
(Zaburi 2:8) Kitabu hiki ambacho
tulikiweka kwenye zile nguzo, kilikuwa ni kikubwa sana kiasi kwamba kuweza
kufungua ukurasa mmoja tulitembea hadi upande mwingine wa ukurasa.
Tulijaribu kusoma kile ambacho kilikuwa ndani ya kile kitabu, kama Bwana alivyo
alivyo tuambia. Mwanzoni ilikuwa ni vigumu kusoma kwa sababu ilikuwa
imeandikwa kwa njia ambayo hatuijui hivyo hatukuelwa. Ilikuwa ni tofauti
na lugha yeyote ile ya duniani; kilikuwa ni kitu cha kimbinguni. Lakini
kwa msaada wa Roho Mtakatifu, tulipewa neeema ya kuelewa.Ni kama vile kitambaa
kiliondolewa machoni mwetu na tuli weza kuyaelewa yale maaandaiko; vile vile
kama lugha yetu.
Tuliweza kuona kuwa
majina yetu wote saba yalikuwa yame andikwa kwenye kile kitabu.Bwana alituambia
kuwa kilikuwa ni kitabu cha uzima. (Ufunuo 3:5) Tuligundua kuwa majina
yaliyo kuwepo kwenye kile kitabu siyo yale tunayo tumia duniani; majina haya
yalikuwa ni mapya, hivyo neno la Mungu l;iweze kutimia linaposema kuwa Atatupa
majina mapya ambayo hakuna mtu yeyote anayelijua isipo kuw yule tuu anaye
lipokea. (Ufunuo 2:17)
Kule mbinguni tuliweza
kuyatamka majina yetu, lakini mara Bwana alipo tuleta duniani, majina yale
yaliondolewa kwenye ufahamu wetu na rohoni mwetu. Neno la Mungu ni la
milele na litatimia. Rafiki zangu,Bibilia inasema, (Ufunuo 3:11) Usiruhusu mtu
akaichukua taji yako, usiruhusu mtu yeyote akaondoa nafasi ambayo tayari Baba
anayo tayari kwa ajili yako. Mbinguni kuna vitu millioni nyingi sana
ambavyo ni vya ajabu, hatuwezi kuvielezea kwa midomo yetu. Lakini nataka
kukuambia kitu hiki, "Mungu anakusubiri!" Hatahivyo, ni kwa
yule atakaye vumilia hadi mwisho ndiye atakaye okoka! (Mark
13:13)
--- (Ushuhuda wa pili, Ariel) ---
Wakati tulipo anza kwenda juu kwenye Ufalme wa
mbinguni , tulifika eneo zuri lenye milango ya dhamani.Mbele ya Milango
walikuwepo malaika waili.Walianza kuongea.Lakini maneno yao yakikuwa ni ya
kimalaika na hatukuweza kujua kile walicho kuwa wakiongea.Lakinio Roho
Mtakatifu alitupa ufahamu.Walikuwa wakitukaribisha.Bwana Yesu aliweka mkono
wake kwenye milango na ikafunguka.Kama Yesu hakuwa pamoja nasi, tusingeweza
kuingia Mbinguni.
Tulianza kufurahia kila kitu mbinguni.Tuliona mti mkubwa,
Bibilia inaelezea mti huu kama "Mti
wa Uzima." (Ufunuo
2:7) Tulikwenda kwenye mto, na tuliona samaki wengi sana ndani.Kila
kitu kilikuwa ni cha kushangaza kiasi kwamba mimi na rafiki zangu tuliingia
ndani ya yale maji. Tulianza kuogelea chini ya yale maji.Tuliona samaki
wakiogelea na kuigusa miili yetu.Hawakuwa wakituimbia kama ilivyo kawaida
duniani; Uwepo wa Bwana ulituliza samaki.Samaki walituamini kwa sababu walijua
kuwa tusinge waumiza. Nilikuwa nimebarikiwa sana na kushangazwa kiasi kwamba
nilimshika mmoja wa wale samaki na kumtoa nje majini.Cha kushangaza ni kwamba
yule samaki alikuwa mtulivu sana akiufurahia uwepo wa Bwana hata mikononi
mwangu.Nili mrudisha samaki kwenye maji.
Niliweza kuona kwa mbali kwamba kulikuwa na farasi
weupe Mbinguni,kama ilivyo andikwam katika neno la Mungu katika Ufunuo
19:11. "Kisha nikaziona mbingu
zimefunuka, na tazama, farasi mweupe, na yeye aliyempanda, aitwaye mwaminifu na
wa kweli, naye kwa haki ahukumu na kufanya vita." Farasi
wale ni wale amabo Bwana atawatumia atakapo kuja duniani kuwachukua watuwake,
kanisa lake.Niliwaendea wale farasi na kuanza kuwagusa.Bwana alinifuata na
aliniruhusu kumpanda mmoja wapo.
Nilipo anza kumwendesha , nilisikia kitu ambacho
sikuwahi kukisikia duniani.Nilianza kisikia amani, uhuru, upendo, utakatifu
ambao mtu anaweza kuwa nao katika eno lile zuri.Nilianza kufurahia kila kitu
ambacho macho yangu yalikiona.Nilitaka kufurahia kila kitu katika eneo lile
zuri ambalo Bwana ameandaa kwa ajili yetu.
Tuliweza pia kuona meza ya sherehe ya harusi, kila
kitu kilikuwa tayari kime andaliwa.Haina mwanzo wala mwisho.Tuliona viti
vimeandaliwa kwa ajili yetu.Kulikwepo pia mataji ya uzima wa milele ambayo
yalikuwa yapo tayari kwa ajili yetu.Tuliona vyakula vizuri vikiwa yatari kwa
ajili ya wote watakao alikwa kwenye meza ya mwana kaondoo.
Malaika walikuwepo pale
na vitambaa nyeupe kwa mavazi ambayo Bwana anatuandalia. Nilishangaa sana
nikiangalia vitu vyote hivi.Neno la Mungu linatuambia ni lazima tuupokee Ufalme
wa Mungu kama watoto wadogo. (Mathayo 18:3) Tulipo kuwa
mbinguni tulikuwa kama watoto wadogo. Tulianza kufurahia kila kitu pale; maua,
makazi... Bwana alituruhusu hata kuingia ndani ya yale makazi.
Baadaye Mungu alituchukua hadi kwenye eneo lenye watoto wengi.Bwana alikuwepo katikati yao na alianza kucheza nao.Alihakikisha kuwa anatumia muda wa kutosha na kila mmoja wao. na alifurahia kuwa pamoja nao.Tulimsogelea Bwana na kumuuliza, "Bwana je! hawa watoto ndio watakao kwenda kuzaliwa duniani?". Bwana alijibu, "Hapana, hawa ni wale ambao mimba zao zilitolewa duniani". Kwa kusikia vile,nilisiia kitu ndani yangu kilicho nifanya nitetemeke.
Nilikumbuka kitu fulani
ambacho nilikuwa nimekifanya huko nyuma,wakati ambapo sikumjua Bwana.
Kipindi kile nilikuwa na uhusiano na mwana mke na alipata mimba. Alipo
niambia kuwa kwamba alikuwa nja mzito, sikujua nini cha kufanya hivyo
nilimwomba anipe muda ili nifanye maamuzi.Muda ulipita na nilipo kwenda kwake
kumweleza maaamuzi yangu, ilikuwa tayari nimechelewa kwa sababu alikuwa tayari
amechatoa ile mimba.. Hili liliweka doa kwenye maisha yangu. Hata baada
ya kumpokea Yesu moyoni mwangu, utoaji mimba ule ulinifanya nisiweze
kujisamehe.Lakini Mungu alifanya kitu siku ile, aliniruhusu kuingia eneo lile
na aliniambia, "Ariel, unamwona yule
msichana pale?Msichana yule ni mtoto wako." Alipo
niambia vile nilimwona msichana,nilisikia kidonda kilichokuwa ndani yangu kwa
muda mrefu kikianza kupona. Bwana aliniruhusu kutembea karibu yake na
alinikaribia.Nilimchukua mikononi mwangu na niliyaona macho yake.Neno moja
nilisikia toka kwenye kinywa chake,"Daddii". Nilielewa
na nilijisikia kuwa Mungu anayo rehema juu yangu na amenisamehe,lakini ilibidi
nijifunze kujisamehe mwenyewe.
Rafiki yangu, yeyote
anayesoma habari hii, nataka kukuambia jambo moja.Mungu amekwisha kukusamehe
dhambi zako, sasa nilazima ujifunze kujisamehe wewe binafsi. Ninampa
Mungu shukrani kwa kuniruhusu kuushiriki ushuhuda huu na wewe. Bwana
Yesu nakupa wewe heshima na utukufuLord! Ushuhuda huu ni wa
Bwana,alituruhusu sisi kuupokea ufunuo huu. Nina tumaini kuwa kila mmoja wetu
atakaye usoma atapokea baraka za ushuhuda huu na ataupeleka ili
kuwabarikia na wengine wengi.
Mungu akubariki.
--- (Ushuhuda wa tatu) ---
Naye atafuta kila chozi katika macho
yao,wala mauti haita kuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu
hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.
Wakati tulipo fika, malango haya makubwa
yalitufungikia, na nilianza kuona bonde lilojaa maua.Maua yalikuwa ni mazuri na
harufu yake ilikuwa ni ya kipekee.Tulianza kutembea na kuzoelea uhuru
kamili kuliko tulio wahi kuwa nao duniani.Tulisikia amani iliyo ujaza miyoyo
yetu na tulipo yaangalia maua tuligundua kuwa yalikuwa ni ya kipekee; kila
kiini cha ua kilikuwa tofauti,halisi na yenye rangi ya kipekee Ndani ya moyo wangu, nilimwambia Bwana kuwa
nilitaka kuwa na ua kama moja wapo ya haya.Bwana alitoa ishara ya kunikubalia,
nilisogelea ua na kuanza kulivuta. Lakini hakuna kilicho tokea, sikuweza
kuling, oa ua toka aridhini. Sikuweza hata kuvuta kiini cha ua hata majani yake
toka kwenye ua.Baadaye Bwana alivunja ukimya na kusema, "Hapa kila kitu ni lazima kifanyike kwa upendo."
Aligusa ua
na ua lilijiachilia lenyewe kwenye mikono ya Bwana . Baadaye alinipa lile
ua.Tuliendelea kutembea na harufu ya maua bado ilikuwa pamoja nasi.
Tulifika eneo lenye
milango mizuri sana inayo fuatana.Milango hii haikuja ya kawaida, ilikuwa ni
kazi ya usitadi mkubwa na kulikuwa na mawe ya dhamani yaliyo chimbiwa
ndani yake. Milango ilifunguka na tuliingia ndani ya chumba kilicho kuwa na
watu wengi.Kila mmoja alikuwa akikimbia hapa na pale akifanya maandalizi.Baadhi
yao walibeba majohoro ya vitambaa vyeupe juu ya mabega yao mashine zenye
nyuzi za dhahabu, na bado wengine walikuwa wakibeba aina fulani ya sahani zenye
kitu kama ngao ndani yake.Kila mmoja alikuwa akikimbia kwa jitihada
Tulimuuliza Bwana ni kwa
nini kulikuwa na juhudi kubwa vile na haraka. Hivyo Bwana alimwamuru kijana
mmoja kuja karibu. Mtu huyu alikuwa na johora la kitambaa
mabegani mwake. Alikuja na kumwangalia Bwana kwa heshima. Wakati Bwana alipo muuliza
kwa nini alikuwa amebeba johora lile la kitambaa, alimwangalia Bwana na kusema,
"Bwana unajua kitambaa hiki ni cha nini! Kitambaa kinatumika kutengezea
mavazi ya walio kombolewa, avazi kwa ajili ya Bibi arusi mkuu." Katika
kusikia hili, tulijisikia furaha kuu na amani. Ufunuo 19:8 Inatuambia: "Naye amepewa kuvikwa kitani nzuri, ing,arayo, safi; kwa
maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifuk."
Tulipo toka nje ya mahali pale , tulijisikia amani zaidi,kwa sababu lilikuwa ni jambo zuri kuona kuwa Bwana mwenyewe alikuwa akiandaa kitu kizuri kwa ajili yetu. Analo eneo na muda kwa ajili yako kwa sababu wewe ni wa muhimu kwake. Tulipo toka nje ya mahali pale, macho yetu yalichuliwa katika kila maelezo ya mbinguni. Ni kama kila kitu kilikuwa na uhai wake pekee yake, na kila kitu pale kilikuwa kina mpa Mungu utukufu.
Baadaye tulikuja kwenye eneo lililokuwa na watoto milioni na milioni, wa kila umri. Walipo mwona Bwana, wote walitaka kumkumbatia, kusikia zaidi upendo wake, kwa sababu yeye ndiye upendo wao. Yesu aalikuwa ni upendo wa kila mtoto pale. Tulijisikia kama kulia tulipo ona jinsi Bwana alivyo mhudumia kila mmoja wa watoto wale, jinsi alivyo wa busu na kuishika mikono yao.
Tuliona jinsi malaika walivyo kuja karibu na Bwana,
wakimletea watoto, wakimletea watoto waliofunikwa na nguo maalumu. Bwana
aliwajali, aliwagusa,aliwapa busu juu ya upaji wa nyusso zao na baadaye malaika
waliwarudisha. Tulimuuliza Bwana ni kwanini kulikuwa na watoto wengi vile pale,
je watot hawa ndio watakao kwenda kutumwa duniani.Bwana alio nyesha kuguswa kwa
muda, na alisema, "Hapana, watoto hawa
hawatatumwa duniani! Hawa ni wale ambao mimba
zao zilitolewa duniani, ambao wazazi wao hawakupenda kuwa nao.Hawa ni
watoto wangu na nina wapenda." Niliinamisha kichwa changu,
hata sauti yangu ilitetemeka kuuliza swali kama lile.
Wakati ule ambao sikumjua Bwana , yeye ambaye ndiye
maisha ya kweli,nilifanya makosa na kutenda dhambi kama wati wengine. Kati ya
dhambi hizo ni ile ya kutoa mimba. Kuna wakati nilikuwepo mbele ya uso wa Bwana
na nilimuuliza, "Bwana, je! mtoto yule aliye tolewa mimba yake zamani
yupo hapa?". Bwana alinijibu, "Ndio." Nilianza kutembea upande
mmoja wapo na nilimwona mtoto mzuri wa kiume. Karibu ya miguu yake
alisimama malaika. Malaika alikuwa akimtazama Bwana, na kijana yule alitugeuzia
mgongo wake.
Bwana aliniambia, "Angalia, yule ni mtoto wako."
Nilitaka kumwona hivyo nilimkiimbilia, lakini malaika alinisimamisha na mkono
wake.Alini onyesha kuwa nilitakiwa kumsikiliza yule kijana kwanza. Nilianza
kusikia kile yule mtoto alikuwa akisema .Alikuwa akiongea na kutazama upande
ule wa watoto wengine. Alimuuliza malaika, "Je baba yangu na mama yangu
watakuja mahali hapa mapema?" Malaika, alini angalia, akamjibu,
"Ndiyo,baba yako na mama yako karibu watauja sasa."
Sijui ni kwa nini
nilipewa upendeleo wa kuyasikia maneno yale, lakini ndani ya moyo wangu nilijua
kuwa maneno yale yalikuwa ni zawadi kubwa mabayo Bwana angeweza kunipa.
Mtoto huyu hakuwa akiongea kwa hasira, wala maumivu,labda kwa kujua kuwa
hatukumruhusu azaliwe.Alikuwa akingojea tuu kwa upendo ambao Bwana alikuwa
ameuweka moyoni mwake
Tuliendelea kutembea,
lakini niliweka sura ya yule mtoto moyoni mwangu. Najua kuwa kila siku natakiwa
kufanya jitihada kuhakikisha kuwa nitakuwa pamoja naye siku moja. Nina sababu
moja nyingine ya kwenda pale, kwa sababu kuna mtu ananisubiri kwenye ufalme wa
Mbinguni. Neno la Mungu lina tuambia katika Isaya 65:19, "Nami nitaufurahia Yerusalemu, nitawaonea shangwe
watu wangu; sauti ya kulia haitasikiwa ndani yake tena, wala sauti ya
kuomboleza."
Tulikuja eneo lenye
milima midogo, na Bwana Yesu alikuja huku akicheza. Mbele yake walikuwepo umati
wa watu wakiwa wamevaa mavazi meupe na waliinyanyua mikono yao juu ikiwa na
matawi mabichi ya mizeituni. Walipo yanyoosha yale matawi hewani, waliachilia
mafuta.Mungu anakitu kikubwa alicho kiandaa kwa ajili yako! Sasa ni wakati wako
wa kuandaa moyo wako kwa ajili yake.
Mungu akubariki.
--- (Ushuhuda wa nne) ---
Kwenye Ufalme wa mbinguni, tuliona vitu vya
ajabu kama ilivyo andikwa katika neno la Mungu, 1
Wakorintho 2:9, "Mambo ambayo jicho
halikuyaona, wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa
mwanadamu,Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampenda."
Tulifika wasili kwenye ufalme wa mbinguni ilikuwa ni
ya kuvutia na kustaajabisha kuona vitu vingi vile; vitu vingi sana na kuusikia
utukufu wa Mungu. Ilikuwa ni ya kipekee sana;eneo lenye watoto wengi sana.Tuna
weza kusema kuna watoto millioni nyingi eneo lile.
Tuliwaona watoto wa umri tofauti tofauti, mbingu
ilikuwa imegawanywa kwenye maeneo tofauti.Tuliona aina ya nyumba za kutunzia watoto
wenye umri mdogo wa miaka kama 2-4 .Tuligundua kuwa watoto mbinguni huendelea
kukua na pia kuna shule ambapo watoto hufundishwa neno la Mungu. Waalimu ni
malaika na wanawafundisha watoto nyimbo za kuabudu na jinsi ya kumtukuza Bwana
Yesu.
Wakati Bwana alipofika, tuliweza kuona furaha kuu ya
mfalme wetu. Japo hatukuweza kuuona uso wake, tuliweza kuona tabasamu lake,
lilijaza eneo lote lile . Alipo wasili, watoto wote walimkimbilia! Katikati ya
watoto wote wale, tulimwona Maria, mama wa Bwana Yesu duniani. Ni mwanamke
mwenye sura nzuri sana. Hatukumwona akiwa kwenye kiti cha enzi wala hakuna
yeyote aliyekuwa akimwabudu. Alikuuwepo pale sawa kabisa na wanawake wengine
walioko mbinguni,kama watu wengine duniani alitakiwa aweze kuupata wokovu wake.
Alikuwa na vazi jeupe na mshipi wa dhahabu matitini mwake na nywele zake ndefu
zilifika chini ya kifua.
Duniani, tumesikia watu wengi sana wakimwabudu
Maria kama mama wa Yesu , lakini nataka kukuambia kuwa neno la Mungu
linasema, "Mimi ndimi njia na kweli na uzima
; mtu haji kwa baba, ila kwa njia ya mimi." (Yohana
14:6) Mlango pekee wa kuingia kwenye ufalme wa mbinguni ni Yesu wa
Nazarethi.
Tuligundua pia kuwa
hakuna jua wala mwezi. Neno la Mungu linasema katika Ufunuo 22:5 " Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa
wala ya nuru ya jua; kwakuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata
milele na milele."
Tuliweza kuuona utukufu
wa Mungu. Ni vigumu kuuelezea ubaya tulio uona kuzimu, lakini pia ni vigumu
kuuelezea ukuu na uzuri wa vitu tulivyo viona na ukamilifu wa aliyevifanya.
Tulipo kuwepo pale tulitaka kukimbia na kuona kila kitu.. Tuliweza kulala chini
kwenyemajani, na tuliweza kuusikia utukufu wa Mungu. Mluzi mwororo; upepo mzuri
ulio jali nyuso zetu, kilikuwa ni kitu cha kushangaza.
Katikati ya anga tuliweza
kuona msalaba mkubwa wa dhahabu. Tunaamini kuwa hii haikuwa ni ishara ya sanamu
bali ni ishara ina yo onyesha kuwa kwa kifo cha Yesu tuna mlango wa kuingilia
kwenye Ufalme wa mbinguni.
Tuliendelea kutembea
mbinguni.Lilikuwa ni jambo la kuvutia sana kutembea na Bwana Yesu Kristo . Pale
tulijua kwa hakika ni Mungu yupi tunaye mtumikia ...Yesu wa Nazarethi.
Wengi wetu tuna waza kuwa kuna Mungu juu mbinguni anaye tusubiri tufanye dhambi
ili aweze kutuadhibu na kutupeleka Kuzimu.Lakini hili si sawa.Tuliweza kuuona
upande mwingine wa sura ya Yesu; Yesu aliye rafii, Yesu anayelia unapolia
.Yesu ni Mungu wa upendo mwenye huruma na rehema; Anatubeba mikononi mwake ili
tuendelee kwenye njia ya Wokovu.
Bwana Yesu pia
alituruhusu kukutana na Mtu aliye kwenye Bibilia . Tulikutana na Daudi, Mfalme
Daudi aliye tajwa kwenye maandiko.. Ni mtu mzuri, mrefu na sura yake ina
akisi Utukufu wa Mungu . Muda wote tulipo kuwa kwenye Ufalme wa Mbinguni,
kitu pekee ambacho mfalme Daudi alikuwa akikifanya ni kucheza, kucheza, kucheza
na kumpa Mungu Utukugu wote na heshima.
Kwa wote wanao usoma
ushuhuda huu, nataka kukuambia kuwa, kwenye neno la Mungu inasema kwenye Ufunuo 21:27 "Na ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho
kinyonge, wala yeye afanyaye machukizo na uongo, bali wale walioandikwa katika
kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo." Na pia nataka
kukuambia kuwa wenye nguvu ndio wanao uteka ufalme wa Mbinguni.
Mungu akubariki.
--- (Ushuhuda wa tano) ---
Kwa maana imetupasa sisi sote
kudhihirishwa mbele za kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya
mambo aliyo tenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya.
Kwenye Ufalme wa Mbinguni, tuliweza kuiona Yerusalemu
Mpya ambayo Bibilia inatuelezea habari zake katika Yohana
14:2, "Numbani kwa Baba yangu makao ni
mengi;kama sivyo, ningaliwaambia;maana nakwenda kuwaandalia mahali."
Tuli weza kuuona mji na kuingia ndani yake, ni mji wa kweli na wa ajabu! Yesu
alikwenda kutuandalia mji huu wa kuishi.
Kwenye jiji lile, tuliweza kuona kuwa kila jumba
lilikuwa na jina la mtu anaye limiliki mbele yake . Jiji hili bado halikaliwi
na mtu yeyote, lakini lipo tayari kwa ajili yetu. Tuliruhusiwa kuingia ndani ya
zile nyumba na kuona vitu vyote mle ndani. Lakini baada tuu ya kuondoka mle
ndani tulisahaulishwa kila kitu tulicho kuwa tumekiona, kumbukumbu zote
ziliondolewa. Hata hivyo tunaweza kukumbuka nguzo za nyumba zimepambwa na
vito vya dhamani na zina aina tofauti ya mawe ya dhamani ndani yake.Pia kuna
dhahabu halisi ndani yake.
Dhahabu ya Jiji lile ni
kama vile Bibilia inavyo elezea; Ni angavu, na inayo ngaa sana. Dhahabu ya
duniani haiwezi kulinganishwa na kwa uzuri na umbo la ile ya Mbinguni.
Baada ya hivi,
tulichukuliwa hadi kwenye eneo lenye vyombo vingii sana. Ndani ya vile vyombo
kulikuwepo na machozi kama vile barafu iliyo ganda. Haya ni machozi ambayo watu
wa Mungu wameya mwaga wakiwa duniani mbele za Mung, siyo machozi ya malalamiko,
bali machozi ya toba, machozi ya kiuungwana. Mungu huyahifadhi machozi haya
kama kitu cha dhamani Mbinguni,kama vile ilivyo tajwa katika Zaburi 56:8, "Umehesabu kutanga- tanga kwangu; Uyatie machozi yangu
katika chupa yako;je hayamo katika kitabu chako?"
Tulifika eneo pia ambalo kuna malaika wengi sana. Japo mbinguni tuliweza kuona aina nyingi za malaika,, eneo hili lina aina maalumu tuu ya malaika.Tuliona kuwa Yesu, ana malaika maalum,u kwa kila mtu.Alituonyesha kuwa malaika wale wangekuwa na sisi kwa muda wote wa sisi kuwepo .Alitutambulisha kwa malaika aliye pewa kuwa nasisi. Tulikwenda kuwaangalia na kujua tabia zao , lakini Mungu alitunyima tusi waambie watu mambo haya. Tunasoma katika Zaburi 91:11, "Kwa kuwa atakuangizia malaika zake wakulinde katika njia zako zote."
Tulikuja kwenye eneo lenye makabati mengi, ndani yake kulikuwa na maua ya aina tofauti. Baadhi ya maua yalichaua na, mazuri na yenye kung,aa . Lakini mengine yalikuwa yame inama na yamesinyaa .Tulimuuliza Yesu ninini maana ya yale maua ? Alijibu "Ni kwa sababu maisha ya kila mmoja wenu ni kama moja wapo ya maua haya." Alichukua moja wapo ya ua linalo ng,aa na kusema, "Ua hili lina onyesha aina ya uhusiano mlionao na mimi." Aliliacha lile ua na kuchukua jingine lilo kuwa chini. Alisema, "Angalia, mtu huyu yupo chini kwa sababu anapitia majaribu au magumu. Kuna kitu katika maisha kina cho ingilia mahusiano yetu na huyu mtu. Una fahamu kile ninacho fanya na maua haya yanapo kuwa chini ili kuya fanya kuchangamka na kuwa na afya tena?" Akachukua ua mkononi mwake na alisema, "Nina dondosha chozi langu juu yake na nina liinua tena." Tuliona ni kwa nguvu kiasi gani ua hili lilivyo weza kuwa na uhai tena na kuinuka na rangi zake zake kuanza kuonekana tena.
Baadaye alichukua moja
wapo ya ua lililo sinyaa na alilitupa kwenye moto na kusema, "Angalia mtu huyu alinijua na ameniacha na kwenda mbali
nami.Sasa amekufa bila ya kuwa na mimi na ametupwa motoni."
(Yohana 15:5-6)
Tulipo ondoka pale, tuliona kasiri zuri kwa mbali. Hakuna hata mmoja aliye dhubutu kulisogelea kasiri lile, na tuna amini hivi ndiyo vile maandiko yanavyo sema katika Ufunuo 22:1, "Kisha akanionyesha mto wa maji ya uzima, wenye kung,aa kama bilauri, ukitoka kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana Kondoo." Tuna amini kuwa kasiri lile lilikuwa karibu na uwepo na kiti cha enzi.
Wakati tuki yapitia yote hata kwenye Ufalme wa Mbinguni, tulikuwa na furahja kubwa sana miyoyoni mwetu, tulikuwa na amani ipitayo ufahamu wote. (Wafilipi 4:7) Tulielewa kama ilivyo andikwa katika 1 Petro 1:4, "tupate na uridhi usio haribika, usio na uchafu, usio nyauka, ulio tunzwa mbinguni kwa ajili yetu."
--- (Ushuhuda wa sita) ---
"mpate kula na
kunywa mezani pangu katika Ufalme wangu; na kuketi katika vitivya enzi, huku
mkiwa hukumu makabila 12 ya izraeli."
Kwenye eneo lile la ajabu, Mungu alituruhusu kuona
eneo zuri na la ajabu sana jumba la mapokezi ambalo hatuku wahi kufikiri
kama lima weza kuwepo mahali popopte kwenye sayari yetu. Tuliona Kiti cha enzi kikubwa na
tuliona viti viwili vya dhahabu halisi na mawe ya dhamani ambayo hayapo popote
dunaini. Mbele ya kiti kile kikubwa cha enzi kulikuwepo meza kubwa isiyo na
mwisho, na juu yake kulikuwa na kitambaa cheupe. Kilikuwa ni cheupe sana kwamba
hatukuweza kukilinganisha na kitu chochote duniani humu.Aina zote za vyakula
vizuri na vya kipekee vilikuwepo mezani.Tuliona dhabibu kubwa kama usawa wa
machungwa, ma Bwana Yesu alituruhusu kuonja baadhi yake. Bado tunaweza
kukumbuka ladha yake, ni kitu cha kipekee sana! Kaka zangu na rafiki zangu
huwezi kufikiria jinsi kila kitu kilivyo andaliwa tayari kwenye ufalme wa
mbinguni na kile ambacho tayari Mungu amekwisha kuandalia.(1
Wakorintho 2:9)
Pia kwenye meza ile, Mungu alituruhusu kuuona ule
Mkate, "Manna".Huu ulikuwa ni mkate wa Mungu ambao Bibilia inatuambia
habari zake. Tuliruhusiwa kuufurahia ladha yake pamoja na mambo mengine mengi
ya ajabu yasiyo patikana duniani.
Vitu hivi vinatusubiri kama uridhi wetu usio haribika
Kwenye Ufalme wa Mbinguni. Tutafurahia vitu vya kushangaza sana vya
kipekee na vyakula vyenye ladha nzuri wakati tutakapo urithi Ufalme wa
Mbinguni. Tulishangaa kuona kuwa viti vilikuwa vimeizunguka ile meza pande
zote. Viti hivi vizuri vina majina kila kimoja. Tuliweza kusoma bila shida
majina yetu katika viti vile, lakii majina yetu hayakuwa ni yale tunayo yatumia
huku duniani. Yalikuwa ni majina mapya ambayo hakuna mtu yeyote anaye yajua ila sisi
wenyewe. ( Ufunuo 2:17)
Kile kilichoandikwa
katika neno la Mungu kilitu shangaza, "Lakini
msifurahi kwa vile pepo wanavyo watii, bali furahinikwa sababu majina yenu
yameandikwa Mbinguni." (Luka 10:20) Kulikuwa na viti vingi
sana! Kuna nafasi kwa kila mmoja anayetaka kwenda kwenye ufalme wa Mbinguni..
kulikuwepo pia viti ambavyo viliondolewa kwenye meza. Hii ina maana kuwa
kuna wanaume na wanawake ambao walikuwa wamechoka kumtumikia Mungu, na majina
yao yalifutwa kwenye Kitabu cha Uzima na walitengwa na Karamu ya Mwana Kondoo.
Mungu pia alituruhusu kuwaona watu walio kwenye Bibilia, watakatifu wa ajabu sana ambao tuna wasoma kwenye maandiko.Tulishangaa kumwona Ibrahimu. Ibrahimu alikuwa ni mzee sio kwa umbo lake wala kuonekana kwake. Alikuwa ni mzee kwa hekima aliyo kuwa nayo. Nywele za Ibrahimu zilikuwa nyeupe kabisa, lakini kila unywele ulikuwa ni kama kiooo au kama mng,ao wa almasi. Kilicho tushangaza zaidi ni kuona kuwa alikuwa kijana zaidi hata kuliko sisi.Mbinguni kila mmoja wetu atahuishwa upya na kuwa vijana. Tulishangazwa zaidi na maneno yake. Ibrahimu alituambia neno ambalo hatutakisahau. Alitukaribisha kwenye Ufalme wa Mbinguni na alituambia kwamba ni muda mfupi ujao tutakuwa kwenye eneo lile, kwa sababu kuja kwake Bwana Yesu Kristo kuna karibia haraka sana.
No comments:
Post a Comment