MAFUNDISHO NA JAMES F.MNZAVA
FAHAMU KUTUMIA NAFASI YAKO
YA ULINZI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
EZEKIEL 33;7 Nimekuweka kuwa mlinzi kwa nyumba ya Israel
basi ulisikie neno la BWANA ukawape maonyo yangu.
>>> Ukianza mstari wa 1-9 utaona jinsi MUNGU
alipokuwa anamwambia Ezekiel kuhusu wajibu wa ulinzi aliokuwa amepewa.jikumu
lake kama mlinzi ni kutoa taaarifa kwa wale anaowalinda.
>>>Kama mtu angekufa kama mlinzi hakutoa taarifa
kwa wale anaowalinda damu yake inakuwa
juu ya huyo mlinzi ,lakini kama mtu akifa lakini aliambiwa na mlinzi damu yake
inakuwa juu yake mwenyewe.
ISAYA
62;6-7…Nimeweka walinzi juu ya kuta zako
…
Kazi ya walinzi hawa wa isaya ni kumkumbusha Bwana kufanya
kile alicho ahidi kufanya juu ya mji huo kwa kutonyamaza usiku wala mchana
>>>mfumo wa walinzi hawa ulikuwa wa kulinda kupitia
vinywa vyao
>>>Ezekiel anatuambia
kuhusu ``mlinzi wa nyumba ya Israel``na Isaya anatuambia kuhusu habari ya
``walinzi juu ya kuta za yerusalem``
Tofauti hizi za ulinzi zinatujulisha
kwa habari ya nafasi mbalimbali katika ulimwengu wa roho
FAHAMU KWAMBA ; kufanikiwa kwa kusudi la Mungu
duniani kunategemea utiifu wa walinzi wake duniani kwenye nafasi ambazo amewapa
katika ulimwengu war oho.
MAMBO{5} MUHIMU
YA KUJUA NA KUZINGATIA KUHUSU NAFASI YA ULINZI KATIKA ULIMWENGU WA ROHO
{i}…Mwanadamu amepewa kuwa mlinzi wa kusudi la Mungu katika
ulimwengu wa roho akali hapa duniani .maadamu umeokoka tambua wewe ni mlinzi wa
kusudi la Bwana.Na hilo kusudi la Bwana ambalo umepewa kulinda lina muunganiko
wa maisha yako ya kiroho ya watoto wa
Mungu au wa nyumbani kwako.Kwa lugha nyingine kama umeokoka wewe ni mlinzi eneo
ulilopo.
{ii}… Ni wajibu wa kila mlinzi kusimama kwenye nafasi yake
khakikisha kusudi la Mungu linafanikiwa.Sehemu kubwa ya majanga ,maafa au
matatizo ambayoyanatupata sisi kama watoto wa Mungu ni kwa sababu hatukusimama
kwenye zamu zetu.
{iii}…Mungu huwa anatoa taarifa kwa walinzi tegemeana na
nafasi zao pia maeneo yao ya ulinzi. Huwa anatoa taarifa kwa walinzi kwa
kuzingatia nafasi walizonazo kwenye ulimwengu wa roho.Ndio maana nasisitiza
ujifunze kukaa kwenye nafasi yako ili mungu anapotafuta mtu wa kumpa taarifa
akuone kwenye eneo lako.
{iv}…Jifunze
kuitazama``taarifa`` unayopewa na Mungu kama fursa ya uponyaji wako
binafsi na kwa wale walioko chini ya lindo lako.
{v}…Mtu mmoja anaweza akapewa zaidi ya eneo moja la ulinzi
katika ulimwengu wa roho.Hapa jambo lililomuhimu kwa mlinzi ni utiifu kwa Bwana
wake.Mambo mengi mabaya yasingetokea kama sisi walinzi tungesimama kwenye zamu
zetu za ulinzi.Mungu alijiwekea utaratibu wa kutoa taarifa kwa walinzi wakejuu
ya kile ambacho shetani amekusudia kukifanya hapa duniani.
UMUHIMU WA
TAARIFA NA MAWASILIANO MAZURI BAINA YA MLINZI NA WATU WA ENEO LAKE
{i}…MATHAYO25;1-13 …lakini usiku wa manane …pakawa na
kelele… kilichowaamsha hawa wanawali kumi ni zile kelele za tarifa ambazo ninaamini zilikuwa ni za walinzi ambao
jukimu lao ni kutoa taarifa katika eneo lao la ulinzi.Kutokana na mfano huu
tunajifunza kwamba taarifa ya mlinzi/walinzi iliwasaidia wanawali wale kumi
kutoka katika usingizi wao.Pili taarifa ile iliwapelekea wanawali wale
kujiandaa kwa kuziandaa taa zao ona mstari ule wa saba
Wale wanawali wapumbavu hawakuwa na uhusiano mzuri kati yao
na walinzi.Baada ya Bwana harusi kuja ndio wakakumbuka kuwa taa zao hazina
mafuta ya kutosha hadi wakafungiwa nje.
WIMBO ULIOBORA 3;3-4
Walinzi wamewekwa kwenye nafasi zao ili kuleta ufumbuzi juu
ya changamoto zinazowakabili watu wa maeneo yao ya ulinzi
MAENEO YANAYOHITAJI WALINZI
{i} …Nyumba ya Israel/mlinzi wa Israel
>>>ezekiel 33;7
{ii}…Mji au taifa/mlinzi wa mji au
taifa>>>2wafalme 9;17
{iii}…Nyakati/muda na majira>>>isaya 21;11-12
{iv}…Mtu au watu/mlinzi au walinzi wa watu>>>
1samweli 14;16,,yeremia 6;17,,ezekiel33;7
{v}…Kanisa au nyumba ya bwana/mlinzi wa
kanisa>>>2wafalme 11;18
MAMBO YA MUHIMU YA KUZINGATIA
{a}…Mlinzi anapaswa kusogea mbele za Mungu ili
kusikilizishwa mambo ya watu wake
{b}…Mlinzi ndiye mwenye fursa ya kuruhusu au kuzuia vitu
kwenye eneo lake la ulinzi.Hpa ni muhimu kwa mlinzi kuwa na ufahamu katika neon
la Mungu.
{c}… Kumbuka vita vya kiriho ni vita vya matakwa ya Mungu au
shetani {yeremia 29;11}
{d}…kufanikiwa kwa kusudi la Mungu kunategemea utiifu wa
walinzi wake.
MWISHO
Somo zuri Sana Mungu akubariki
ReplyDelete