Monday, November 9, 2015

DAKIKA 23 KUZIMU (23 Minutes in Hell)


                 DAKIKA 23 KUZIMU 

 Mike Bickle, ambaye ninafanya kazi nae katika Nyumba ya Kimataifa ya Maombi (International House of Prayer), alinisihi nifundishe juu ya somo la Kuzimu. Wakati najifunza somo hilo, nilipewa kanda na rafiki aitwaye Steve Carpenter, kwenye kanda hiyo kulikuwa na ujumbe ambao jutaenda kusikia kutoka kwa Bill Wiese na mke wake Annette. Ujumbe wake ulibadili Dunia yangu. Na moja kwa moja ilibadili namna ambavyo familia yangu, marafiki zangu, na hata watu nisiowajua. Iliwabadili moja kwa moja. Siongezi chumvi,kwa hiyo usifikirie naongea kwa kuzidisha maneno hapa, Ilibadili jinsi navyotazama kweye miaka michache niliyobakiza hapa duniani. Ni maombi yangu kwamba Mungu atafanya hivyo hata kwako leo. Siongezi chumvi umuhimu wa ujumbe huu. Bill ni Mkristo. Aliyatoa maisha yake kwa Kristo alipokuwa na umri wa miaka 16. Amemjua Bwana kwa miaka 32. Alihamia California mwaka 1976 na alitumia miaka 10 akiwa chini ya huduma ya Mchungaji Chuck Smith pale Costa Mesa , California. Bill ni muonaji, kama alivyo mke wake. Kwa miaka 15 iliyopita , Bill amekuwa katika mikutano na katika uongozi kwa misimu tofauti ya Eagles Nest, chini ya uchungaji wa Dk Gary Greenwald , pale Orange County, California. Mchungaji huko Eagles Nest aitwaye Mchungaji Raul alikuja kwa Bill na alisema miezi kadhaa iliyopita , "Bill, Mungu atakwenda kufanya kazi ya uamsho atakwenda kuanzia Cansas City kwa America. Atakupeleka pale na inabidi uende". Bill na Annette hawakuwahi kwenda Kansas City katika maisha yao yote. Siku iliyofuata, mimi nilimpigia Bill na nikasema," Je, unaweza kufikiria kuja Mji wa Kansas? Nimeona video yako na nadhani unatakiwa kuja . " Naamini wako hapa kwa ajili ya amri ya Mungu. Utaenda kusikia maono ya Kuzimu, lakini muhimu zaidi, utakwenda kusikia maono ya uhusiano wa karibu na Yesu Kristo na upendo alionao kwa dunia nzima. Bill alikuwa kuzimu. Hakuwa akiangalia kwa kawaida, kama watu wengi wamekuwa katika maono halali, lakini alipata uzoefu wa mateso ya kuzimu kwa muda wa nusu saa na hakuwa na matumaini kabisa ya kutoka milele. Bill na mke wake wamejitoa kwa Yesu Kristo kikamilifu, na kwa kazi ya Mungu, na kwa uongozi wa Roho Mtakatifu. Utakwenda kumsikiliza pia. Tafadhali nawakaribisha Bill na Annette Wiese. 2 (Bill Wiese anaongea) Ni heshima kuwa hapa. Safari hii yote imekuwa baraka sana kwetu. Kama Hal alivyosema, Tuko katika biashara isiyotambulika sana. Hatufanyi hivi kwa ajili ya kuishi. Hatufanyi hivi kwa fedha. Sisi tunachojua ni kwamba Mungu ametuambia kwenda na kuwaambia dunia kuhusu upendo wake kwa watu na mahali pale Yeye hataki yoyote wa viumbe wake kwenda. Hiyo ndiyo sababu tuko hapa. Hivyo, kwa ajili ya muda, nitakwenda kufupisha ushuhuda huu na kusimulia moja kwa moja. Lakini kwanza nataka kusema mambo kadhaa, maswali ambayo yanaweza kuwa katika akili yako. Swali la kwanza kwangu kama ingekuwa najisikiliza, ingekuwa, “Umejuaje haikuwa ndoto tu uliyoisikia? Ndoto mbaya?" mambo kazaa ya kuzingatia, kwanza kabla ya yote, Niliuacha mwili wangu. Nikauona mwili wangu wakati narudi, umelazwa juu ya sakafu. Hivyo nilijua kwa uhakika nilikuwa nje ya mwili (out of body experience). Baadhi ya wakristo wamesema, "Oh Mkristo hawezi kuuacha mwili wake." Lakini hiyo si kweli, Katika 2 Wakorintho 12:2, wakati Paulo alipokuwa juu katika mbingu ya tatu, Alisema, "kama katika mwili, au nje ya mwili sijui." Hivyo kama hujui hii inamaanisha kuwa inawezekana. Na pia alisema katika mstari wa kwanza kwamba ilikuwa ni maono, hivyo naamini hii inakuja chini ya uainishaji wa maono. Katika Ayubu 7:14 inasema, "unitishapo kwa ndoto na kunishangaza mimi kwa maono." Hivyo hii ni dhahiri hiki ndicho Bwana alifanya, alinishangaza kwa njia ya maono. Pia niliporudi kutoka katika uzoefu huu, ilinichukua mwaka mzima kutulia, na kuwa kama mtu wa kawaida tena. Nilikuwa nimezimia moyo na kuchanganyikiwa kutokana na hofu kwamba ilibadili mtizamo wangu wa jinsi ya kushuhudia na kiasi gani kutambua kile nini Mungu alituokoa nacho. Nitamuomba mke wangu aje kwa dakika chache ili aweze kushiriki tu kilichotokea wakati yeye aliponikuta katika sebule, kwa sababu mimi sikumbuki kwa sehemu hiyo. Hivyo nataka yeye aseme maneno machache. Asante. (Mke wa Bill anaongea) Ilikuwa yapata saa 09:23 alfajiri nilipoamka. Nimekumbuka hilo kwa sababu nilitazama saa yetu ya digital, na niliona Bill hakuwa karibu na mimi, nikasikia kelele zinatokea sebuleni. Nilianza kutembea/kushuka koridoni. Nilimuona mume wangu kwa namna ambayo sikuwahi kumwona kabla. Kama kuna mtu anamjua Bill, yeye ni mtu wa misimamo kwa asili, mtaratibu sana, na mtu mtaalamu. Yeye si mtu wa kupata msisimko tu au kupata hisia za haraka juu ya kitu chochote, isipokuwa Mungu anapokuwa kazini. Lakini, hatahivyo, nilimuona pale akiwa ameshikwa na butwaa/mshangao, akiwa ameshika kichwa chake, akiwa ameweka kichwa chake katika mikono yake akipiga kelele na mayowe. Alikuwa katika hali ya kujilaza chali sakafuni amejikunja. Sikujua nini cha kufanya. Nilidhani alipatwa na ugonjwa wa moyo. Nilianza kuomba na alilia na akasema, "Omba kwa Bwana ili aliondoe hili nje ya akili yangu! Bwana amenipeleka Kuzimu. Najisikia kama mwili wangu umekufa, siwezi kulibeba hili." Kwa hiyo nikaendelea kuomba juu yake, na katika muda wa dakika kumi hadi ishirini alianza kutulia. Alikuwa katika hali ya mshangao, kama mtu ambaye alikwenda Vietnam na akatokea tena kwa mara ya pili, au mtu aliyeponea ajali ya gari ya kutisha. Haikuwa tu mtu ambaye alikuwa anaota ndoto mbaya na akaamka. Hivyo ndivyo nilitaka kushuhudia. (Bill Wiese anaongea) Nimebarikiwa kuwa na mwanamke mzuri. Kweli namshukuru Mungu. Nimekuwa katika ndoa kwa miaka minne, na nimemjua kwa miaka sita ya maisha yangu, ninaweza kusema, asifiwe Mungu. Nilitaka kujua zaidi niliporudi kutoka katika uzoefu huu, kama kuna yoyote katika Biblia ambaye amewahi kupata uzoefu huu. Kwa hiyo nikaanza kufanya utafiti. Huwa namsikiliza Chuck Missler sana. Yeye ni mwalimu wa 3 Biblia katika mataifa mengi, msomi halisi na yeye alisema kuwa Yona alipatwa na uzoefu wa Kuzimu. Katika Yona 2:2 inasema, "katika Kuzimu alipiga kelele." Na Katika Yona 2:6 inasema, " Nalishuka hata pande za chini za milima; Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele; Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni, Ee Bwana, Mungu wangu, Basi angalau kulikuwa na mtu katika Biblia mwenye uzoefu na kuzimu, Yona. Nilitaka kujua, kwa sababu nilikulia katika siku za mwanzo za kanisa la Calvary, uzoefu wowote wa kiroho ambao uliupata ni lazima uendane na Neno la Mungu. Hivyo nilijua kuwa kama uzoefu huo ni kweli, basi utakuwa tayari upo katika maandiko. Kwa hiyo nikaanza kufanya utafiti na nimeona zaidi ya maandiko 400 ambayo yanaonyesha kila kitu nilichokiona, nilichosikia, nilichohisi, na kila kitu kinachohusiana na Kuzimu. Tayari kimeandikwa, hivyo chochote nawaambia tayari kiko pale. Nitafanya kukuhakiki baadhi ya maandiko. Siwezi kunukuu yote 400, lakini nitafanya kwa baadhi. Pia walipatikana watu 14 wengine ambao tayari walikuwa na uzoefu wa baadhi ya sehemu ya Kuzimu. Wengi wao walikuwa karibu na kifo, watu katika hospitali waliokufa wakarudia tena uhai wao. Hivyo kwa haraka tu: Mimi na mke wangu tulikuwa katika mkutano wa Jumapili usiku wa maombi ambao sisi mara nyingi hudhuria na wachungaji wetu. Na baadae tukaenda nyumbani kama kawaida ili kulala. Ilipofika saa 09:00 asubuhi nilichukuliwa. Sikujua jinsi nilivyoondoka pale mpaka wakati niliporudi. Kisha Bwana alianza kunielezea. Hata hivyo nilitupwa tu katika chumba cha gereza, kama gereza lolote unaloweza kufikiria, lenye kuta mbaya na mihimili ya mlango. Sikujua bado ambapo nilikuwa. Nilichojua ni kwamba kulikuwa na joto sana, joto sana. Sikuamini, kwamba nilikuwa bado hai. Nilihisi kama ningekufa na kujitenga na moto huu, lakini bado nilikuwa hai. Kulikuwa na mwanga mdogo katika chumba kwa muda kidogo, na nikaamini kuwa uwepo wa Bwana ulikuwa pale kwa ajili yangu ili niweze kuona tukio zima kwa uzuri, lakini baada ya dakika moja giza liliingia tena Katika Isaya 24:22 inasema: " Nao watakusanywa pamoja kama vile wakusanywavyo wafungwa katika shimo nao watafungwa katika gereza…. Mithali 7:27 " Nyumba yake ni njia ya kwenda kuzimu, Hushuka mpaka vyumba vya mauti" Kwa chemba ina maana ya vyumba". Kwa hiyo sehemu ya kuzimu ina selo, vyumba, mashimo ya moto, na maeneo makubwa ya moto, hivyo nilikuwa katika selo ya kuzimu. Katika Yona 2:6, "Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele…; " Na Ayubu 17:16 "Litashuka kwenye makomeo ya kuzimu,… " Kwa hiyo tena, kila kitu nilichokiona kilikuwa katika Neno. Mawe yanaongelewa katika Isaya 14:19. Nikajikuta katika selo, na viumbe hawa 4 walikuwa katika selo na mimi. Sikujua walikuwa mapepo wakati huo, kwa sababu nilikwenda huko kama mtu ambaye hajaokoka. Mungu aliliondoa hili katika akili yangu kwamba mimi ni Mkristo niliyeokoka. Sikuelewa kwa nini, lakini alinifafanulia kwangu juu ya hili hapo nilipokuwa nikirudi. Viumbe hawa, sikuweza kutambua kwamba walikuwa mapepo, lakini walikuwa wakubwa. Walikuwa kama futi 12 au 13 kwa urefu, mmoja utamuona katika video. Mmoja wa watu ambao walitoa ushuhuda wao, aliona pepo sawa na yule niliyemuona. Hivyo utaona mmoja anavyofanana. Kuna picha nzuri kwa kweli katika video ambapo kijana mmoja alivutwa hadi katika misingi ya Kuzimu. Ni ushuhuda wa Kenneth Hagin.. Kivyovyote walikuwa wanatisha. Huyu mmoja alikuwa na magamba juu ya mwili wake wote, taya kubwa na meno makubwa, na makucha yamejitokeza, pamoja na macho yalioingia ndani. Yaani walikuwa wakubwa. Na huyu pepo mwingine hakuwa anaonekana kama huyu kabisa, lakini alikuwa na mapezi makali pote na mkono mmoja mrefu na miguu isiyo na uwiano. Kila kitu kilikuwa kimekaa vibaya na vilicheza pasipo uwiano, hakuna 4 ulinganifu, hakuna ulinganifu, mkono mmoja mrefu na mmoja mfupi yaani ni viumbe visivyo na muonekano mzuri, vinatisha, vya kuogofya. Basi, walikuwa wanamtukana Mungu. Muda wote walikuwa wanamlaani Mungu. Mimi nikajiuliza, "Kwa nini wanamlaani Mungu? Kwa nini wanamchukia Mungu hivyo?" Kisha wakanigeukia mimi, na mimi nikahisi vivyo hivyo wanavyojisikia kwa Mungu na mimi wananichukia na tena Nilifikiri: Kwa nini wanachukia?Na sijafanya lolote kwao" Lakini wananichukia mimi na chuki ambayo sijawahi kuiona katika dunia; kwa namna zaidi ya mwanadamu anaweza kunichukia. Kabisa walinichukia mimi, na mimi nilifahamu walikuwa wameletwa ili wanitese. Kulikuwa na mambo ambayo nitakwenda kusema, ambayo sijui ni jinsi gani niliyajua. Kule kuzimu fahamu zako ni halisi zaidi, unafahamu zaidi ya miili yetu. Niliweza kufahamu umbali, Nilifahamu muda, na kadhalika, nilifahamu mengi zaidi kuliko unapokuwa hapa. Nilijua mapepo hayo yaliwekwa pale kwa ajili yangu, ili yanitese milele mahali hapo. Nilikuwa nimelala juu ya sakafu katika selo hii na sikuwa na nguvu kabisa katika mwili wangu. Nikajiuliza, "Kwa nini siwezi hata kujisogeza, nina tatizo gani?" Nilikuwa nafahamu kuwa sina nguvu, na sikuwa na msaada wowote. Pepo moja likanibana na kunichukua na kunirusha kwenye ukuta kama kioo. Alinichukua kama uavyochukua kioo. Hivyo ndivyo jinsi nilivyokuwa mwepesi, au jinsi nguvu zake zilivyokuwa. Na Alinirusha katika ukuta, na kila mfupa katika mwili wangu ulivunjika. Na nilihisi maumivu! Nikawa nimejilaza sakafuni nikipiga kelele za kutaka msaada, lakini viumbe hawa hawana huruma yoyote wakati wote, hawana huruma kabisa. Mmoja alininyanyua, na mwingine mmoja, mwenye makucha makali mithili ya wembe, aliukata mwili wangu. Akaurarua kabisa, na hakuwa anajali kabisa kwa habari ya mwili huu wa ajabu ambao Mungu aliuumba. Alikuwa na chuki ambayo ilikuwa ni kali sana dhidi yangu. Nikajiuliza, "Kwa nini niko hai, kwa nini ningali hai katika hili? Sielewi kwa nini sijafa." Mwili wangu ukawa umetundikwa katika riboni/cheni. Na hapakuwa na damu, ila ni mwili tu umetundikwa, kwa sababu maisha yako katika damu, na hakuna maisha Kuzimu. Na hakuna maji katika Kuzimu. Katika Isaya 14:9-10 inasema Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi. Hao wote watajibu na kukuambia, Je! Wewe nawe umekuwa dhaifu kama sisi! Wewe nawe umekuwa kama sisi! Zaburi 88:4 Nimehesabiwa pamoja nao washukao shimoni; Nimekuwa kama mtu asiye na msaada. 5 Na tunafahamu ya kuwa shetani anazo nguvu, katika maandiko ambapo palikuwa na mtu mwenye pepo akiishi katika eneo la makaburi, biblia inasema: Marko 5:1-4 Wakafika ng'ambo ya bahari mpaka nchi ya Wagerasi.Na alipokwisha kushuka chomboni, mara alikutana na mtu, ambaye ametoka makaburini, mwenye pepo mchafu; makao yake yalikuwa pale makaburini; wala hakuna mtu ye yote aliyeweza kumfunga tena, hata kwa minyororo; kwa sababu alikuwa amefungwa mara nyingi kwa pingu na minyororo, akaikata ile minyororo, na kuzivunja-vunja zile pingu; wala hakuna mtu aliyekuwa na nguvu za kumshinda. Hawakuweza kumfunga, alivunja minyororo vipande vipande. Na huyo alikuwa tu mtu mwenye nguvu ya mapepo. Nilielewa mapepo haya yalikuwa na nguvu mara 1000 zaidi ya mtu. Hivyo hata kama nilikuwa na nguvu yangu ya asili, sikuweza kupigana nao kuwashinda. Hivyo nilikuwa pale nikitegemea huruma yao, ambapo hawakuwa na huruma yoyote. Mapepo huongoza maisha yako kuzimu. Harufu ya mapepo haya na harufu ya Kuzimu ilikuwa mbaya inatisha, Siwezi hata kukuelezea wewe. Kulikuwa na harufu ya mwili unaoungua, na ya salfa. Harufu ya mapepo haya ilikuwa kama mfereji wa maji machafu ulio wazi, yaliyooza, nyama iliyooza, mayai yaliyoharibika, maziwa yaliyochacha na kila kitu ambacho unaweza kufikiria. Zidisha, mara 1000, na uiweke juu ya pua yako. Na uvute hewa ndani. Ilikuwa na sumu sana,ambayo inaweza kuua, kama ungekuwa hapa katika mwili huu, unaweza ukafa. Na mimi nilijiuliza, "Kwa nini naweza kuishi katika harufu hii, na ni mbaya sana ya kutisha?" Lakini tena huwezi hata kufa, unatakiwa kuivumilia. Makufuru, ambayo walikuwa wakimkufuru Mungu yameelezwa katika Ezekieli 22:26 " nami nimetiwa unajisi kati yao. " Kufuru, lugha ya matusi na kukashifu. Mateso waliyokuwa wakinifanyia yametajwa katika Kumbukumbu la Torati 32:22-24. Maana, moto umewashwa kwa hasira yangu, Unateketea hata chini ya kuzimu, Unakula dunia pamoja na mazao yake, Unaunguza misingi ya milima. Nitaweka madhara juu yao chunguchungu; Nitawapiga kwa mishale yangu hata ikaishe;Watakonda kwa njaa, wataliwa na makaa ya moto, Na uharibifu mkali; Nitawapelekea meno ya wanyama wakali, Pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini. Hivyo kuna meno ya mnyama juu yako. 2 Samueli 22:6 inasema: Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili. Na katika Mika 3:2 kuna mstari wa mzuri ambapo wafilisti, waliowachukia waisraeli walisema: Ninyi mnaoyachukia mema, na kuyapenda mabaya; ninyi mnaowachuna watu ngozi yao, na nyama mifupani mwao. 6 Hivyo ndivyo walivyowafanyia watu wa Israeli. Hiyo ilikuwa katika uhalisia, je ni wapi walipata wazo hilo? Hilo wazo la kufanya hivyo lilitoka kuzimu. Hivyo ndivyo mapepo hufanya, na rehema je? Kuna rehema Mbinguni tu. Rehema inatoka kwa Mungu, na shetani hana maarifa yeyote kuhusu wema wowote ule, yuko kinyume kabisa kuhusu hilo. Zaburi 36:5 " Ee Bwana, fadhili zako zafika hata mbinguni, Uaminifu wako hata mawinguni.." Na Zaburi 74:20 inasema: Ulitafakari agano; Maana mahali penye giza katika nchi Pamejaa makao ya ukatili. Ni mahali pa kutisha penye ukatili, huzuni ambao unatakiwa uvumilie. Unatakiwa kuvumilia mambo haya yote. Mungu amemfanya mwanadamu kwa kiwango cha juu cha uumbaji, na mapepo haya ni uumbaji wa kiwango cha chini. Sisi kama binadamu tunafanya kazi kwa bidii ili kuendelea mbele na maisha, tunajifanyia ubora sisi wenyewe, tunajifunza. Lakini kule kuzimu, maisha yako yanaongozwa na mapepo. Viumbe hawa wana IQ sifuri, viumbe hawa ni wajinga kabisa. Kile wanacho kijua ni chuki kwa Mungu, chuki kwako wewe na mateso. Na wanaongoza maisha yako, na huwezi kufanya lolote kuhusu hilo. Kuna maandiko kuhusu udhalilishaji unaotakiwa kukabiliana nao. "Jambo hili linakwenda kuongoza maisha yangu, siwezi kuliacha!" Katika Isaya 5: 14-15 Kwa hiyo kuzimu kumeongeza tamaa yake, kumefunua kinywa chake bila kiasi; na utukufu wao, na wingi wao, na ghasia yao, naye pia afurahiye miongoni mwao, hushuka na kuingia humo. Na mtu mnyonge ainamishwa, na mtu mkubwa amedhilika, na macho yao walioinuka hunyenyekezwa, Isaya 57:9-16 Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hata kuzimu. Ulikuwa umechoka kwa ajili ya urefu wa njia yako; lakini hukusema, Hapana matumaini; ulipata kuhuishwa nguvu zako; kwa sababu hiyo hukuugua. Tena ni nani uliyemwogopa na kumhofu, hata ukasema uongo, wala hukunikumbuka mimi, wala kuweka hayo moyoni? Je! Mimi sikunyamaza tangu zamani, hata huniogopi?Mimi nitatangaza haki yako, na matendo yako hayatakufaa. Utakapolia, na wakuponye hao uliowakusanya; lakini upepo utawachukua; uvuvio tu utawachukulia mbali; lakini yeye anayenitumaini ataimiliki nchi, na kuurithi mlima wangu mtakatifu. Naye atasema, Tutieni, tutieni, Itengenezeni njia, Kiondoeni kila kikwazacho Katika njia ya watu wangu. Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye milele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu na kunyenyekea, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu. Kwa kuwa sitashindana na watu siku zote, wala sitakuwa na hasira siku zote; maana roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi nilizozifanya. Ezekieli 32:24 Elamu yuko huko, na watu wake wote jamii, pande zote za kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka hali hawana tohara hata pande za chini ya nchi; ambao 7 waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni. Inaendelea na kuendelea. Hiyo ilikuwa ni kitu kibaya kuona maisha yako yanaongozwa na viumbe hawa, ambao hawana hata huruma kwa lolote lile! (Giza na vilio kuzimu) Nilikuwa nimelala katika selo na mara pakawa giza, kiini, kiini cha weusi wa giza. Namaanisha giza ambalo sijawahi kuliona kabla. Na nilikuwa chini kabisa katika mapango, ni chini sana kama katika migodi ya chuma kule Arizona. Kulikuwa na giza ambalo huwezi hata kufikiria. Niliweza kutambaa kuelekea nje, kwa namna fulani niliweza kutambaa na waliniacha kidogo. Nilikumbuka ambapo mlango ulikuwa hivyo nikatambaa kuelekea kwenye mlango na nikatoka nje ya selo. Nikaangalia mwelekeo mmoja, na tazama ni peusi pote, na nilichosikia ilikuwa ni mayowe, mabilioni ya watu walipiga mayowe mahali hapo. Nilijua kulikuwa na mabilioni, na kulikuwa na sauti kubwa. Kama umewahi kusikia mtu akipiga kelele, huwa inachukiza. Naam kama wewe ukisikia mabilioni ya watu wakipiga mayowe, huwezi kufikiria ni jinsi gani inaathiri akili yako. Hauwezi kuvumilia. Unajaribu kushikilia masikio yako kwa sababu sauti ni kubwa lakini inapenya. Huwezi ukakimbia mayowe haya. Na hofu inayokujia inakuwa ya ajabu. Kila kitu kinaongozwa na hofu. Hakuna uwepo wa Mungu katika sehemu hii, hivyo inakupasa kuishinda hofu na mateso na giza wewe mwenyewe. Huwezi kuona chochote. Huwezi hata kuona ni kitu gani kinakuja dhidi yako. Maandiko yanasema sana kuhusu giza hili Zaburi 88: 6 Mimi umenilaza katika shimo la chini, Katika mahali penye giza vilindini. Ufunuo16:10 Na huyo wa tano akakimimina kitasa chake juu ya kiti cha enzi cha yule mnyama; ufalme wake ukatiwa giza; wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu, Yuda 1:13 Ni mawimbi ya bahari yasiyozuilika, yakitoa aibu yao wenyewe kama povu; ni nyota zipoteazo, ambao weusi wa giza ndio akiba yao waliowekewa milele. Na kulikuwa na giza ambalo unaweza ukalihisi, kama ilivyoonyeshwa Kutoka 10:21 Bwana akamwambia Musa, Nyosha mkono wako kuelekea mbinguni, kuwe giza juu ya nchi ya Misri, watu wapapase-papase gizani. Unaweza ukalihisi giza hili. (Hofu kuzimu) Hofu niliyopata niseme tu, ilikuwa kubwa sana. Inakukamata. Kama umewahi kuona muvi(tamthilia) za kutisha,ambapo hofu inakukamata mpaka kwenye koo, sasa unaweza ukachukulia hiyo na ukazidisha mara 1000 hivi, na ukawa nayo hiyo wakati wote, na ninafahamu kitu kuhusu hofu. Nilipokuwa mdogo nilikuwa nikiogelea. Nilipokuwa mdogo sana tulikuwa katika ufukwe wa Coco Frolida tukiogelea na kulikuwa na kundi la papa walikuwa wakinizunguka. Na papa wa karibu futi 9 alikuja na kuupiga ubao wangu wa kuogelea kwa katikakati. 8 Alinichuchuka kwa mguu wangu na kunivuta chini. Hivyo mguu wangu ulikuwa kwenye mdomo wa huyu papa mkubwa. Nilikuwa bado sijawa mkristo, nilikuwa hata sijaokolewa. Na mara gafla aliniacha ili niondoke. Nafahamu Mungu alifungua kinywa cha Yule papa. Lakini kwa muda mfupi huo hofu inayokuijia ni kubwa sana ya kushangaza. Kama yeyote amewahi kuona mataya ya papa, hofu ile ni kubwa sana huwezi kufananisha mpaka ikutokee. Hofu ilikuwa ni ya kutisha. Aliyekuwa pembeni yangu alikuwa futi chache mbali kidogo, papa huyu alimtafuna mguu wake! na wakamvuta pembeni ya ufukwe, na damu kila mahali. Alikuwa akilia na mguu ukiwa umeliwa tayari. Kwa hiyo naifahamu hofu lakini ile hofu haikuwa kitu ukilinganisha na hofu niliyopitia Kuzimu, Hakuna jinsi ya kufananisha. Nafikiri hofu niliyoipata juu ya papa ni moja ya hofu kubwa ambayo tunaweza kupitia hapa duniani. Kwa hiyo haya ni mambo machache tunayotakiwa kuyashinda kule kuzimu.Isaya 24:17-18 inasema: Hofu, na shimo, na mtego, vi juu yako, Ee mwenye kukaa duniani. Itakuwa kila akimbiaye sauti ya hofu ataanguka katika shimo; na kila apandaye na kutoka shimoni atanaswa na mtego; kwa maana madirisha yaliyo juu yamewekwa wazi, na misingi ya dunia inatikisika. Ted Koppel, alipokuwa akifundisha alifundisha akiwa na mada ya "Night Line" mwaka mmoja na nusu uliopita, aliwatembelea wafungwa baadhi nchini na akakaa nao usiku mzima mahali pale. hakuweza kuamini jinsi kulivyokuwa na kelele, hakuweza kulala, kila mmoja alipiga kelele za juu sana kwa nguvu zake zote. Alisema alishagazwa jinsi watu walivyopiga kelele na kuunguruma usiku kucha. Hivyo hata katika magereza yetu ya duniani, watu hupiga kelele, je ni kiasi gani kule kuzimu. Katika Ayubu 18:14 inazungumzia maovu ya mwanadamu, kwa mtu atakayemkataa Bwana... Atang'olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa kwake mfalme wa utisho. Shetani hakika ni mfalme wa Hofu. (Kuachwa Kuzimu) Sasa nilikuwa nje ya selo na niliangalia upande huu Niliona miali ya moto, kama maili 10 hivi kutokea nilipokuwa. Nilifahamu kuwa ilikuwa maili 10. Na shimo la moto kama maili 3 kwa upana, lilikuwa na moto uliokuwa ukiwaka mpaka angani ulioweza kunifanya kuona ardhi ya kuzimu kidogo. Giza lilikuwa ni nene; liliweza kula mwanga wote. Lakini angalau kulikuwa na mwanga wa kuweza kuona anga. Palikuwa ni kahawia na ukiwa. Namaaanisha hakuna hata kijani kimojawapo, hakuna hata maisha ya aina yeyote, ni jiwe/mwamba, kuchafu na anga nyeusi na moshi katika anga. Miali ilikuwa ni mirefu hivyo niliweza kuiona. Kuna andiko katika Mambo ya nyakati 29:23 Ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua Bwana kwa ghadhabu yake na hasira zake; Hakuna maisha hata hivyo kuzimu. Inatisha kama nini kuwepo kwenye ulimwengu ambao hauna maisha. Hapa tunafurahia miti na hewa safi, lakini mahali pale kila kitu kimekufa. 9 (Moto) Moto ulikuwa ni mkubwa sana, huwezi hata kuelezea. Mambo ya nyakati 32:24 inasema; Watakonda kwa njaa, wataliwa na makaa ya moto, Na uharibifu mkali; Nitawapelekea meno ya wanyama wakali, Pamoja na sumu ya wadudu watambaao mavumbini. Yuda1:7 Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyokuwa kando-kando, waliofuata uasherati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wakiadhibiwa katika moto wa milele. Zaburi 11:6 Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa hari, Na viwe fungu la kikombe chao. Hicho ndicho kilichokuwa kikiendelea Kuzimu, pana joto kali. Hivi vitu vyote vilitosha kabisa kukuua, lakini hufi! Unatakiwa kuendelea kuvumilia haya mateso. Nilihitaji amani ya moyo, kuondokana na vilio hivi na kutoka mahali pale. Ni kama ambavyo unataka kwenda nyumbani usiku baada ya siku ngumu, unahitaji amani ya moyo. Lakini pale unavumilia mateso yote na vilio. na hauwezi kamwe kutoka mahali pale. Isaya 57:21 inasema: " Hapana amani kwa wabaya; asema Mungu wangu.” Pia kuzimu unakuwa uchi. Ni kitu kingine ambacho inakupasa uvumilie. Aibu! Ezekiel 32:24 inaongelea kuhusu aibu ndani ya kuzimu. Elamu yuko huko, na watu wake wote jamii, pande zote za kaburi lake; wote pia wameuawa, wameanguka kwa upanga, walioshuka hali hawana tohara hata pande za chini ya nchi; ambao waliwatia watu hofu katika nchi ya walio hai, nao wamechukua aibu yao, pamoja nao washukao shimoni. Na katika Ayubu 26:6 Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko. Hii inamaanisha Mungu anaweza kuona Kuzimu, Hivyo inaonekana kwake. (Ukame) Hakuna maji kuzimu, kabisa, hakuna. Hakuna unyevunyevu katika anga na maji ya aina yeyote. Kuna ukame sana Unakuwa unahitaji maji ya kunywa hata tone la maji tu, moja tu. Kama vile ambavyo maadiko yanasema katika Luka 16:23-24, Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. 10 Ibrahimu akasema, "Mwanangu kumbuka", na kisha aliendelea kuzungumzia ndugu zake. Alimtaka tu achovye ncha ya kidole chake katika maji, apate tone moja tu. Hiyo ingekuwa ni kitu cha thamani, tone moja, lakini haiwezekani, kupata hata tone. Ni vigumu kupata picha ni jinsi gani mdomo wako unakuwa mkavu. Kama unaweza kufikiria kufanya mbio za marathoni za kufa na kupona na ukawa na pamba katika mdomo wako na unaendelea kuwa huko kwenye bonde la uvuli wa mauti kwa muda wote, iendelee hivyo, kukame, kabisa, unahitaji tone la maji. Kitu kingine andiko hili limebainisha kwangu tunajua kuna shimo kubwa sana limewatenganisha kati yao, kuzimu; kati ya peponi na Kuzimu. Na mtu huyu aliyekuwa tajiri akamwona Abrahamu kwa mbali. Kwa asili, anawezaje kumtambua Lazaro na Ibrahim? Awali ya yote kamwe hakuwahi kukutana na Ibrahimu na kisha kuona mtu kwa mbali namna ile, usingeweza kujua ni nani hao. Lakini kuna mambo fulani tu unajikuta unayajua kuzimu. Unaelewa, kama nilivyosema, kuhusu kina, umbali wake na kadhalika. Kisha pepo mojawapo likanikamata, na kunirudisha tena selo na nikarudia yale mateso tena, ambayo sipendi kuyaongelea, kwa sababu sipendi kuendelea kukumbushia mateso yale. Walianza kuniponda fuvu langu. Pepo moja likanikamata nakujaribu kupasua kichwa changu. Nalikuwa nalia mayowe na kuomba rehema, lakini hakuna rehema! Kwa wakati huu sasa kila pepo lilishika mkono na mguu wangu na walikuwa karibu kuniachanisha. Nilifikiri kichwani “siwezi kuvumilia hili, siwezi kuvumilia hili!" (Jirani na shimo) Na mara gafla, kitu kikanishika na kunivuta nje ya selo. Najua alikuwa ni Bwana, lakini wakati huo sikuwa nimejua. Nilikuwa mahali pale kama mtu asieokoka, kwa hiyo sikujua vitu hivi. Nilikwenda pale kama sikuwahi kumpokea Bwana. Niliwekwa jirani kidogo na moto niliouona. Nilikuwa nimesimama peke yangu pembeni mwa shimo lile. Nilikuwa chini ya pango, kama pango kubwa, lenye tanuru iliyokwenda juu. Ndani ya moto ule niliweza kuona ndani miili na watu ndani ya moto wakilia mayowe, walilia rehema, huku wakiungua! Na nilifahamu sikutaka kwenda mahali pale. Maumivu niliyoyapata tayari yalikuwa ni makubwa lakini moto uliokuwa ukitokea mle kwenye miali ile ya moto nilitambua ilikuwa ni hari zaidi sana. Watu hawa waliomba kutoka nje. Kulikuwa na viumbe hawa wakubwa wamejipanga wamezunguka pembezoni mwa shimo hilo, na watu walipokuwa wakijaribu kutoka nje, walirudishwa tena kwenye moto wasiweze tena kutoka. Nikafikiri, “Oh, hii sehemu ni mbaya, mbaya sana na inatisha sana.” Haya yote yanafanyika kwa wakati mmoja. Una kiu, una njaa, umechoka. Pia kuzimu hupati muda wa kulala. Unahitaji usingizi kama unavyohitaji sasa. Mwili wako unakuwa unahitaji kulala. Ufunuo 14:11 inasema, Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele na milele, wala hawana raha mchana wala usiku,… Hata huwezi kulala. Unaweza kufikiri ni jinsi gani kulivyo, yaani hakuna kulala. Kuhusu maji, Zakaria 9:11, ... Nimewatoa wafungwa wako katika shimo lile lisislo na maji. 11 Hakuna maji kabisa kuzimu. Nilitambua kuwa mahali ilipo kuzimu ni katikati ndani ya duni. Hapo ndipo mahali ilipo, ndani katikati ya dunia. Nilitambua hivyo nilipokuwa kama maili 3700 ndani chini ya dunia.Tunafahamu kwamba kipenyo cha dunia ni maili 8000. Na nusu ya kipenyo hicho ni kama Maili 4000. Nilikuwa kama maili 3700. Katika waefeso 4:9 inasema kwamba Yesu alishuka mpaka chini pande za dunia/nchi. Hesabu 16:32 inasema, Na nchi ikafunua kinywa chake na kuwameza,na watu wa nyumba zaona wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote. Hapo ndipo Kuzimu ilipo sasa. Baadae Kuzimu na mauti vitatupwa katika moto wa Jehanamu na kutupwa katika giza kuu. Hiyo ni baada ya hukumu, Lakini kwa sasa iko duniani. (Pepo) Nilikuwa pembezoni mwa shimo la kuzimu na nikaona mapepo yote haya yamejipanga katika kuta, yana ukubwa tofauti tofauti na maumbo ya kila namna, mabaya, viumbe vibaya kiasi unachoweza kufikiri. Walikuwa wamejikunja, wameharibika, wakubwa na wadogo. Kulikuwa na ng”e wakubwa, wakubwa hivi. (uefu futi5) Panya, nyoka na minyoo, kwa sababu biblia inaongelea kuhusu minyoo yenye inayoambaa (Isaya 14:11). Kuna kila aina ya viumbe wabaya kila eneo na inaonekana kana kwamba imefungwa kwa minyororo kwenye kuta.Nikashangaa "Kwa nini vitu hivi vimefungwa kwenye kuta". Sikuelewa, lakini kulikuwa na andiko katika Yuda 1:6 linasema, "Na malaika wasioilinda enzi yao wenyewe, lakini wakayaacha makao yao yaliyowahusu, amewaweka katika vifungo vya milele chini ya giza kwa hukumu ya siku ile kuu;" Na hivyo ninahisi hiki ndicho nilikiona, sijui, lakini hicho ndicho kilichonitokea. Nilifurahi kwa sababu sikutaka wanisogelee. Walionyesha kunichukia sana! Hiko kilikuwa kitu kingine ambacho sikukielewa, hawakuwa tu ni viumbe, walikuwa na chuki kubwa kwa wanadamu. Hivyo nilifurahia kuona wamefungwa kwenye kuta. Nilianza kupaa shimo hili kwenye tanuru hili, na kuachana na miali. Mara kukawa na giza, lakini niliweza kuona mapepo yote haya pembeni ya tanuru na walikuwa na nguvu kubwa sana. Nikafikiri,"Nani anayeweza kupigana nao viumbe hawa. Hakuna anayeweza kupigana nao viumbe hawa." Lakini bado,Hofu ile ilikuwa ni kubwa sana, sikuweza kabisa kusimama juu ya hofu hii. (Hakuna Matumaini) Kitu kibaya Kuzimu, kitu kibaya, kitu kibaya kuliko mateso yote, niliweza kutambua, kwamba kuna maisha yanaendelea hapa duniani. Na ya kuwa watu hapa juu, watu wengi, hawana hata habari kuwa ulimwengu huu uko hapa chini na ni halisi! Hawajui kabisa kuwa ni ulimwengu mwingine na halisi huko hapa chini na kuna mabilioni ya watu wanaumia na kuomba nafasi nyingine ya pili, kama wangekuwa na nafasi ya kutoka tu mahali pale. Lakini hawawezi kupata nafasi nyingine tena, na wanakuwa vichaa kabisa kuona kuwa hawawezi kuwa na fursa ya kuwa na Yesu, kwamba wameishia mahali pale maisha yao yote. Hiki ndicho kitu kibaya kuliko vyote, kwamba hakukuwa na matumaini ya kutoka nje. Nilifahamu hivyo. Nilitambua umilele. Niliweza kuelewa umilele. Hapa duniani, hatuwezi kuwazia, Hatuwezi kuujua. lakini pale niliuelewa. Nilijua nitakuwa huko milele na milele, wala sikuwa na matumaini ya kutoka nje. Niliwaza kuhusu mke wangu. Sikuweza kwenda kwa mke wangu! Nimekuwa nikimwambia kama tukitenganishwa na kitu chochote kwa namna yeyote labda tetemeko au kitu cha kutisha, 12 nilisema "Nitarudi. Nitakutafuta. Nitakurudia kama tumeachanishwa." Lakini hapa sikuweza kumrudia. Sikuweza kumuona tena. Hakuwa hata na wazo lolote ni wapi nilikuwa na sikuweza kamwe kuongea naye tena milele. Hilo wazo tu lilinisumbua sana! Kutokuwa na uwezo wa kuongea naye, kuwa naye, na kwa yeye kutojua ambapo mimi nipo, na sikuwa na matumaini kwa milele kutoka nje! Unakuwa unaelewa, kuwa huwezi kutoka hapo, milele! Angalia duniani kuna matumaini siku zote. Hata watu katika kambi za mateso huwa na matumaini ya kutoka nje, au kufa angalau, ili waondokane na taabu. Lakini hatujawahi kabisa kukosa matumaini kama ilivyo kuzimu. Katika Isaya 38:18 inasema, "Wale washukao shimoni hawawezi kuitarajia kweli yako." Hakuna matumaini, na kweli ni Yesu (Yesu akatokea) Wakati huu, nilikwenda juu ya tanuru hili, na nikiwa na hofu kubwa, sina matumaini nimepotea, na nikiwa naogopa mapepo haya. Kwa ghafla, kwa ghafla tu, Yesu akajitokeza! "Usifiwe wewe Bwana", Yesu alijitokeza. Mwanga huu mkali ulimulika mahali pale. Mimi niliona tu umbo lake, umbo la mwanadamu. Sikuweza kuona uso wake, mwanga ulikuwa mkali sana. Niliangalia katika mwanga huu na kuona umbo lake tu. Na mimi nikapiga magoti yangu nikaanguka. Sikuweza kufanya jambo lolote tofauti na kuabudu. Nilijisikia furaha. Sekunde moja iliyopita nilikuwa nimepotea milele, na sasa ghafla natoka nje ya eneo hili, kwa sababu nilikuwa tayari nimemjua Yesu. Watu wale hawawezi kutoka nje, lakini mimi naweza kwa sababu nilikuwa tayari nimeokolewa. Nilijua na kuelewa kwamba kulikuwa hakuna njia a kutoka nje ya eneo hili, ni kwa Yesu pekee. Yeye ni njia pekee ya kukufanya usiende mahali hapa. Ufunuo 1:6 inasema Yohana, alipokwenda mbinguni, alimuona Yesu, na sura yake ilikuwa kama jua liking'aa kwa nguvu zake. Naye alipomuona kwake, akaanguka mbele ya miguu yake kama mtu aliyekufa. Hivyo ndivyo nami nilifanya. Nilianguka mbele ya miguu yake kama mtu aliyekufa. Sasa unaweza kufikiria nilikuwa na maswali milioni ya kumuuliza, lakini wakati uko pale, kile unachoweza kufanya ni kumwabudu na kumtukuza jina lake Takatifu, na kumshukuru kwa kile alichotuokoa. Nilipotulia sasa, angalau kiasi ambacho naweza kuanza kutengeneza mawazo, Niliwaza kumwaambia Bwana, Hata sikumbuki kama nilimuuliza kwa sauti kubwa, niliwaza tu na akanijibu. Mimi nikasema, "Bwana kwa nini umenileta mahali hapa? Kwa nini umenileta mahali hapa?" Akaniambia "Kwa sababu watu hawaamini kwamba eneo hili ni halisi." Alisema "Hata baadhi ya watu wangu mwenyewe hawaamini eneo hili ni halisi." Nilishitushwa kwa usemi huo. Nilidhani kila Mkristo anaamini Kuzimu. Lakini si kila mtu anaamini katika uhalisi wa moto wa Kuzimu. Nilisema Bwana "kwa nini umenichukua mimi?" Lakini hakujibu swali hilo. Mimi sijui ni kwa nini yeye alinichukua mimi kwenda huko. Uwezekano wa mimi kwenda mahali hapo ulikuwa ni mdogo. Mke wangu na mimi huwa tunachukia sinema za maovu. Tunachukia lolote baya. Sipendelei hata maisha ya majira ya kiangazi, sana napendelea kiasi kidogo cha joto. Ni machafu. Hakuna mpangilio. Ni kero muda wote na machafuko na machukizo. Na mimi upendelea kila kitu chenye utaratibu na ubora. Hakunijibu swali hilo. Akaniambia, "Nenda ukawaambie kwamba ninachukia mahali hapa, kwamba si mapenzi yangu kwa yeyote mmoja wa viumbe wangu kwenda mahali hapa, hata mmoja! Sikuumba hili kwa ajili ya mtu. Hii ilifanyika kwa ajili ya shetani na malaika zake. Unatakiwa kwenda na kuwaambia! Nimekupa kinywa, wewe nenda na uwaambie. " Nikajifikiria, "Bwana, hawatakwenda kuniamini. Watanifikiria mimi ni kichaa au nilikuwa na ndoto mbaya." Namaanisha je wewe usinge fikiria hivi? Kama Nilipofikiria hivi, Bwana akanijibu akasema, "Siyo kazi yako 13 kuwashawishi. Ni kazi ya Roho Mtakatifu! Wewe nenda na uwaambie!" Na niliitika ndani, "Ndiyo Bwana!" Ni sahihi kabisa, nitakwenda na kuwaambia." Hutakiwi kuwa na wasiwasi na hofu juu ya mtu anafikiria nini juu yako, wewe unachotakiwa tu ni kwenda na kufanya hivyo na kumuachia Mungu afanye yaliyobakia. Amina? Nami nikasema," Bwana, kwa nini wananichukia sana? "" Kwa nini viumbe hawa wananichukia? "Akasema," Kwa sababu umefanywa kwa mfano wangu na wananichukia mimi. "Unajua shetani hawezi kufanya kitu chochote dhidi ya Mungu. Hawezi kumdhuru Mungu, kwa kusema, lakini anaweza kuumiza viumbe vyake. Ndiyo maana shetani anachukia watu, na anawadanganya na kuwapeleka kuzimu. Naye anaweka magonjwa juu yao, kitu chochote anaweza kufanya ili mradi auumize viumbe wa Mungu. (Amani ya Mungu) Na kisha Mungu akanijaza Mawazo yake. Aliniruhusu niguse kiasi cha moyo wake, ni kiasi gani anampenda mwanadamu. Ajabu, sikuweza hata kulichukulia hili. Ilikuwa ni zaidi hakuna mfano wake. Upendo alionao kwa mtu, huwezi ukauchukulia katika mwili huu. Unajua ni kiasi gani tunawapenda wake zetu na watoto wetu? Naam upendo tulionao hatuwezi hata kuulinganisha na upendo wa Mungu kwetu sisi. Upendo wake ni mkubwa zaidi kuliko upendo wetu na uwezo wetu wa kupenda. Ni sawa tu kama inavyosemwa katika Waefeso 3:19, "... ili kujua upendo wa Kristo ambao hupita maarifa ..." Inakwenda mbali kupita maarifa, huwezi hata ukapata ufahamu wake. Sikuamini kuona ni kiasi gani alimpenda mwanadamu, kwamba anakufa kwa ajili ya mtu mmoja tu ili asiende mahali hapo. Na anakuwa na uchungu mwingi kuona mmoja wa viumbe vyake anakwenda mahali hapo. Inamuumiza Bwana, Analia kuona mtu mmoja anakwenda. Na nilijihisi vibaya kwa Bwana. Nilihisi moyo wake, basi akaniacha niguse kidogo moyo wake. Alijisikia huzuni kwa viumbe wake kwenda mahali pale. Nikawaza "Imenipasa kutoka nje na kushuhudia na kuchukua kila pumzi ya mwisho kuwaambia dunia habari za Yesu, Jinsi alivyo mzuri." Naama ka kuwa, tuna injili. Ni habari njema. Ni habari njema, na dunia haijui. Imewapasa kuambiwa! Unajua, inabidi tushiriki maarifa haya. Watu wanakosa elimu katika eneo hili. Mungu anataka sisi tushiriki pamoja nao jinsi yeye alivyo mzuri, na jinsi Yeye anachukia mahali hapo. Akaniambia pia, "Waambie ninakuja hivi karibuni, karibu sana." Akasema tena, "Waambie ninakuja hivi karibuni, karibuni sana." Sasa nafkiri, kwa nini sikumwambia, "Ni nini umaaanisha Bwana?'hivi karibuni' ikoje kwako?" Hivyo ndivyo jinsi tunafikiri. Lakini sikuweza kuuliza vitu hivyo wakati huo. Unataka tu uendelee kumwabudu sana. Amani ya Mungu inayokuja juu yako kuwa karibu naye haielezeki. Nimekuwa katika huduma za upako, lakini hakuna cha kulinganisha na upendo na amani ya Mungu unayojisikia kuwa karibu naye. Na kisha nikatazama juu na nikaona mapepo hayo juu ya ukuta, walionekana wakiwa na uso wa ukali, walikuwa wanaonekana kama mchwa kwenye ukuta! Walionekana kama mchwa! Bado walikuwa ni wakubwa, lakini kwa uwezo wa Mungu uliokaribu nawe, nguvu zote za uumbaji wa Mungu, walikuwa wanaonekana kama mchwa kwenye ukuta. Sikuweza kwenda juu yake. Nikafikiri, "Bwana ni kama mchwa tu hawa!" Naye akasema, "Wewe unachotakiwa tu ni kuwafunga na kuwatoa nje kwa jina langu." Nikafikiri "Kijana, nguvu alizotoa kwa kanisa." Hivi vitu ambayo vilikuwa na ukali, tusingeweza kushindana navyo bila Yesu, hakuna. Wanahasira, lakini unapokuwa pamoja naye, ni bure tu ! Ujasiri ukaja ndani yangu, nilipoona viumbe hawa nilihisi kama niseme, "Nyie viumbe mliokuwa mnanitesa, mkataka kunigawana? Haya njooni! Haya njooni sasa!" Labda inawezekana nafsi yangu ilijiinua au kitu kingine, unajua, Niliwaza, "Yesu wafate." (Kuondoka Kuzimu) Tulipoondoka, tukapanda juu ya uso wa dunia. Tulikwenda juu, kwa sababu tulikuwa bado katika shimo. Punde sikuweza kuiona tena, lakini ilikuwa ni kama upepo wa kisulisuli, kimbunga kikubwa nasi tuko ndani yake. Ilibidi 14 kuendelea kwenda juu, ili tutoke nje yake ilivyoonekana. Tulipofika juu yake, nikaangalia chini duniani na tulikuwa juu namna hii. Mviringo wa dunia ulionekana kama hapo. Nifuraha kuangalia tena katika nchi! Najua Mungu aliruhusu hilo kwa ajili yangu. Tungeweza kuondoka kwenye handaki kwa namna yoyote ambayo Angetaka. Alijua ndani ya moyo wangu, kwamba nilipokuwa mtoto siku zote nilitamani kuona dunia inaonekana vipi kutokea angani. Labda ni kwasababu niliangalia sana, Safari ya nyota au kitu, unajua? Nilijiwadhia itakuwa vizuri kweli kuona dunia, na kuona ikielea angani bila kushikiliwa na chochote. Kama Biblia inavyosema. Inasema katika Ayubu 26: 7, Yeye hutandaza kaskazi juu ya nafasi isiyo na kitu, Yeye lipo duniani juu ya chochote. Kama ukiangalia, unafikiri, "Ni nini kinashikilia hii dunia juu? Nini kinafanya izunguke kwa ukamilifu?" Mungu anadhibiti hilo. Uwezo wa Mungu ulionifunika, ulikuwa ni wa kutisha. Ana uwezo sana. Kila kitu kimoja kimoja viko chini ya udhibiti wake. Si tu nywele juu ya kichwa chako zishukazo mpaka chini kwamba hawezi kuzijua kwa idadi. Sio tu ndege aliyeanguka sakafuni kwamba hawezi kujua. Nilikuwa nimejazwa na mawazo haya. Mungu ana nguvu sana. Ilinishangaza sana. Kuna maandiko katika Isaya 40:22 yanayosema Bwana anaketi katika muhimili wa nchi/dunia. Pale nilikuwa juu ya mhimili wa dunia. Hata nikawaza pia, "Bwana, kwa nini kabla ya Christopher Columbus wasingesoma maandiko na kujua kuwa nchi/dunia ilikuwa ni mviringo." Unajua? Watu walishangaa, walidhani ilikuwa ni tambarare? Hata hivyo, tuliporudi chini tulipita katikati ya ngao; Nilijua tulikuwa tukipita katikati ya ngao za joto lililokuwa lililozunguka duniani. Nilijua tu hivyo. Hata niliwaza mawazo ya kijinga, hapa niko na Mungu, na “sijui atakwendaje kupita katikati ya ngao ile ya moto?" Unajua jinsi ambavyo angani wanavyotakiwa kupenya ngao hiyo kwa pembe/makadirio sahihi. Tulikwenda kwa njia hiyo na hakuna tatizo lolote gani lillilotokea. Hakuna cha kushangaa! Nina hakika Bwana alitazama kwa macho yake na kusema ninaweza tu kupita, Kuna maandiko Zaburi 47: 9 inasema kwamba, ... Kwa ngao za dunia ni zake Mungu ... Mungu yuko katika udhibiti wa kila kitu, kila kitu. Sikutaka aondoke. Nilitaka kuwa katika uwepo wake. Tulikuwa tunashuka kutokea juu kwa kasi California. Tulikuwa tunashuka kwa haraka, haraka sana, tukaingia mpaka nyumbani kwetu. Na niliangalia nikaweza kuona kutokea kwenye paa la nyumba yetu. Na niliweza kujiona mwenyewe nimelala juu ya sakafu. Hili kweli lilinishangaza sana, kwa sababu niliona mwili wangu umelala hapo, nikawaza, "Huyo hawezi kuwa mimi, mimi niko hapa, huyu ni mimi!" Unajua, wewe hujawahi kuona wawili ambao ni wewe mwenyewe. Hapa nilikuwa nimelala pale nikawaza, "Huyo si mimi halisi." Na kwamba andiko Paulo analolisemea, kwamba tuko ndani ya hema (2 Wakorintho 5:1), likanijia kwa nguvu. Nikawaza "hiyo ni hema, si kitu. Huyo ni wa muda. Huyu ni mimi halisi." Hiyo ndiyo umilele inavyokuwa. Kwamba haya ndiyo maisha tunayojisumbua nayo, nikakumbuka pia sisi ni mvuke, maisha haya ni kama mvuke kama katika Yakobo 4:14 inazungumzia juu ya ufupi wa maisha haya. Ni muda mfupi. Miaka mia moja kama ukiwa hai, si kitu! inapotea kama mvuke. Na nikawaza, "Imetupasa kuishi kwa ajili ya Mungu." Tunachofanya sasa, hapa, kinaandaa umilele. Imetupasa kushuhudia. Imetupasa kutoka nje na kuokoa waliopotea. Hatuwezi kuwa tunajisumbua na vitu hivi vidogo kila siku vimetufunga na tunahangaika navyo. Tunahitaji kweli kutoka nje na kuhubiri injili na habari njema, kwa sababu hii ni zaidi ya haraka sana. Nikaona mwili wangu umelala hapo na nilifikiri ilikuwa tu kama vile umetoka nje ya gari yako na ukangalia nyuma tena kwenye gari yako. Huyo si wewe, ni gari yako. Ni vile imekuzunguka tu. Hivyo ndivyo jinsi ilionekana kwangu. mwili huo umenizunguka tu hapa duniani, lakini huyu ndiye mimi halisi. Na nikafikiri, 15 "Bwana usiondoke, usiondoke". Nataka kuendelea kuwa na wewe kwa muda. Lakini aliondoka. Nikaurudia mwili wangu, na kitu kikanivuta kwenye mwili wangu, kama vile nimerudishwa kwenye pua yangu au kinywa changu. Wakati huo, alipoondoka, hofu yote, mateso, na adhabu zote zilinirudia kwenye mawazo yangu! Kwa sababu inasemwa katika Biblia (1 Yohana 4:18), "Upendo wa kweli hufukuza mbali hofu." Hivyo nilikuwa karibu na upendo kamili muda wote huo, sasa akaniacha, na alipoondoka, kwa ghafla hofu yote na machungu ya kuzimu yaliingia mawazoni mwangu. Sikuweza kuvumilia, sikuweza kuvumilia! Nikapiga mayowe. Nilikuwa katika maumivu/uchungu makali/mkali. Sikuweza kuishi nayo. Nilijua kuwa mwili huu haukuwa na uwezo wa kujisimamia kwa aina hiyo ya hofu. Huwezi ukajizuia juu ya shinikizo hiyo. Mwili wako hauna nguvu za kutosha kujizuia. Hivyo wakati huo sasa niliomba na niliweza wa kuomba, "Ondoa katika akili yangu!" Kwa asili, ni lazima upitie kila aina ya ushauri nasaha ili kutoka nje ya aina hii ya kiwewe, lakini Mungu aliondoa hili nje, papo hapo aliondoa kiwewe, majeraha. Aliniachia kumbukumbu, lakini aliniondolea kiwewe na hofu. Nilimshukuru. Hata hivyo, baada ya hayo, mambo mengi yaliyotokea, Ningependa tungekuwa na muda wa kugusia yote ambayo Mungu alithibitisha yangetokea kwangu. Kama kuna mtu hapa usiku wa leo, ambaye hamjui Bwana; unatakiwa ujiulize swali. Unatakiwa kusema, "Je, nawaamini watu hawa, kile walichokiona ni halisi, watu wote hawa na mimi mwenyewe?" Lakini cha muhimu zaidi, nini Neno la Mungu linasema kuhusu Kuzimu. Je, unataka kuchukua nafasi hiyo na kusema, "Hapana mimi siamini hii kama ni kweli,. "Basi tupa Neno la Mungu lote, na sisi sote tunaojaribu kukuambia. Je, uko tayari kuchukua nafasi hiyo milele yako yote? hiyo naona ni ujinga kwangu. Huwezi ukamruhusu shetani akudanganye. kile kiumbe kikubwa pale mwishoni kikicheka. (inavyoonekana katika video) hivyo ndivyo jinsi shetani atakuwa ukifika kuzimu. Atakucheka, kwa sababu ulikuwa na nafasi ya kupokea Bwana na umeikosa. Lakini utakapokuwa pale, hakuna kurudi nyuma. hakuna kabisa kurudi nyuma. Utakuwa huko pale umepotea milele. Unaweza kuwa unajisemea wewe mwenyewe. "Mimi mzuri. Mimi ni mtu mzuri sana. Sistahili mahali pale." Na pengine ni mzuri, ukilinganishwa na watu wengi. Lakini sivyo ambavyo unahitaji kujilinganisha mwenyewe. Tunahitaji kujilinganisha wenyewe na kiwango cha Mungu. Kiwango cha chake kiko juu sana kuliko chetu. Anasema katika Neno kwamba kama ukisema uongo mara moja, mara moja tu katika maisha yako yote, inakufanya mwongo. Kama ukiiba kitu kimoja tu katika maisha yako, kwa mfano kibanio cha karatasi, dakika kadhaa za bosi wako, au kitu chochote, mara moja tu. Inakufanya uwe mwizi. Kama ukiwa na hasira bila sababu, kama haukumsamehe mtu aliyekufanyia kitu kibaya juu yako, kama ukimtamani mwanamke, chochote ya mambo hayo mojawapo, kama wewe ulifanya hayo mara moja tu, Hii inakufanya uwe mwenye dhambi, na hivyo hauwezi kuingia mbinguni. Hivyo unaweza kuona kila mmoja wetu amepungukiwa. Sote tumepungukiwa na hatuwezi kufika pale kwa matendo yetu wenyewe. Tito 3:5 inasema, Wala si kwa matendo ya haki ambayo tumefanya, bali kwa rehema yake alituokoa ... Amina, inategemea na jinsi unavyolinganisha. Ni kama mwanamke ambaye ameona kundi la kondoo katika mlima, na wote walikuwa weupe sana na wazuri upande wa mlima. Akasema, “Angalia hao kondoo weupe, angalia jinsi walivyowazuri, weupe." Kisha alikwenda kitandani na ghafla usiku barafu ikaanguka. Alitazama asubuhi yake na kuona kondoo wote wakiwa katika hali ya kufa, wachafu na wakijivu kulinganisha na barafu 16 nyeupe. Hivyo tunapaswa kujilinganisha sisi wenyewe na Mungu. Viwango vyake viko juu zaidi ya vyetu. Hivyo tunamuhitaji Mkombozi. Hatuwezi kufika pale sisi wenyewe. Mungu alifanya hii kuwa zawadi ya bure. Alisema katika Yohana 14:6, “mimi ni njia, kweli na uzima. hakuna awezaye kuja kwa baba , isipokuwa kupitia mimi.” Yeye ni njia pekee ya kutoka hapo. Kwa hivyo kama kuna yeyote Yule asiyemjua Bwana, yeyote Yule mahali hapa ambaye hakuwahi kumsihi Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yake. Haukuwahi kufikia maamuzi haya ambapo inakubidi upaze sauti yako kwa mdomo wako na kumsihi aje maishani mwako, Unaweza kusimama? Kama kuna yeyote mahali hapa unaweza ukasimama, Kwa ajili ya Yesu? Usimruhusu shetani, kile kiumbe kikucheke. Simama hivi sasa, ukiwa bado unanafasi, kwa sababu haujui ni muda gani tulionao. Haujui labda kesho unaweza kuaga dunia, na kuishia mahali pale. Ngoja nikueleze, mahali pale, moto tu wenyewe ni ngumu kuweza kuvumilia. wale watu tuliowaona wakiruka kutokea katika minara wa new York. Wanashikana mikono yao na kuruka. Inatisha kiasi gani. Unajua kama umewahi kuwa juu na ukaangalia chini, kuruka ni kitu kisichofikirika. Lakini kule ni lazima ukabiliane na moto. Na hiyi ni kwa muda wa sekunde tano,unakuwa umeungua tayari, na moto wa pale ni kama digrii elfu mbili. Wanasayansi wanasema katikati ya dunia ni kama digrii kumi nna mbili elfu. Kwa hiyo inakupaswa kuvimilia moto ule kwa umilele. Kama uko tayari kupitia hayo, huo utakuwa ni ujinga sana. Sasa ni wakati muafaka…. (mtangazaji anaongea) Biblilia iko wazi sana, isi wote ni wenye dhambi,na yeyote atakayeliita jina la Bwana ataokolewa. Yesus anasema kama ukinikiri mimi mbele za watu , naye mbele zao atakiri jina lako mbele ya baba yake na malaika watakatifu. na kama ukinikataa mimi mbele ya watu, nitakukana mbele ya baba yangu. Nataka nikuambia jambo la kufanya kama haujawahi mbele za watu kumkiri Yesu Kristo kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yako,au kama hauna uhakika kuwa mbinguni ni mahali ppako pa milele, kumbuka Yesu alisulubiwa uchi msalabani, sokoni,alisulubiwa pale kwa ajili yako, Alivumilia aibu yako. Kama ukiomba ombi hili kutokea moyoni, Mungu ataokoa nafsi yako, na atakupa nafasi kwa wakati ujao kulithibitisha hili mbele za watu. Omba nasi, hasa wale walio kwenye kongamano hili na wanajua imewapasa hivi. "Mungu naamini katika wewe. Wewe ni muumbaji wangu. mimi ni mwenye dhambi. Nimetenda dhambi katika maeneo mengi, kwa kukusudia, na kwakutokusudia. Nimepungukiwa na utukufu wako.Nimekosa chapa yako Ninanuka uovu. Yesu naamini katika wewe. Wewe ni mtoto pekee wa Mungu. wewe ni kondoo wa Mungu, uichukuae dhambi ya ulimwengu, uliyechukua dhambi zangu. Naamini ulukufa msalabani.Ukamwaga damu yako isiyo na hatia kwa ajili ya nafsi yangu. Naamini ulizikwa na siku ya tatu ulifufuka. Uko hai millele na milele. Nitakuita wewe Bwana. Nakuita wewe mwokozi wangu. Nakupa wewe maisha yangu. Nitakupenda, nitakutumikia siku zote za maisha yangu. Nitakuwa wako, chema, kibaya, uovu, mipango, ndoto zangu nakupa kila kitu. Mapenzi yako yafanyike kwangu. Naamini nimeokolewa. Si kwa matendo mema, lakini kwa imani, kwa kukuamini. Kwa jina la Yesu ninaomba. Amen." >>>>> MUITO MKUU KABISA<<<<< Jibu hilo ni sahihi kabisa. Biblia inasema mbingu inazizima kwa furaha kwa mwenye dhambi mmoja anayetubu. Na sisi tunajua mfano wa yale yanayoendelea mbinguni wakati mbingu inaposhuhudia nini umefanya leo. Nataka niwatangazie baadhi yenu, kisha nitahairisha mazungumzo haya. Nataka kutoa wito wa mabadiliko kwa wale baadhi yetu walioshuhudia haya. Tuna neema ya kipekee kusikia yale ambayo kaka yetu Bill aliyapitia. Nakwenda 17 kutoa changamoto kwako na Ninakuonya, usikubali hili isipokuwa uwe tayari kwa ajili ya maisha ya Roho maishani mwako. Sijaribu kukutania, nasema tu usifanye hili kuwa ni ukiri wako labda uwe umeamua kweli kweli. hivi ndivyo ilivyo. Kuna sehemu mbili. Moja, sitaendelea tena kuogopa uso wa mwanadamu. Kizuizi kimojawapo kikubwa kwetu sisi ni kutofanya kama vile unajua kuwa kuna Mbingu na kuna Kuzimu. Sitaendelea kuogopa uso wa mwanadamu. Mbili, Nitaongea na kila mmoja ninayemjua, Kuhusu Yesu, mbinguni na kuzimu, kwa maisha yangu yote. Hiyo ni dhamira/ahadi kubwa. Kila mtu ninayemjua mimi ambaye anahubiri/anawafikia watu kwa ajili ya Kristo anakuwa amefanya maamuzi haya. Kwa nini sasa ufanye uhusiano na mtu yeyote tu, kama si huu wa kushiriki pamoja nao habari njema yenye utukufu iokoayo roho zao na moto wa Kuzimu. Ni kosa katika Roho kumjua mtu, kuzungumza nao, na kufurahi pamoja nao, kufurahia uwepo wao, na kamwe huwaambii kuhusu hili, ya kuwa bila Kristo, watakwenda kuzimu. Kila uhusiano unapaswa kuwa ni mlango wa kuwasiliana kuhusu kweli ambayo umeshuhudia leo. Hiyo inaleta mantiki. Kama wewe hauko tayari kufanya hivyo, nitakuelewa. Lakini kama uko tayari kufanya maazimio hayo mawili, kama unakubaliana, sema haya kwa Mungu, "Mungu nakumini Wewe. Naamini katika Yesu Mwana wako, na Roho Mtakatifu wako wa thamani. Napokea changamoto ya muda. Natangaza mwenyewe, huu ni ukiri wangu. sitaendelea kuhofu uso wa mwanadamu. Sitatumikishwa na maoni ya mtu. Utu wangu si kitu. Nachukia hofu ya mtu. Nitamueleza kila mtu kwa muda wa maisha yangu yote yaliyobakia kuhusu Wewe Bwana Yesu. Kuhusu Mbinguni na sehemu inayoitwa Kuzimu. Nachukua hatua. sitaendelea kuwa wa tofauti, mtaabikaji wa maisha yangu mwenyewe, nisiyejali. Nakubali neno lako. sitaogopa, nitalisema. Huu ni ukiri wangu kwa Mwenyezi Mungu. " Inua jeshi lako Mungu, mji huu wote, taifa, na dunia, watu ambao wamebainisha majira vyema kwa wakati huu wanaoishi. Watu ambao wamekuja kuelewa umilele ni kipindi tu kifupi kijacho, kuona kwa uwazi katika utukufu wa Mbinguni na ubaya wa Kuzimu, na wameamuru vipaumbele vyao viwe ni kumtii Mungu. Sasa, tunaomba neema. Wameweza kufanya uamuzi huu wa kijasiri Mungu. Bila neema yako, hayatatokea haya. Tunaamini neema yako inatosha kutufanya tuishi katika neno la Mungu kama linavyoagiza. Neema, Neema, Neema iwe juu ya watu wako hapa, katika jina Yesu. Purchase his complete testimony "23 Minutes in Hell"

No comments:

Post a Comment

AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1)

http://bit.ly/3JGDJ4d MWL. JAMES F. MZAVER Minister Truth 0762759621 jamesmzava@gmail.com              AKILI ILIYOFANYWA UPYA. (1) Ukuaji ha...