Sunday, November 1, 2015

USIPITE BILA KUSOMA USHUHUDA HUU

Theo Nez alikulia katika taifa wa Wanavajo karibu na pembe 4 za USA. Bado anaishi katika eneo hilo. Mwaka 1995 alinunua kitabu cha Mary Baxter “Ufunuo wa kuhusu Kuzimu” akifikiri ataishi tena miaka 30 ijayo hivyo angeweza kuwa na muda mzuri kurekebisha na Mungu. Akakiweka kandolakini, miezi sita baadae alipokuwa akifanya Meth nyumbani kwake alikufa kwa sababu ya kutumia nyingi (over dose). Yesu Kristo mwenyewe akamchukua Theo kwa mkono wake na akampeleka katika shimo lake la Kuzimu. Kwa masaa mawili alimsihi Yesu asimpeleke pale….. Lakini Yesu hakuweza kubadili kitu. Mpaka pale aliposikia mke wake, muamini, akimuombea….Yesu akamueleza kuwa atakwenda kujibu maombi yake kwa sababu alisimama katika neon na hakurudi nyuma… Yesu akampeleka Mbinguni na kwa masaa mawili alimuonyesha mambo yajayo na akamuamuru awaambie wengine kwamba tunaishi katika nyakati za mwisho naya kwamba Bwana amekaribia kurudi. Ujumbe wake ni kuwa hatuwezi kuwatumikia mabwana wawili. Hello Kaka na dada zangu wapendwa. Jina langu ni Theo nez na ninnaishi Farmington New Mexico. Leo ningependa kushiriki nanyi ushuhuda wangu, Jinsi Mungu alivyofanya kitu cha ajabu sana, Kwangu mimi na kwa familia yangu. Alileta Wokovu wake katika nyumba yetu. Mwaka 1995, Nilikuwa ni mtu wa asili. Nilikunywa na kutumia madawa, sikujali kitu chochote.Siku moja, Nilitumia zaidi kupindukia kwa haraka na moyo wangu ukasimama. Nikafa kwa masaa. Kile nachotaka kuwaeleza, kitawafanya mfikiri mara mbili kwa habari ya maisha na kifo. Moyo wangu uliposimama, kelele za ulimwengu zikatoweka kabisa na giza kuu likaja kwangu. Nikaona mapepo matatu yakitoka kwenye moyo wangu, yakienda nje ya dirisha huku yakicheka. Nilipotoka kwenye Mwili wangu, Niligeuka nyuma nikamuona Yesu alikuwa amesimama nyuma yangu. Nywele zake zilikuwa ni dhahabu yenye weupe; Alikuwa amevalia vazi jeupe lenye mshipi wa dhahabu. Viatu vyake vilikuwa ni sandosi za dhahabu, na alisogea na akaongea kwa sauti ya upole.Viatu sandosi za dhahabu. Viatu vyake vilikuwa ni sandosi za dhahabu, na alisogea na akaongea kwa sauti tulivu. Kulikuwa na mwanga uliomzunguka na Roho yangu ikawa imekwisha mtambua. Nilitembea mpaka kwake na kumuuliza; Yesu ulikuwa wapi, nilikuwa nikikutafuta. na akaongea kwa upole na kusema; sikuwahi kukuacha, nimekuwa pembeni yako siku zote. Nilikuwa nikisubiri wewe utubu na kufanya kusudi la Baba. Unafahamu, nilikuwa nimeitwa kuhubiri miaka michache iliyopita. Nikasema, Nitakwenda,lakini nilikimbia. Nikasema siwezi kufanya, Bado ni kijana sana. Mungu anapokuita na kuingilia maisha yako huna uchaguzi mwingine lakini inakupasa useme ndiyo Bwana. Kisha nikamwambia Yesu, nilifikiri ningeishi miaka mingine thelathini. Njoo, imekupasa kuona mengi. Alinishika mkono wangu na tukaanza kutembea kuelekea chini kwenye njia. Ilikuwa ni giza na Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu Yesu mwenyewe ndiye alikuwa mwanga. Mara nikaanza kuona pepo wametuzunguka. Walikuwa wakijaribu kunirarua, lakini nikamshikilia Yesu mkononi kama mtoto mdogo. Alikuwa ni kinga yangu na akaanza kuongea nami. Akasema, unajua Baba anahasira nawe. Ni kwa sababu nilikuwa na cheza na kanisa na kukimbia kama Yona. Biblia inasema Yona aliitwa kuhubiri lakini alimkimbia Mungu. Nimefanya hivi kwa muda wa miaka mingi. Sasa imenishika mimi pia. Nilifahamu kuwa nilikuwa nimekufa katika dhambi zangu, na nilikuwa nimekwisha chelewa. Tulipoendelea mbele, Yesu akaongea mambo mengi na nikamuuliza maswali mengi. Tukasima mahali fulani na yesu akaniambia, angalia mbele. Niliweza kuona aina fulani ya mwanga kwa mbali. Yesu akaniuliza; Unafikiri hiyo ni nini? Nikasema, Bwana hiyo inaonekana kama kuzimu, Labda ni miali ya moto wa kuzimu. Hakika, tuliposogelea karibu, tukafika juu ya bonde. Bonde lilikuwa kama maili mbili kwa kina na maili tatu kwa upana Chini niliweza kuona miali ya moto, kila kitu kilikuwa ni orenji nyekundu, Nikaanza kutetemeka, Nikaanza kuogopa. Nilifahamu kuwa nitawenda kuishia mahali pale.Yesu akaniambia niangalie chini. Sikuweza hata kuangalia chini, nilianza kulia huku nikimkimbilia Yesu nyuma. Nikaanza kutubu, na kuliakwa Bwana ili anisamehe. Nitahubiri sasa, nipe nafasi moja ya mwisho. Nililia kama mtoto mdogo. Tuliendelea mpaka tukafika chini kabisa kwenye shimo la kuzimu. Nilona vitu vingi ambavyo maneno hayawezi kusimulia. Sehemu ile ilijaa roho za watu, na mapepo yalikuwa kila eneo. Biblia inasema Isaya 5:14 Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo. Kulikuwa na Roho za watu zikiwaka katika miali ya moto. Vilio na kelele zilikuwa kila sehemu. Hakukuwa na tumaini, hakukuwa na tumaini kwa roho zilizopotea. Kwa nini ? Kwa sababu walimkataa Yesu. Wengine walisubiri muda mrefu. Wengi walifanya mdhaa na wakamkimbia Mungu. Kumkimbia Mungu kutakufanya uingie Kuzimu. Ukishaingia mule huwezi kutoka. Tafadhali, ningependa uinue mikono yako na kumwambia Bwana; Usiruhusu hili kutokea kwangu. Tulipoendelea kutembea, Niliona mamia ya elfu ya mashimo. Nilikuwa nikilia na kuomboleza tulipokuja kwenye shimo moja ambalo ni tupu. lilikuwa na moto uliokuwa ukitoka ndani yake. Yesu akaniambia; Hili ndilo shimo ambalo shetani amekuchimbia. Kisha nikaanza kupiga mayowe, nikilia, Bwana sitaki kwenda pale. Nililia na kutubu, NikimuombaYesu anipe nafasi moja nyingine tena. Nililia kama Yona alipokuwa kwenye tumbo la Kuzimu. Katika Kitabu cha Luka 16, tunasoma kwa habari ya Lazaro na Tajiri mmoja. Tajiri alikuwa na kila kitu. 20 Kulikuwa pia na maskini mmoja jina lake Lazaro, aliyekuwa amejaa vidonda na alikuwa analazwa mlangoni pa nyumba ya huyo tajiri. 21 Lazaro alitamani kula makombo yaliyoanguka kutoka meza ya tajiri; na zaidi ya hayo, mbwa walikuwa wanakuja na kulamba vidonda vyake! 22 Ikatokea kwamba huyo maskini akafa, malaika wakamchukua, wakamweka Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu karibu na Abrahamu. Na yule tajiri pia akafa, akazikwa. 23 Huyo tajiri, alikuwa na mateso makali huko kuzimu, akainua macho yake, akamwona Abrahamu kwa mbali na Lazaro karibu naye. 24 Basi, akaita kwa sauti: Baba Abrahamu, nionee huruma; umtume Lazaro angalau achovye ncha ya kidole chake katika maji, auburudishe ulimi wangu, maana ninateseka mno katika moto huu. 25 Lakini Abrahamu akamjibu: Kumbuka mwanangu, kwamba ulipokea mema yako katika maisha, naye Lazaro akapokea mabaya. Sasa lakini, yeye anatulizwa, nawe unateswa. 26 Licha ya hayo, kati yetu na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wanaotaka kuja kwenu kutoka huku wasiweze, wala wanaotaka kutoka kwenu kuja kwetu wasiweze. 27 Huyo aliyekuwa tajiri akasema: Basi baba, nakuomba umtume aende nyumbani kwa baba yangu, 28 maana ninao ndugu watano, ili awaonye wasije wakaja huku kwenye mateso. 29 Lakini Abrahamu akamwambia: Ndugu zako wanao Mose na manabii; waache wawasikilize hao. 30 Lakini yeye akasema: Sivyo baba Abrahamu, ila kama mtu atafufuka kutoka wafu na kuwaendea, watatubu. 31 Naye Abrahamu akasema: Kama hawawasikilizi Mose na manabii, hawatajali hata kama mtu angefufuka kutoka wafu." Oh Watu , tafadhali mnisikilize,hii ni halisi,weka mambo yako sawa na Mungu vile uwezavyo .Tulipotoka nje, tulisimama katika eneo lenye ukiwa. Yesu akasema;sikia. Na nikaanza kusikia mwanamke akisali niliweza kusikia sauti yake vizuri wakati akiomba alisema; Bwana mrudishe tena! Mpe tena nafasi nyingine. Bwana ana watoto wawili wa kiume wa kuwalea. Yeye ndiye pekee niliyenaye. Usimchukue Bwana! Unaamini maombi ya imani yanaweza kuamisha chochote? Biblia inasema, chochote mnachohitaji mkiomba , amini umekwisha pokea,na hakika mtapokea. Mwanamke huyu akaendelea kuomba. Yesu akaniuliza, Unafikiri huyo ni nani? Nikamwambia huyo ni mke wangu. Bwana akasema, unasikia hicho,nina watoto wawili wa kuwalea. Nikaanza kumshika Bwana kwenye mabega, siwezi kufa sasa, familia yangubado inanihitaji. Nikaanza kutoa sababu mbalimbali, lakini hakukuwa na jibu. Nikaanza kulia tena. Mke wangu aliendelea kuomba. Kulikuwa na kipindi cha kusubiri ambacho kilikuwa kama masaa na mwisho Mungu Baba akajibu hili, Akaongea na sauti yake ilikuwa kama Maji mengi. Akasema Mwanangu; nakwenda kukupa tena nafasi nyingine kwa sababu ya maombi na imani ya mke wako,nitakuhifadhi. Nikikurudisha, nitakwenda kukutumia. Hapo nikaanza kusema kwa viapo,Bwana nitahubiri. Nitafanya chochote, Nitawaeleza watu kuhusu sehemu hii, Nikasema Bwana ,Nitakusaidia kuokoa roho . Kisha tukatembea kuelekea kwenye chumba chenye kioo kikubwa kama Televisheni. Nilionyeshwa wakati wangu uliopita,wa sasa na utakaokuja. Nikaweza kuona ,maisha yangu kuanzia mtoto mpaka nilipokuwa mkubwa. Yesu alinipa ufunuo, maono. Alinionyesha mambo mengi sana ambayo ni lazima yatokee. Akasema, kweli tunaishi katika nyakati za mwisho. Nenda na uwaeleze watu. waambie watembee katika njia sahihi na watubu. Waeleze waache kucheza na mimi na waanze kushika amri zangu. Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu Akanionyesha jinsi watu wanavyojificha nyuma ya Biblia, wanayaficha matendo yao,na wanaishi katika dhambi. Mungu anasikia na kuona kila kitu. Akasema watu hawa wanamuheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nae. Oh jinsi wanavyopenda kufundisha amri kwa watu, lakini wanaziacha amri za Mungu. Akasema , usogope,Mimi ni alpha na omega, wa kwanza na wa mwisho, Unachokisikia ni haki. Akasema; yeye aliye na sikio, na sikie kile Roho anasema kwa kanisa. Akanipa mistari mitatu,Ta hadhari. Wa kwanza ni Kumbukumbu la torati 6:15. (15 kwani Bwana, Mungu wako, aliye katikati yako ni Mungu mwenye wivu;) isije ikawaka juu yako hasira ya Bwana, Mungu wako, akakuangamiza kutoka juu ya uso wa nchi. Mstari wa pili katika Luka 16:13. Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au ataambatana na mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. Msitari wa tatu katika kitabu cha Ufunuo 3:3 Basi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Walakini usipokesha, nitakuja kama mwivi, wala hutaijua saa nitakayokuja kwako. Kaka na dada, Hatujui ni siku gani tutaonndoka katika ulimwengu huu, hatujui kesho imebeba nini ,kwa hivyo ninaomba kwamba uweke mambo yako sawa na Mungu wakati bado unaweza. Baada ya hili Yesu akanichukua mpaka mbinguni na tukatembea katika malango haya ya dhahabu katika mtaa wa dhahabu. Nikaona watu wengi wa kila taifa na walikuwa wamesimama mbele ya kiti kile cha enzi, wamevalia mavazi meupe, Baadhi yao ni watu niliowafahamu, wachungaji na manabii wa kwenye biblia. kila kitu kilikuwa ni kizuri,kila mtu alikuwa ni mwenye furaha;ungeweza kuona upendo wao kwenye sura zao. Nilianza kuhisi furaha na amani.Nilipokuwa nikitembeatembea, sikutaka tena kurudi. Yesu akanifunulia saa kubwa. Mkono wa saa ulikuwa umekaribia kufikia kamili kwenye 12,wakati unakimbia haraka,wakati wa kwenda sasa. Nikasema Bwana, sitapenda kwenda, nataka nibaki. Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu Lakini ilinipasa kurudi. Tulipokuwa tukirudi niliona dunia kama kampira kadogo kama ule wa golf. Alinileta tena kwenye chumba changumwili wangu ulipokuwa umelala. Alisogelea mahali ambapo moyo wangu ulikuwepo. Nyama iliyozungukza moyo wanguilifunguka. Yesu akachukua moyo wangu wa kale nje, na akautupa katika ziwa la moto, Kisha akanipa moyo mpya, na mwanga ukaja juu yake. Nilisimama pale nikiagalia na kutafakari,wow; hata ngozi na mifupa inasikia Yesu. Baadae nilitafuta katika biblia yangu na nikakuta Ezekieil sura 36 :26-27, Nililia kama mtoto mdogo kwa sababu ilikuwa imeandikwa, Pale Biblia inasema hivi: 26 Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. 27 Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Baada ya Yesu kurejesha roho yangu kwenye mwili wangu, lakini moyo wangu mpya haukuwa unafanya kazi bado.Nilimuona mke wangu ameshika mikono yangu anaomba. Muda nikaona chumba changu kimezungukwa na maelfu ya malaika, walikuwa wakisifu na kuimba kwa nyimbo nzuri ambazo sikuwahi kuzisikia. Muziki tu wenyewe ulikuwa ni waajabu sana,Malaika mmoja akatokeza kwa nje na akatamka, akisema; Damu ya Yesu inakuja. Na malaika wote wakaanza kusifu na kuabudu. Kisha Damu ya Yesu ikaja tulipo,na kunisafisha mimi kuanzia kichwani mpaka kwenye vidole vyangu vya miguu ikasafisha dhambi zangu zote. Pombe na madawa vikatoka nje ya mwili. Nikahisi kama maji ya moto. Nilipojiangalia, ule weusi wote wa mwili wangu ukaondoka. Nilikuwa mweupe na msafi. Baadae malaika Yule Yule akatoka nje tena na akasema; Roho Mtakatifu anakuja.Malaika wakaanza kuimba na kuabudu tena. Holy spirit akaja kwetu tulipo na kutujaza. Roho yangu ikaanza kuruka tena juu na chini. Kisha nikampata Roho Mtakatifu. Roho ya Bwana ilikuwa na moto kama umeme; ilikuwa kama moto unaowaka kwenye mifupa yangu. Malaika walikuwa bado wakiimba na kusifu Yesu aliposema; Mwanangu, nenda kawaambie watu nilicho kushuhudia wewe. Akaugusa moyo wangu mpya kwa vidole vyake na ukaanza kufanya kazi. Ndipo kidogo kidogo macho yangu yakaanza kufunguka. Nikagundua mwili wangu umekuwa wa baridi, ilikuwa ni vigumu kidogo kuongea. Nikamuuliza mke wangu kilichotokea. Akaniangalia na kuniambia; Uko sawa? Kisha akaanza kulia. Kulikuwa bado kuna maumivu kwenye kifua changu chote, nikaona kama ninaopresheni. Nilikuwa mdhaifu na kiu; Kitu cha kwanza kuuliza ilikuwa ni maji. Kisha fahamu zangu Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu zikaanza kunirudia na nikakumbuka kilichonitokea. Kisha nikaanguka kwa Magoti na kuomba kwa muda wa masaa matatu mpaka jua likachomoka. Kutoka siku hiyo maisha yangu yamekuwa tofauti. Nilikuwa muasi, Lakini Mungu akanishusha kwa magoti , nikaanza kulia kama mtoto mdogo, nikiomba rehema. Nilikuwa nikifikiri, nikienda kuzimu, haitajalisha. Lakini sikuwa najua ni kiasi gani kuzimu ni chungu mpaka pale Bwana aliponifunulia. Sasa namshukuru Bwana kila siku kwa maisha ambayo amenirejeshea, familia, na huduma aliyonipa. Kaka na dada ,Ninaomba kwamba msichezee kanisa na kuwa na mabwana wawili, Kwa sababu huwezi ukacheza na Mungu. Ni kitu cha kutisha kama nini kuangukia katika mikono ya Mungu aliyehai. Hivyo usidanganyike,Mungu hadhiakiwi. Biblia inasema;Apandacho mtu, ndicho atakachovuna, Yeye apandaye uovu, atavuna huo. Ndiyo Mungu ni Mungu wa upendo; amejaa huruma na rehema. ni Mungu wa nafasi ya pili, lakini ni Mungu wa hukumu .Biblia inasema Yeye ni moto ulao.hivyo imetupasa tujiandae, kwa sababu hujui ni lini utakwenda kufa, Bilblia inasema katika waebrania 9:27, kama inavyoamriwa kwa wanadamu kufa mara moja, lakini baada ya hili ni Hukumu. Siku inakuja ambayo sote tutasimama mbele zake Mungu, na vitabu vyetu vitafunguliwa. Utakw enda kuwa pale. Kila Mtu ambaye anasikiliza ushuhuda huu atakwenda kuwa pale. Hiyo itakuwa ni mwito ambao huwezi kukosa. Hii inaweza kuwa ni mwito wako wa mwisho, usiasi mbele zak e Mungu. Tafakari kwa makini kuhusu hili, Itaenda kuwa peponi au kuzimu. Unaweza usipate na fasi nyingine kama mimi; Ni kwa neema ya Mungu tu. Niko hapa leo ilikushiriki nanyi ushuhuda huu, ningependa unyanyue mikono yako na uongee na Bwana, Mshukuru Yeye kwa kuwatahadharisha, Mshukuru Yeye kwa maisha haya ya thamani. Kama ungependa kuokoka, unahitaji sala hii, Ngoja niombe sala hii pamoja nawe hivi sasa. Bwana Yesu ,nisamehe. Ninakupokea wewe kama Bwana Mwokozi wangu. Njoo moyoni mwan gu na maishani mwangu. Nipe Uzima wa milele, ili niweze kuishi nawe milele. Nipe maisha ya a mani na furaha. Aksante Bwana. Katika Jina la Yesu, Amen. Imefasiriwa na Peter Kahale kwa Neema aliojaliwa na Mungu Kama ukipenda kuniandikia anuani yangu ni: Last living days Ministries P.O. Box 3701 Farmington, NM 87499 USA Unachokisikia kwenye ushuhuda huu ni simulizi ya kweli. Mimi ni Mtu wa India Mnavajo.Ninaishi Four Corners. Nina rasimisha kan da hii kwa Wamarekani wenyeji wote Marekani nzima. Ninatoa Ruhusa kunakili ushuhuda huu. Ndugu aliyefasiri ufunuo huu ni Peter Kahale ni kijana aliyeokoka na anampenda Yesu na mwenye shauku ya kuhubiri injili ya Yesu Kristo. Simu ya Mkononi: +255-769-610460, +255-653-610460. Barua Pepe: kahalepeter@gmail.com

1 comment:

  1. Ni kweli hatuwezi kufuata nuru na giza kwa wakati mmoja. MUNGU atusaidie kupata ufahamu na uelewa katika mambo kama haya. BARIKIWA NA BWANA

    ReplyDelete

AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1)

http://bit.ly/3JGDJ4d MWL. JAMES F. MZAVER Minister Truth 0762759621 jamesmzava@gmail.com              AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1) Ukuaji ha...